Pre GE2025 Ushauri kwa Mkurugenzi Mkuu wa TISS Kuhusu Kero Sugu ya Uhalifu wa Kiuchaguzi Unaofanywa na Wanasiasa Matapeli Wakati wa Chaguzi tangu 2010 hadi 2024

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Doctor Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
2,159
2,925
1740297331454.png

I. USULI

Usanifu wa hoja makini hufanyika kwa ajili ya kufanikisha angalau lengo mojawapo kati ya malengo manne yafuatayo: kutafuta jawabu la swali linaloleta mahangaiko kwenye akili za watu (inquiry), kufanya ushawishi ili watu baki wakubali hitimisho lako la kiutafiti (convincing), kufanya ushawishi ili watu baki wakubali hitimisho lako na kuchukua hatua za kivitendo (persuading), na kusuluhisha tofauti za kimtazamo juu ya suala fulani kati ya pande mbili hasimu (mediating). (Crusius and Channell 2015:13-15).

Nimeamua kuandika dokezo la kisera, lenye kubeba taarifa za intelijensia ya kisiasa na kijasiriadola, nikiwalenga wasomaji makini, walioko ndani na nje ya Idara ya Usalama wa Taifa, kwa ajili ya kutimiza malengo yote manne kuhusiana na pendekezo lifuatalo:

Kwamba, kwa kuwa uhalifu wa kiuchaguzi unaofanywa na wanasiasa matapeli wakati wa chaguzi zetu umekithiri kwa miaka 15 sasa kutokana na mapungufu yaliyomo kwenye mifumo yetu ya kikatiba na kisheria, basi, tunapaswa kurekebisha ratiba ya uchaguzi mkuu wa 2025, kisha tufanye mageuzi ya kikatiba na kisheria, na hatimaye tufanye uchaguzi mkuu baadaye, na sio kinyume chake.

Kwa ajili ya kufanikisha lengo hili dokezo hili nimeligawanya kwenye sehemu zifuatazo: (1) Usuli, (2) Utangulizi, (3) Methodolojia, (4) Matokeo ya utafiti, (5) Majumuisho na majadiliano, (6) Mapendekezo, (7) Mapingamizi na majibu yake, (8) Hitimisho, na (9) Rejea muhimu zilizotumika.

II. UTANGULIZI : HIVI KUNA TATIZO GANI?

Katika miaka ya 1990, mhariri Mkuu wa jarida lililoitwa "A Letter to My Superiors," Padre Bernard Joinet, aliyekuwa mhadhiri wa somo la saikolojia kwenye Chuo Kikuu cha Muhimbili, Dar es Salaam, aliandika makala kuhusu kanuni za demokrasia.

Katika makala hiyo alitufundisha kwamba, kimuundo, demokrasia ya vyama vingi vya siasa ni kama mwavuli wenye spoku kadhaa, nguzo ya kati inayoshikilia spoku hizo, na kitambaa cha kuzuia miale ya jua na matone ya mvua, kinachokunjuliwa na kukunjwa kwa msaada wa spoku.

Alieleza kwamba, kwa njia ya mantiki ya ufananisho, nguzo ya mwavuli ni Katiba ya nchi; kwamba kila spoku kwenye mwavuli wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa inawakilisha chama cha siasa; kwamba kifyatulio/kifungio cha mwavuli kinawakilisha sheria, kanuni na taratibu za vyama vingi nchini; kwamba miale ya jua na matone ya mvua yanawakilisha dhuluma, uonevu, ukatili na ubadhirifu wa mali ya umma; na kwamba kila spoku inawakilisha chama cha siasa; na kwamba spoku hizi hushirikiana na kitambaa hufanya kazi ya kutoa ulinzi wa umma dhidi ya dhuluma, uonevu, ukatili na ubadhirifu wa mali ya umma.

Yaani, kwa pamoja, Katiba ya nchi, vyama vya siasa, sheria na kanuni za uchaguzi ni mfumo unaopaswa kufanya kazi ya hufanikisha "checks and balances" katika Taifa kwa kutoa ulinzi wa umma dhidi ya maadui wa ndani na nje ya nchi.

Lakini, Chadema wanasema kwamba, tangu miaka ya 2010, tumekuwa na mfumo wa vyama vingi vya siasa ambao hauna uwezo wa kutulinda dhidi ya maadui wa ndani na maadui wa nje ya nchi yetu, kiasi kwamba, kwa sasa uhuru, umoja, usalama na maendeleo yetu vimewekwa rehani. Wanahimiza mageuzi ya kimfumo.

Chadema wanajenga hoja kwamba tunapaswa kubadilisha "mfumo wa kanuni za mchezo wa maisha ya kisiasa, kiuchumi na kijamii" kwanza kabla ya kuingia uwanjani kwa ajili ya kuanza kucheza mchezo wenyewe.

Hivyo, napendekeza kuanza dokezo hili kwa nukuu muhimu kuhusiana na mtazamo wa Chadema kuhusu sababu zao za kusogeza mbele ratiba ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika 2025.

"Mtu yeyote mwenye akili na macho ya kuona anajua kuwa chaguzi za nchi hii zimekuwa za hovyo sana na kwamba ni za hovyo kwa sababu mfumo mzima wa kiutawala wa nchi hii ni mfumo wa hovyo" -- Tundu Lissu, Mwenyekiti CHADEMA.

“Hatuzungumzii kususuia uchaguzi, hatutasusia bali tutaenda kuwaambia Watanzania, jumuiya ya kimataifa na walimwengu kwamba kama CCM na Serikali hawako tayari kufanya mabadiliko kwenye mfumo wa uchaguzi ili kuwepo chaguzi huru na haki, uchaguzi wa mwaka huu usifanyike kabisa” -- Tundu Lissu, Mwenyekiti CHADEMA.

“Sisi ni watu tunatumia brain (akili) tume-engage (kushirikisha) tumeandika mapungufu 16 ya uchaguzi ambayo hayamuwezeshi mpinzani yoyote kushinda uchaguzi, nani miongoni mwenu anaweza kusema kwamba anaweza kushinda uchaguzi kwa utaratibu huu tulionao?” -- John Heche, Makamu Mwenyekiti CHADEMA.

“Tumewaona viongozi wa dini tumezungumza nao na tumewapelekea ripoti ya mapungufu na nini tunachotaka ili twende kwenye uchaguzi, tumeonana na NGO na tutaonana na mashirika ya kimataifa ndani nan je ya nchi na Mwenyekiti wetu hivi karibuni atakuwa nje ya nchi ku engage” -- John Heche, Makamu Mwenyekiti CHADEMA.

Huu ndio msimamo ulioibuliwa na Chadema kuhusu kile ambacho baadhi ya vyombo vya Habari, kama vile gazeti la Mwananchi la leo, vinakiita “Njiapanda ya Chadema Kuhusu Ratiba ya Uchaguzi Mkuu wa 2025.”

Lakini, napendekeza kwamba, kutokana na uzito wa hoja yenyewe, hasa tunapaswa kuwa tunaongelea “Njiapanda ya Watanzania Kuhusu Ratiba ya Uchaguzi Mkuu wa 2025.” Hii ni changamoto inayowaweka njiapanda Watanzania wote kwa sababu iliyo wazi.

Ukweli ni kwamba, "mfumo wa kanuni za mchezo wa maisha ya kisiasa, kiuchumi na kijamii" hauwahusu Chadema pekee, maana uwanja wa siasa za vyama vingi unao wachezaji wengi zaidi.

Nataka tuelewane kuhusu ninachokiita "mfumo wa kanuni za mchezo wa maisha ya kisiasa, kiuchumi na kijamii" ili tuweze tukatofautisha mbinu na malengo na hivyo kuwasaidia kina Aliy Happi wa CCM kuelewa ajenda iliyo mezani. Bado hawajaelewa kinachoongelewa.

Maneno "mfumo wa kanuni za mchezo wa maisha ya kisiasa, kiuchumi na kijamii" yanamaanisha dhana ile ambayo Rawls(2001) aliitaja kama "the basic structure of society."

Kwa mujibu wa Hart (1961), mfumo huu unajumuisha kanuni za daraja la kwanza na kanuni za daraja la pili, yaani "primary and secondary rules of society".

Kanuni za daraja la kwanza ("primary rules") ni kanuni zinazoongoza matendo ya watu kila siku zikiwa zinataja majkumu yao, kama vile "usiibe" au "usiendeshe gari wakati taa nyekundu za barabarani zinawaka." Kanuni hizi zinataja adhabu kwa anayezikiuka.

Na Kanuni za daraja la pili ("secondary rules") zinaratibu zoezi la kutunga na kubadilisha kanuni za daraja la kwanza, zikiwa zinajumuisha utaratibu wa kutunga na kubadilisha katiba na sheria zinazotokana na katiba hiyo.

Na kwa mujibu wa Rawls(2001:10), "mfumo wa kanuni za mchezo wa maisha ya kisiasa, kiuchumi na kijamii" unazo sifa zifuatazo:

  • Unaeleza namna ambavyo taasisi kuu za kisiasa, kiuchumi na kijamii katika Taifa zinapaswa kufanya kazi pamoja kwa kukamilishana na hivyo kuunda mfumo mkubwa mmoja unaoliwezesha Taifa kuongea lugha moja kisiasa, kiuchumi na kijamii;
  • Unaeleza mgawanyo wa haki, majukumu na adhabu zinazopaswa kuambatana na ukiukwaji wa majukumu husika; na
  • Unaratibu mgawanyo halali wa manufaa na maumivu, faida na hasara, zinazojitokeza kutokana na ulazima wa kila mtu kujitoa na kushiriki katika kutekeleza mradi mpana wa kufukuzia maslahi ya pamoja katika Taifa siku hadi siku.
Hii maana yake ni kwamba, "mfumo wa kanuni za mchezo wa maisha ya kisiasa, kiuchumi na kijamii" unajumuisha Katiba ya nchi, sheria za Bunge, na Kanuni za serikali, yote haya yakiwa yanaundwa kutokana na mwafaka wa kitaifa.

Hivyo, “njiapanda” inayoongelewa kwenye vyombo vya habari, ndani na nje ya Chadema pia, inaweza na inapaswa kueleweka kwa njia ya swali lifuatalo:

Je, kwa kuzingatia uhalifu wa kiuchaguzi ambao umekuwa ukifanyika nchini Tanzania tangu 2010 kutokana na uwepo wa milima, mabonde na makorongo yaliyopo kwenye uwanja wa uchaguzi wa vyama vingi nchini Tanzania, tufumbe macho na kuendelea na utekelezaji wa ratiba ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025 au tusogeze ratiba hii mbele kidogo ili uchaguzi huu ufanyike baada ya mageuzi ya kikatiba na kisheria kufanyika ili kuboresha kanuni mama za mchezo wa maisha ya kisiasa, kiuchumi na kijamii?

Kutokana na utafiti nilioufanya, dokezo hili linapendekeza kwamba, tunapaswa kusogeza ratiba ya uchaguzi mkuu mbele kidogo ili uchaguzi huu ufanyike baada ya mageuzi ya kikatiba na kisheria kufanyika ili kusawazisha milima, mabonde na makorongo yaliyopo kwenye uwanja wa kisiasa.

1740051879008.png

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akiwa anamwapisha Suleiman Abubakar Mombo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Ikulu ya Magogoni, Dar es Salaam , Tarehe 11 Julai 2024.

III. UTARATIBU WA UTAFITI: METHODOLOJIA

Katika utafiti wangu nilikusudia kujibu maswali yafuatayo:

  1. Chadema wanasemaje kuhusu changamoto ya uhalifu wa kiuchaguzi unaotokana na milima, mabonde, makorongo na miiba kwenye uwanja wa siasa za Tanzania?
  2. Je, ni kweli kwamba kuna milima, mabonde, makorongo na miiba kwenye uwanja wa siasa za Tanzania?
  3. Kama jawabu kwa swali la kwanza ni “ndiyo,” milima, mabonde, makorongo na miiba hiyo imekuwa na madhara gani katika matokeo ya uchaguzi?
  4. Kutokana na majibu ya maswali haya mawili hapo juu, nah atua gani zichukuliwe tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa 2025.
Vyanzo vyangu vya taarifa ni kuona matukio kwa macho, kujadiliana na wadau baki walioona matukio kwa macho, na kusoma nyaraka kama vile sheria za Bunge, Katiba ya nchi, kusikiliza video, na makala nyingine kwa ajili ya kupanua maarifa yangu juu ya suala hili.

IV. MATOKEO YA UTAFITI

Wasemavyo Chadema Kuhusu "Mabadiliko Kwanza, Uchaguzi Baadaye"

Kulingana na taarifa zilizoko kwenye hotuba za Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chadema, mawazo yafuatayo yanawakilisha msimamo rasmi wa Chadema kuhusu sababu za kaulimbiu ya “Mabadiliko Kwanza, Uchaguzi Baadaye.”

1. Takwimu za uchaguzi wa serikali za mitaa kati ya mwaka 2014 na 2019 zinathibitisha kwamba kwa mujibu wa utaratibu wa sasa wa kisheria, kikanuni, kikatiba na wa kiserikali, uchaguzi salama usioambatana na mauaji, ulio huru, wenye uwazi na unaofanyika kwa haki hauwezekani tena kufanyika ktk nchi hii. Takwimu ziko hivi:

(a) Katika uchaguzi wa mitaa na vijiji wa 2014: Jumla ya vijiji vilikuwa 11,748; CCM ilishinda vijiji 9,378 (80%); na CHADEMA vijiji 1,754 (15%). Jumla ya mitaa yote ilikuwa 3,875; CCM ilishinda mitaa 2,583 (67%); na CHADEMA ilishinda mitaa 980 (25.29%).

(b) Katika uchaguzi wa vijiji na mitaa 2019: Jumla ya vijiji ilikuwa 12,262; CCM ikashinda 12,260 (99.99%); na CHADEMA haikutajwa kabisa. Jumla ya mitaa nchini 4,263; CCM ikashinda mitaa 4,263 (100%); na CHADEMA haikutajwa kabisa.

(c) Katika uchaguzi wa vijiji na mitaa mwaka 2024: Jumla ya vijiji ni 12,271; CCM ikashinda vijiji 12,150 (99%); na CHADEMA ikashinda vijiji 97 (0.79%). Jumla ya mitaa ni 4,264; CCM ikashinda mitaa 4,213 (99%); na CHADEMA ikashinda mitaa 36 (0.84%).

2. Takwimu hizi maana yake ni kuwa, mfumo wetu wa uchaguzi wa sasa unayo matatizo mengi, kiasi kwamba, bila kufanyika kwa mabadiliko ya kisheria, kikanuni na kikatiba, kwanza, basi chaguzi za kiinimacho zenye kuwaumiza wapinzani na kuipendelea CCM zitaendelea milele kwa sababu zilizo wazi.

(a) Mosi, chaguzi za mwaka 2019, 2020 na 2024 zimeweka rekodi za kuenguliwa kwa wagombea wengi wa vyama vya upinzani kwa vigezo visivyo vya kikatiba, mfano kukosea jina, na kukosea kuandika jina la chama. Lakini wagombea wote wa CCM wanabakizwa kwa madai kuwa wao hawana dosari yoyote.

(b) Mfumo wa sasa wa uchaguzi ni mfumo wenye sura ya siasa za chama kimoja. Ulitengenezwa na CCM, kwa ajili ya CCM, unaifaidisha CCM na kwa sababu hiyo si mfumo wa kidemokrasia na unawaumiza wananchi na nchi yote.

