List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

Mchambuzi na Mtanzania mnaonekana kama mnalala. Nikiwauliza kuwa ni chama kipi kiko well organised, well disciplined, policies nzuri na uwezo wa kuexecute policies bila shaka, jibu litakuwa ni CCM. Na nikiuliza which political party is most corrupt Tanzania jibu litakuwa ni CCM, then how do you explain this? In our context what does policies have anything to do with the fight on corruption?
 
the question still remains 'WHAT ARE YOU GOING TO DO ABOUT IT'??

Haswa!! Mimi nilikuwa mpigaji simu wa kwanza jana pale Mwanakijiji aliporuhusu watu kupiga simu na kuuliza maswali. Swali langu lilikuwa rahisi tu lakini la msingi kabisa. Majina yametajwa hadharani (ingawa sikushangazwa nayo kwani tumeanza kuzisikia hizo tuhuma muda mrefu sasa), sasa ni nini kitakachofuatia? What's next? Hii sio mara ya kwanza vigogo serikalini kutajwa hadharani kuwa wanahusika na ufisadi, je hao walikwishatajwa siku nyuma nini kiliwatokea? Tuliwahi kuambiwa mambo ya Bibi Sitti Mwinyi...haya...mpaka leo nini kilitokea? Kama nia ya kuyataja hayo majina hadharani ni kuitambulisha jamii juu ya ufisadi unaoendelea basi hapo hamna jipya! Wananchi wanajua fika. Sio lazima mtu uwe mwanasayansi wa maroketi kutambua hilo.

Je, kama wapinzani wakiamua kufungua kesi mahakamani dhidi ya viongozi waliotajwa, wana uhakika kweli wa kushinda? Kwa sababu hata mahakama zenyewe zimejaa ma-appointees wa CCM.
 
Kina kabwe wanapoteza tu muda huko mikoani, this was an aopportunity for them kunadi sera zao na mwishoni mwishoni ndio kutaja mambo ya rushwa kama mifano.

Mchambuzi hiyo approach yako ya kunadi sera kwanza, kwa watanzania ambao tumelala zaidi ya miaka 40 ingekuwa sawa na kutwanga maji kwenye kinu!

Lakini hii approach ya kuwaamsha kwanza watu waone jinsi wanavo liwa nadhani ni super!

Sema cha msingi kinachotakiwa sasa baada ya kuamsha ari za watu wakajitambua wanavo ibiwa mchana kweupe ndo ifate sasa ya kunadi sera zao zinazo elekeza jinsi ya kuondokana na ufisadi huu.

Lakini bila kuwaeleza na kuwaonyesha watu ubovu wa CCM wala wapinzani wasingeweza kubalika!

Kwa mfano, Watanzania walio wengi tuliamini JK ni malaika, lakini kama kuna udhibitisho unao onyesha kwamba naye ni mfisadi kwa watanzania makini watajua kwamba CCM yote kaputi!

Na hivo itakuwa rahisi sasa kumshawishi mtu aachane na chama kaputi utakapo anza kujinadi!
 
Nadhani tunahitaji watu walio more serious na intelligent kupigana na rushwa, na sio kuendeleza siasa za udaku. You can not go to Jangwani grounds and shout out loud kuwa Mkapa amepokea rushwa, au Karamagi amepokea rushwa hii inaweza tu kukupa umaarufu wa siku tatu nne na ukaonekana kwenye magazeti, hiawezi hata kukusaidia kuchaguliwa kuwa mbunge. Tumeona watu waliokuwa wakubwa ndani ya serikali walioona uchafu zaidi ya huo wa Zito Kabwe, where are they now? half dead! Nadhani the fight against corruption in Tanzania should be more scientific na sio domo. PCCB imeprove failure, sidhana hata kubadilisha jina kutasaidia kitu" same wine , different bottle". Labda wakijaribu kupambana na rushwa kutoka nje ndio wataweza kidogo kuonesha mafanikio. Huu ni ukweli unaosikitisha
 
Mchambuzi,
Mimi kidogo nianze kukubaliana na wewe ulipoweka hoja moja tu... what are we gonna do about it?... Hii ikitukusanya sote ktk pakacha moja linalovuja.

