Kweli Max Ndiye Yeye: Kwanini Sina Hofu

Kweli Max Ndiye Yeye: Kwanini Sina Hofu

Tuache unafiki

Humu jamiiforums udikteta kwenda mbele watu wanapigwa ban bila kujulishwa ssababu moderators wamekuwa miungu watu wana moderate kutokana na moods zao

Sasa Leo kibao kimegeuka mnalalamika?

Mshajiuliza why members hawapewi options za kukuta threads zao walizoanzisha? Kwa nini JF inataka. Kuhodhi kila kitu?

Au why hakuna namna ya members kujitoa au kujifuta uanachama?

Uongozi haijulikani ni akina nani maana kila mtu anaclaim kuwa yeye ni kiongozi na mwanzilishi na shareholder lakini mbona hakuna shareholders agreements au leadership elections na objectives na strategic plan??

We complain about govt repression huku ndani tunarepress members
2b5086174c23fe3d53b44dd4bcc3abbb.jpg

Haya maswali yako yote majibu yake yamo humu humu JF, tatizo unataka kujua kila kitu kwa muda mafupi.
 
Niseme tu kuwa Max aachiliwe bila masharti y0yote ndani ya masaa 24 yajayo, kinyume cha hivyo mtatulazimisha waanzilishi hasa wa mtandao huu kufunga JamiiForums Tanzania na ofisi zake na kuurudisha gizani na hivyo siyo tu kuwakosesha hata nafasi ya kuwafikia wananchi wengi ambao wanatumia mtandao huu kupata habari kwa usahihi ndani na nje ya nchi lakini pia kutoa nafasi kwa watoa maoni wa ndani ya serikali kuwafikia wapiga kura na wananchi.

Nadhani bado hatujafikia huko. Kwa masilahi ya 360.000 members nadhani ukiangalia kwa mapana tunazungumzia 3m ya members ambao hawakosi kuchungulia JF.
Mkuu MMM bado JF ni taasisi mbadala kwa ustawi wa Tanzania kufikia ndoto ya Maendeleo kwa leo na Kesho. Ni muhimu tumtakie mwenzetu Max -Afya njema na Moyo wa kutokukata Tamaa.
 
Hivi kuna namna yoyote ya kufikisha ishu hii ya Bem kwenye media za nje kama cnn,bbc na aljazira?
 
Ndio ni serikali yenu na nchi yenu, ila mkumbuke na sisi tunahaki yetu kwenye serikali yenu na nchi yenu.!
serikali yenu wewe na nani bila cc?
tuoneshe sisi wana JF serikali nyingine tofauti na yako basi!
 
You can fool some people for some times....but you can not fool all the people at all times - Bob Marley
[HASHTAG]#free[/HASHTAG] Maxence Mello
 
Na. M. M. Mwanakijiji

  • Mimi ni Miongoni mwa Waasisi wa JF
  • Uhuru wa Maoni na Kujieleza Usitishiwe
  • Max Mello Aachiliwe Ndani ya Masaa 24
  • Kuungwa Mkono Haina Maana Kukubaliwa Lolote

Kwanza kabisa niseme kuwa mimi ni mmoja wa waanzilishi wa mtandao huu. Siyo tu miongoni mwa wanachama wa mwanzo lakini pia miongoni mwa watu waliokaa na kufanya majadiliano ya kuihamisha jukwaa la mijadala tangu ikiwa bcstimes na baadaye Jambo Forums na hatimaye Jamiiforums.

Tulihamisha kutoka bcstimes kwa sababu haikuwa na facilities na uwezo tunaoutaka kuweka kuisimamia. Tulihama kutoka Jambo Forums hadi JamiiForums kufuatia kukamatwa kwa Max na Mike mwezi Februari 2008 na mtu mmoja (alikuwa kada wa chama fulani) kuchukua jina la Jambo Forums na kugoma kuturudishia! Ili tusipotee sana tukaamua kuiita JamiiForums (ili kubakia na initial zile zile za JF - ikiwa ni sababu mojawapo).

Mimi ndiye mbunifu wa msemo wa "where we dare (to) talk openly".

Walipokamatwa kina Max nilienda hadi BBC na kujenga hoja ya kuwa uhuru wa maoni haulindi maoni mazuri tu nayale tunayoyapenda, bali unalinda hasa maoni mabovu, tusiyoyapenda na nikasema kuwa "unalinda hata maoni ya kijinga"! Ukweli huu wa miaka nane nyuma naamini bado ni ukweli uliopo sasa.