(c) Ni mfumo wa CCM kwa kuwa, uchaguzi mkuu unasimamiwa na Tume ya Uchaguzi ambayo ni ya CCM ambayo huteuliwa na kupewa maelekezo na Mwenyekiti wa CCM ambaye mara zote huwa ndiye Rais wa nchi.

(d) Aidha, Mwenyekiti wa CCM ambaye naye mara zote huwa ni mshiriki na mshindani ktk uchaguzi ndiye anayeteua Mwenyekiti wa Tume, wajumbe wote wa Tume na mkurugenzi wa uchaguzi wa Tume. Ndiye mwajiri na mteuzi wa wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo (wakurugenzi wa halmashauri za miji, wilaya, manispaa na majiji), watendaji wa kata na wa vijiji. Katika mazingira haya, hawa kamwe hawawezi kutenda haki Bpbali watampendelea aliyewateua.

(e) Mfumo wa ugawaji majimbo ya uchaguzi sio wa haki kwa kuwa hauzingatii idadi ya watu ambao ni wakazi. Maeneo ambayo CCM ina uhakika wa kushinda imeyagawa katika vijimbo vingivingi Ili mradi iingize wabunge wengi bungeni. Mfano Dar Es Salaam yenye wapiga kura wengi 3,427,000, ambazo ni takwimu za Tume ya Uchaguzi za mwaka 2020, iko sawa na wapiga kura wa mikoa ya Rukwa, Pwani, Songwe, Iringa, Katavi na Njombe kwa pamoja. Lakini DSM ina majimbo 10 tu, sawa na na wastani wa wapiga kura 327,000 kila jimbo la Dar. Lakini, katika mikoa hiyo sita (6) kwa ujumla ikiwa na majimbo 37, kuna wastani wa wapiga kura 91,000 katika kila Jimbo. Wapiga kura 91,000 katika kila Jimbo kwenye mikoa hiyo ni mara 3.5 ya wapiga kura 327,000 katika jimbo la Dar. Hakuna usawa hapo.

(f) Kwa upande wa Zanzibar, majimbo ya uchaguzi yana wastani wa wapiga kura 10,000. Hii maana yake ni kwamba mbunge kutoka Zanzibar anaweza kuchaguliwa na watu wasiozidi 2,500 akaja Dodoma na akawa na haki sawa na mbunge anayehudumia wapiga kura 327,000 mkoani Dar Es Salaam. Hakuna usawa hapo.

3. Kwa hiyo, hitimisho la ikimantiki ni kwamba, Watanzania tunapaswa kuzuia chaguzi za kiinimacho zisifanyike kwa kujenga hoja kwa wananchi, wanachama wetu, taasisi za kiraia na za kidini, viongozi wa dini, nchi wahisani wa Tanzania, taasisi za haki za kibinadamu za kitaifa na kimataifa hadi waelewe na kutuunga mkono. Hii ndio maana ya msemo kwamba “Mabadiliko Kwanza, Uchaguzi baadaye,” yaani “No Reforms, No Election.

4. Kutokana na hitimisho hapo juu, mapendekezo ya msingi kuhusu mabadiliko yanayotakiwa kufanyika kwa sasa yanapatikana kwenye Ripoti za Tume mbalimbali. Kuna Tume ya Jaji Francis Nyalali (1991) iliyoundwa na Rais Hayati Ally Hassan Mwinyi; Tume ya Jaji Robert Kissanga (1998) iliyoundwa na Rais Hayati Benjamin Mkapa; Tume ya Jaji Mark Bomani (2003) iliyoundwa na Rais Hayati Benjamin Mkapa; na Tume ya mabadiliko ya Katiba ya Jaji Joseph Sinde Warioba (2014/2015) iliyoundwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Tume hizi zote zilipendekeza mabadiliko yafuatayo:

(a) Lazima tuwe na Tume Huru ya uchaguzi yenye Mwenyekiti na wajumbe wake wanaoteuliwa na mtu baki badala ya Rais; yenye bajeti inayojitegemea kutoka Bungeni kwa ajili ya kuendesha shughuli zake; yenye wafanyakazi wake wa kudumu na wa mikataba ya muda mfupi/maalumu inayowajiri yenyewe wakiwajibika kwa Tume pekee; na yenye wasimamizi wa vituo vya kupigia kura hadi kwa Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na wakurugenzi wa Tume wasiowajibika kwa Rais.

(b) Ugawaji wa majimbo lazima ufanyike upya kwa kuzingatia kigezo cha idadi ya watu kama ilivyokuwa katika sheria za uchaguzi na katiba kuanzia mwaka 1961 hadi 1991. Kigezo cha miumdombinu na jiografia ya eneo hakifai.

(c) Daftari la wapiga kura litengenezwe upya kwa kuandikisha wapiga kura wote upya kwa kuondoa wapiga kura hewa wote. Aidha, daftari la wapiga kura lisiwe Siri Bali lazima liwe wazi (accessible) kwa yeyote anayetaka kuliangalia Ili mradi kuweka utaratibu rahisi na wa wazi kufanya hivyo.

(d) Utaratibu wa kuengua wagombea wote iwe wa CCM, CHADEMA au chama chochote kwa sababu ambazo si za kikatiba ukomeshwe na kupigwa marufuku na sheria tutakazotunga.

(e) Utaratibu wa vyombo vya dola kuwafanyia vurugu wagombea wa vyama pinzani na CCM upigwe marufuku na sheria na sheria iweke utaratibu wa kuwashitaki, kuwalipisha fidia na kufukuzwa kazi mwenye mamlaka yeyote atakayetumia mamlaka yake vibaya kwenye eneo hili.

(f) Barua rasmi tu ya chama cha siasa ambako wakala anatoka ili kusimamia kura za mgombea wake inatosha kumfanya wakala atambuliwe na msimamizi wa kituo cha uchaguzi. Hivyo, utaratibu wa Sasa wa mawakala wa wagombea wa vyama vya siasa kuapishwa kiapo cha kutunza siri ni batili na hauna sababu na unaleta urasimu usio na maana yoyote kwa sababu kwenye kituo cha kupigia kura hakuna Siri ya kutunzwa hapo kwa sababu kila kitu kinatakiwa kufanyika kwa uwazi huku kila mtu akiona.

(g) Utangazaji wa matokeo ya uchaguzi kwa nafasi zote kuanzia kwenye kituo cha kupigia kura ufanyike tu pale ambapo mawakala wa wagombea wote wameridhika na kusaini fomu za matokeo. Kwenye kituo cha majumuisho matokeo yatangazwe pale tu ambapo wagombea wote wameridhika na kusaini fomu ya matokeo. Kama mgombea au wakala wa mgombea hajaridhika kwa sababu yoyote sheria iseme ni marufuku kwa msimamizi wa kituo kutangaza matokeo hayo. Na ikitokea hivyo, basi mgogoro wa namna hiyo uende mahakamani kuamuliwa.

Milima, mabonde, makorongo na miiba kwenye uwanja wa kisiasa

Tuhuma kwamba chaguzi zote za 2010, 2015, 2019, 2020 na 2024 unaonyesha kuwa tunayo mifumo ya kikatiba na kisheria inayowapatia wanasiasa matapeli fursa ya kufanya uhalifu wa kiuchaguzi kwenye chaguzi zetu, kiasi kwamba, kwa kipindi cha miaka 15, tumekuwa tukiongozwa na serikali haramu zilizotokana na mbinu haramu, nazi zinao ushahidi wa kuziunga mkono kama ifuatavyo:

(a) Uchaguzi unaosimamiwa na ma-WEO, ma-DED, ma-DC, ma-DAS, na ma-RAS unakosa uhuru, uwazi na ushindani wa kweli, kwa sababu wao ni watumishi wa serikali ya chama tawala, na hivyo kufanya uhalifu wa kiuchaguzi kwa faida ya chama tawala.

(b) Sheria za uchaguzi zinawaruhusu Watumishi wa umma kuvaa kofia za Watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakati w auchaguzi na hivyo kufungua milango ya uhalifu wa kiuchaguzi.

(c) Tume ya Taifa ya Uchaguzi imo kwapani mwa Rais wa nchi, ambaye ndiye huteua wajumbe wake, na hivyo kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria pekee kwa sababu ya kuyumbishwa na maagizo kutoka Ikulu.

(d) Tume ya Taifa ya Uchaguzi haina uwezo wa kisheria wala kifedha wa kusimika watumishi wake kwenye kila jimbo la uchaguzi kwa mujibu wa sheria.

(e) Katiba inamruhusu Rais wa nchi aliye madarakani na ambaye ni mgombea kuendelea kutekeleza majukumu yake ya Urais wakati wa kampeni za uchaguzi ilihali yeye ni Amiri Jeshi Mkuu, Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, na Msimamizi Mkuu wa Jeshi la Polisi.

Jambo hili linafungua mianya kwa baadhi ya vyombo vya ulinzi na usalama, kama vile Jeshi la Polisi na TISS, kufanya uhalifu wa kiuchaguzi ili kumsaidia “bosi” wao kushinda.

(f) Katiba inaruhusu Rais wa nchi kushika nafasi ya mwenyekiti wa chama cha siasa, kabla na wakati wa uchaguzi, na hivyo, kufungua mlango wa Rais huyu kuvitumia vyombo vya ulinzi na usalama kwa faida ya chama tawala.

(g) Katiba na sheria zetu vinazuia matokeo ya uchaguzi wa Rais yanayobishaniwa kupingwa mahakamani kisheria. Hivyo, uhalifu wa kiuchaguzi kuhusiana na kura za urais hauwezi kukosolewa kimahakama.

(h) Sheria na Katiba havijapiga marufuku tabia ya uhalifu wa kiuchaguzi wa kugeuza mchakato wa uchaguzi kuwa mashindano ya kujaza fomu za wagombea, jambo ambalo linazalisha wagombea wa kupigiwa “kura za ndio au Hapana,” na hivyo kukiuka kanuni ya uchaguzi wenye ushindani.

(i) Sheria ya TAKUKURU chini ya kifungu cha 31 inairuhusu TAKUKURU kuwakamata watu wote wanaotumia madaraka yao vibaya kabla, wakati na baada ya uchaguzi. Lakini hili halijawahi kutokea kuhusiana na uhalifu wa kiuchaguzi. Tatizo ni kwamba sheria hiyo inamfanya Mkuu wa TAKUKURU kuripoti kwa Mkuu wa nchi, kabla, wakati na baada ya uchaguzi, bila kujali kwamba kuna wakati Mkuu wa nchi ni mgombea anayeweza kuwazuia watumishi wa TAKUKURU kufanya kazi yao katika namna ambayo itamkwamisha bosi wao mkuu, yaani "Rais ambaye pia ni mgombea."

(j) Sheria ya Jeshi la Polisi inawapa mamlaka polisi kukamata wahalifu wa kiuchaguzi chini ya kifungu cha 21. Lakini hawajawahi kudanya hivyo dhidi ya mkubwa yeyote. Sababu ni kwamba polisi wanawajibika kwa Rais na mgombea Urais wa chama tawala. Hivyo hawawezi kutekeleza jukumu hilo.

1740052621381.png

Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, Mwasisi na Mfadhili wa "vikosi kazi" vya kutekeleza uhalifu wa kiuchaguzi wa "kukomboa" majimbo ya uchaguzi kinyemela

Madhara ya milima, mabonde, makorongo na miiba ya kisiasa

Makorongo haya kwenye uwanja wa siasa za vyama vingi yamekuwa na madhara ya kisiasa tangu zamani, hata kabla ya hayati Magufuli hajakanyaga Ikulu. Mfano:

(a) Mwaka 2010 na 2015 enzi za Kikwete

Katika zama hizi kulikwa na “vikosi kazi” vya kukomboa majimbo yaliyo hatarini.

Kwa kila jimbo ambalo tayari lilithibitika kuanguka mikononi mwa wapinzani, vikosi hivi vilikuwa vinashirikiana na baadhi ya ma-WEO, ma-DC, ma-DAS, ma-DED, ma-DSO, ma-OCD, ma-RSO, ma-RAS na ma-RC kufanya “ukombozi.”

Mfano mmoja ni ule wa Jimbo la Karagwe mwaka 2010. Mgombea wa CCM, Gosbert Blandes Begumisa, alipoteza jimbo hilo kwa tofauti ya kura zipatazo 500. Mgombea wa Chadema alishinda.

Kikosi kazi kikafika Karagwe haraka. Kiongozi wa kikosi kazi kile alikuwa ni Afisa Usalama aliyeitwa “Haule.” Wakachakachua takwimu Blandes akatangazwa mshindi.

Niliambiwa kuwa, Kila kikosi kilikuwa kinapewa magari, fedha taslimu na wakati mwingine helikopta. Na kwa kila jimbo lililokuwa linakombolewa “malipo ya kazi maalumn” yalikuwa fedha ipatayo TZS 100,000,000 (soma milioni mia moja).

Hivyo, wajumbe wa “vikosi kazi” hivi enzi za Kikwete walifanikiwa kujenga majumba, kununua magari, na kuanzisha biashara kubwa. Kwao, wakati wa msimu wa uchaguzi wajibu wao ulikuwa ni kuiba majimbo na ulikuwa ni msimu wa “mavuno” makubwa.

1740052317790.png

Gosbert Blandes Begumisa, Mbunge wa zamani wa Karagwe

(b) Mwaka 2019 na 2020 enzi za Magufuli

Wakati wa JPM idadi ya “vikosi kazi” iliongezeka, kiasi kwamba uhalifu wa kiuchaguzi ikawa sera rasmi ya kila jimbo la uchaguzi. Ma-WEO, ma-DC, ma-DAS, ma-DED, ma-DSO, ma-OCD, ma-RSO, ma-RAS na ma-RC wote walipewa maagizo rasmi ya kusimamia ushindi wa wagombea wa CCM.

Uliotegemewa kuwa uchaguzi haali uligubikwa na uhalifu wa kiuchaguzi wenye sura zifuatazo:

  • Kutoandikisha wapiga kura kwenye ngome za wapinzani,
  • Kuwaengua wagombea wao wengi,
  • Kutowaruhusu mawakala wa vyama vya upinzani
  • Kuingiza kwenye sanduku la kura kura feki zilizipigwa na ma-WEO wiki kadhaa kabla ya siku ya uchaguzi (premarked ballots), na
  • Kutowatangaza wapinzani hata pale walipoonekana kushinda.
Hatimaye wapinzani hawakuambulia kitu.

images (36).jpeg

Kura feki Jimbo la Kawe mwaka 2020 kwa ajili ya kumpitisha Askofu Gwajima kuwa Mbunge kinyemela

(c) Mwaka 2024 enzi za Samia Suluhu Hasan

Wakati wa Rais Samia utaratbu wa hayati Magufuli ulifufuliwa na kutekelezwa kikamilifu.

Ma-WEO, ma-DC, ma-DAS, ma-DED, ma-OCD, ma-RAS na ma-RC wote walipewa maagizo rasmi ya kusimamia ushindi wa wagombea wa CCM.

Kutokana na maagizo haya Wapinzani hawakuambulia kitu pia.