Nachoshindwa kuelewa ni pale wewe na Mtanzania mnaweka madai yenu dhidi ya Mh. Slaa na Mrema kwa sababu tu hawa watu wanatoka vyama vya upinzani!. Sijaona hata sehemu moja mkipinga na kutoa maelezo yenu kukanusha siasa hizi za fitna isipokuwa mnachokifanya ni kubisha, kuomba ushahidi wakati nyie wenyewe roho zenu zinawasuta kwa kumezeaukweli uliokuwa wazi.

Nitakubaliana nanyi tu ikiwa kuna baadhi ya majina mnayawekea wasiwasi lakini sio kupuuza kabisa habari hii ambayo inakutaka wewe, mimi, yule na Watanzania wote wenye upendo na nchi yetu kujiuliza swali hili - What we gonna do about it?

Je, mnayafanya haya kwa sababu ya mapenzi ya chama CCM ama kwa sababu mnawapenda hao viongozi waliotajwa! Hivi kweli leo hii CCM imekuwa chama cha hao watu wachache waliotajwa kiasi kwamba wananchi wazalendo wananchama wa chama hiki makini wamefikia mahala wanashindwa kufikiria Chama nje ya majina hayo hapo?...Na ndio maana kweli wanakuwa na msemo usemao hizi ni kelele za mlangoni, haziwazuii kupata usingizi! wakijua kwamba ujinga unaanzia ndani ya CCM ambako wao ni MIUNGU watu.

Ndugu zangu kumbukeni tena kuwa Mapinduzi ya Kiuchumi China yalitanguliwa na kukamatwa kwa viongozi wa juu (The big Four) ktk Utawala ule aliouacha Mao Tse Tung. Hawa ndio walioachiwa urithi na Mzee Mao alipoondoka tu duniani waligeuza Maslahi ya China kuwa ni yao. Hawa ndio akina Mkapa na wengineo.

Ask yourself, what you gonna do not what Mrema or Slaa will do for you!
 
Nadhani tunahitaji watu walio more serious na intelligent kupigana na rushwa, na sio kuendeleza siasa za udaku. You can not go to Jangwani grounds and shout out loud kuwa Mkapa amepokea rushwa, au Karamagi amepokea rushwa hii inaweza tu kukupa umaarufu wa siku tatu nne na ukaonekana kwenye magazeti, hiawezi hata kukusaidia kuchaguliwa kuwa mbunge. Tumeona watu waliokuwa wakubwa ndani ya serikali walioona uchafu zaidi ya huo wa Zito Kabwe, where are they now? half dead! Nadhani the fight against corruption in Tanzania should be more scientific na sio domo. PCCB imeprove failure, sidhana hata kubadilisha jina kutasaidia kitu" same wine , different bottle". Labda wakijaribu kupambana na rushwa kutoka nje ndio wataweza kidogo kuonesha mafanikio. Huu ni ukweli unaosikitisha

Exactly. Look at warioba, look at Hassy Kitine, look at mrema, look at mtikila. Wapo wapi sasahivi? Actions zao zimesaidiaje mkulima na mfanyakazi mwenye maisha duni Tanzania? And kipi tofauti kina kabwe na slaa wanakifanya? In my view, kuna waliofanya better than kina kabwe na slaa in terms of kupayuka wala rushwa....Hawa ni just a few ambao wana habari zaidi ya hao kina kabwe, zitto...
The only difference ni kwamba kina zitto na kabwe ni wapya na watazoeleka tu na kusahaulika kwasababu hawana any new approach and it has proved not to be sustainable. Sana sana watashinda majimbo yao ya uchaguzi kama mrema jimbo la temeke 1995 and then phase out leaving ccm prospering.

CCM bado wana advantage kubwa sana kutokana na wrong approach ya hawa wapinzani. When it comes push to shovel, ccm wenyewe wataeunguana kukinusuru chama na kina kabwe, slaa wataishiwa hoja sababu siasa zao ni za hoja, sio za sera.
 
