Kwenye mahojiano yake Lissu hajaonesha ni kivipi CHADEMA itakuwa mbadala wa CCM

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,328
24,211
Nimeisikiliza kwa makini ile interview ya Tundu Lissu na ITV jana jumatatu saa tatu jioni. Tundu Lissu naona kama amekuwa confused. Namwonea huruma kwa jaribio la maisha yake, si hali nzuri binadamu kuipitia kamwe.

Lakini yote bin yote, Lissu hajonyesha ni kwa vipi CHADEMA inaweza kufanya tofauti kwa wananchi kuliko CCM.
Hilo nilikuwa nalisubiri kwa makini, lakini in that regards ilikuwa dissapointment.

~ Ni kweli ameonewa.
~ Ni kweli ana stahiki zake binafsi anazodai.
~ Ni kweli CHADEMA ilimimnywa kisiasa kwa wananchama wake kufungiwa abatini.

Lakini ni bora CHADEMA ijifikirie kwanza kuwa ni kitu gani kitawashauri Watanzania kuwachagua, na kuwa mbadala wa CCM. Hilo sijalisikia toka kwa Lissu au Mbowe mwenyewe.

~ Sera za uchumi.
~ Sera za Maendeleo.
~ Sera za Ulinzi na usalama.
~ Sera za Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Wasiishie eti kulia tu Katiba Mpya ya kuwapeeka Ikulu, ili na wao wakale keki ya Taifa. Wananchi hawataki eti kuichagua CHADEMA kwa vile tu Lissu na Mbowe yuko kule. Wanataka kuona FAIDA ya sera zao kubinafsi na kitaifa kwa ujumla.
 
Lissu alikuwa akijibu maswali aliyokuwa anaulizwa. Hakuwa akihutubia. Hoja yako ningeielewa iwapo ungewalaumu ITV kwa nini hawakuuliza maswali ya kumwelekez Lissu aseme ni Vipi Chadema itakuwa Mbadala wa CCM

Basi ninaona Lissu kuwa a very poor politician, not to see rare opportunities kukitangaza chama chake.

Pale ameongea mambo ya kuchumia tumbo tu n hana lolote lq maana aliloongea kwa Mtanzania kwa ujumla.

Akilipwa, na atalipwa tu stahiki zake- so what?
 
Nimeisikiliza kwa makini ile interview ya Tundu Lissu na ITV jana jumatatu saa tatu jioni.
Tundu Lissu non kama amekuwa confused.
Namwonea huruma kwa jariio la maisha yake, si hali nzuri bnadamu kuipitia kamwe.

Lakini yote bin yote, Lissu hajonyesha ni kwa vipi CHADEMA inaweza kufanya tofauti kwa wananchi kuliko CCM.
Hilo nilikuwa nalisubiri kwa makini, lakini in that regards ilikuwa dissapointment.

Ni kweli ameonewa
Ni kweli ana stahiki zake binafsi anazodai
Ni kweli CHADEMA ilimimnywa kisiasa kwa wananchama wake kufungiwa abatini

Lakini ni bora CHADEMA ijifikirie kwanza kuwa ni kitu gani kitawashauri watanzania kuwachagua, na kuwa mbadala w CCM
Hilo sijalisikia toka kwa Lissu au Mbowe mwenyewe.
Sera za uchumi
Sera za Maendeleo
Sera za Ulinzi na usalama
Sera za Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa

Wasiishie eti kulia tu Katiba Mpya ya kuwapeeka Ikulu, ili na wao wakale keki ya Taifa.

Wananchi hawataki eti kuichagua CHADEMA kwa vile tu Lissu na Mbowe yuko kule.
Wanataka kuona FAIDA ya sera zao kubinafsi na kitaifa kwa ujumla.

Muulize Farhia aliyekuwa mwongoza kipindi kwa nini hakumuuliza maswali hayo
 
Basi ninaona Lissu kuwa a very poor politician, not to see rare opportunities kukitangaza chama chake.
Pale ameongea mambo ya kuchumia tumbo tu n hana lolote lq maana aliloongea kwa Mtanzania kwa ujumla.
Akilipwa, na atalipwa tu stahiki zake- so what?
Sukuma Gang hasira zenu za kutolewa nishai na Msoga Gang mnamalizia kwa Lissu,kwisha habari yenu
 
Muulize Farhia aliyekuwa mwongoza kipindi kwa nini hakumuuliza maswali hayo
Siyo kazi ya mwana habari kueleza sera za chama husika.
Lissu missed the oppurtunity, nilishangaa anaongea tu juu ya mafao yake!
Anastahili ndiyo akini mimi au mtanzania yeyote yanamhusu vipi?
He misssed a rare oppurtunity!
 
