Ukweli ni kwamba chuoni tulistuka wanafunzi wa kike wanatembea na walimu, watumishi wa serikali, wafanyakazi wa mabenki hasa wale teller, wafanya biashara, swagga boys wa mitaani, n.k. Yaani ikitokea mwanafunzi wa kiume kaamua kuwa na girlfriend wa hapo chuoni inabidi amvute geto waishi pamoja zile ndoa za chuoni maana ushindani ni mkubwa, tena wanafunzi tulikuwa hatuheshimiani, wakijua umepata wa chuoni ni kama umepuliza filimbi ya mashindano, watafanya jitihada wakuchapie.
Hii ikafanya na sisi tutafute wanyonge wetu wa nje ya chuo kuanzia mabinti wanaouza maduka, mabinti vya mama ntilie, mabinti wanaoshinda majumbani, mabeki tatu, n.k. hawa walikuwa hawana gharama sana na wengi walituheshimu kwa ile hadhi / status ya kuwa mwanachuo.
dem wangu wa kwanza chuoni alikuwaga wa mtaani ila mabroo waliotutangulia wakanisanua huyo cha wote nikamuacha, nikaja kuwa na mtoto wa mama ntilie, nikahamia kwa anaefua nguo, nikahamia kwa Anaeuza duka la simu, nikaja kwa beki Tatu alieletwa tupo nyumba moja namvusha geto la nje kikomandoo.
Nadhani mada ilibidi iwe kwa wanaume wanaomaliza chuo bila kuwa na dem kabisa.