Matrafiki wa Ubungo Mataa ndio chanzo cha foleni

singojr

JF-Expert Member
Oct 28, 2014
5,308
6,884
Ni Tanzania tu utaona Traffic Police anaongoza magari kwenye round about. Ubungo mataa baada ya mchina kuweka round about watu wengi walishangazwa kuona namna tatizo la foleni pale lilivyopungua kabla hata ya flyover kukamilika.

Cha ajabu baada ya ahueni hiyo matrafiki wamekuja pale na sasa pana jam ya hatari. Siku wasipokuwepo hata kama kuna magari mengi kiasi gani yote yanaenda vizuri na salama. Ninachojiuliza ni lengo lao ni kuweka jam au kuondoa jam? Je wana maslahi binafsi na kuwepo kwa jam pale?

Naomba uongozi walifanyie kazi hili kweli inakera.
 
Back
Top Bottom