Max na wenzetu waliopo nyumbani walichukua jukumu la kujaribu kurasimisha mtandao huu kuwa kampuni ili sehemu yake moja isiwe inafanywa gizani na kuweka taratibu mbalimbali za kuhakikisha uhuru wa maoni unakuwepo na watu wanaotaka kutumia majina halisi wanafanya hivyo -wakati ule karibu wote tulikuwa tunatumia majina ya kiuandishi (pen names). Lakini pia hatukutaka kuzuia watu wengine kuendelea kuandika under pseudonyms. Sababu yake ni kuwa ili kuweza kupata habari, kuchochea mijadala na kuwapatia Watanzania habari kwa undani na maoni bila kuogopa adhabu basi tuliacha iwe hivyo.

Hili lilisaidia mtandao huu kufichua baadhi ya kashfa nyingi na mbalimbali bila ya watu kuhofia kujulikana kwani hadi hivi sasa Tanzania haina Sheria ya kumlinda mfichua uovu! (whistle blower protection act). Hivyo, ni kwa kutumia mitandao hii na namna ya usiri ndio maana hili la kuwa na pen names limeendelea na ninaamini litaendelea kwa muda mrefu ujao.

Ni kwa sababu hiyo kwanza sijashtushwa na kukamatwa kwa Max wala kushtushwa na ujio wa sheria ya Cybercrime. Vyote hivi ni vitu ambavyo nilivitarajia bila kujali nani angekuwa mshindi mwaka jana. Vitu hivyo vingekuwa tofauti tu kama upinzani wa kweli ungeshinda mwaka jana. Hilo pembeni.

Kumkamata Max na kujaribu kumlazimisha au kuilazimisha JamiiForums kutoa majina ya watu ili kufanya kazi ya serikali iwe rahisi au kuwafanyia serikali kazi ambayo wao wanapaswa kuifanya ni dalili ya uzembe uliopitiliza. Hili nililsema mwaka 2008 na nalirudia tu tena. Serikali ina jukumu la kufanya kazi yake lakini ni lazima ijaribu kufanya kazi yake kwa weledi wake wote.

Serikali ina uwezo (wa kifedha na kiutaalam) wa kufuatilia mawasiliano ya watu kwa mujibu wa sheria. Haiwezekani mtu aamue tu kutaka jina la fulani kwenye mtandao kwa sababu tu huyo fulani kaandika habari au kitu ambacho labda serikali inaamini wananchi hawakupaswa kukijua (kiwe cha kweli au la).

Lakini kubwa ni kuwa JF ina wanachama 360,000 hivi, sidhani kuna mtu yeyote anaamini Max anaweza kujua majina yote ya kweli au ya kiuandishi ya wanachama wote. Hata mtu akitumia jina la John Marko, ni vigumu kujua kama kweli ni jina lake kulinganisha na mtu anayejiita "Kifuu cha Nazi". Inawezekana anayeitwa Kifuu cha Nazi ndilo jina lake kweli na yule anayejiita John Marko ndiye anatumia jina la kiuandishi!

Kubwa zaidi hata hivyo ni kuwa badala ya kuhangaika na "nani kasema nini" ni vizuri serikali ihangaike na "Nani kafanya nini"! Lakini kama tunataka kufuatilia "nani kasema nini" ni vizuri zaidi kujali "nini kimesemwa na nani" na hivyo kuangalia na kutoa majibu muafaka na yenye kuridhisha. Tatizo la maswali ni kuwa hata ukamate wote wanaoyauliza kwa kadiri kwamba huyajibu maswali ya, maswali yataendelea kuulizwa tu hata na wale wasiyoyauliza hadharani!.

Hivyo basi, ni maoni yangu na naweza kusema ni wito wangu kuwa vitisho kwa vyombo vya habari, mitandao ya kijamii au watu wanaoikosoa havina sababu ya msingi na Max Mello aachiliwe bila masharti yeyote na kuwa serikali imwombe radhi kwa usumbufu na kutambua mchango mkubwa JamiiForums imeutoa kwa Tanzania na kwa tasnia ya habari kuanzia 2006.

Niseme tu kuwa Max aachiliwe bila masharti y0yote ndani ya masaa 24 yajayo, kinyume cha hivyo mtatulazimisha waanzilishi hasa wa mtandao huu kufunga JamiiForums Tanzania na ofisi zake na kuurudisha gizani na hivyo siyo tu kuwakosesha hata nafasi ya kuwafikia wananchi wengi ambao wanatumia mtandao huu kupata habari kwa usahihi ndani na nje ya nchi lakini pia kutoa nafasi kwa watoa maoni wa ndani ya serikali kuwafikia wapiga kura na wananchi.

Haki ya Watanzania kupata habari, kujieleza kwa uhuru na kutoa maoni ni kubwa zaidi kuliko hata misimamo yetu baadhi yetu ya kuunga mkono mabadiliko ambayo tumeyaona. Kama nilivyowahi kusema kuna gharama ambayo watu wanaweza kukubali kuilipa kwa ajili ya mabadiliko wanayoyataka, lakini kuna gharama nyingine hailipiki.

MMM
heshima yako mkuu nimefurahi kuona uwepo wako na kauli yako umeelezea real fact
 
Siamini km Mwanakijijj anaweza kuunga mkono ccm na km kweli alifanya hivo ntajaribu kumpuuza.....Aliposema "upinzani wa kweli" sijui amemaanisha nn[/SIZE]
pale aliposema upinzani wa kweli kuna controductary, fuatilia upya uone, japo siyo hoja ya uzi huu
 
Kuna watu humu ndani hamjajua nchi hii hasa ccm.watawala wa ccm kila wanapokaa iwe lumumba au ikulu uwa wanajiuliza nn sababu ya kura zao kushuka na idadi kubwa ya watu kuichukia ccm.Moja ya sababu kubwa ni mitandao ya kijamii,magazeti na ndio maana sheria zinakuwa kali sana kila kukicha.wao kwa imani yao na tafiti zao za wataalamu wa rumumba wamezunguka nchi nzima wanajua kuwa ili waendelee kutawala vema ni kufungia vyombo vyote vya habari na kuweka sheria kali.na ndio maana mkuu wa nchi aliwai tamka kuwa anatamani kuzima mitandao ya kijamii ili siku anafungua watu waone nn kinafanyika utadhani mitandao ndonitaonyesha sisi tumelala
kama ana jeuri azime vyote!

Azime Tv zote,
Azime Simu zote,
Azime Mordem zote
Azime na Redio zote
Halafu Tuone hii inakuwa nchi ya aina gani
 
Nakupata, Mkuu. Ila kumbuka kwamba JPM siyo tu ni Rais bali ni Mwenyekiti wa chama chake cha CCM. Mwenyekiti wa Chama ndiye "top" kwenye chama na ana uwezo wa kuwaambia hao "washauri" wake: asanteni kwa ushauri ila hili nitafanya na lile sitafanya. He has that power; kama tulivyoshuhudia hivi juzi akienda kinyume na maamuzi ya wasaidizi wake waliokuwa wametoa amri ya kuwaondoa wamachinga huko kanda ya ziwa, lakini yeye akaja na "move" ya tofauti kama kiongozi Mkuu akatengua hayo maamuzi. Kwahiyo mimi bado nipo palepale. Tatizo ni yeye wala siyo wasaidizi wake au chama. After all, yeye ndiye kiongozi mkuu wa chama chake.
Kweli kabisa rais anaweza sema ili likawa kutokana na madaraka yake.lkn suala kinakuja na ambalo hatulijui sana.ccm kama chama kinapoamuaga au kukubaliana hata rais ana maamuzi,maana uwa wanaangalia kunusuru chama chao ambacho wao uona ndo kinawapa maisha kupitia kupewa mamlaka au kupora ushindi.Angalia suala la katiba mpya kikwete alionyesha nia ya kutaka serikali 3,kama chama kilivyoona kuwa serikali 3 italeta kudondoka kwa chama chao ndo hatima ilipofikia.Pia kule ccm ukienda tofauti hata uwe rais wako tayari kukunyanganya kadi yao.na ndio maana magu anasema nyie ndo mmenifanya niwe rais bila ccm asingekuwa so lazima atii maagizo ya chama.Magufuri anatumia maagizo mengi ya chama.nashindwa hata niendelee kusema nn,ishu ni ccm,kuna kautafiti kalifanyika wakajua wakifanya haya tunayoyalilia na kulalamikia ndo wataendelea kutawala maana wanajua na kuamini kuwa kushuka kwa umaarufu na kura kwa chama chao mojawapo ni haya.wanajua wanachofanya.Tuombe mungu atuepushie na mabaraaa haya
 