Kwa mara nyingine tena, uliotegemewa kuwa uchaguzi haali uligubikwa na uhalifu wa kiuchaguzi wenye sura zifuatazo:

  • Kutoandikisha wapiga kura kwenye ngome za wapinzani,
  • Kuwaengua wagombea wao wengi,
  • Kutowaruhusu mawakala wa vyama vya upinzani
  • Kuingiza kwenye sanduku la kura kura feki zilizipigwa na ma-WEO wiki kadhaa kabla ya siku ya uchaguzi (premarked ballots), na
  • Kutowatangaza wapinzani hata pale walipoonekana kushinda.
Kwa mara nyingine tena wapinzani hawakuambulia kitu.

(d) Uchakachuaji wa uchaguzi wa serikali za mitaa, 2014 mpaka 2019

Kwa ujumla, takwimu za uchaguzi wa serikali za mitaa kati ya mwaka 2014 na 2019 zinathibitisha kwamba kwa mujibu wa utaratibu wa sasa wa kisheria, kikanuni, kikatiba na wa kiserikali, uchaguzi salama usioambatana na mauaji, ulio huru, wenye uwazi na unaofanyika kwa haki hauwezekani tena kufanyika ktk nchi hii. Takwimu ziko hivi:

(i) Katika uchaguzi wa mitaa na vijiji wa 2014: Jumla ya vijiji vilikuwa 11,748; CCM ilishinda vijiji 9,378 (80%); na CHADEMA vijiji 1,754 (15%). Jumla ya mitaa yote ilikuwa 3,875; CCM ilishinda mitaa 2,583 (67%); na CHADEMA ilishinda mitaa 980 (25.29%).

(ii) Katika uchaguzi wa vijiji na mitaa 2019: Jumla ya vijiji ilikuwa 12,262; CCM ikashinda 12,260 (99.99%); na CHADEMA haikutajwa kabisa. Jumla ya mitaa nchini 4,263; CCM ikashinda mitaa 4,263 (100%); na CHADEMA haikutajwa kabisa.

(iii) Katika uchaguzi wa vijiji na mitaa mwaka 2024: Jumla ya vijiji ni 12,271; CCM ikashinda vijiji 12,150 (99%); na CHADEMA ikashinda vijiji 97 (0.79%). Jumla ya mitaa ni 4,264; CCM ikashinda mitaa 4,213 (99%); na CHADEMA ikashinda mitaa 36 (0.84%).

1740119579893.png

Albert Chalamia, RC wa Dar es Salaam, rafiki yake Joseph Selasini wa NCCR Mageuzi

V. MAJUMUISHO NA MAJADILIANO

Nimeandika hili dokezo la kisera, nikiwalenga wasomaji makini, walioko ndani na nje ya Idara ya Usalama wa Taifa, kwa ajili ya kutafuta hitimisho la ukweli juu ya jambo fulani (inquire), kufanya ushawishi ili watu hao wakubali hitimisho langu (convince), kufanya ushawishi ili watu hawa wakubali hitimisho lako na kuchukua hatua za kivitendo (persuade), na kusuluhisha tofauti za kimtazamo juu ya suala mahsusi kati ya pande mbili hasimu za CCM na Chadema (mediate), ambapo pendekezo lifuatalo linahisika:

Kwamba, kwa kuwa uhalifu wa kiuchaguzi unaofanywa na wanasiasa matapeli wakati wa chaguzi zetu umekithiri kwa miakasasahadi sasa kutokana na mapungufu yaliyomo kwenye mifumo yetu ya kikatiba na kisheria, basi, tunapaswa kurekebisha ratiba ya uchaguzi mkuu wa 2025, kisha tufanye mageuzi ya kikatiba na kisheria, na hatimaye tufanye uchaguzi mkuu baadaye, na sio kinyume chake.

1740233824953.png

Crusius and Channell (2015:15)

Kutokana na matokeo ya utafiti yaliyorekodiwa hapo juu, sasa ni wakati wa kufanya majumuisho yafuatayo na majadiliano husika:

Urasimishaji wa hoja ya Chadema kimuundo na kimaudhui

Maneno ya Tundu Lissu kuhusu msimamo wa kisera wa chama chake juu ya umuhimu na ulazima wa kusogeza mbele ratiba ya Uchaguzi Mkuu ujao yanaweza kufafanuliwa katika muundo wa hoja rasmi kama ifuatavyo:

1. Kama tungekuwa na mifumo ya kikatiba na kisheria inayowanyima wanasiasa matapeli fursa ya kufanya uhalifu wa kiuchaguzi kwenye michakaato ya chaguzi zetu basi tungekuwa na sababu nzuri ya kushiriki Uchaguzi Mkuu Ujao kabla ya kufanyika kwa mageuzi ya kimfumo.

2. Lakini, uzoefu wetu kutokana na chaguzi zote za 2010, 2015, 2019, 2020 na 2024 unaonyesha kwamba tunayo mifumo ya kikatiba na kisheria inayowapatia wanasiasa matapeli fursa ya kufanya uhalifu wa kiuchaguzi kwenye chaguzi zetu, kiasi kwamba, kwa kipindi cha miaka 15, tumekuwa tukiongozwa na serikali haramu zilizotokana na mbinu haramu.

3. Hivyo, bila kufanya mageuzi ya kuboresha mifumo ya kikatiba na kisheria inayowapatia wanasiasa matapeli fursa ya kufanya uhalifu wa kiuchaguzi kwenye chaguzi zetu hatuwezi kupata serikali halalai iliyotokana na mbinu halali.

Screenshot_20250222_205250_Chrome.jpg

IGP WAMBURA Bosi wa Jeshi la Polisi

4. Kwa mujibu wa kifungu cha 22 katika Sheria ya Makosa ya Jinai (Sura ya 16, Toleo la 2002), kama ilivyotafsiriwa kwenye Kesi ya Abdallah Zombe na wenzake 12 dhidi ya Ephraim Chigumbi na wenzake wawili, Kesi ya Mahakama Kuu Na. 26/2006, kuna njia nne za mtu mmojawapo kushiriki katika kitendo cha uhalifu wa kiuchaguzi, kabla, wakati na baada ya mchakato wa uchaguzi:

(a) Ama kwa mtu huyo kutekeleza uhalifu wa kiuchaguzi kwa kutumia mikono yake mwenyewe; au

(b) kwa mtu huyo kumpa msaada wa aina yoyote mtu baki mwenye nia ya kutenda uhalifu wa kiuchaguzi na hivyo kumsaidia mtu baki kufanikisha utekelezaji wa uhalifu; au

(c) kwa mtu huyo kumpa ushauri mtu baki ili ajenge nia ya kutenda uhalifu wa kiuchaguzi na hivyo kumshawishi mtu baki kufanikisha utekelezaji wa uhalifu; au

(d) kwa mtu huyo kuficha taarifa muhimu zinazohitajika kwa ajili ya ama kuzuia uhalifu wa kiuchaguzi kutendeka au zinazoweza kusaidia kuwatia hatiani watu waliotenda uhalifu wa kiuchaguzi.

5. Hivyo, kama tunao wajibu wa kupigania ujio wa serikali halali iliyotokana na mbinu halali, basi, tunapaswa kupigania ujio wa serikali halali kwa kufanya mambo yafuatayo:

(a) Ama kujizuia na kumshawishi kila mtu baki kujizuia kutekeleza uhalifu wa kiuchaguzi kwa kutumia mikono yake mwenyewe; au

(b) Kujizuia na kuwashawishi watu baki kujizuia kutoa msaada wa aina yoyote kwa mtu mwenye nia ya kutenda uhalifu wa kiuchaguzi na hivyo kumfanya mtu baki asifanikishe utekelezaji wa uhalifu; au

(c) Kujizuia na kuwashawishi watu baki kujizuia kumhimiza mtu yeyote kujenga nia ya kutenda uhalifu wa kiuchaguzi na hivyo kumfanya mtu baki asifikirie kutekeleza uhalifu wa kiuchaguzi; au

(d) Kufichua taarifa muhimu zinazohitajika kwa ajili ya ama kuzuia uhalifu wa kiuchaguzi kutendeka au zinazoweza kusaidia kuwatia hatiani watu waliotenda uhalifu wa kiuchaguzi.

6. Kwa hakika, tunao wajibu wa kisheria na kimaadili wa kupigania ujio wa serikali halali, jambo linalomaanisha kwamba tunao wajibu wa kisheria na kimaadili wa kuzuia ujio wa serikali haramu, kwa sababu zifuatazo:

(a) Kisheria, ibara ya 28(1) ya Katiba ya Tanzania (1977) inampa kila raia “wajibu wa kulinda, kuhifadhi na kudumisha uhuru, mamlaka, ardhi na umoja wa taifa.”

(b) Kimaadili, sheria ya maadili asilia inatupa jukumu la kutekeleza matendo mema na kuzuia matendo maovu, kwa kuhakikisha kwamba, kisiasa, inasimikwa serikali iliyotokana na wapiga kura halali, inayofanya kazi kwa niaba ya watu wote, na yenye kutekeleza majukumu yake kwa faida ya watu wote.

7. Kwa hiyo, raia wa Tanzania tunao wajibu wa kupigania uchaguzi utakaofanikisha ujio wa serikali halali na kupinga uchaguzi utakaofanikisha ujio wa serikali haramu. Hii ndio mantiki ya kaulimbiu isemayo kwamba “Bila Kufanya Mageuzi Kwanza Hakuna Kufanya Uchaguzi,” yaani “No Reforms, No Elections.”

Nakishi katika utekelezwaji wa majukumu ya TISS

Ni kituko kwamba uhalifu wa kiuchaguzi tangu 2010 mpaka 2024 umeshamiti katika Taifa ambalo linayo IDARA YA USALAMA WA TAIFA yenye jukumu la kutafiti, kuchambua, na kushauri serikali ipasavyo kuhusu njia bora za kuzuia uhalifu huu.

Ama idara hii ilitekeleza wajibu wake lakini ushauri wake ukapuuzwa na walioupokea au haikufanya hivyo.

Lakini kubwa ni kwamba idara hii inao wajibu wa kufanya kazi hii kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.

Chini ya kifungu cha 14 cha Sheria ya Huduma za Kiintelijensia na Kiusalama nchini Tanzania (Tanzania Intelligence and Security Service Act) Na. 15/1996 Idara hii inawajibika kisheria kukusanya, kuchakata na kusambaza taarifa za kiintelijensia kwa wizara na idara zote za serikali kusudi hatua stahiki za kuzuia uhalifu zichuliwe na wahusika.

Kuhusu suala la uhalifu wa kiuchaguzi hatujaona matokeo ya kazi yake kwa kipindi cha 2010 hadi 2024, maana wahalifu wa kisiasa wanaowafahamika kwa sura na majina wako mitaani na maofisini wanaendelea na kazi zao .

Hivyo basi tunahitimisha kwamba kuna tatizo mahali fulani ama ndani ya idara yenyewe kwenye kanuni zake au nje ya idara kwenye sheria mama.

Swali kuu la kujiuliza hapa ni hili: Je Idara ya Usalama wa Taifa inao wajibu wa kisheria wa kushirikiana na serikali inayofanya uhalifu wa kiuchaguzi ili kuisaidia serikali hiyo kuendelea kubaki madarakani kinyume cha utaratibu wa kisheria na kikatiba uliopo?

Kwa vyovyote vile mageuzi ya kimfumo na kimtazamo yanahitajika kwenye idara hii kusudi tusirudi kwenye matope haya katika siku za usoni.

Wanatakiwa ma-DSO, ma-RSO, ma-ZSO, maafisa vipenyo (penetration officers) na maafisa nusa nusa (field officers) wanaotekeleza kazi zao kwa weledi katika namna ambayo inalunda tunu, maadili na sheria za nchi ili siku zote usalama wetu uwe thabiti.

Lakini kwa sasa Kadiri kashfa ya uhalifu wa kiuchaguzi tangu 2010 mpaka 2024 inavyohusika TISS haiwezi kujivua lawama. Wanayo kazi ya kujisahihisha.
1740314269730.png

Suleiman Abubakar Mombo, DGIS

Kashfa ya wanasiasa matapeli kubaki maofisini

Ni wazi kwamba ma-WEO, ma-DC, ma-DAS, ma-DED, ma-OCD, ma-RAS na ma-RC walioshiriki kwenye uhalifu wa kiuchaguzi wanalo taji la wanasiasa matapeli maana walitenda jinai.

Lakini mpaka sasa wamechiwa huru watembee huru mitaani kana kwamba hakuna kosa la kisheria wametenda.

Baadaye kidogo watu hawa hawa ndio wanaonekana maofisini wakisimamia amani na utulivu ("law and order enforcement") kwa madai kuwa wanahakikisha kuwa watenda jinai wanaadhibiwa kwa mujibu wa sheria.

Jambo hili ni sawa na mtu mwenye kipara kuuza dawa ya kuotesha nywele. Na kwa kweli, undumila kuwili huu umeleta dharau kubwa kwa serikali tulizo wahi kuwa nazo tangu miaka ya 2010. Hatua za kusafisha ofisi za serikali zichukuliwe.

Ukasuku wa falsafa ya 4R inayonadiwa na Rais Samia

Kubuniwa kwa falsafa ya 4R lilikuwa ni jibu sahihi kwa changamoto zinazotokana na haya mabonde, milima, makorongo na miiba ya kisiasa, japo hadi sasa utekelezaji wake hauonekani kutibu ugonjwa ulipo.

Falsafa hii ilibuniwa na mwanazuoni mmoja ambaye kwa sasa bado anafanya shahada yake ya kwanza ya Sheria katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Hii ni falsafa yenye kumaanisha "Reconciliation, Resilience, Reforms and Rebuilding."

Yaani, "Upatanisho, Ustahimilivu, Ukarabati wa mifumo, na Ujenzi wa Mifumo mipya," kwa maana ya "4U" kama tunataka kuongea kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Katika falsafa hii ya "4R/4U" maneno "Upatanisho" na "Ukarabati wa mifumo" yanahusika zaidi kwenye changamoto za uchaguzi tulizoshuhudia kwa miaka 15 sasa.

Kwa mujibu wa mwasisi wa falsafa hii, kunahitajika "Upatanisho" kati ya watu waliotangazwa washindi isivyo halali na washindi halali ambao hawakutangazwa na kisha wakadhulumiwa ushindi wao, wakapoteza fedha zao za kampeni, na wakati mwingine kufilisika kabisa mara tu baada ya dhuluma hizo.

Aidha anasema kuwa kunahitajika "ukarabati wa mifumo" ya uchaguzi ili kuziba mianya ya uhalifu wa kiuchaguzi unaofanywa na vyombo vya dola kama vile ma-WEO, ma-DC, Ma-DED, ma-DAS, ma-RAS na ma-RC.

Hivyo, nje ya hatua hizi za kimakusudi, "falsafa ya 4R" au tuseme "falsafa ya 4U" inabaki ni ukasuku mtupu.

Hata Stephen Wassira Makamu Mwenyekiti CCM haonekanu kuelewa lolote kuhusu chimbuko la falsafa ya 4Rs.

Anasema eti maridhiano yanayoongelewa yanahusu MAKUNDI YOTE YA KUJAMII. Maajabu!

Na bahati mbaya mwanazuoni aliyeibuni falsafa ya 4R/4U hana fursa wa kuidadavua zaidi mbele ya wakubwa zake walioipenda na kuibeba.

Tatizo kubwa ni kwamba wale wakubwa zake walioipokea na kuanza kuitekeleza hawaielewi vema maana wao hawajui mwasisi wa wazo alikuwa anafkiria nini, na hawampi nafasi ya kufanya ufafanuzi.

