Laana kuu Ubungo mataa!

Nimetazama ule ujenzi sijaelewa kwanini wameweka ghorofa mbili na ground floor itatumika kwa shughuli ipi, kadhalika mwendokasi watapita wapi?
Mwendokas wanapita Juu huko Juu ni Magari yote yanayoenda Mwenge yakitokea Tabata moja Kwa moja na Juu Kabisa yatapita Kimara Posta au Posta Kimara huko huko kuna njia mbili Kama unvyoona ss

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya kukaa foleni masaa mawili pae ubungo mataa ninaomba kujua yafuatayo.
Ni hasara kiasi gani tumepata kama Taifa katika kipindi cha miaka kumi mpaka Leo kutokana na foleni hizi.
TRA imeingiza pesa nyingi kupitia foleni sababu ukiwa foleni mafuta yanaliwa Sana inabidi ujaze mengine na kila Lita Kuna Kodi kea hiyo ukijaza zaidi TRA wanapata pesa na wafanyabiashara wa vituo vyao mafuta pesa zinaongezeka.

Foleni zinasaidia TRA na wafanya biashara wa vituo vya mafuta

Foleni Zina faida kwa taifa

Makusanyo mengi TRA husaidia nchi.Njia moja ya kuongeza mapato ni foleni

Foleni hoyeeeee!!!
 
Mwendokas wanapita Juu huko Juu ni Magari yote yanayoenda Mwenge yakitokea Tabata moja Kwa moja na Juu Kabisa yatapita Kimara Posta au Posta Kimara huko huko kuna njia mbili Kama unvyoona ss

Sent using Jamii Forums mobile app
Top layer ni Tabata to Mwenge
Middle layer ni Kimara to City center
Nikategemea Uvunguni layer iwe ya mwendokasi ili wasiingiliwe
 
Tatizo wabongo wengi mbulula halafu wanajifanya wanajua kuchangia upuuzi, flyover ndo huwa suluhisho la foleni sio lazima ujenge zote kwa pamoja mfano bara bara kutoka manzini swaziland to mbabane kuna flyver za kumwaga ambazo wala hazioneshi kuwa gharama sana pia kutoka Johburg mpaka pretoria so mchezo ,najua watakuja kutetea ule uf.a.la wao ku SA imeendelea kiuchumi je swazi wana uchumi gani? Nairobi je Nigeria je,nadhani Tanzania ndo nchi ambayo haina flyover hata moja,swala kwamba barabara zipigwe grader ni hoja chakavu japo itasaidia kidogo coz kila m2 atataka kupita huko kwa tunaojua chocho za bongo liko wazi hili,halmashauri nyingi najua hazina foleni kabisa ukiacha majiji magreda yanatosha ila provision ya bara bara nyingi tena za flyover zinatakiwa sio barabara mbili kila cku kwenye majukwaa na tv juu mnajicfia wakati kila kukicha mko ulaya mnaona wanaume wenzenu walivyotumia akili zao na rasilimali.
Huko watasema wazungu walijenga sasa hapo nairobi na Ghana kila mji flyover alijenga beberu? Ni ushamba tu wa kutofikili na kushindwa kuchagua vipaombele
Miaka 5 imekwisha barabara alizoanzisha JK hazijamalizika bado mikoa hadi mikoa ni matope kwenda mbele
 
Jamani, kujenga madaraja sio suluhisho. Tatizo la nchi yangu ni kwamba hatuna wataalam wa mipango ya aina yeyote. Wanawaza sasa hivi tu. Mbona mji flani niliona ma flyovers na hakuna foleni? Huo si utaalam wala sio mpango. Kujenga flyover Ubungo Mataa hakutaleta suluhisho kwani msururu utaanzia magomeni mpaka magari yatakuwa hapo juu yamekwama.
Tutengeneze michepuko tu na hizo hela ka zipo mzee Magufuli. Michepuko ikiwa mizuri na yenye lami ikiwezekana nnani atapoteza mda wake Ubungo Mataa?
Watu wanakuja na solutions rahisi rahisi tu. Watu hawataki kufikiri ni kutamka tu. Unaamuru watu waende Mabwepande. Unaenda kumtupa mtu msituni na kumwacha huko. Hujali watoto walio athirika na usumbufu huo, hujali wamama walio athirika na usumbufu huo. Ni majambazi tu unazalisha kwa ile chuki kuwa umemtoa mjini ukampeleka porini na kumtupa huko. Unaamua, boda boda zisifike mjini, unataka watu watembee toka wapi mpaka wapi. Ati, sababu ni kwamba boda boda zinatumiwa na wezi. Hivi hilo ndo tatizo kweli? Ama kweli, vichaa wanapopewa rungu, tujiandae.
Tafuta suluhisho la tatizo kwanza halafu ndo marufuku isimamie. Tanzania bila uongozi huu uliopo, yawezekana. Watu wamekata tamaa, hata kupiga kura hawataki. Anaona heri alale usingizi kuliko kwenda mchagua kichaa mwingine kwani ni wale wale tu kila siku. Ahadi kibao na flana na chepeo tu, sana sana na wali maharage sinia moja watu 10. Hiyo yaitwa Takrima. Nasema, Tanzania bila huu uongozi uliopo, YAWEZEKANA.
Nasema flyover sio suluhisho. Tengenezeni michepuko.
Kila kwenye critical junction lazima ijengwe hoja sio kujenga interchange moja bali kadhaa na kuimalisha barabara za pembeni,sio tu Dar na miji yote Tzn yenye hali kama hiyo,mbona nchi za waafrika wenzetu zinaweza shida ni ipi hapa bongo?
 
Kutafutwe njia nyingine ya kuingia mjini. Wachepukie Chalinze na kuteremkia Pugu na wengine wapitie Bagamoyo
 
Wakuu nimetazama pale sijaelewa watumiaji hawa watafanyaje:

Anayetoka Kimara kwenda Buguruni
Anayetoka Mwenge kwenda Kimara
Anayetoka Manzese kwenda Mwenge
Anayetoka Tabata kwenda Manzese watapitaje kwenye hilo daraja
 
Hii thread ingefunguliwa kuanzia mwaka 2016 kwenda mbele hizo comment zake

ungehisi wachangiaji ni kina mama wajawazito wenye uchungu wanakaribia kujifungua.
 
Wakuu nimetazama pale sijaelewa watumiaji hawa watafanyaje:

Anayetoka Kimara kwenda Buguruni
Anayetoka Mwenge kwenda Kimara
Anayetoka Manzese kwenda Mwenge
Anayetoka Tabata kwenda Manzese watapitaje kwenye hilo daraja
Watapita ground floor, pale kutakuwa na muingiliano wa magari yanayopinda kushoto/kulia, sijui itakuwa roundabout au vipi. First floor ni Kimara-Posta(including mwendokasi), second floor ni mwenge-buguruni.
Check link hiyo lazima uelewe kinachoendelea:
 
Nashukuru sana Mkuu nimeona wanavyotofautiana katika kupita

Barikiwa sana
 
Baada ya kukaa foleni masaa mawili pae ubungo mataa ninaomba kujua yafuatayo.

1.) Ni hasara kiasi gani tumepata kama Taifa katika kipindi cha miaka kumi mpaka Leo kutokana na foleni hizi.

2.) Inagharimu kiasi gani kujenga daraja la magari kupita juu pale junction.

3.) Tukijua hizi data basi tutaweza kukadiria ni kwa kiasi gani serikali Yetu imelala.
Serikali ikiboresha miundombinu mnabeza, mnasema mnataka maendeleo ya watu siyo vitu. Leo unakuja kulialia hapa ili iweje ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali hii ni gesi ya Azam Cola hata siku 3gesi ipo tu,,,,,,
Tunasubiria uchaguzi ukaribie ndio waseme na Machinjio ya vingunguti japo alipita katikati ya mabati kwenda kukagua na huko Coco beach sijui kunaendeleaje
Nanukuu—-“Isingekuwa Niaa ningestaafu”

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jiandae kuikabili the same laana pale mbezi mwisho

Back
Top Bottom