Mkuu kuna point iliyotutofautisha. Angekuwa mnafiki asingemgeuka JPM. Ukiwa huru bila unafiki unapaswa kusimama na ukweli. Ndio maana Chadema walipokuja na ujinga tuliohuru tukawageuka bila kusita ....na sasa serikali inafanya ukuda kama huu tunaikosoa bila soni. Hata wewe lazima ufike point uwe huru kukosoa bila kujali chochote ....usitetee uchadema tu bila kukosoa na mwisho kujenga chama cha upinzani cha kudumu ....
Naunga mkono hoja yako!

kuna tofauti kati ya upinzani wakweli na uongozi mahili

kama yule unaempenda amefanya vibaya mkosoe, maana hukumpenda kwa mabaya, na kma habadiliki una haki na uhuru wa kuachana nae
 
Tuache unafiki

Humu jamiiforums udikteta kwenda mbele watu wanapigwa ban bila kujulishwa ssababu moderators wamekuwa miungu watu wana moderate kutokana na moods zao

Sasa Leo kibao kimegeuka mnalalamika?

Mshajiuliza why members hawapewi options za kukuta threads zao walizoanzisha? Kwa nini JF inataka. Kuhodhi kila kitu?

Au why hakuna namna ya members kujitoa au kujifuta uanachama?

Uongozi haijulikani ni akina nani maana kila mtu anaclaim kuwa yeye ni kiongozi na mwanzilishi na shareholder lakini mbona hakuna shareholders agreements au leadership elections na objectives na strategic plan??

We can't complain about govt repression huku ndani tunarepress members
 
Na. M. M. Mwanakijiji

  • Mimi ni Miongoni mwa Waasisi wa JF
  • Uhuru wa Maoni na Kujieleza Usitishiwe
  • Max Mello Aachiliwe Ndani ya Masaa 24
  • Kuungwa Mkono Haina Maana Kukubaliwa Lolote

Kwanza kabisa niseme kuwa mimi ni mmoja wa waanzilishi wa mtandao huu. Siyo tu miongoni mwa wanachama wa mwanzo lakini pia miongoni mwa watu waliokaa na kufanya majadiliano ya kuihamisha jukwaa la mijadala tangu ikiwa bcstimes na baadaye Jambo Forums na hatimaye Jamiiforums.

Tulihamisha kutoka bcstimes kwa sababu haikuwa na facilities na uwezo tunaoutaka kuweka kuisimamia. Tulihama kutoka Jambo Forums hadi JamiiForums kufuatia kukamatwa kwa Max na Mike mwezi Februari 2008 na mtu mmoja (alikuwa kada wa chama fulani) kuchukua jina la Jambo Forums na kugoma kuturudishia! Ili tusipotee sana tukaamua kuiita JamiiForums (ili kubakia na initial zile zile za JF - ikiwa ni sababu mojawapo).

Mimi ndiye mbunifu wa msemo wa "where we dare (to) talk openly".

Walipokamatwa kina Max nilienda hadi BBC na kujenga hoja ya kuwa uhuru wa maoni haulindi maoni mazuri tu nayale tunayoyapenda, bali unalinda hasa maoni mabovu, tusiyoyapenda na nikasema kuwa "unalinda hata maoni ya kijinga"! Ukweli huu wa miaka nane nyuma naamini bado ni ukweli uliopo sasa.

Max na wenzetu waliopo nyumbani walichukua jukumu la kujaribu kurasimisha mtandao huu kuwa kampuni ili sehemu yake moja isiwe inafanywa gizani na kuweka taratibu mbalimbali za kuhakikisha uhuru wa maoni unakuwepo na watu wanaotaka kutumia majina halisi wanafanya hivyo -wakati ule karibu wote tulikuwa tunatumia majina ya kiuandishi (pen names). Lakini pia hatukutaka kuzuia watu wengine kuendelea kuandika under pseudonyms. Sababu yake ni kuwa ili kuweza kupata habari, kuchochea mijadala na kuwapatia Watanzania habari kwa undani na maoni bila kuogopa adhabu basi tuliacha iwe hivyo.

Hili lilisaidia mtandao huu kufichua baadhi ya kashfa nyingi na mbalimbali bila ya watu kuhofia kujulikana kwani hadi hivi sasa Tanzania haina Sheria ya kumlinda mfichua uovu! (whistle blower protection act). Hivyo, ni kwa kutumia mitandao hii na namna ya usiri ndio maana hili la kuwa na pen names limeendelea na ninaamini litaendelea kwa muda mrefu ujao.