Lakini yote bin yote, Lissu hajonyesha ni kwa vipi CHADEMA inaweza kufanya tofauti kwa wananchi kuliko CCM.
Hilo nilikuwa nalisubiri kwa makini, lakini in that regards ilikuwa dissapointment.
si matatizo yako tu kushindwa kumwelewa Lissu bali ni kwa timu mapambio yote ya CCM. Point kuu ya Lissu amesema wazi kabisa bila KATIBA MPYA tusitegemee maajabu kutoka mbinguni. Katiba iliyopo imeegemea upande mmoja ambao unaamua ufanye nini, Katiba ya sasa haifanyi check and balance.

Nchi haiwezi kupata maendeleo bila kuwa na mifumo imara & Mihimili thabiti ya dola inayojitegemea na hii yote lazima iainishwe vizuri na Katiba yetu. Kwa sasa ni Rais ndiye mwenye mwamuzi ya mwisho kwa kila jambo, sasa ukipata Rais wa ajabu ndiyo madhara kama haya tunayohangaika nayo sasa kuyarekebisha.
 
Siyo kazi ya mwana habari kueleza sera za chama husika.
Lissu missed the oppurtunity, nilishangaa anaongea tu juu ya mafao yake!
Anastahili ndiyo akini mimi au mtanzania yeyote yanamhusu vipi?
He misssed a rare oppurtunity!
Kwani ule ulikwa mkutano wa kampeni? Kazi haijaanza ile ni introduction tu mnaanza kupiga kelele. Hakuna hata siku mtaona jema toka kwa Lissu na Chadema
 
Siyo kazi ya mwana habari kueleza sera za chama husika.
Lissu missed the oppurtunity, nilishangaa anaongea tu juu ya mafao yake!
Anastahili ndiyo akini mimi au mtanzania yeyote yanamhusu vipi?
He misssed a rare oppurtunity!
Anazo opportunity za kutosha kuelezea hayo

Ww endelea kumfatilia utafaidi vingi kutoka kwake

Amesharudi nyumbani.
 
Basi ninaona Lissu kuwa a very poor politician, not to see rare opportunities kukitangaza chama chake.
Pale ameongea mambo ya kuchumia tumbo tu n hana lolote lq maana aliloongea kwa Mtanzania kwa ujumla.
Akilipwa, na atalipwa tu stahiki zake- so what?
Ni ngumu sana kuridhishwa na kila interview ya TL..
Wakati wew unataka hili yupo mwingine anataka lile...

Alafu kutangaza namna chama chako kitafanya kikichukua Dola, ni sawa na kupiga kampeni, sas unajiuliza huu ni muda wake??

Nadhani TL na chadema wanao muda wa kutosha kuishawishi jamii iwaamini na kuwachagua pindi uchaguzi utapofika.

Hakuna mageuzi ya overnight hasa kwa watu ambao hawajabanwa na dhiki kwa 100% kwenye maisha yao
 
si matatizo yako tu kushindwa kumwelewa Lissu bali ni kwa timu mapambio yote ya CCM. Point kuu ya Lissu amesema wazi kabisa bila KATIBA MPYA tusitegemee maajabu kutoka mbinguni...
Watu msioweza kufikiri kwa upeo mpana mna matatizo.

Hata leo tukipata Katiba Mpya -so what?

Kwa mathalani sema CHADEMA imeshinda -so what?

Uchumi unaendesha vile vile, Maendeleo mtazamo ule ule, Elimu msimamo ule ule na mambo ya kuendesha serikali yako vile vile, sema sasa CHADEMA wako madarakani na wanasindikizwa na misafara ya magari 100.

Think outside the Katiba Mpya Box!
 
Kwa risasi zile hata ingekuwa mm umakini wangu ungepotea lisu siyo yule wa mwanzoni kbsa lissu huyu Ni tofauti Sana anaonekana kuwa na mfadhaiko mkubwa hata kuongea yake inatatiza kidgo

Anyway wale waburundi walio jaribu kumuuwa naamini wote kwa Sasa ni marehemu moja kwa moha

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom