Laana kuu Ubungo mataa!

Jamani, kujenga madaraja sio suluhisho. Tatizo la nchi yangu ni kwamba hatuna wataalam wa mipango ya aina yeyote. Wanawaza sasa hivi tu. Mbona mji flani niliona ma flyovers na hakuna foleni? Huo si utaalam wala sio mpango. Kujenga flyover Ubungo Mataa hakutaleta suluhisho kwani msururu utaanzia magomeni mpaka magari yatakuwa hapo juu yamekwama.
Tutengeneze michepuko tu na hizo hela ka zipo mzee Magufuli. Michepuko ikiwa mizuri na yenye lami ikiwezekana nnani atapoteza mda wake Ubungo Mataa?
Watu wanakuja na solutions rahisi rahisi tu. Watu hawataki kufikiri ni kutamka tu. Unaamuru watu waende Mabwepande. Unaenda kumtupa mtu msituni na kumwacha huko. Hujali watoto walio athirika na usumbufu huo, hujali wamama walio athirika na usumbufu huo. Ni majambazi tu unazalisha kwa ile chuki kuwa umemtoa mjini ukampeleka porini na kumtupa huko. Unaamua, boda boda zisifike mjini, unataka watu watembee toka wapi mpaka wapi. Ati, sababu ni kwamba boda boda zinatumiwa na wezi. Hivi hilo ndo tatizo kweli? Ama kweli, vichaa wanapopewa rungu, tujiandae.
Tafuta suluhisho la tatizo kwanza halafu ndo marufuku isimamie. Tanzania bila uongozi huu uliopo, yawezekana. Watu wamekata tamaa, hata kupiga kura hawataki. Anaona heri alale usingizi kuliko kwenda mchagua kichaa mwingine kwani ni wale wale tu kila siku. Ahadi kibao na flana na chepeo tu, sana sana na wali maharage sinia moja watu 10. Hiyo yaitwa Takrima. Nasema, Tanzania bila huu uongozi uliopo, YAWEZEKANA.
Nasema flyover sio suluhisho. Tengenezeni michepuko.
Kwahiyo watu wanachagua vichaa, jiheshimu
 
Kutatatua foleni Dar ni rahisi sana wala hakuhitaji kupoteza fedha kujenga Midaraja mikuubwa, ni kuhakikisha tu kila halmashauri br. zake zote zinapitika, siyo lazima waweke lami hata wahakikishe tu kila baada ya Miezi 3 zinapigwa greda, hilo litapunguza foleni kwa zaidi ya 1/3 na kwa gharama ndogo sana, unafikiri kwa nini Oysterbay hamna foleni? Ni kwa sababu Serikali wamejenga br. zote na zinapitika hivyo kuna njia nyingi sana, kwa hiyo walipaswa wafanye kama Oysterbay kupitisha greda tu br. za Mitaani kunatosha sana tu!
Wangerekebisha barabara za mitaani tu.

Barabara za michepuko,

Swali la kimahesabu. Daraja la tazara likitema magari buguruni magari yakijaa buguruni junction siyatakwama?

Ubungo ikitema mabibo external kwenye junction sitayakwama, mandera ikitema mwenge junction siyatakwama, viongozi wetu wanafikiria kwa urefu wa rula.

Akili lazima zifikirie mbali. Dsm bado haina magari mengi. Barabara za juu ni anasa.
 
Binafsi napinga Kujengwa Daraja Ubungo Mataa kwa sasa na badala yake hizo Fedha kama zipo zipelekwe kujenga Br. za Mikoani na Wilayani! Bado kuna Mikoa Mingi sana haijaunganishwa na Br. za Uhakika na Dar tayari ina miundombinu mizuri na ya kutosha! Kwa Mf. waunganishe Mbeya mpaka Tabora na mwishowe Kigoma n.k
Ukitoa hiyo barabara uliyoitaja, ni barabra gani nyingine za mikoa hazijaunganishwa na wala hazipo kwenye mpango au ujenzi?
 
Wangerekebisha barabara za mitaani tu.

Barabara za michepuko,

Swali la kimahesabu. Daraja la tazara likitema magari buguruni magari yakijaa buguruni junction siyatakwama?

Ubungo ikitema mabibo external kwenye junction sitayakwama, mandera ikitema mwenge junction siyatakwama, viongozi wetu wanafikiria kwa urefu wa rula.

Akili lazima zifikirie mbali. Dsm bado haina magari mengi. Barabara za juu ni anasa.
Yaani wewe ni pingapinga tuuu!! Anzisha nchi yako!
 
Baada ya kukaa foleni masaa mawili pae ubungo mataa ninaomba kujua yafuatayo.

1.) Ni hasara kiasi gani tumepata kama Taifa katika kipindi cha miaka kumi mpaka Leo kutokana na foleni hizi.

2.) Inagharimu kiasi gani kujenga daraja la magari kupita juu pale junction.

3.) Tukijua hizi data basi tutaweza kukadiria ni kwa kiasi gani serikali Yetu imelala.


Nimetazama ule ujenzi sijaelewa kwanini wameweka ghorofa mbili na ground floor 😀itatumika kwa shughuli ipi, kadhalika mwendokasi watapita wapi?
 
Back
Top Bottom