Umuhimu na ulazima wa "mageuzi kwanza na uchaguzi baadaye"

Ni wazi kwamba, ili tupate mabadiliko ya kweli kwa maslahi mapana ya Taifa sehemu pekee ya kukomalia ni kwenye Mabadiliko Ya Katiba.

Tukumbuke kwamba kitu pekee kinachowapa CCM ujasiri wa kufanya watakavyo ni maudhui ya katiba tuliyoanayo kwa sasa.

Kwa sababu ya Katiba hii, nchini kwetu sio kura za wananchi zinazoamua mshindi wa Uchaguzi awe nani.

Wanaoamua wagombea wa upinzani wapewe kura ngapi na wagombea wa CCM wabaki na kura ngapi ni Ikulu, viongozi wa CCM, mamluki wa CCM walioko kwenye Tume ya Uchaguzi, na vibaraka wa CCM walioko kwenye Halmashauri zetu, kwa maana ya Wakurugenzi wa Halmashauri ambao ni Wasimamizi wa Chaguzi.

Ushahidi wa mambo haya uko bayana. Kuna maneno aliyoyasema Nape Nnauye, akiwa bado Waziri wa Habari jimboni kwa Byabato Mkoani Kagera.

Ushahidi mwingine ni maneno aliyosema aliyekuwa Mkuu wa Wilaya wa Longido, Ndugu Marko Henry Ng'umbi.

Aidha, ushahidi wa haya ni maneno aliyowahi kuyatamka Rais Magufuli pale alipouliza kuwa:

Inawezekanaje nikuteue wewe Mkurugenzi na nikulipe Mshahara, alafu Wapinzani washinde kwenye Uchaguzi unaosimamia na uwatangaze?

Lakini, kwa nini tufanye uchaguzi wakati sio kura zetu zinazoamua mshindi wa uchaguzi?

Kwa nini tufanye uchaguzi wakati kuna watu wana uwezo wa kukaa mahali na kuamua tu kwamba sasa hebu tuondoe majina ya wagombea wote wa upinzani ili CCM kishinde kwa asilimia 100?

Ukweli ni kwamba watu wanaoiba uchaguzi hawawezi kuwa na mamlaka ya kimaadili ya kukemea wizi wa mali ya umma wala fedha ya umma.

Tusipokuwa makini, mali na fedha za umma zitakuwa zinaibwa na wanasiasa matapeli kila kukicha na kutuacha Wananchi tukiishi maisha magumu na kukosa huduma muhimu milele.

Tusisahau kwamba, watu wanaoiba uchaguzi hawawezi kuacha kuiba na kutumia vibaya kodi zetu.

Hawawezi kuzitumia kodi zetu vizuri kutujengea miondombinu bora ya Barabara, maji, hospitali, masoko, stendi za mabasi, na mambo kama haya.

Tusimame pamoja ili kuitengeneza TANZANIA bora kwa ajili yetu na kwa ajili ya vitukuu wa vitukuu wetu.

Kwa maslahi mapana ya nchi yetu, sasa sote tupaze sauti na kusema Pamoja na Chadema kwamba “NO REFORM NO ELECTION.”

VI. MAPENDEKEZO YA HATUA ZINAZOPASWA KUCHUKULIWA

Kutokana na yaliyojadiliwa hapo juu, napenda kutoa wito na mapendekezo yafuatayo kwa Serikali, Bunge, Makanisa, Misikiti, Azaki, Wanazuoni wa Vyuo Vikuu na watu wote wenye mapenzi mema kwa Tanzania:

1. Kwa kuwa Tanzania sio dola ya Kiimla, wala Himaya ya Kifamle wala Taifa la Kijeshi, bali ni Dola ambayo ni Jamhuri ya Kikatiba na Kidemokrasia, inayofuata demokrasia ya vyama vingi vya siasa tangu mwaka 1992;

2. Kwa kuwa, sifa kuu ya dola ambayo ni Jamhuri ya Kikatiba na Kidemokrasia ni uchaguzi unaofanyika kwa uhuru, uchaguzi unaofanyika kwa uwazi, uchaguzi unaofanyika kwa haki na uchaguzi unaofanyika kwa ushindani wa hoja za kisera;

3. Kwa kuwa chaguzi za 2019, 2020 na 2024 zilifanyika kwa njia ya udanganyifu ulioratibiwa na matapeli wa kisiasa waliokuwa wanafuata nyayo za Hayati JMP;

4. Kwa kuwa udanganyifu wa kisiasa katika chaguzi za 2019, 2020 na 2024 ulitekelezwa na ma-WEO, ma-DED, ma-DC, ma-DAS, ma-DAS na Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya sasa;

5. Kwa kuwa udanganyifu wa kisiasa ulifanikiwa kwa sababu ya uwepo wa mifumo mibovu ya kikatiba na kisheria;

6. Kwa kuwa sheria na Katiba ya sasa vinasabaisha kuwepo kwa uwanja wa uchaguzi usio tambarare bali uwanja wenye milima, mabonde na makorongo yanayowakandamiza wagombea wa vyama vya upinzani;

7. Na kwa kuwa serikali inayoingia madarakani kwa njia za udanganyifu inakuwa haina uhalali ikiwa ni sawa na serikali zilizokuwepo enzi wa ukoloni chini ya wazungu na serikali zilizokuwepo enzi za utumwa chini ya waarabu;

8. Kwa kuwa vyombo vya dola vilivyoundwa kikatiba na kisheria kama vile Idara ya Usalama wa Taifa, Jeshi la Polisi, Takukuru na Tume ya Haki za Binadamu zimeshindwa kutekeleza majukumubyake kwa mujibu wa sheria katika nyakati za uchaguzi, kwa sababu ya ukweli kwamba vyombo hivi viko kwenye kwapa la Rais wa nchi ambaye pia anakuwa ni mgombea Urais.

9. Na kwa kuwa njia pekee ya kuondokana na uhalifu wa kiuchaguzi unaoendelea nchini Tanzania tangu 2010 ni kuibomoa na kuijenga upya mfumo wa uchaguzi unaojumuisha Katiba, Sheria na Kanuni zake.

10. Hivyo basi, natoa wito kwamba, Serikali na Bunge vinapaswa kuandaa vikao maalum vya Bunge kwa ajili ya kupitisha Mabadiliko ya 15 ya Katiba ya Tanzania (1977) pamoja na marekebisho stahiki ya sheria za uchaguzi ili mambo yafuatayo yawezekane kabla ya uchaguzi mkuu wa 2025:

(a) Sheria na Katiba vikataze ma-WEO, ma-DED, ma-DC, ma-DAS, ma-RAS kusimamia chaguzi.

(b) Sheria na Katiba vitamke kuwa chaguzi zote nchini zitasimamiwa na Watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliyo huru.

(c) Tume ya Taifa ya Uchaguzi iondolewe kwapani mwa Rais wa nchi kusudi iweze kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria pekee bila kuyumbishwa na maagizo kutoka Ikulu.

(d) Tume ya Taifa ya Uchaguzi iweke watumishi wake kwenye kila jimbo la uchaguzi kwa mujibu wa sheria.

(e) Katiba ikataze Rais wa nchi aliye madarakani na ambaye ni mgombea kuendelea kutekeleza majukumu yake ya Urais wakati wa maandalizi na uendeshaji wa kampeni za uchaguzi.

(f) Katiba ikataze Rais wa nchi kushika nafasi ya mwenyekiti wa chama cha siasa.

(g) Katiba na sheria zetu viruhusu matokeo ya uchaguzi wa Rais yanayobishaniwa kupingwa mahakamani kisheria.

(h) Sheria na Katiba vipige marufuku tabia ya udanganyifu wa kugeuza mchakato wa uchaguzi kugeuzwa mashindano ya kujaza fomu za wagombea.

(i) Rais Mstaafu wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, anayejua vizuri sana haya "mambo mambo" alisaidie Taifa kuondokana na hii Kero Sugu ya Uhalifu wa Kiuchaguzi, hata kama chama chake cha CCM kitangoka madarakani kwa sababu hiyo. Tanzania ni kubwa kuliko vyama vya siasa.

(j) Wanasheria wa Tanganyika Law Society watusaidie kuandaa miswada ya sheria zinazopaswa kuwasilishwa Bungeni muda wowote kwa ajili ya kutekeleza mapendekezo hapo juu. Washirikiane na Wizara ya Sheria na Katiba. Tumechelewa sana, hivyo inabidi tukimbie.

Screenshot_20250222_205941_Chrome.jpg

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Salum Hamduni

(k) Sheria ya TAKUKURU kwa ajili ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa irekebishwe namfanya Mkuu wa TAKUKURU kuripoti Bungeni badala ya kuripoti Iklu kwa Rais wa nchi.

(l)Padre Charles Kitima akae na muumini wake mmoja Joseph Selasini ili kumkanya na kumwongoza kwenye sala ya toba. Huyu jamaa alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Walei Taifa, chini ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC).

Lakini anayoyafanya sasa hivi sio sawa kabisa. Anahujumu jitihada za kuimarisha siasa za vyama vingi nchini Tanzania. Tangu ampindue James Mbati wa NCCR-Mageuzi kazi yake ni kuhakikisha NCCR-Mageuzi wanatekeleza sera za CCM kwa moyo mkunjufu.

Mara nyingi vikao vyake na RC Chalamila vinafanyika pale Kisuma Hotel Magomeni. Kwa sasa Selasini amekuwa kama Lyatonga Mrem katika siku zake za mwisho. Anajikomba CCM hadi inatisha.

1740119914817.png

Padre Kitima wa TEC ambaye ni Mlezi wa kiroho wa Joseph Selasini wa NNCR-Mageuzi

VII. MAPINGAMIZI NA MAJIBU YAKE

Mapendekezo yangu hapo juu yanaweza kupingwa na watu kadhaa kwa njia mbalimbali. Baada ya mapingamizi ninayoyatarajia na ambayo nataka kuyajibu kabla hayajaibuka ni kama ifuatavyo:

Pingamizi Na. 01: “Hoja ni nzuri, utafiti mzuri, ila sio realistic, kwa maana kuwa hayana uhalisia kama tukiangalia muda uliobaki.”

Majibu: Naamini kuwa hoja yangu inatekelezeka kwa kuwa kazi ya kuandaa miswada kwa hati ya dharula inawezekana. Bajeti ya kuitisha Bunge maalum kwa ajili ya kupitisha miswada hiyo iko ndani ya uwezo wa serikali. Wabunge bado wapo maana Bunge halijavunjwa.

Pingamizi Na. 02: “Uchaguzi ni process inayosimamiwa na serikali. Ratiba yake haiwezi kubadilishwa na mtu baki kama Tundu Lissu.”

Majibu: Kumbuka kuwa serikali ipo kwa ajili ya watu, na inatokana na watu. Hivyo, serikali inapaswa kufanya mambo yale wananchi wanayoyataka. Pia uchaguzi upo kwa ajili ya watu na sio watu kuwepo kwa ajili ya uchaguzi. Pia, ratiba ya uchaguzi sio msahafu.

Pingamizi Na. 03: Tundu Lissu na Chadema yake hawana uwezo wala mamlaka ya kusema “no reforms no election” na kauli yake ikatekelezwa na serikali. Kwa hiyo, hakuna mageuzi yoyote na uchaguzi utafanyika.

Majibu: Mawazo hayo yana-personalise hoja yangu. Lissu ameanzisha hoja. Mie nimejielekeza kwenye hoja na kumweka pembeni. Tujiepushe na tatizo hilo la ARGUMENTUM AD HOMINEM. Yaani tutofautishe hoja na mleta hoja. Tufikirie juu ya uwezekano kwamba hoja ni nzuri, serikali itaweza kuipenda, Bunge litaweza kuichagamkia. Let us think positively. Namna hiyo, tutakuwa na mchango ambao sio biased sana.

Pingamizi Na. 04: Nchini Tanzania hatujawahi kubadilisha ratiba ya uchaguzi na kuisogeza mbele. Kwa hiyo pendekezo la kubadilisha ratiba ya uchaguzi mkuu wa 2025 haliungwi mkono na historia yetu.

Majibu: Ukweli ni kwamba, kuna siku uchaguzi mkuu ulishawahi kusogezwa mbele. Ni wakati ule alipokufa DR Omary Ali Juma. Lakini pia, hata kama ingekuwa ni kweli kwamba huko nyuma hatujawahi kufanya jambo fulani, ukweli huo haumaanishi kuwa leo au kesho hatuwezi kufanya jambo hilo.

Pingamizi Na. 05: Tukifanya mageuzi ya kimfumo kwa ajili ya kuondoa mabonde, milima, makorongo na miiba kwenye uwanja wa siasa, Wapinzani wa Chadema watapata fursa ya kukiangusha chama tawala cha CCM, wakati bila CCM nchi inaweza kuyumbishwa na Chadema kwa sababu ya ukabila wao.

Majibu: Tulipoanzisha mfumo wa vyama vingi tulikubaliana kwamba uchaguzi wa chama kimoja dhidi ya vyama baki ndio mtindo wa maisha yetu ya kisiasa. Hiyo maana yake ni kwamba tulikubali kwamba, kwa kuwa sauti ya wengi ni kama sauti ya Mungu, basi chama kitakachopata kura nyingi ndicho kinapaswa kuongoza nchi.

Chama hicho kinaweza kuwa Chadema au chama kingine. Na kuhusu tuhuma kwamba Chadema inaumwa ugonjwa wa ukabila wa kichaga, tuhuma hiyo sasa umepatiwa tiba.

Ujio wa Timu Lissu umekivua chama cha Chadema gamba la ukabila wa kichaga uliokuwa unaelezwa kwa njia ya maneno kwamba "CHADEMA maana yake ni Chagga Development Manifesto."

Pingamizi Na. 06: Kuongelea ajenda ya "NO REFORM NO ELECTION" ni siasa za kusadikika tu kwa maana ya utopian politics (illusory politics) kwani hilo jambo halina uhalisia kwa sasa.

Majibu: Napenda kujibu hivi:

  • Je, Siasa za kujaza kura feki kwenye masanduku ya kura, kuwateka wakosoaji wa serikali, kuwaua wapinzani na kuwabambikizia kesi hewa wananchi ndio realistic politics?
  • Je, Kutokuwepo kwa usawa wa mgawanyo wa majimbo ya uchaguzi wa wabunge ndio realistic poliyics?
  • Je, Habari ya Zanzibar yenye wapiga kura 500,000 kuwa na majimbo 50 ya uchaguzi huku mkoa wa Dar Es Salaam wenye wapiga kura 3,000,000 kuwa na majimbo 10 tu ya uchaguzi ndio realistic politics?
  • Je, Mwenyekiti wa CCM ambaye automatically huwa mgombea U - Rais kuwa mteuaji wa wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili wasimamie uchaguzi ambao naye ni mshiriki kama mgombea ndio realistic politics?
  • Je, Wagombea wa upinzani pekee kuonekana kwamba hawajui kusoma wala kuandika, lakini wagombea wote wa chama tawala kujua kusoma na kuandika, wakati wote wamesoma shule zile zile na kufund8shwa na walimu wale wale, ndio realistic politics?
  • Je, Tabia ya kumshambulia mleta hoja badala ya kujibu hoja ndio realistic politics?
  • Na je, KUKATAA WITO wa kutaka tukae pamoja kama nchi ili tujadiliane na kuamua kuhusu mabadiliko ya mifumo ya kikatiba, kisheria na kikanuni yanayotakiwa kabla ya uchaguzi, ili hatimaye tuweze kutengeneza nfumo mpya wa uchaguzi ulio huru, wenye uwazi, wenye ushindani wa hoja na wenye kutoa haki kwa kila mshiriki ndio realistic politics?
Maswali haya yote yanalo jawabu moja tu la HAPANA. Hivyo Chadema wanapinga illusory and utopian politics na kuhimiza kinyume chake, yaani wanahimiza realistic politics. Period.

