Laana kuu Ubungo mataa!

Laana kuu Ubungo mataa!

Ujenzi wa flyovers ni kiini macho.unahamisha tatizo kutoka junction A kwenda B.nafikiri tujikite zaidi kwenye ujenzi wa ring roads hii itasaidia. Kwa mfano ukijenga daraja Tazara utahamishia tatizo Buguruni na kwingineko au ukijenga Ubungo unaogeza volume Magomeni na kwingineko kwenye junction .tuache tabia ya kutaka kujionesga na tujikite kwenye utaalamu.

Hapana Mkuu.. kuna maeneo ni kero mno.. sasa ili ku-neutralize hayo maeneo madaraja yanahitajika, kwani ukiweka flyover ubungo na magari yakapita pale bila kusubiriana si itasaidia sana..?
 
Tatizo wabongo wengi mbulula halafu wanajifanya wanajua kuchangia upuuzi, Flyover ndo huwa suluhisho la foleni sio lazima ujenge zote kwa pamoja mfano barabara kutoka Manzini Swaziland to Mbabane kuna Flyver za kumwaga ambazo wala hazioneshi kuwa gharama sana pia kutoka Johburg mpaka pretoria so mchezo ,najua watakuja kutetea ule uf.a.la wao ku SA imeendelea kiuchumi je swazi wana uchumi gani?

Nairobi je Nigeria je, nadhani Tanzania ndio nchi ambayo haina Flyover hata moja, swala kwamba barabara zipigwe grader ni hoja chakavu japo itasaidia kidogo coz kila mtu atataka kupita huko kwa tunaojua chocho za bongo liko wazi hili, halmashauri nyingi najua hazina foleni kabisa ukiacha majiji magreda yanatosha ila provision ya bara bara nyingi tena za Flyover zinatakiwa sio barabara mbili kila cku kwenye majukwaa na TV juu mnajisifia wakati kila kukicha mko ulaya mnaona wanaume wenzenu walivyotumia akili zao na rasilimali.
 
Baada ya kukaa foleni masaa mawili pae ubungo mataa ninaomba kujua yafuatayo. 1.) Ni hasara kiasi gani tumepata kama Taifa katika kipindi cha miaka kumi mpaka Leo kutokana na foleni hizi. 2.) Inagharimu kiasi gani kujenga daraja la magari kupita juu pale junction. 3.) Tukijua hizi data basi tutaweza kukadiria ni kwa kiasi gani serikali Yetu inawazimu.

Si nasikia wewe ni ccm damu,tena damu yako niya kijani eti!
 
Umeleta bonge la topic mkuu hii ni moja ya hoja zinazogusa maisha yetu ya kula cku uwe kwenye dala dala kwenye vx, uwe mfanyabiashara wa nchi jirani inapitishia mizigo yake bandar yetu foleni ipo na dar ndo kitovu cah uchumi,wale jamaa huwez kuwaona hapa!
 
Bado haunielewi, nimekwambia gharama ya kupitisha greda ni ndogo sana ukilingisha na kujenga daraja kubwa ama kuweka lami, Halmashauri zote zina magreda hivyo ni swala la kuweka mafuta tu... Ni kazi rahisi sana Mimi diwani wangu huwa anafanya kwenye Kata yetu na hatuna shida, kila baada ya miezi 3 greda linapita!

Wazo zuri mkuu nitalifikisha kwa diwani wangu.
 
Baada ya kukaa foleni masaa mawili pae ubungo mataa ninaomba kujua yafuatayo. 1.) Ni hasara kiasi gani tumepata kama Taifa katika kipindi cha miaka kumi mpaka Leo kutokana na foleni hizi. 2.) Inagharimu kiasi gani kujenga daraja la magari kupita juu pale junction. 3.) Tukijua hizi data basi tutaweza kukadiria ni kwa kiasi gani serikali Yetu inawazimu.
ha ha ha ha! kikwete rais bora africa mwaka 2013!
 
Bado haunielewi, nimekwambia gharama ya kupitisha greda ni ndogo sana ukilingisha na kujenga daraja kubwa ama kuweka lami, Halmashauri zote zina magreda hivyo ni swala la kuweka mafuta tu... Ni kazi rahisi sana Mimi diwani wangu huwa anafanya kwenye Kata yetu na hatuna shida, kila baada ya miezi 3 greda linapita!

unafikiri grader ni bajaj? acha utani bana!
 
Baada ya kukaa foleni masaa mawili pae ubungo mataa ninaomba kujua yafuatayo. 1.) Ni hasara kiasi gani tumepata kama Taifa katika kipindi cha miaka kumi mpaka Leo kutokana na foleni hizi. 2.) Inagharimu kiasi gani kujenga daraja la magari kupita juu pale junction. 3.) Tukijua hizi data basi tutaweza kukadiria ni kwa kiasi gani serikali Yetu inawazimu.