Mchambuzi you are right. Ndio maana sioni upinzani in the near future kuleta mabadiliko Tanzania, siasa zao za hoja mara nyingi ni za nguvu ya Soda, wanasahau kuwa CCM sio shetani kabisa, ina uzuri wake. Just because JK anayumba haina maana kuwa CCM inayumba. So far in policeis zenye nguvu, ila utekelezaji wake ndio una mgogoro kwa sababu wameingia watu kama kina Karamagi ambao naweza kusema hawajui a wala be, wanaangalia pafupi hawana over role picture ya mambo na hawaangalii broader issues zinazowaumiza watanzania. Lakini timu ikipangwa vizuri, everything will be fine, na wapinzani watakufa kifo cha kawaida
 
Mchambuzi,
Mimi kidogo nianze kukubaliana na wewe ulipoweka hoja moja tu... what are we gonna do about it?... Hii ikitukusanya sote ktk pakacha moja linalovuja...
Nachoshindwa kuelewa ni pale wewe na Mtanzania mnaweka madai yenu dhidi ya Mh. Slaa na Mrema kwa sababu tu hawa watu wanatoka vyama vya upinzani!. Sijaona hata sehemu moja mkipinga na kutoa maelezo yenu kukanusha siasa hizi za fitna isipokuwa mnachokifanya ni kubisha, kuomba ushahidi wakati nyie wenyewe roho zenu zinawasuta kwa kumezeaukweli uliokuwa wazi.

Kina slaa na kabwe hawaji na kitu kipya. Ni ile ile approach iliyofanywa na kina mrema, mtikila as upinzani na pia kina warioba, hassy kitine wakiwa wana ccm. Nothing changed. Wakija hawa watafanya yale yale ambayo wanayanyooshea vidole. Mwananchi akipigia kura upinzani just because wanasema watasimamia vita dhidi ya rushwa kwa nguvu, wanasiasa wa namna hii ni wa kuwakimbia kama ukoma. There is more to that. We need sustainable approaches ambazo zita lead to sustainable solutions, kwa mifano kama hiyo ya china ambayo ni correct in all colors. Lakini so far upinzani hauonyeshi anything like that. As a result, mimi naishia kuwa na view kwamba we still can correct CCM ikatupeleka kuzuri kwa sababu kuna baadhi ya viongozi kama mwandosya ambao i believe they can do good for our country.

Pia EL i am not ruling him out as long as anajirekebisha kama alivyosema mwalimu. Najua hii hoja inawachoma wengi sana humu na pia inaonekana nimo humu kumfagilia EL. Mimi bado nina imani sana na ccm kama chama cha kutuongoza na viongozi naodhania wanao huo uwezo ni kama mwandosya, lowassa mwenyewe, vijana chipukizi kama tom mwang'onda, john nchimbi, Dr. Buriani, Dr. Migiro na wengine wachache. Haya ni maoni yangu, tujibishane kwa hoja, sio matusi jamani.
Msisahau kwamba hata mwalimu saw a lot in Lowassa na akasema akijirekebisha anayo nafasi nzuri. tazama tena ile interview ya nyerere on ITV 1995. Tatizo on lowassa ni kwamba nyerere alimweka hadharani na hiyo ndio ime set tone for the rest of his political career. But believe me or not, lowassa ni kifaranga, kuna ma mbuni.

Again, lowassa ile issue ya nyerere imem affect sana and it makes him panic and work to prove the public wrong. Hii ingeweza mtokea mwasiasa yeyote kama angechafuliwa na sumu ya nyerere. You end up performing based on proving something to the public. What EL needed and still needs ni washauri wazuri.

2015, ni EL au Mwandosya. Nje ya hapo ni some body else ambao mtandao will put kum challenge Mwandosya assuming mwandosya will remain nje ya mtandao.
 
Exactly. Look at warioba, look at Hassy Kitine, look at mrema, look at mtikila. Wapo wapi sasahivi? Actions zao zimesaidiaje mkulima na mfanyakazi mwenye maisha duni Tanzania? And kipi tofauti kina kabwe na slaa wanakifanya? In my view, kuna waliofanya better than kina kabwe na slaa in terms of kupayuka wala rushwa....Hawa ni just a few ambao wana habari zaidi ya hao kina kabwe, zitto...
The only difference ni kwamba kina zitto na kabwe ni wapya na watazoeleka tu na kusahaulika kwasababu hawana any new approach and it has proved not to be sustainable. Sana sana watashinda majimbo yao ya uchaguzi kama mrema jimbo la temeke 1995 and then phase out leaving ccm prospering.

