S. S. Phares
JF-Expert Member
- Nov 27, 2006
- 2,138
- 82
Umeuliza ningefanya nini if it was me - ninge behave kama chama cha siasa na kuja na sera in that context, kuteka majimbo mengi as much as i can kwa nguvu ya hoja, sio kutishia wananchi kwamba wana viongozi wala rushwa. Pia ningeanzisha a very good media network ya kuelimisha wananchi kuhusu haki zao based on sera zilizopo under the current government. Wananchi hawajui haki zao ni nini sababu hakuna communication and dissemination ya information. Hii indirectly ingewaumiza sana serikali. Upinzani need to challenge ccm sera kwa sera, sio kudakia only pale ambapo hata wananchi wanaona kuna issue, mfano madini. Thats very low as a political party.
Wapinzani wamekuwa makini so far kwa sababu wanashirikiana kwa karibu na NGO mbalimbali na pia sasa wana media mbali mbali ambazo zinasaidia kufikisha ujumbe wao wa Sera...lakini pamoja na jitihada hizi ambazo mimi naona zinaweza kuboreshwa zaidi kama unavyopendekeza bado naona kuna umuhimu wananchi wakiangalia CCM kama chama cha siasa na sio dhehebu la dini. Watanzania wengi hawakipigii ccm kuwa kwa sababu ni chama chenye sera nzuri [ingawa ni kweli ccm wana sera nzuri] ila wanakipigia kura kwa sababu ni chama tawala, kilicholeta uhuru, kinachoshikilia dola n.k
Hii imani ya kuwa ccm ni baba na mama inatakiwa iwatoke wananchi kwa kuwekewa hadharani kuwa ccm hii ndio inayowanyima maendelea kwa kusaini mikataba mibovu, kukumbatia wala rushwa, kubana demokrasia bungeni n.k
Mrema 1995 hakupata kura zile alizopata kwa sababu alitoa sera nzuri sana bali aliweza kuonekana mbele ya wapiga kura kuwa ataweza kuwasaidi kufikia maisha bora kwa kupiga vita wala rushwa, kupambana na ujambazi n.k
Sera ni muhimu; lakini Je wapiga kura wetu walio wengi wako makini kuchambua sera na kuangalia sera mbadala; kwa maoni yangu naona huko bado hatujafika.