VIII. HITIMISHO

Katika dokezo hili nimejadili mambo kadhaa na kuyagawanya kwenye sehemu zifuatazo: (1) Usuli, (2) Utangulizi, (3) Methodolojia, (4) Matokeo ya utafiti, (5) Muhtasari na majadiliano, (6) Mapendekezo, (7) Mapingamizi na majibu yake, (8) Hitimisho, na (9) Rejea muhimu zilizotumika.

Nawasilisha.

1740119739408.png

James Mbatia wa NCCR Mageuzi aliyepinduliwa na Joseph Selasini

1740141582704.png

Joseph Selasini, Mwenyekiti Mpya wa NCCR Mageuzi aliyempindua James Mbatia

IX. REJEA ZILIZOTUMIKA

1. Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Mwaka 1977.

2. Sheria ya Makosa ya Jinai, Sura ya 16, Toleo la 2002.

3. Kesi ya Mahakama Kuu Na 26/2006, Jamhuri Vs ACP. ABDALLAH ZOMBE na Wenzake 12.

4. Taarifa mbalimbali za Waangalizi w Uchaguzi wa Tanzania, 2010-2024.

5. Video za Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chadema, Kuhusu "No Reform No Election".

6. Hotuba za Stephen Wasira, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Kuhusu Falsafa ya 4R.

7. Hotuba za Alli Happy, Mwenyekiti Wazazai wa CCM, Kuhusu "No Reform No Election".

8. Hotuba za Rais Samia Kuhusu Falsafa ya 4R.

9. Mahojiano na mwanazuoni aliyebuni Falsafa ya 4R anayoinadi Rais Samia.

10. Makullo, A. and Others(2016), Election Management Bodies in East Africa: A Comparative Study of the Contribution of Electoral Commissions to the Strengthening of Democracy (New York: Open Society Foundation)

11. Rawls, John (2001), Justice as Fairness: A Restatement (Cambridge: Harvard University Press)

12. Hart, H.L.A. (1961), The Law as a Union of Primary and Secondary Rules (Oxford, United Kingdom).

13. Crusius, T.W. and Channell, C.E. (2015), The Aims of Argument: A Text and Reader, 8th Edition (New York: McGraw-Hill Education)

14. Sheria ya Takukuru sura ya 329 Toleo la 2022

15. Sheria ya Huduma za Kiintelijensia na Kiusalama nchini Tanzania (Tanzania Intelligence and Security Service Act) Na. 15/1996
 
Aisee hongera sana. Andiko murua sana. Natumaini wenye akili TISS watalisoma na kumshauri ipasavyo DGIS.

Inatia moyo kuona bado tuna Watanzania wenye akili na maarifa ambao wanatumia akili zao kuhamasisha positive changes nchini mwetu.

Mleta mada ukija Dubai nitafute nikupe lunch.
 
Nitarejea 😃

Nimesoma andiko na kulielewa

Labda mleta Hoja utufafanulie " Mpiga Kura ni nani?

Je, Tanzania tunao Wapiga Kura Kwa maana Halisi ya Kupiga Kura?

Katika kunijibu unaweza kutumia mfano wa uchaguzi wa Chadema kuchagua Mwenyekiti kama akina Yeriko na Ntobi ndio sample ya Wapiga Kura wa Tanganyika specifically

Nimekaa pale 🐼
 
tunapaswa kurekebisha ratiba ya uchaguzi mkuu wa 2025, kisha tufanye mageuzi ya kikatiba na kisheria, na hatimaye tufanye uchaguzi mkuu?

Kutokana na utafiti nilioufanya, dokezo hili linapendekeza kwamba, tunapaswa kusogeza ratiba ya uchaguzi mkuu mbele kidogo ili uchaguzi huu ufanyike baada ya mageuzi ya kikatiba na kisheria kufanyika ili kusawazisha milima, mabonde na makorongo yaliyopo.
Hoja nzuri, utafiti mzuri, ila sio realistic!.

Uchaguzi is a process, kuna siku Uchaguzi mkuu uliwahi kusogezwa mbele kwassbabu ya kurekebisha jambo lolote?.

TAL anayo the capacity & capability yoyote kusema no reforms no election?.

Hana!.

There will be no reforms, na uchaguzi utafanyika!. TAL na Chadema has no capacity wala capability kuzuia uchaguzi usifanyike!.

Nashauri watu wenye uwezo wa kusaidia, tumsaidie TAL, tuisadie Chadema iachane na Utopian politics and come to face with the real polititcs, TAL wala Chadema hawawezi kuzuia uchaguzi mkuu.
P
 
. Lakini, uzoefu wetu kutokana na chaguzi zote za 2010, 2015, 2019, 2020 na 2024 unaonyesha kwamba tunayo mifumo ya kikatiba na kisheria inayowapatia wanasiasa matapeli fursa ya kufanya uhalifu wa kiuchaguzi kwenye chaguzi zetu, kiasi kwamba, kwa kipindi cha miaka 15, tumekuwa tukiongozwa na serikali haramu zilizotokana na mbinu haramu.
Hizi ndio zile mada za Kwa Masilahi ya Taifa.

Pascal Mayalla
 
Hoja nzuri, utafiti mzuri, ila sio realistic!.

Uchaguzi is a process, kuna siku Uchaguzi mkuu uliwahi kusogezwa mbele kwassbabu ya kurekebisha jambo lolote?.

TAL anayo the capacity & capability yoyote kusema no reforms no election?.

Hana!.

There will be no reforms, na uchaguzi utafanyika!. TAL na Chadema has no capacity wala capability kuzuia uchaguzi usifanyike!.

Nashauri watu wenye uwezo wa kusaidia, tumsaidie TAL, tuisadie Chadema iachane na Utopian politics and come to face with the real polititcs, TAL wala Chadema hawawezi kuzuia uchaguzi mkuu.
P
Wewe jamaa ni mjinga sana. Ukishawekwa kwenye payroll unajizimaga data na kujitoaga kabisa ufahamu.

Hoja ya No Reform No Election ni ya Tundu Lissu au Chadema?

Alafu sio wewe ulieandika nyuzi mbili humu kupinga maigizo yaliyofanyika ya kujifanya tunarekebisha Sheria za Uchaguzi? Sasa kama uliandika nyuzi kabisa kuelezea kasoro zilizofanyika kwenye kile kilichoonekana mabadiliko ya Sheria za Uchaguzi na Demokrasia kwa nini unasema haiwekeni uchaguzi kupelekwa mbele?

Kwani uchaguzi ukipelekwa mbele kuna watu watakufa? Kuna watu watashindwa kuishi? Hewa tunayovuta tuliyopewa na mwenyezi Mungu itakatika hadi useme haiwezekani?

Pia Kwani Samia akikubali hiyo hoja na Ikafanyika hizo reforms sifa zinaenda kwa Samia au Tundu Lissu?

Wewe mwenyewe ulimsikia Nape alivyokuwa anaongea jimboni kwa Byabato kuwa sio kura zinazoamua mshindi ila ni anayetanganza matokeo. Kama mwandishi na mwanasheria kwa akili za kawaida tu ile statement ya Nape ingekufanya na wewe uje na utafiti wako ambao it's obvious ungekuja na mapendekezo kama aliyokuja nayo mleta mada. Hii ni kwa sababu it's obvious nchi hii hatuna uchaguzi tuna uchafuzi na maigizo ya futuhi kupitia sanduku la kura.
 
Hoja nzuri, utafiti mzuri, ila sio realistic!.

Uchaguzi is a process, kuna siku Uchaguzi mkuu uliwahi kusogezwa mbele kwassbabu ya kurekebisha jambo lolote?.

TAL anayo the capacity & capability yoyote kusema no reforms no election?.

Hana!.

There will be no reforms, na uchaguzi utafanyika!. TAL na Chadema has no capacity wala capability kuzuia uchaguzi usifanyike!.

Nashauri watu wenye uwezo wa kusaidia, tumsaidie TAL, tuisadie Chadema iachane na Utopian politics and come to face with the real polititcs, TAL wala Chadema hawawezi kuzuia uchaguzi mkuu.
P
CCM kutokujibu hoja za Lissu maana yake pumzi zinawaishia pole pole, ikifika August mbivu na mbichi zitajulikana. Maono yangu hakutakuwa na uchaguzi mwaka huu.
 
hao usalama wenyewe wame choka, ni Kama mlevi tu.

hawako tayari kufanya kazi kwenye malengo na kanuni zao, mtu ana kuja na kuondoka ila kanuni Zina paswa zifatwe.

Leo hii uki wauliza maono na malengo Yao, wata kwambia kulinda watu.
hawajui Kuna UCHUMI, afya.
Kagame na Museveni wana long term plans za kutawala Afrika hii.

Wanapeleka majasusi wao nje kwenye vyuo bora kwenda kujifunza na wanapeleka kwenye mission za maana ili kuwajenga kufanikisha vision za maana.

Huku Tanzania CCM wanawafundisha usalama kuiba hadi uchaguzi wa kijiji alafu utategemea tuwe na taifa imara?

Huku CCM wamewekeza kwenye uchawa tu. Sasa kwa nini Taasisi isiwe kwenye njia panda.

Kuna haja ya Watanzania wote kuungana kushinikiza reforms ambazo zitaliokoa Taifa letu na kulifanya kuwa imara in the long run.

Na hii ni watanzania wote waliopo ndani na nje ya vyombo vya ulinzi na usalama.
 
Umechambua vizr mkuu, shida ni ubinafsi, wa wanakina kikwete, wanajua sana, ila wapo kwa ajili ya masilai yao, na sio taifa. Wanapesa nyingi sana ndani na nje ya nchi, lakin BAdo hawariziki, hiyo ni ngumu sana kufanyika, suluhisho bora ni nguvu ya uma, wakuna mwanasiasa atakuja kufanya hayo yote, kwa sbb ya extremely egoism
View attachment 3242826
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akimwapisha Suleiman Abubakar Mombo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Ikulu ya Dar es Salaam , 11 Julai 2024.

I. USULI

Naandika dokezo la kisera, lenye kubeba taarifa za intelijensia ya kisiasa na kijasiriadola, kwa ajili ya kutetea rai ifuatayo:

Kwamba, kwa kuwa uhalifu wa kiuchaguzi unaowafanywa na wanasiasa matapeli wakati wa chaguzi zetu umekithiri kwa miaka 15 sasa kutokana na matobo ya kikatiba na kisheria, basi, tunapaswa kurekebisha ratiba ya uchaguzi mkuu wa 2025, kisha tufanye mageuzi ya kikatiba na kisheria, na hatimaye tufanye uchaguzi mkuu baadaye, na sio kinyume chake.

II. UTANGULIZI

Napendekeza kuanza dokezo hili kwa nukuu muhimu kuhusiana na mtazamo wa Chadema kuhusu Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika 2025.

"Mtu yeyote mwenye akili na macho ya kuona anajua kuwa chaguzi za nchi hii zimekuwa za hovyo sana na kwamba ni za hovyo kwa sababu mfumo mzima wa kiutawala wa nchi hii ni mfumo wa hovyo" -- Tundu lissu, Mwenyekiti CHADEMA.

“Hivyo, hatuzungumzii kususuia uchaguzi, hatutasusia bali tutaenda kuwaambia Watanzania, jumuiya ya kimataifa na walimwengu kwamba kama CCM na Serikali hawako tayari kufanya mabadiliko kwenye mfumo wa uchaguzi ili kuwepo chaguzi huru na haki, uchaguzi wa mwaka huu usifanyike kabisa” -- Tundu lissu, Mwenyekiti CHADEMA.

Huu ndio msimamo ulioibuliwa na Chadema kuhusu kile ambacho baadhi ya vyombo vya Habari, kama vile gazeti la Mwananchi la leo, vinakiita “Njiapanda ya Chadema Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa 2025.”

Lakini, napendekeza kwamba, kutokana na uzito wa hoja yenyewe, hasa tunapaswa kuwa tunaongelea “Njiapanda ya Watanzania Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa 2025.”

Kwa njia ya swali, “njiapanda” inayoongelewa kwenye vyombo vya habari, ndani na nje ya Chadema pia, inaweza kusomeka hivi:

Je, kwa kuzingatia uhalifu wa kiuchaguzi ambao umekuwa ukifanyika nchini Tanzania tangu 2010 kutokana na uwepo wa milima, mabonde na makorongo yaliyopo kwenye uwanja wa uchaguzi wa vyama vingi nchini Tanzania, tufumbe macho na kuendelea na utekelezaji wa ratiba ya uchaguz mkuu wa Oktoba 2025 au tusogeze ratiba hii mbele kidogo ili uchaguzi huu ufanyike baada ya mageuzi ya kikatiba na kisheria kufanyika ili kusawazisha milima, mabonde na makorongo yaliyopo?

Kutokana na utafiti nilioufanya, dokezo hili linapendekeza kwamba, tunapaswa kusogeza ratiba ya uchaguzi mkuu mbele kidogo ili uchaguzi huu ufanyike baada ya mageuzi ya kikatiba na kisheria kufanyika ili kusawazisha milima, mabonde na makorongo yaliyopo.

III. UTARATIBU WA UTAFITI (METHODOLOJIA)

Katika utafiti wangu nilikusudia kujibu maswali yafuatayo:
  1. Hoja ya Chadema kuhusu changamoto ya uhalifu wa kiuchaguzi nchini Tanzania inasema kitu gani kuhusu uwanja wa siasa za uchaguzi wa vyama vingi?
  2. Je, ni kweli kwamba kuna milima, mabonde na makorongo kwenye uwanja wa siasa za uchaguzi wa vyama vingi nchini Tanzania?
  3. Kama jawabu kwa swali la kwanza ni “ndiyo,” milima, mabonde na makorongo haya yamekuwa na madhara gani katika matokeo ya uchaguzi?
  4. Kutokana na majibu ya maswali haya mawili hapo juu, nah atua gani zichukuliwe tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa 2025.

IV. MATOKEO YA UTAFITI

Hoja ya Chadema

Maneno ya Tundu Lissu kuhusu msimamo wa kisera wa chama chake juu ya umuhimu na ulazima wa kusogeza mbele ratiba ya Uchaguzi Mkuu ujao yamenukuliwa hapo juu.

Kwa maoni yangu, haya ndio maneno yanayotueleza msimamo rasmi wa Chadema. Maneno haya yanaweza kufafanuliwa katika muundo wa hoja rasmi kama ifuatavyo:

1. Kama tungekuwa na mifumo ya kikatiba na kisheria inayowanyima wanasiasa matapeli fursa ya kufanya uhalifu wa kiuchaguzi kwenye michakaato ya chaguzi zetu basi tungekuwa na sababu nzuri ya kushiriki Uchaguzi Mkuu Ujao kabla ya kufanyika kwa mageuzi ya kimfumo.