CCM bado wana advantage kubwa sana kutokana na wrong approach ya hawa wapinzani. When it comes push to shovel, ccm wenyewe wataeunguana kukinusuru chama na kina kabwe, slaa wataishiwa hoja sababu siasa zao ni za hoja, sio za sera.

No, advantage waliyonayo CCM ni ujinga walionao Watanzania wengi wanaoendelea kuwachagua kwa kura nyingi licha ya maisha yao kuwa duni beyond belief. Mtu yoyote mwerevu hawezi kuwachagua watu kama akina Lowassa na Kikwete. Hawa jamaa kama wangekuwa Marekani they would have faded into 'bolivion' (to borrow from Mike Tyson). Ni ujinga huu ndio uliowafanya wananchi waamini kuwa pengine bila CCM hakuna Tanzania kitu ambacho hakina chembe ya ukweli hata kidogo. Wananchi wengi wanaoipigia kura CCM, kama wangekuwa werevu na uwezo angalau wa wastani wa kuchanganua mambo, ungeona hata bunge letu lingekuwa na idadi nzuri ya wabunge wa upinzani au hata wabunge makini wa CCM na sio a bunch of yes men and women like they are now.
 
Kinachotakiwa hapa ni majina dhidi ya kashfa zao na si blaa blaa.

Hivi mkuu MMJ, kuna uwezekano wa kina Slaa kutoa hasa maovu ya hao wakuu, tuna-appreciate majina lakini demokrasia inadai uchafu wao kusemwa ili waweze kujitetea kwenye public kwanza kbala ya sheria,

kama mnayo maovu yao tuwekeeni hapa, tuyachambue!
 
Mchambuzi,

hakika mzee wangu unaipenda CCM.. Kiasi kwamba unashindwa kuona kuwa hii mada inawahusu Viongozi fulani na sio chama CCM. Unachojaribu kufanya hapa ni kupotosha kabisa hoja nzima ya mada hii kuifanya kuwa swala la CCM vs Wapinzani.

CCM wanaendelea kutumyonya kwa sababu ya wajinga fulani ndani ya chama hicho wanaozidi kuwabeba viongozi hawa! Hili sio swala la Mrema, Slaa, Kabwe..

Ebu tuambie kama wewe ungelifanya nini?.. Imean mjomba kuwa na option hata kidogo ktk maelezo yako. Umewasimamia Vyama vya Upinzani kama vile wao ndio hushikilia masanduku ya Kura!..

Jiuliza wewe kwa nini unaendelea kukichagua CCM? kwa sababu huwaamini Mrema na Slaa?...

Duh hii mpya sawa na mwanamke anayekubali kubakia ktk abuse relationship ati kwa sababu haoni mwanaume mwingine huko nje zaidi ya Mumewe!
 
Mimi ninachohoji, ni usiri katika mikataba ya serikali.Huu usiri unakuwaje unaishia kwa waziri na mbunge asiwe na haki ya kuiona au kuihoji?Ni vipi waziri endapo hatakuwa waziri katika awamu ijayo na akaendelea kuwa mbunge,je hatakuwa anajua usiri wa baadhi ya mambo ya serikali?
 
Mchambuzi,
hakika mzee wangu unaipenda CCM.. Kiasi kwamba unashindwa kuona kuwa hii mada inawahusu Viongozi fulani na sio chama CCM. Unachojaribu kufanya hapa ni kupotosha kabisa hoja nzima ya mada hii kuifanya kuwa swala la CCM vs Wapinzani.
CCM wanaendelea kutumyonya kwa sababu ya wajinga fulani ndani ya chama hicho wanaozidi kuwabeba viongozi hawa! Hili sio swala la Mrema, Slaa, Kabwe..
Ebu tuambie kama wewe ungelifanya nini?.. Imean mjomba kuwa na option hata kidogo ktk maelezo yako. Umewasimamia Vyama vya Upinzani kama vile wao ndio hushikilia masanduku ya Kura!..
Jiuliza wewe kwa nini unaendelea kukichagua CCM? kwa sababu huwaamini Mrema na Slaa?...
Duh hii mpya sawa na mwanamke anayekubali kubakia ktk abuse relationship ati kwa sababu haoni mwanaume mwingine huko nje zaidi ya Mumewe!

