SHERRIF ARPAIO
JF-Expert Member
- Aug 25, 2010
- 9,539
- 5,923
Go Reds
Japokuwa nataka Liverpool imnyamazishe the special idiot one , draw inaweza kuwa ni matokeo mazuri kwa Arsenal positioning at the moment
C&P KUTOKA FACEBOOK
KUELEKEA MCHEZO WA LIVERPOOL VS MAN UNITED.
.
1. KIUNGO.
Liverpool wanaweza kuwakosa Wijnaldum na Lallana ambao wameweza kuwapa uwiano mkubwa kwenye kiungo. Sidhani kama Klopp ataingiza wachezaji wapya wawili kikosini ila kuna uwezekano Coutinho akarejea katikati na Emre Can kuongezeka. Mourinho anatakiwa kutumia nafasi hii kuwanyima raha Liverpool hasa kabla hawajatulia katikati mwa uwanja. Pogba akicheza mbele kidogo umbo lake una ubunifu vinaweza kumfanya Henderson akose ubora wa kukimbia uwanjani na mpira. Hiki ndicho Mourinho anatakiwa kuhakikisha kinatokea ili aweze kutoka salama Anfield. .
2. FALSAFA
Hii inaweza kuwa mara ya kwanza msimu huu ambapo Manchester United itaukana mpira. Mourinho anajua kuwa Liverpool wanapenda kupress na ili wakupress watataka uwe na mpira. Sasa Mourinho anatakiwa kukaa nyuma huku akitumia wachezaji warefu kupokea mipira mirefu kwa ajili ya counter attacks huku pia akijitahidi kila nafasi ya mipira ya adhabu na kona anaitumia. Liverpool wataendelea kutaka kuadhibu kupitia mnyumbuliko wa Coutinho, Firmino na Mane na hapa ndipo ambapo Mourinho atahitaji presha ya hawa itulizwe na kiungo mmoja ambaye hatokuwa na tamaa ya kwenda mbele. Herrera anaweza kutenda haki bahati nzuri anajua kutumia mpira mguuni.
.
3. FALSE 9 VS CENTRE FORWARD.
Inawezekana Liverpool wakaendelea kutumia mfumo wa false 9 kupitia kwa Firmino. Huyu ana advantage mbele ya mabeki wa United kwa sababu kutokana na kupress vyema atawafanya wasiwe huru na mpira lakini pia kutokutulia kwake eneo moja kutafanya eneo la ulinzi lisiwe limetulia. Kwa Upande wa United watakuwa na Zlatan Ibrahimovic ambaye ni Center forward mzuri na ambaye ana nafasi ya kuwadhuru Liverpool kwa kupitia mipira ya juu. Liverpool hawapo vyema juu na hili Mourinho atahitaji Ibrahimovic awe vyema huku ikiwezekana kabisa Lovren akapewa kazi maalumu.
.
4. Udhaifu wa Liverpool ni zonal marking yao ambayo wachezaji wa United wakitumia counter vyema watapata kitu.
.
5. Udhaifu wa United upo kwenye kiungo. Hawajatulia hapa na Liverpool wana kasi zaidi eneo hili kuliko klabu nyingine yoyote. United wasipotulia wataumia. Liverpool inafunga sana kupitia viungo. .
Nicasius Coutinho Agwanda ( Coutinho Suso )
Soma Mwananchi kila Jumatatu na Jumapili. Ukurasa unaitwa Gozi la ng'ombe.
Kwani kama kitu ni kizuri hakitakiwi kuletwa humu? wonders shall never endYaani wewe ulioleta uchambuzi wa kifacebook humu kwrnye jukwaa la watu wanaojua mpira umeniharibia siku kabisa.
Yani serius kabisa kutoka facebook?Usitushushe bana.
Peleka facebook uchambuzi wa humu...sio kuuleta humu uchambuzi wa facebook.
Humu kuna vichwa tosha kabisa kutoka kwa wanaoijua liverpool nje ndani.Usirudie..mi niponipo hapa nawasoma.Nikikereka natokea kama hivi
Kiukweli kabisa nikiambiwa nichague kati ya hizi options mbili ninachagua ya pili kama wote Lallana na Gini hawatakuwepo.
1. Nafasi ya Gini aje Can.Nafasi ya Lallana arudi coutinho ili Sturridge aingie mbele acheze na Firmino na Mane.Huku nyuma kushoto akiwa Milner vilevile.
2.Nafasi ya Gini aje Can.Nafasi ya Lallana aje Milner.Kule mbele kuwe undisturbed kabisa.Mane,Firmino na Coutinho
Naenda na ya pili kwasababu Sturridge hatengenezi partnership nzuri pale mbele.Yupo slow na anapoteza mipira mingi sana pale mbele.Kupoteza mipira inayoelekea goli la manure leo ni kosa kubwa sana.Pia utatu wa mane,cou na firmino ni moja ya strength zetu msimu huu.It is named as the best premier trio by respected people.
So i better see moreno on pitch today than seeing our best frontline disturbed.Honestly.