2. Lakini, uzoefu wetu kutokana na chaguzi zote za 2010, 2015, 2019, 2020 na 2024 unaonyesha kwamba tunayo mifumo ya kikatiba na kisheria inayowapatia wanasiasa matapeli fursa ya kufanya uhalifu wa kiuchaguzi kwenye chaguzi zetu, kiasi kwamba, kwa kipindi cha miaka 15, tumekuwa tukiongozwa na serikali haramu zilizotokana na mbinu haramu.

3. Hivyo, bila kufanya mageuzi ya kuboresha mifumo ya kikatiba na kisheria inayowapatia wanasiasa matapeli fursa ya kufanya uhalifu wa kiuchaguzi kwenye chaguzi zetu hatuwezi kupata serikali halalai iliyotokana na mbinu halali.

4. Kwa mujibu wa sheria ya makosa ya jinai, kama ilivyotafsiriwa kwenye Kesi ya Abdallah Zombe na wenzake 12, Kesi ya Mahakama Kuu Na. 26/2006, kuna njia tatu za mtu mmojawapo kushiriki katika kitendo cha uhalifu wa kiuchaguzi, kabla, wakati na baada ya mchakato wa uchaguzi:
  • (a) Ama kwa mtu huyo kutekeleza uhalifu wa kiuchaguzi kwa kutumia mikono yake mwenyewe; au
  • (b) kwa mtu huyo kumpa ushirikiano wa aina yoyote mtu baki mwenye nia ya kutenda uhalifu wa kiuchaguzi na hivyo kumsaidia mtu baki kufanikisha utekelezaji wa uhalifu; au
  • (c) kwa mtu huyo kuficha taarifa muhimu zinazohitajika kwa ajili ya ama kuzuia uhalifu wa kiuchaguzi kutendeka au zinazoweza kusaidia kuwatia hatiani watu waliotenda uhalifu wa kiuchaguzi.
5. Hivyo, kama tunao wajibu wa kupigania ujio wa serikali halali iliyotokana na mbinu halali, basi, tunapaswa kupigania ujio wa serikali halali kwa kufanya yafuatayo:
  • (a) Ama kujizuia na kumshawishi kila mtu baki kujizuia kutekeleza uhalifu wa kiuchaguzi kwa kutumia mikono yake mwenyewe; au
  • (b) Kujizuia na kuwashawishi watu baki kujizuia kumpa ushirikiano wa aina yoyote mtu mwenye nia ya kutenda uhalifu wa kiuchaguzi na hivyo kumfanya mtu baki asifanikishe utekelezaji wa uhalifu; au
  • (c) Kufichua taarifa muhimu zinazohitajika kwa ajili ya ama kuzuia uhalifu wa kiuchaguzi kutendeka au zinazoweza kusaidia kuwatia hatiani watu waliotenda uhalifu wa kiuchaguzi.
6. Kwa hakika, tunao wajibu wa kisheria na kimaadili wa kupigania ujio wa serikali halali, jambo linalomaanisha kwamba tunao wajibu wa kisheria na kimaadili wa kuzuia ujio wa serikali haramu, kwa sababu zifuatazo:
  • (a) Kisheria, ibara ya 28(1) ya Katiba ya Tanzania (1977) inampa kila raia “wajibu wa kulinda, kuhifadhi na kudumisha uhuru, mamlaka, ardhi na umoja wa taifa.”
  • (b) Kimaadili, sheria ya maadili asilia inatupa jukumu la kutekeleza matendo mema na kuzuia matendo maovu, kwa kuhakikisha kwamba, kisiasa, inasimikwa serikali iliyotokana na wapiga kura halali, inayofanya kazi kwa niaba ya watu wote, na yenye kutekeleza majukumu yake kwa faida ya watu wote.
7. Kwa hiyo, raia wa Tanzania tunao wajibu wa kupigania uchaguzi utakaofanikisha ujio wa serikali halali na kupinga uchaguzi utakaofanikisha ujio wa serikali haramu. Hii ndio mantiki ya kaulimbiu isemayo kwamba “Bila Kufanya Mageuzi Kwanza Hakuna Kufanya Uchaguzi,” yaani “No Reforms, No Elections.”

Kwa ujumla, ni wazi kwamba hitimisho hili lisemalo linawaweka njiapanda baadhi ya wanachama wa Chadema wanaotaka kugombea Udiwani, Ubunge na Urais kwa tiketi ya Chadema.

Pia, ni wazi kwamba vyama vingine vinaweza kuendelea na maandalizi ya uchaguzi, maana hii sio sera yao. Na wanachadema wanaopinga sera hii wanayo hiari ya kutafuta jukwaa jingine la kisiasa lisilotambua sera hii ili wapewe fursa ya udhamini wanaoutaka.

Milima, mabonde na makorongo ya kisiasa

Tuhuma kwamba chaguzi zote za 2010, 2015, 2019, 2020 na 2024 unaonyesha kuwa tunayo mifumo ya kikatiba na kisheria inayowapatia wanasiasa matapeli fursa ya kufanya uhalifu wa kiuchaguzi kwenye chaguzi zetu, kiasi kwamba, kwa kipindi cha miaka 15, tumekuwa tukiongozwa na serikali haramu zilizotokana na mbinu haramu, nazi zinao ushahidi wa kuziunga mkono kama ifuatavyo:

(a) Uchaguzi unaosimamiwa na ma-WEO, ma-DED, ma-DC, ma-DAS, na ma-RAS unakosa uhuru, uwazi na ushindani wa kweli, kwa sababu wao ni watumishi wa serikali ya chama tawala, na hivyo kufanya uhalifu wa kiuchaguzi kwa faida ya chama tawala.

(b) Sheria za uchaguzi zinawaruhusu Watumishi wa umma kuvaa kofia za Watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakati w auchaguzi na hivyo kufungua milango ya uhalifu wa kiuchaguzi.

(c) Tume ya Taifa ya Uchaguzi imo kwapani mwa Rais wa nchi, ambaye ndiye huteua wajumbe wake, na hivyo kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria pekee kwa sababu ya kuyumbishwa na maagizo kutoka Ikulu.

(d) Tume ya Taifa ya Uchaguzi haina uwezo wa kisheria wala kifedha wa kusimika watumishi wake kwenye kila jimbo la uchaguzi kwa mujibu wa sheria.

(e) Katiba inamruhusu Rais wa nchi aliye madarakani na ambaye ni mgombea kuendelea kutekeleza majukumu yake ya Urais wakati wa kampeni za uchaguzi ilihali yeye ni Amiri Jeshi Mkuu, Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, na Msimamizi Mkuu wa Jeshi la Polisi.

Jambo hili linafungua mianya kwa baadhi ya vyombo vya ulinzi na usalama, kama vile Jeshi la Polisi na TISS, kufanya uhalifu wa kiuchaguzi ili kumsaidia “bosi” wao kushinda.

(f) Katiba inaruhusu Rais wa nchi kushika nafasi ya mwenyekiti wa chama cha siasa, kabla na wakati wa uchaguzi, na hivyo, kufungua mlango wa Rais huyu kuvitumia vyombo vya ulinzi na usalama kwa faida ya chama tawala.

(g) Katiba na sheria zetu vinazuia matokeo ya uchaguzi wa Rais yanayobishaniwa kupingwa mahakamani kisheria. Hivyo, uhalifu wa kiuchaguzi kuhusiana na kura za urais hauwezi kukosolewa kimahakama.

(h) Sheria na Katiba havijapiga marufuku tabia ya uhalifu wa kiuchaguzi wa kugeuza mchakato wa uchaguzi kuwa mashindano ya kujaza fomu za wagombea, jambo ambalo linazalisha wagombea wa kupigiwa “kura za ndio au Hapana,” na hivyo kukiuka kanuni ya uchaguzi wenye ushindani.

Madhara ya milima, mabonde na makorongo haya

Makorongo haya kwenye uwanja wa siasa za vyama vingi yamekuwa na madhara ya kisiasa tangu zamani, hata kabla ya hayati Magufuli hajakanyaga Ikulu. Mfano:

(a) Mwaka 2010 na 2015 enzi za Kikwete

Katika zama hizi kulikwa na “vikosi kazi” vya kukomboa majimbo yaliyo hatarini.

Kwa kila jimbo ambalo tayari lilithibitika kuanguka mikononi mwa wapinzani, vikosi hivi vilikuwa vinashirikiana na baadhi ya ma-WEO, ma-DC, ma-DAS, ma-DED, ma-DSO, ma-OCD, ma-RSO, ma-RAS na ma-RC kufanya “ukombozi.”

Mfano mmoja ni ule wa Jimbo la Karagwe mwaka 2010. Mgombea wa CCM, Gosbert Blandes Begumisa, alipoteza jimbo hilo kwa tofauti ya kura zipatazo 500. Mgombea wa Chadema alishinda.

Kikosi kazi kikafika Karagwe haraka. Kiongozi wa kikosi kazi kile alikuwa ni Afisa Usalama aliyeitwa “Haule.” Wakachakachua takwimu Blandes akatangazwa mshindi.

Niliambiwa kuwa, Kila kikosi kilikuwa kinapewa magari, fedha taslimu na wakati mwingine helikopta. Na kwa kila jimbo lililokuwa linakombolewa “malipo ya kazi maalumn” yalikuwa fedha ipatayo TZS 100,000,000 (soma milioni mia moja).

Hivyo, wajumbe wa “vikosi kazi” hivi enzi za Kikwete walifanikiwa kujenga majumba, kununua magari, na kuanzisha biashara kubwa. Kwao, wakati wa msimu wa uchaguzi wajibu wao ulikuwa ni kuiba majimbo na ulikuwa ni msimu wa “mavuno” makubwa.

View attachment 3242827
Gosbert Blandes Begumisa, Mbunge wa zamani wa Karagwe

(b) Mwaka 2019 na 2020 enzi za Magufuli

Wakati wa JPM idadi ya “vikosi kazi” iliongezeka, kiasi kwamba uhalifu wa kiuchaguzi ikawa sera rasmi ya kila jimbo la uchaguzi. Ma-WEO, ma-DC, ma-DAS, ma-DED, ma-DSO, ma-OCD, ma-RSO, ma-RAS na ma-RC wote walipewa maagizo rasmi ya kusimamia ushindi wa wagombea wa CCM.

Uliotegemewa kuwa uchaguzi haali uligubikwa na uhalifu wa kiuchaguzi wenye sura zifuatazo:
  • Kutoandikisha wapiga kura kwenye ngome za wapinzani,
  • Kuwaengua wagombea wao wengi,
  • Kutowaruhusu mawakala wa vyama vya upinzani na
  • Kutowatangaza wapinzani hata pale walipoonekana kushinda.

Hatimaye wapinzani hawakuambulia kitu.

(c) Mwaka 2024 enzi za Samia Suluhu Hasan

Wakati wa SSH utaratbu wa hayati Magufuli ulifufuliwa na kutekelezwa kikamilifu. Ma-WEO, ma-DC, ma-DAS, ma-DED, ma-DSO, ma-OCD, ma-RSO, ma-RAS na ma-RC wote walipewa maagizo rasmi ya kusimamia ushind wa wagombea wa CCM. Wapinzani hawakuambulia kitu pia.

Kwa mara nyingine tena, uliotegemewa kuwa uchaguzi haali uligubikwa na uhalifu wa kiuchaguzi wenye sura zifuatazo:
  • Kutoandikisha wapiga kura kwenye ngome za wapinzani,
  • Kuwaengua wagombea wao wengi,
  • Kutowaruhusu mawakala wa vyama vya upinzani na
  • Kutowatangaza wapinzani hata pale walipoonekana kushinda.
Tena wapinzani hawakuambulia kitu.

View attachment 3242833
Jakaya Mrisho Kikwete

V. MAPENDEKEZO YA HATUA ZINAZOPASWA KUCHUKULIWA

Kutokana na yaliyojadiliwa hapo juu, napenda kutoa wito na mapendekezo yafuatayo kwa Serikali, Bunge, Makanisa, Misikiti, Azaki, Wanazuoni wa Vyuo Vikuu na watu wote wenye mapenzi mema kwa Tanzania:

1. Kwa kuwa Tanzania sio dola ya Kiimla, wala Himaya ya Kifamle wala Taifa la Kijeshi, bali ni Dola ambayo ni Jamhuri ya Kikatiba na Kidemokrasia, inayofuata demokrasia ya vyama vingi vya siasa tangu mwaka 1992;

2. Kwa kuwa, sifa kuu ya dola ambayo ni Jamhuri ya Kikatiba na Kidemokrasia ni uchaguzi unaofanyika kwa uhuru, uchaguzi unaofanyika kwa uwazi, uchaguzi unaofanyika kwa haki na uchaguzi unaofanyika kwa ushindani wa hoja za kisera;

3. Kwa kuwa chaguzi za 2019, 2020 na 2024 zilifanyika kwa njia ya udanganyifu ulioratibiwa na matapeli wa kisiasa waliokuwa wanafuata nyayo za Hayati JMP;

4. Kwa kuwa udanganyifu wa kisiasa katika chaguzi za 2019, 2020 na 2024 ulitekelezwa na ma-WEO, ma-DED, ma-DC, ma-DAS, ma-DAS na Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya sasa;

5. Kwa kuwa udanganyifu wa kisiasa ulifanikiwa kwa sababu ya uwepo wa mifumo mibovu ya kikatiba na kisheria;

6. Kwa kuwa sheria na Katiba ya sasa vinasabaisha kuwepo kwa uwanja wa uchaguzi usio tambarare bali uwanja wenye milima, mabonde na makorongo yanayowakandamiza wagombea wa vyama vya upinzani;

7. Na kwa kuwa serikali inayoingia madarakani kwa njia za udanganyifu inakuwa haina uhalali ikiwa ni sawa na serikali zilizokuwepo enzi wa ukoloni chini ya wazungu na serikali zilizokuwepo enzi za utumwa chini ya waarabu;

8. Hivyo basi, natoa wito kwamba, Serikali na Bunge vinapaswa kuandaa vikao maalum vya Bunge kwa ajili ya kupitisha Mabadiliko ya 15 ya Katiba ya Tanzania (1977) pamoja na marekebisho stahiki ya sheria za uchaguzi ili mambo yafuatayo yawezekane kabla ya uchaguzi mkuu wa 2025:

(a) Sheria na Katiba vikataze ma-WEO, ma-DED, ma-DC, ma-DAS, ma-RAS kusimamia chaguzi.

(b) Sheria na Katiba vitamke kuwa chaguzi zote nchini zitasimamiwa na Watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliyo huru.

(c) Tume ya Taifa ya Uchaguzi iondolewe kwapani mwa Rais wa nchi kusudi iweze kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria pekee bila kuyumbishwa na maagizo kutoka Ikulu.

(d) Tume ya Taifa ya Uchaguzi iweke watumishi wake kwenye kila jimbo la uchaguzi kwa mujibu wa sheria.

(e) Katiba ikataze Rais wa nchi aliye madarakani na ambaye ni mgombea kuendelea kutekeleza majukumu yake ya Urais wakati wa maandalizi na uendeshaji wa kampeni za uchaguzi.

(f) Katiba ikataze Rais wa nchi kushika nafasi ya mwenyekiti wa chama cha siasa.

(g) Katiba na sheria zetu viruhusu matokeo ya uchaguzi wa Rais yanayobishaniwa kupingwa mahakamani kisheria.

(h) Sheria na Katiba vipige marufuku tabia ya udanganyifu wa kugeuza mchakato wa uchaguzi kugeuzwa mashindano ya kujaza fomu za wagombea.

(i) Rais Mstaafu wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, anayejua vizuri sana haya "mambo mambo" alisaidie Taifa kuondokana na hii Kero Sugu ya Uhalifu wa Kiuchaguzi, hata kama chama chake cha CCM kitangoka madarakani kwa sababu hiyo. Tanzania ni kubwa kuliko vyama vya siasa.

(j) Wanasheria wa Tanganyika Law Society watusaidie kuandaa miswada ya sheria zinazopaswa kuwasilishwa Bungeni muda wowote kwa ajili ya kutekeleza mapendekezo hapo juu. Tumechelewa sana, hivyo inabidi tukimbie.

Nawasilisha.
Mkuu, hongera kwa ushauli mzuri sana, ila ni ngumu sana kufanyika kwa sbb ya egoism ya wanasiasa.kikwete anajua vzr sana, wanamapesa mengi sana ndani nje wameificha, lakin BAdo wanangangana humo kuliibia taifa. Solulu pekee, ni nguvu ya uma ova. Hakuna wanasiasa ambae atakuja kufanya hivyo, kwa sbb ya mfumo wa mamlaka kukosa, uwadilfu na uwajibikaji kwa wananchi.
 
Jumuiya ya kimataifa na hao walimwengu hawawezi kuingilia mambo ya ndani ya dola huru.....

Tundu Lissu afahamu kuwa EU na Brussels wako "busy" kupambana na sera za kiuchumi za Marekani ya Trump" 25 % tarrifs imposed on processed goods is havoc to them".
EU na Brussels wako "busy" kujipanga na sera zisizotabirika za Trump "they are really at limbo" hawajui what will be at the corner...wanawazua kutengwa kwao kwa maneno makali kuukosa ule mwaliko wa kule Saudi Arabia.

EU na Brussels nao wanaelekea kufuata nyayo za USAID....

Zipi athari za kisiasa kwa akina Tundu Lissu ?!!

-NGO's zinakwenda kuathirika kiuchumi....baadhi ya hizo taasisi ni chanda na pete na sera za vyama visivyo na dola ikiwemo CHADEMA.

-Athari hizo hazitomuacha Robert Amsterdam ,rafiki kipenzi cha ndg.Tundu Lissu katika zile harakati zao za kuishtaki serikali ya Tanzania pale mshirika wake huyo anapokuwa hajaridhika kuona ANAYOYATAKA....

Hayati JPM(rest easy) alituandaa kisaikolojia kuwa huko NJE(ng'ambo) hatuna WAJOMBA anaowaamini na kuwategemea ndugu yetu Tundu Lissu....

Mh.Rais Donald Trump hataki "uchawa wa kibwege" kutoka mataifa ya kigeni....ni GAME CHANGER wa kuhitaji tu maslahi mapana ya nchi yake kutoka kwa WATU WENYE KUJIAMINI NA KUTHAMINI MAMBO YAO....

Leo hii ameamua kukaa mezani na Mh.Rais Vladimir Putin anayeonekana kuwa mtu mwenye kukandamiza sauti ya vyama vya upinzani nchini mwake........

"""""""""""""""""""""""""""""""""
Ushauri :

-Tuzijali na kuzithamini nchi zetu ,malengo na maoni makubwa ya kulisimamisha dola letu la JMT !
-Siamini katika demokrasia inayolazimishwa kuwa "uniform" duniani kote-kila nchi inatakiwa iwe na tafsiri ya demokrasia yake kulingana na asili ya watu wake na asili ya ardhi yake.
-Nje hatuna wajomba....tusimame wenyewe na kupita njia ya kuelekea huko tunakokutaka KIJAMII NA KIUCHUMI.

#Tanzania a sovereign state!!
#Taifa Kwanza Kwa vyovyote vile iwavyo !!
 
Hoja nzuri, utafiti mzuri, ila sio realistic!.

Uchaguzi is a process, kuna siku Uchaguzi mkuu uliwahi kusogezwa mbele kwassbabu ya kurekebisha jambo lolote?.

TAL anayo the capacity & capability yoyote kusema no reforms no election?.

Hana!.

There will be no reforms, na uchaguzi utafanyika!. TAL na Chadema has no capacity wala capability kuzuia uchaguzi usifanyike!.

Nashauri watu wenye uwezo wa kusaidia, tumsaidie TAL, tuisadie Chadema iachane na Utopian politics and come to face with the real polititcs, TAL wala Chadema hawawezi kuzuia uchaguzi mkuu.
P
....utafiti hauna REALISTISM....

Awesome ,kudos !!
 
Uchaguzi mkuu ulishafanyika na matokeo tunayo tunasubiria siku ya kutangazwa tu🐼
 
Hoja nzuri, utafiti mzuri, ila sio realistic!.

Uchaguzi is a process, kuna siku Uchaguzi mkuu uliwahi kusogezwa mbele kwassbabu ya kurekebisha jambo lolote?.

TAL anayo the capacity & capability yoyote kusema no reforms no election?.

Hana!.

There will be no reforms, na uchaguzi utafanyika!. TAL na Chadema has no capacity wala capability kuzuia uchaguzi usifanyike!.

Nashauri watu wenye uwezo wa kusaidia, tumsaidie TAL, tuisadie Chadema iachane na Utopian politics and come to face with the real polititcs, TAL wala Chadema hawawezi kuzuia uchaguzi mkuu.
P
Sikudhani kwamba umefirisika kwa hoja kiasi hiki!
 
Honger
View attachment 3242826
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akimwapisha Suleiman Abubakar Mombo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Ikulu ya Dar es Salaam , 11 Julai 2024.

I. USULI

Naandika dokezo la kisera, lenye kubeba taarifa za intelijensia ya kisiasa na kijasiriadola, kwa ajili ya kutetea rai ifuatayo:

Kwamba, kwa kuwa uhalifu wa kiuchaguzi unaowafanywa na wanasiasa matapeli wakati wa chaguzi zetu umekithiri kwa miaka 15 sasa kutokana na matobo ya kikatiba na kisheria, basi, tunapaswa kurekebisha ratiba ya uchaguzi mkuu wa 2025, kisha tufanye mageuzi ya kikatiba na kisheria, na hatimaye tufanye uchaguzi mkuu baadaye, na sio kinyume chake.

II. UTANGULIZI

Napendekeza kuanza dokezo hili kwa nukuu muhimu kuhusiana na mtazamo wa Chadema kuhusu Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika 2025.

"Mtu yeyote mwenye akili na macho ya kuona anajua kuwa chaguzi za nchi hii zimekuwa za hovyo sana na kwamba ni za hovyo kwa sababu mfumo mzima wa kiutawala wa nchi hii ni mfumo wa hovyo" -- Tundu lissu, Mwenyekiti CHADEMA.

“Hivyo, hatuzungumzii kususuia uchaguzi, hatutasusia bali tutaenda kuwaambia Watanzania, jumuiya ya kimataifa na walimwengu kwamba kama CCM na Serikali hawako tayari kufanya mabadiliko kwenye mfumo wa uchaguzi ili kuwepo chaguzi huru na haki, uchaguzi wa mwaka huu usifanyike kabisa” -- Tundu lissu, Mwenyekiti CHADEMA.

Huu ndio msimamo ulioibuliwa na Chadema kuhusu kile ambacho baadhi ya vyombo vya Habari, kama vile gazeti la Mwananchi la leo, vinakiita “Njiapanda ya Chadema Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa 2025.”

Lakini, napendekeza kwamba, kutokana na uzito wa hoja yenyewe, hasa tunapaswa kuwa tunaongelea “Njiapanda ya Watanzania Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa 2025.”

Kwa njia ya swali, “njiapanda” inayoongelewa kwenye vyombo vya habari, ndani na nje ya Chadema pia, inaweza kusomeka hivi:

Je, kwa kuzingatia uhalifu wa kiuchaguzi ambao umekuwa ukifanyika nchini Tanzania tangu 2010 kutokana na uwepo wa milima, mabonde na makorongo yaliyopo kwenye uwanja wa uchaguzi wa vyama vingi nchini Tanzania, tufumbe macho na kuendelea na utekelezaji wa ratiba ya uchaguz mkuu wa Oktoba 2025 au tusogeze ratiba hii mbele kidogo ili uchaguzi huu ufanyike baada ya mageuzi ya kikatiba na kisheria kufanyika ili kusawazisha milima, mabonde na makorongo yaliyopo?

Kutokana na utafiti nilioufanya, dokezo hili linapendekeza kwamba, tunapaswa kusogeza ratiba ya uchaguzi mkuu mbele kidogo ili uchaguzi huu ufanyike baada ya mageuzi ya kikatiba na kisheria kufanyika ili kusawazisha milima, mabonde na makorongo yaliyopo.

III. UTARATIBU WA UTAFITI (METHODOLOJIA)

Katika utafiti wangu nilikusudia kujibu maswali yafuatayo:
  1. Hoja ya Chadema kuhusu changamoto ya uhalifu wa kiuchaguzi nchini Tanzania inasema kitu gani kuhusu uwanja wa siasa za uchaguzi wa vyama vingi?
  2. Je, ni kweli kwamba kuna milima, mabonde na makorongo kwenye uwanja wa siasa za uchaguzi wa vyama vingi nchini Tanzania?
  3. Kama jawabu kwa swali la kwanza ni “ndiyo,” milima, mabonde na makorongo haya yamekuwa na madhara gani katika matokeo ya uchaguzi?
  4. Kutokana na majibu ya maswali haya mawili hapo juu, nah atua gani zichukuliwe tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa 2025.

IV. MATOKEO YA UTAFITI

Hoja ya Chadema

Maneno ya Tundu Lissu kuhusu msimamo wa kisera wa chama chake juu ya umuhimu na ulazima wa kusogeza mbele ratiba ya Uchaguzi Mkuu ujao yamenukuliwa hapo juu.

Kwa maoni yangu, haya ndio maneno yanayotueleza msimamo rasmi wa Chadema. Maneno haya yanaweza kufafanuliwa katika muundo wa hoja rasmi kama ifuatavyo:

1. Kama tungekuwa na mifumo ya kikatiba na kisheria inayowanyima wanasiasa matapeli fursa ya kufanya uhalifu wa kiuchaguzi kwenye michakaato ya chaguzi zetu basi tungekuwa na sababu nzuri ya kushiriki Uchaguzi Mkuu Ujao kabla ya kufanyika kwa mageuzi ya kimfumo.

2. Lakini, uzoefu wetu kutokana na chaguzi zote za 2010, 2015, 2019, 2020 na 2024 unaonyesha kwamba tunayo mifumo ya kikatiba na kisheria inayowapatia wanasiasa matapeli fursa ya kufanya uhalifu wa kiuchaguzi kwenye chaguzi zetu, kiasi kwamba, kwa kipindi cha miaka 15, tumekuwa tukiongozwa na serikali haramu zilizotokana na mbinu haramu.

3. Hivyo, bila kufanya mageuzi ya kuboresha mifumo ya kikatiba na kisheria inayowapatia wanasiasa matapeli fursa ya kufanya uhalifu wa kiuchaguzi kwenye chaguzi zetu hatuwezi kupata serikali halalai iliyotokana na mbinu halali.

4. Kwa mujibu wa sheria ya makosa ya jinai, kama ilivyotafsiriwa kwenye Kesi ya Abdallah Zombe na wenzake 12, Kesi ya Mahakama Kuu Na. 26/2006, kuna njia tatu za mtu mmojawapo kushiriki katika kitendo cha uhalifu wa kiuchaguzi, kabla, wakati na baada ya mchakato wa uchaguzi:
  • (a) Ama kwa mtu huyo kutekeleza uhalifu wa kiuchaguzi kwa kutumia mikono yake mwenyewe; au
  • (b) kwa mtu huyo kumpa ushirikiano wa aina yoyote mtu baki mwenye nia ya kutenda uhalifu wa kiuchaguzi na hivyo kumsaidia mtu baki kufanikisha utekelezaji wa uhalifu; au
  • (c) kwa mtu huyo kuficha taarifa muhimu zinazohitajika kwa ajili ya ama kuzuia uhalifu wa kiuchaguzi kutendeka au zinazoweza kusaidia kuwatia hatiani watu waliotenda uhalifu wa kiuchaguzi.
5. Hivyo, kama tunao wajibu wa kupigania ujio wa serikali halali iliyotokana na mbinu halali, basi, tunapaswa kupigania ujio wa serikali halali kwa kufanya yafuatayo:
  • (a) Ama kujizuia na kumshawishi kila mtu baki kujizuia kutekeleza uhalifu wa kiuchaguzi kwa kutumia mikono yake mwenyewe; au
  • (b) Kujizuia na kuwashawishi watu baki kujizuia kumpa ushirikiano wa aina yoyote mtu mwenye nia ya kutenda uhalifu wa kiuchaguzi na hivyo kumfanya mtu baki asifanikishe utekelezaji wa uhalifu; au
  • (c) Kufichua taarifa muhimu zinazohitajika kwa ajili ya ama kuzuia uhalifu wa kiuchaguzi kutendeka au zinazoweza kusaidia kuwatia hatiani watu waliotenda uhalifu wa kiuchaguzi.
6. Kwa hakika, tunao wajibu wa kisheria na kimaadili wa kupigania ujio wa serikali halali, jambo linalomaanisha kwamba tunao wajibu wa kisheria na kimaadili wa kuzuia ujio wa serikali haramu, kwa sababu zifuatazo:
  • (a) Kisheria, ibara ya 28(1) ya Katiba ya Tanzania (1977) inampa kila raia “wajibu wa kulinda, kuhifadhi na kudumisha uhuru, mamlaka, ardhi na umoja wa taifa.”
  • (b) Kimaadili, sheria ya maadili asilia inatupa jukumu la kutekeleza matendo mema na kuzuia matendo maovu, kwa kuhakikisha kwamba, kisiasa, inasimikwa serikali iliyotokana na wapiga kura halali, inayofanya kazi kwa niaba ya watu wote, na yenye kutekeleza majukumu yake kwa faida ya watu wote.
7. Kwa hiyo, raia wa Tanzania tunao wajibu wa kupigania uchaguzi utakaofanikisha ujio wa serikali halali na kupinga uchaguzi utakaofanikisha ujio wa serikali haramu. Hii ndio mantiki ya kaulimbiu isemayo kwamba “Bila Kufanya Mageuzi Kwanza Hakuna Kufanya Uchaguzi,” yaani “No Reforms, No Elections.”

Kwa ujumla, ni wazi kwamba hitimisho hili lisemalo linawaweka njiapanda baadhi ya wanachama wa Chadema wanaotaka kugombea Udiwani, Ubunge na Urais kwa tiketi ya Chadema.

Pia, ni wazi kwamba vyama vingine vinaweza kuendelea na maandalizi ya uchaguzi, maana hii sio sera yao. Na wanachadema wanaopinga sera hii wanayo hiari ya kutafuta jukwaa jingine la kisiasa lisilotambua sera hii ili wapewe fursa ya udhamini wanaoutaka.

Milima, mabonde na makorongo ya kisiasa

Tuhuma kwamba chaguzi zote za 2010, 2015, 2019, 2020 na 2024 unaonyesha kuwa tunayo mifumo ya kikatiba na kisheria inayowapatia wanasiasa matapeli fursa ya kufanya uhalifu wa kiuchaguzi kwenye chaguzi zetu, kiasi kwamba, kwa kipindi cha miaka 15, tumekuwa tukiongozwa na serikali haramu zilizotokana na mbinu haramu, nazi zinao ushahidi wa kuziunga mkono kama ifuatavyo:

(a) Uchaguzi unaosimamiwa na ma-WEO, ma-DED, ma-DC, ma-DAS, na ma-RAS unakosa uhuru, uwazi na ushindani wa kweli, kwa sababu wao ni watumishi wa serikali ya chama tawala, na hivyo kufanya uhalifu wa kiuchaguzi kwa faida ya chama tawala.