Tunavyo vipaumbele vingi kuliko hiyo foleni ya Ubungo. mfano Sitta amekodi ndege kuwapeleka wabunge kuona kaburi la Sokoine. kitu kama hichi ni priority zaidi kuliko foleni
 
Kutatatua foleni Dar ni rahisi sana wala hakuhitaji kupoteza fedha kujenga Midaraja mikuubwa, ni kuhakikisha tu kila halmashauri br. zake zote zinapitika, siyo lazima waweke lami hata wahakikishe tu kila baada ya Miezi 3 zinapigwa greda, hilo litapunguza foleni kwa zaidi ya 1/3 na kwa gharama ndogo sana, unafikiri kwa nini Oysterbay hamna foleni? Ni kwa sababu Serikali wamejenga br. zote na zinapitika hivyo kuna njia nyingi sana, kwa hiyo walipaswa wafanye kama Oysterbay kupitisha greda tu br. za Mitaani kunatosha sana tu!

Mkuu

Nimekupata vizuri!

Ila nafikiri suala la kupitisha greda kila baada ya miezi mitatu siyo sustainable!

Hebu imagine kila baada ya miezi mitatu tunapiga greda barabara zote za kuchepuka zilizo karibu na junction au barabara za mitaa ya jiji la Dar es salaam ili kuzuia foleni kila mwaka!Unakjua ni kiasi kingi sana cha pesa ambacho tutakuwa tunakitumia!!!?Tofauti na kujenga flyovers ambazo ni rahisi na siyo ghali kama unavyotuaminisha!

Kwa mfano barabara nyingi za wenzetu zimeinuliwa za upande mmoja km mita 8 au kumi kupisha upande mwingine wa barabara upite kwa chini!

Nafikiri wale mnaosafiri barabara hasa zile njia zenye reli hasa ya kati mna experience ya kuona huko barabarani wakati treni inapopita juu ya barabara bila kuwasimamisha wale wanaosafiri kwa magari pale mnaposafiri!

Huu ndio mfano wa daraja hizo!Ni cheap ,sustainable na zinadumu muda mrefu sana bila kufanyiwa maintanance tofauti na kuweka hayo magreda ya kusembua ambao uwepo wake tu wenyewe ndani ya kila baada ya miezi mitatu ni foleni tosha.
 
Ujenzi wa flyovers ni kiini macho.unahamisha tatizo kutoka junction A kwenda B.nafikiri tujikite zaidi kwenye ujenzi wa ring roads hii itasaidia. Kwa mfano ukijenga daraja Tazara utahamishia tatizo Buguruni na kwingineko au ukijenga Ubungo unaogeza volume Magomeni na kwingineko kwenye junction .tuache tabia ya kutaka kujionesga na tujikite kwenye utaalamu.

mzee kwani hizo gari hata bila flyover si zinaendaga huko huko...kwa hiyo flyover itakuwa imetatua tatizo ubungo ambalo ndio lengo..
 
Jamani, kujenga madaraja sio suluhisho. Tatizo la nchi yangu ni kwamba hatuna wataalam wa mipango ya aina yeyote. Wanawaza sasa hivi tu. Mbona mji flani niliona ma flyovers na hakuna foleni? Huo si utaalam wala sio mpango. Kujenga flyover Ubungo Mataa hakutaleta suluhisho kwani msururu utaanzia magomeni mpaka magari yatakuwa hapo juu yamekwama.

Tutengeneze michepuko tu na hizo hela ka zipo mzee Magufuli. Michepuko ikiwa mizuri na yenye lami ikiwezekana nnani atapoteza mda wake Ubungo Mataa?

Watu wanakuja na solutions rahisi rahisi tu. Watu hawataki kufikiri ni kutamka tu. Unaamuru watu waende Mabwepande. Unaenda kumtupa mtu msituni na kumwacha huko. Hujali watoto walio athirika na usumbufu huo, hujali wamama walio athirika na usumbufu huo. Ni majambazi tu unazalisha kwa ile chuki kuwa umemtoa mjini ukampeleka porini na kumtupa huko. Unaamua, boda boda zisifike mjini, unataka watu watembee toka wapi mpaka wapi. Ati, sababu ni kwamba boda boda zinatumiwa na wezi. Hivi hilo ndo tatizo kweli? Ama kweli, vichaa wanapopewa rungu, tujiandae.

Tafuta suluhisho la tatizo kwanza halafu ndo marufuku isimamie. Tanzania bila uongozi huu uliopo, yawezekana. Watu wamekata tamaa, hata kupiga kura hawataki. Anaona heri alale usingizi kuliko kwenda mchagua kichaa mwingine kwani ni wale wale tu kila siku. Ahadi kibao na flana na chepeo tu, sana sana na wali maharage sinia moja watu 10. Hiyo yaitwa Takrima. Nasema, Tanzania bila huu uongozi uliopo, YAWEZEKANA.

Nasema flyover sio suluhisho. Tengenezeni michepuko.
 
mzee kwani hizo gari hata bila flyover si zinaendaga huko huko...kwa hiyo flyover itakuwa imetatua tatizo ubungo ambalo ndio lengo..

Tatizo sio kutokuwa na flyover ila utaratibu mbovu,foleni dar vinasababishwa na vitu vya ajabu,unaweza kuta hata lori limekwama barabarani.
 
Mawazo yangu mimi kwa hili ni kuimalisha usafiri wa public.watu wapaki magari yao nyumbani sote tupande public transport kwenda na kurudi ma kazini..nadhn hii itasaidia..
 
Tatizo sio kutokuwa na flyover ila utaratibu mbovu,foleni dar vinasababishwa na vitu vya ajabu,unaweza kuta hata lori limekwama barabarani.
hiyo ni kwa kiwango kidogo sana...!
 
Back
Top Bottom