Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 118,182
- 219,328
Mtego alioutega Lissu wa KATIBA MPYA , KATIBA MPYA , KATIBA MPYA kama una akili ya kawaida huwezi kuelewa .Nimeisikiliza kwa makini ile interview ya Tundu Lissu na ITV jana jumatatu saa tatu jioni. Tundu Lissu naona kama amekuwa confused. Namwonea huruma kwa jaribio la maisha yake, si hali nzuri binadamu kuipitia kamwe.
Lakini yote bin yote, Lissu hajonyesha ni kwa vipi CHADEMA inaweza kufanya tofauti kwa wananchi kuliko CCM.
Hilo nilikuwa nalisubiri kwa makini, lakini in that regards ilikuwa dissapointment.
~ Ni kweli ameonewa.
~ Ni kweli ana stahiki zake binafsi anazodai.
~ Ni kweli CHADEMA ilimimnywa kisiasa kwa wananchama wake kufungiwa abatini.
Lakini ni bora CHADEMA ijifikirie kwanza kuwa ni kitu gani kitawashauri Watanzania kuwachagua, na kuwa mbadala wa CCM. Hilo sijalisikia toka kwa Lissu au Mbowe mwenyewe.
~ Sera za uchumi.
~ Sera za Maendeleo.
~ Sera za Ulinzi na usalama.
~ Sera za Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Wasiishie eti kulia tu Katiba Mpya ya kuwapeeka Ikulu, ili na wao wakale keki ya Taifa. Wananchi hawataki eti kuichagua CHADEMA kwa vile tu Lissu na Mbowe yuko kule. Wanataka kuona FAIDA ya sera zao kubinafsi na kitaifa kwa ujumla.
Utaratibu wa kuongoza nchi hautokani na utashi wa vyama , unawekwa ndani ya Katiba ya Nchi , mle itajulikana ukivurunda utafanywaje , Lissu angekuwa katibu mwenezi wa Chadema tungemwambia asome sera za chama .
Lakini huyu ni Presidential Material