(b) Sheria za uchaguzi zinawaruhusu Watumishi wa umma kuvaa kofia za Watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakati w auchaguzi na hivyo kufungua milango ya uhalifu wa kiuchaguzi.

(c) Tume ya Taifa ya Uchaguzi imo kwapani mwa Rais wa nchi, ambaye ndiye huteua wajumbe wake, na hivyo kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria pekee kwa sababu ya kuyumbishwa na maagizo kutoka Ikulu.

(d) Tume ya Taifa ya Uchaguzi haina uwezo wa kisheria wala kifedha wa kusimika watumishi wake kwenye kila jimbo la uchaguzi kwa mujibu wa sheria.

(e) Katiba inamruhusu Rais wa nchi aliye madarakani na ambaye ni mgombea kuendelea kutekeleza majukumu yake ya Urais wakati wa kampeni za uchaguzi ilihali yeye ni Amiri Jeshi Mkuu, Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, na Msimamizi Mkuu wa Jeshi la Polisi.

Jambo hili linafungua mianya kwa baadhi ya vyombo vya ulinzi na usalama, kama vile Jeshi la Polisi na TISS, kufanya uhalifu wa kiuchaguzi ili kumsaidia “bosi” wao kushinda.

(f) Katiba inaruhusu Rais wa nchi kushika nafasi ya mwenyekiti wa chama cha siasa, kabla na wakati wa uchaguzi, na hivyo, kufungua mlango wa Rais huyu kuvitumia vyombo vya ulinzi na usalama kwa faida ya chama tawala.

(g) Katiba na sheria zetu vinazuia matokeo ya uchaguzi wa Rais yanayobishaniwa kupingwa mahakamani kisheria. Hivyo, uhalifu wa kiuchaguzi kuhusiana na kura za urais hauwezi kukosolewa kimahakama.

(h) Sheria na Katiba havijapiga marufuku tabia ya uhalifu wa kiuchaguzi wa kugeuza mchakato wa uchaguzi kuwa mashindano ya kujaza fomu za wagombea, jambo ambalo linazalisha wagombea wa kupigiwa “kura za ndio au Hapana,” na hivyo kukiuka kanuni ya uchaguzi wenye ushindani.

Madhara ya milima, mabonde na makorongo haya

Makorongo haya kwenye uwanja wa siasa za vyama vingi yamekuwa na madhara ya kisiasa tangu zamani, hata kabla ya hayati Magufuli hajakanyaga Ikulu. Mfano:

(a) Mwaka 2010 na 2015 enzi za Kikwete

Katika zama hizi kulikwa na “vikosi kazi” vya kukomboa majimbo yaliyo hatarini.

Kwa kila jimbo ambalo tayari lilithibitika kuanguka mikononi mwa wapinzani, vikosi hivi vilikuwa vinashirikiana na baadhi ya ma-WEO, ma-DC, ma-DAS, ma-DED, ma-DSO, ma-OCD, ma-RSO, ma-RAS na ma-RC kufanya “ukombozi.”

Mfano mmoja ni ule wa Jimbo la Karagwe mwaka 2010. Mgombea wa CCM, Gosbert Blandes Begumisa, alipoteza jimbo hilo kwa tofauti ya kura zipatazo 500. Mgombea wa Chadema alishinda.

Kikosi kazi kikafika Karagwe haraka. Kiongozi wa kikosi kazi kile alikuwa ni Afisa Usalama aliyeitwa “Haule.” Wakachakachua takwimu Blandes akatangazwa mshindi.

Niliambiwa kuwa, Kila kikosi kilikuwa kinapewa magari, fedha taslimu na wakati mwingine helikopta. Na kwa kila jimbo lililokuwa linakombolewa “malipo ya kazi maalumn” yalikuwa fedha ipatayo TZS 100,000,000 (soma milioni mia moja).

Hivyo, wajumbe wa “vikosi kazi” hivi enzi za Kikwete walifanikiwa kujenga majumba, kununua magari, na kuanzisha biashara kubwa. Kwao, wakati wa msimu wa uchaguzi wajibu wao ulikuwa ni kuiba majimbo na ulikuwa ni msimu wa “mavuno” makubwa.

View attachment 3242827
Gosbert Blandes Begumisa, Mbunge wa zamani wa Karagwe

(b) Mwaka 2019 na 2020 enzi za Magufuli

Wakati wa JPM idadi ya “vikosi kazi” iliongezeka, kiasi kwamba uhalifu wa kiuchaguzi ikawa sera rasmi ya kila jimbo la uchaguzi. Ma-WEO, ma-DC, ma-DAS, ma-DED, ma-DSO, ma-OCD, ma-RSO, ma-RAS na ma-RC wote walipewa maagizo rasmi ya kusimamia ushindi wa wagombea wa CCM.

Uliotegemewa kuwa uchaguzi haali uligubikwa na uhalifu wa kiuchaguzi wenye sura zifuatazo:
  • Kutoandikisha wapiga kura kwenye ngome za wapinzani,
  • Kuwaengua wagombea wao wengi,
  • Kutowaruhusu mawakala wa vyama vya upinzani na
  • Kutowatangaza wapinzani hata pale walipoonekana kushinda.

Hatimaye wapinzani hawakuambulia kitu.

(c) Mwaka 2024 enzi za Samia Suluhu Hasan

Wakati wa SSH utaratbu wa hayati Magufuli ulifufuliwa na kutekelezwa kikamilifu. Ma-WEO, ma-DC, ma-DAS, ma-DED, ma-DSO, ma-OCD, ma-RSO, ma-RAS na ma-RC wote walipewa maagizo rasmi ya kusimamia ushind wa wagombea wa CCM. Wapinzani hawakuambulia kitu pia.

Kwa mara nyingine tena, uliotegemewa kuwa uchaguzi haali uligubikwa na uhalifu wa kiuchaguzi wenye sura zifuatazo:
  • Kutoandikisha wapiga kura kwenye ngome za wapinzani,
  • Kuwaengua wagombea wao wengi,
  • Kutowaruhusu mawakala wa vyama vya upinzani na
  • Kutowatangaza wapinzani hata pale walipoonekana kushinda.
Tena wapinzani hawakuambulia kitu.

View attachment 3242833
Jakaya Mrisho Kikwete

V. MAPENDEKEZO YA HATUA ZINAZOPASWA KUCHUKULIWA

Kutokana na yaliyojadiliwa hapo juu, napenda kutoa wito na mapendekezo yafuatayo kwa Serikali, Bunge, Makanisa, Misikiti, Azaki, Wanazuoni wa Vyuo Vikuu na watu wote wenye mapenzi mema kwa Tanzania:

1. Kwa kuwa Tanzania sio dola ya Kiimla, wala Himaya ya Kifamle wala Taifa la Kijeshi, bali ni Dola ambayo ni Jamhuri ya Kikatiba na Kidemokrasia, inayofuata demokrasia ya vyama vingi vya siasa tangu mwaka 1992;

2. Kwa kuwa, sifa kuu ya dola ambayo ni Jamhuri ya Kikatiba na Kidemokrasia ni uchaguzi unaofanyika kwa uhuru, uchaguzi unaofanyika kwa uwazi, uchaguzi unaofanyika kwa haki na uchaguzi unaofanyika kwa ushindani wa hoja za kisera;

3. Kwa kuwa chaguzi za 2019, 2020 na 2024 zilifanyika kwa njia ya udanganyifu ulioratibiwa na matapeli wa kisiasa waliokuwa wanafuata nyayo za Hayati JMP;

4. Kwa kuwa udanganyifu wa kisiasa katika chaguzi za 2019, 2020 na 2024 ulitekelezwa na ma-WEO, ma-DED, ma-DC, ma-DAS, ma-DAS na Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya sasa;

5. Kwa kuwa udanganyifu wa kisiasa ulifanikiwa kwa sababu ya uwepo wa mifumo mibovu ya kikatiba na kisheria;

6. Kwa kuwa sheria na Katiba ya sasa vinasabaisha kuwepo kwa uwanja wa uchaguzi usio tambarare bali uwanja wenye milima, mabonde na makorongo yanayowakandamiza wagombea wa vyama vya upinzani;

7. Na kwa kuwa serikali inayoingia madarakani kwa njia za udanganyifu inakuwa haina uhalali ikiwa ni sawa na serikali zilizokuwepo enzi wa ukoloni chini ya wazungu na serikali zilizokuwepo enzi za utumwa chini ya waarabu;

8. Hivyo basi, natoa wito kwamba, Serikali na Bunge vinapaswa kuandaa vikao maalum vya Bunge kwa ajili ya kupitisha Mabadiliko ya 15 ya Katiba ya Tanzania (1977) pamoja na marekebisho stahiki ya sheria za uchaguzi ili mambo yafuatayo yawezekane kabla ya uchaguzi mkuu wa 2025:

(a) Sheria na Katiba vikataze ma-WEO, ma-DED, ma-DC, ma-DAS, ma-RAS kusimamia chaguzi.

(b) Sheria na Katiba vitamke kuwa chaguzi zote nchini zitasimamiwa na Watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliyo huru.

(c) Tume ya Taifa ya Uchaguzi iondolewe kwapani mwa Rais wa nchi kusudi iweze kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria pekee bila kuyumbishwa na maagizo kutoka Ikulu.

(d) Tume ya Taifa ya Uchaguzi iweke watumishi wake kwenye kila jimbo la uchaguzi kwa mujibu wa sheria.

(e) Katiba ikataze Rais wa nchi aliye madarakani na ambaye ni mgombea kuendelea kutekeleza majukumu yake ya Urais wakati wa maandalizi na uendeshaji wa kampeni za uchaguzi.

(f) Katiba ikataze Rais wa nchi kushika nafasi ya mwenyekiti wa chama cha siasa.

(g) Katiba na sheria zetu viruhusu matokeo ya uchaguzi wa Rais yanayobishaniwa kupingwa mahakamani kisheria.

(h) Sheria na Katiba vipige marufuku tabia ya udanganyifu wa kugeuza mchakato wa uchaguzi kugeuzwa mashindano ya kujaza fomu za wagombea.

(i) Rais Mstaafu wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, anayejua vizuri sana haya "mambo mambo" alisaidie Taifa kuondokana na hii Kero Sugu ya Uhalifu wa Kiuchaguzi, hata kama chama chake cha CCM kitangoka madarakani kwa sababu hiyo. Tanzania ni kubwa kuliko vyama vya siasa.

(j) Wanasheria wa Tanganyika Law Society watusaidie kuandaa miswada ya sheria zinazopaswa kuwasilishwa Bungeni muda wowote kwa ajili ya kutekeleza mapendekezo hapo juu. Tumechelewa sana, hivyo inabidi tukimbie.

VI. MAPINGAMIZI NA MAJIBU YAKE

Mapendekezo yangu hapo juu yanaweza kupingwa na watu kadhaa kwa njia mbalimbali. Baada ya mapingamizi ninayoyatarajia na ambayo nataka kuyajibu kabla hayajaibuka ni kama ifuatavyo:

Pingamizi: “Hoja ni nzuri, utafiti mzuri, ila sio realistic, kwa maana kuwa hayana uhalisia kama tukiangalia muda uliobaki. Tuachane na utopian politics”

Majibu: Naamini kuwa hoja yangu inatekelezeka kwa kuwa kazi ya kuandaa miswada kwa hati ya dharula inawezekana. Bajeti ya kuitisha Bunge maalum kwa ajili ya kupitisha miswada hiyo iko ndani ya uwezo wa serikali. Wabunge bado wapo maana Bunge halijavunjwa.

Pingamizi: “Uchaguzi is a process inayosimamiwa na serikali. Hakuuna siku serikali iliwahi kuahirisha uchaguzi mkuu kwa kuusogeza mbele kwa sababu ya kurekebisha jambo lolote.”

Majibu: Ukweli kwamba huko nyuma hatujawahi kufanya jambo Fulani hakumaanishi kuwa leo au kesho hatuwezi kufanya jambo hilo. Tukumbuke kuwa uchaguzi upo kwa ajili ya watu na sio watu kuwepo kwa ajili ya uchaguzi. Pia, ratiba ya uchaguzi sio msahafu.

Pingamizi: Tundu Lissu na Chadema yake hawana uwezo wala mamlaka ya kusema “no reforms no election” na kauli yake ikatekelezwa na serikali. Kwa hiyo, hakuna mageuzi yoyote na uchaguzi utafanyika.

Majibu: Mawazo hayo yana-personalise hoja yangu. Lissu ameanzisha hoja. Mie nimejielekeza kwenye hoja na kumweka pembeni. Tujiepushe na tatizo hilo la ARGUMENTUM AD HOMINEM. Yaani tutofautishe hoja na mleta hoja. Tufikirie juu ya uwezekano kwamba hoja ni nzuri, serikali itaweza kuipenda, Bunge litaweza kuichagamkia. Let us think positively. Namna hiyo, tutakuwa na mchango ambao sio biased sana.

Nawasilisha.
a sana mama amoni kwa weredi mkubwa uliouonyesha hapa hongera na hongera tena
 
Kagame na Museveni wana long term plans za kutawala Afrika hii.

Wanapeleka majasusi wao nje kwenye vyuo bora kwenda kujifunza na wanapeleka kwenye mission za maana ili kuwajenga kufanikisha vision za maana.

Huku Tanzania CCM wanawafundisha usalama kuiba hadi uchaguzi wa kijiji alafu utategemea tuwe na taifa imara?

Huku CCM wamewekeza kwenye uchawa tu. Sasa kwa nini Taasisi isiwe kwenye njia panda.

Kuna haja ya Watanzania wote kuungana kushinikiza reforms ambazo zitaliokoa Taifa letu na kulifanya kuwa imara in the long run.

Na hii ni watanzania wote waliopo ndani na nje ya vyombo vya ulinzi na usalama.
Viongozi wa Tanzania hawafanani na wa Rwanda na Uganda.....

Hakuna kiongozi wa Tanzania aliyepata kuongoza dola kupitia mapinduzi ya kijeshi....kwa hiyo mfano wa akina Kagame unajifia "natural death".....

Tanzania imejifunza vyema kwa mataifa yanayorugwa na wanasiasa na viongozi wa majeshi wenye tamaa ya MADARAKA MAKUBWA....

Tanzania si taifa lenye historia ya "social stratifications" kufikia kuiga siasa za nchi zenye ubaguzi wa kikabila ,kidini ,kimajimbo na kiuchumi....hoja yako ya sisi watanzania kuwaiga akina Rwanda na Uganda inahiliki "natural death".....
 
mkuu kongole kwa Policy brief murua ila nasikitika kwamba unaotaka kuwaelimisha watalitupia kabatini na kuendelea na mapambio ya kulamba asali.
Na hii ndo hatari inayoukumba nchi yetu sasa na kutufanya kuwa hatarini kumezwa na maadui wa ndani na wa nje.

Mawazo ya watanzania wenye akili na wanaofanya tafiti murua hayafanyiwi kazi badala yale wanasikilizana na kulishana ujinga na machawa wao.
 
Back
Top Bottom