Ni kwa sababu hiyo kwanza sijashtushwa na kukamatwa kwa Max wala kushtushwa na ujio wa sheria ya Cybercrime. Vyote hivi ni vitu ambavyo nilivitarajia bila kujali nani angekuwa mshindi mwaka jana. Vitu hivyo vingekuwa tofauti tu kama upinzani wa kweli ungeshinda mwaka jana. Hilo pembeni.

Kumkamata Max na kujaribu kumlazimisha au kuilazimisha JamiiForums kutoa majina ya watu ili kufanya kazi ya serikali iwe rahisi au kuwafanyia serikali kazi ambayo wao wanapaswa kuifanya ni dalili ya uzembe uliopitiliza. Hili nililsema mwaka 2008 na nalirudia tu tena. Serikali ina jukumu la kufanya kazi yake lakini ni lazima ijaribu kufanya kazi yake kwa weledi wake wote.

Serikali ina uwezo (wa kifedha na kiutaalam) wa kufuatilia mawasiliano ya watu kwa mujibu wa sheria. Haiwezekani mtu aamue tu kutaka jina la fulani kwenye mtandao kwa sababu tu huyo fulani kaandika habari au kitu ambacho labda serikali inaamini wananchi hawakupaswa kukijua (kiwe cha kweli au la).

Lakini kubwa ni kuwa JF ina wanachama 360,000 hivi, sidhani kuna mtu yeyote anaamini Max anaweza kujua majina yote ya kweli au ya kiuandishi ya wanachama wote. Hata mtu akitumia jina la John Marko, ni vigumu kujua kama kweli ni jina lake kulinganisha na mtu anayejiita "Kifuu cha Nazi". Inawezekana anayeitwa Kifuu cha Nazi ndilo jina lake kweli na yule anayejiita John Marko ndiye anatumia jina la kiuandishi!

Kubwa zaidi hata hivyo ni kuwa badala ya kuhangaika na "nani kasema nini" ni vizuri serikali ihangaike na "Nani kafanya nini"! Lakini kama tunataka kufuatilia "nani kasema nini" ni vizuri zaidi kujali "nini kimesemwa na nani" na hivyo kuangalia na kutoa majibu muafaka na yenye kuridhisha. Tatizo la maswali ni kuwa hata ukamate wote wanaoyauliza kwa kadiri kwamba huyajibu maswali ya, maswali yataendelea kuulizwa tu hata na wale wasiyoyauliza hadharani!.

Hivyo basi, ni maoni yangu na naweza kusema ni wito wangu kuwa vitisho kwa vyombo vya habari, mitandao ya kijamii au watu wanaoikosoa havina sababu ya msingi na Max Mello aachiliwe bila masharti yeyote na kuwa serikali imwombe radhi kwa usumbufu na kutambua mchango mkubwa JamiiForums imeutoa kwa Tanzania na kwa tasnia ya habari kuanzia 2006.

Niseme tu kuwa Max aachiliwe bila masharti y0yote ndani ya masaa 24 yajayo, kinyume cha hivyo mtatulazimisha waanzilishi hasa wa mtandao huu kufunga JamiiForums Tanzania na ofisi zake na kuurudisha gizani na hivyo siyo tu kuwakosesha hata nafasi ya kuwafikia wananchi wengi ambao wanatumia mtandao huu kupata habari kwa usahihi ndani na nje ya nchi lakini pia kutoa nafasi kwa watoa maoni wa ndani ya serikali kuwafikia wapiga kura na wananchi.

Haki ya Watanzania kupata habari, kujieleza kwa uhuru na kutoa maoni ni kubwa zaidi kuliko hata misimamo yetu baadhi yetu ya kuunga mkono mabadiliko ambayo tumeyaona. Kama nilivyowahi kusema kuna gharama ambayo watu wanaweza kukubali kuilipa kwa ajili ya mabadiliko wanayoyataka, lakini kuna gharama nyingine hailipiki.

MMM
Kama kuna jema au baya lolote litatukuta kwa miaka hii mitano you have equal share
 
Yote haya.ni ishu ya maiti saba ruvu.tumembana sana.ndo maana roho inamuuma.nchemba.
 
For sure mwigulu anahusika na hili, hivyo apigwe 'life ban' humu jamvin
Sijasoma post yako mwanzo lakini tumewaza pamoja.[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15]
 
Back
Top Bottom