Bob

Najaribu kumsoma Mchambuzi, bado nafikiria namna ya kumjibu...ila point yake moja nimeeielewa na nikiijibu kupitia mfano wako (bolded) ni kuwa kuna uwezekano mkubwa sana kuwa mwanamke huyo akawa anaona ni bora abaki na mumewe mkorofi kwa sababu anaamini pengine kinachompa ukorofi ni pombe i.e viongozi wabaya ndani ya ccm na hivyo kuwa anapata faraja siku moja moja pale mumewe asipokwenda kilabuni kunywa...kwa maana halisi; Ndio CCM imejaaa viongozi wabovu lakini wananchi wanaamini JK au mtu mwingine ndani ya chama akipewa nafasi anaweza kuwaondoa hao mafedhuli wachache. Sasa Je hao mafedhuli wachache wakishaondoka si imani ya maisha bora itarudi tena kwa wananchi...???
 
Mchambuzi,
hakika mzee wangu unaipenda CCM.. Kiasi kwamba unashindwa kuona kuwa hii mada inawahusu Viongozi fulani na sio chama CCM. Unachojaribu kufanya hapa ni kupotosha kabisa hoja nzima ya mada hii kuifanya kuwa swala la CCM vs Wapinzani.
CCM wanaendelea kutumyonya kwa sababu ya wajinga fulani ndani ya chama hicho wanaozidi kuwabeba viongozi hawa! Hili sio swala la Mrema, Slaa, Kabwe..
Ebu tuambie kama wewe ungelifanya nini?.. Imean mjomba kuwa na option hata kidogo ktk maelezo yako. Umewasimamia Vyama vya Upinzani kama vile wao ndio hushikilia masanduku ya Kura!..
Jiuliza wewe kwa nini unaendelea kukichagua CCM? kwa sababu huwaamini Mrema na Slaa?...
Duh hii mpya sawa na mwanamke anayekubali kubakia ktk abuse relationship ati kwa sababu haoni mwanaume mwingine huko nje zaidi ya Mumewe!

Nchi yangu ya tanzania inahitaji kuongozwa na chama cha siasa na so far chadema na wenzake in my view sio vyama vya siasa zaidi ya what t says in their registration, to me hawa ni pressure groups kama DP ya wakati ule ya mtikila. Ndio maana sioni option nyingine zaidi ya ccm itakayojisafisha au ccm itakayovunjika au kuja chama kingine cha kweli cha upinzani, sio kuhangaika na hizi pressure groups za kina slaa, kabwe.

Anachofanya kabwe na slaa kina tofauti gani walichofanya kina mrema, mtikila, hassy kitine, warioba, mengi? Waliyofanya yametupeleka wapi ndugu mkandara.

Umeuliza ningefanya nini if it was me - ninge behave kama chama cha siasa na kuja na sera in that context, kuteka majimbo mengi as much as i can kwa nguvu ya hoja, sio kutishia wananchi kwamba wana viongozi wala rushwa. Pia ningeanzisha a very good media network ya kuelimisha wananchi kuhusu haki zao based on sera zilizopo under the current government. wananchi hawajui haki zao ni nini sababu hakuna communication and dissemination ya information. Hii indirectly ingewaumiza sana serikali. Upinzani need to challenge ccm sera kwa sera, sio kudakia only pale ambapo hata wananchi wanaona kuna issue, mfano madini. Thats very low as a political party.
 
Denny the question is ukijua hayo majina utafanya nini? umeandaa nini ili kusiwe na usiri kwenye mikataba hiyo? Tumejua majina befoe what happened the them. Unasema unachohiji ni usiri, no doubt kuwa huwa usiri ndani yake un rushwa. Kinachotakiwa ni lasting solution ya tatizo la kickbacks na sio porojo au siasa za udaku as mchambuzi put it
 
Kumbukeni Warioba aliwahi kutaja kuwa rushwa tunayoiona mtaani si rushwa bali Wakubwa ndo wanatafuna rushwa katika nchi hii.
Imefikia mahala sasa rushwa hiyo inawapa jeuri mpaka wanaila waziwazi.
Ni nani asiyejua fadhila za wafanyabiashara wakubwa wakati wa kampeni kwa chama tawala?
 
Nchi yangu ya tanzania inahitaji kuongozwa na chama cha siasa na so far chadema na wenzake in my view sio vyama vya siasa zaidi ya what t says in their registration, to me hawa ni pressure groups kama mtikila. Ndio maana sioni option nyingine zaidi ya ccm itakayojisafisha au ccm itakayovunjika au kuja chama kingine cha kweli cha upinzania, sio kuhangaika na hizi pressure groups za kina slaa, kabwe.

Anachofanya kabwe na slaa kina tofauti gani na mrema, mtikila, hassy kitine, warioba, mengi?

Heshima yako Mchambuzi...napenda unavyokata issues.

Hebu niangalie mtazamo wako unaoutetea wa hoja ya sera. Katika siasa zetu Bongo SERA zinachukua nafasi gani? watanzania wanaopiga kura kwa kuangalia sera ni asilimia ngapi ya wapiga kura wote. Je unaweza kuniambia wanakijiji pale Buzwagi ukiwaambia mzungu amepewa mgodi kwa njia zenye mashaka ndio maana hapa kijijini kwenu hakuna hospitali, shule, kituo cha polisi, barabara n.k watakuuliza sera ya chama chako ni ipi. Je kuna kweli hata hapo Dar ambako wapiga kura wenye elimu ni wengi zaidi wanajua kweli sera za CCM kulinganisha na za Chadema, TLP, CUF n.k?
 
Yebo Yebo,
Ndio CCM imejaaa viongozi wabovu lakini wananchi wanaamini JK au mtu mwingine ndani ya chama akipewa nafasi anaweza kuwaondoa hao mafedhuli wachache. Sasa Je hao mafedhuli wachache wakishaondoka si imani ya maisha bora itarudi tena kwa wananchi...???

Safi kabisa ikiwa kuna viongozi ndani ya CCM wanaweza kutuongoza vizuri. Na hakuna kati yetu anayesema hakuna... Hili ndio mnaloshindwa kulielewa. Wanachofanya Mrema na Slaa sio kuishambulia CCM kama ni chama kibaya kisichokuwa na viongozi ila wanachozungumzia ni huu Uongozi wa hawa waliopo madarakani.

Yebo yebo, hizo habari za kusema pengine wakiacha Ulabu ni kujidanganya wenyewe kama vile Zimbabwe wanavyozidi kujidanganya na Mugabe...Mlevi huyu Mrema katoka nyumba ya CCM hakuna anayesema tusikubali posa yoyote toka kwa watoto wa mzee CCM, isipokuwa tunachosema sisi ni kwamba - Sisi waislaam tunasema hivi hadi hapo nyumba ya mzee CCM watakapo acha kula nguruwe (Rushwa)! labda ndio posa yao inaweza kubalika..Pamoja na kwamba uwezekano wa kutokula kitumoto haupo!. Anyway, swala ni hawa walevi tena abusive kutegemea kwamba wanaweza kubadilika duh! hilo tena jingine.

Kama upo uwezekano ndani ya CCM kuwaondoa hawa viongozi madarakani na kuweza kurudisha hadhi ya chama nadhani hili ndilo lengo la Mrema na Slaa. Kwani habari kama hizi wangezitumia siku ya kura 2010 tungesema ni kwa maslahi yao ama ya chama chao na pengine hata ku raise kwa nini hawakuyasema haya toka 2007 yaani leo hii. Hawa jamaa wametupa habari hizi mapema hakuna uchaguzi wala mjomba wake bado tunatafuta vijisababu vya kuwakimga maharamia!

Kwa hiyo ndugu zangu tuwe na mwelekeo, tuwe watu wazima wenye kutazama na kupima kuwa ukombozi wa nchi yetu haumtegemei Mrema, Slaa, wala Zitto ila hawa ni viamsho na wajenga ari ya kuanzisha mapambano yetu.
 
Back
Top Bottom