Kweli Max Ndiye Yeye: Kwanini Sina Hofu

Kweli Max Ndiye Yeye: Kwanini Sina Hofu

Ni kwa sababu hiyo kwanza sijashtushwa na kukamatwa kwa Max wala kushtushwa na ujio wa sheria ya Cybercrime. Vyote hivi ni vitu ambavyo nilivitarajia bila kujali nani angekuwa mshindi mwaka jana. Vitu hivyo vingekuwa tofauti tu kama upinzani wa kweli ungeshinda mwaka jana. Hilo pembeni. MMM

Baada ya kusoma hiyo statement yako hapo juu, nimegundua kwamba wewe ni puppet propagandist tu. Umeguswa tu na UOVU anaofanyiwa Max Mello, kwasababu tu unamfahamu. Lakini una shauku kubwa huo UOVU uendelewa kufanyiwa watu wengine usiowafahamu na ambao pia wana mtizamo tofauti na wewe, kwa kutumia hizo sheria mbovu za cyber crime ie the root causes.

Pia umejitwisha uwezo wa ki-muungu wa kujua kwamba hata wangekuja wapinzani basi nao wangepitisha hizo sheria mbovu. Kitu cha kujiuliza ipi BUSARA kati ya Kumkataa mtu ambaye tayari anakufanyia UOVU na kujaribu mtu mwingine ambaye hujui kwamba atakufanyia UOVU au MAZURI? Be the Juror yourself.

Kuna msemo unaosema hivi insanity is to repeat the same thing expecting different results. BTW, kukiri kwako kwamba na wewe ni muanzilishi wa JF na pia ni shareholder wa JF, those "big brothers" are now after your neck, mark my words.
 
we mzee tulisha kukataa hatupotezi kumbu kumbu we siyo mtu wa kuaminika milele we na pole pol hamna tofauti ndani ya hii nchi ni suala la muda tu! bora ............ msituchanganye kabisa
 
Upo sawa katika yote uliyoeleza kasoro hili tu:

Niseme tu kuwa Max aachiliwe bila masharti y0yote ndani ya masaa 24 yajayo, kinyume cha hivyo mtatulazimisha waanzilishi hasa wa mtandao huu kufunga JamiiForums Tanzania na ofisi zake na kuurudisha gizani na hivyo siyo tu kuwakosesha hata nafasi ya kuwafikia wananchi wengi ambao wanatumia mtandao huu kupata habari kwa usahihi ndani na nje ya nchi lakini pia kutoa nafasi kwa watoa maoni wa ndani ya serikali kuwafikia wapiga kura na wananchi.


Hii ndiyo nia ya kumkamata Melo. Tusiruhusu JF ifungwe kwa namna yoyote ile.
 
kwny 2015 election JF ilitumika sana kuipigia chapuo CCM, hata fungu walivuta kuendesha shughuli zao kiurahisi baada yakuonekana ukawa wananguvu sana kwny mitandao. Nyuzi zikawa zinatupiwa strategically kuwabeba wale mabwana..na wao bila kujua hii zambi ya kula mtoto wa mtu inazunguka sasa wamemaliza wengine wamehamia kwao..vumilieni tu simlikula kubalini kuliwa na nyinyi!.. pole kaka max ukitoka huko na wewe uje utoe povu kuwahusu siwamemwaga mboga ,mwaga ugali!..
 
Tuendelee kuisifu tu serikali hii ya awamu ya tano. Si ndio huyu Mwanakijiji aliyeona ni bora ccm ishinde? Sasa tusilalamike. Hiyo lugha ya "upinzani wa kweli" haina tija kwa taifa letu, la msingi lilikuwa ccm itoke. Tuache tu tupate matokeo ya kuunga mkono ccm. Bado kwa staili hii kila mtu atafikiwa, ni zamu mpaka tuisome namba.

Toka mwanzo tulitoa Tahadhari kuwa tusimchekee mtu anayefanya mambo yake kutokana na kichwa chake na kusigina katiba, kanuni, sheria na taratibu lakini tulibezwa kwa kisingizio wacha Nchi inyooshwe tupo kwenye kipindi cha mpito.

Udikteta ni kama kula nyama ya mtu, ukishauonja tu basi ni lazima utanogewa na utatamani kuendelea kuchinja watu zaidi ili kupata kitoweo zaidi.

Hakika tukiendelea kukaa kimya tutafikiwa wote nakuambia, tusikubali kuendelea kusomeshwa namba kwa misingi ya uvunjifu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni.
 
Mwanakijiji wewe una sehemu ya haya yanayoendelea. Pale wapinzani walipolalamika kuwa serikali hii inatupeleka kwenye udikteta, wewe ulikenua meno aisee, nakuchukia kweli: nisamehe tuu, maana siwezi kuzuia chuki yangu kwako. Ulitetea madudu ya JPM tangu mwanzo ya ukandamizaji wa demokrasia nchini. Aisee kwa dhati ya moyo wangu nakuchukia wewe, umekuwa sehemu ya haya tuliyofikia na tunakoenda, huwezi kujivua haya. I hate you. Kutoka kuwa mtu niliyependa kumsoma makala zake mpaka kuwa mtu ninayekuchukia. NAKUCHUKIA NA VIONGOZI WAKANDAMIZI WA CCM ULIOUNGANA NAO KUTUUMIZA. I HATE YOU
 
Ni hatari kuzuia watu wasiseme chochote kuhusu namna wanavyo tawaliwa...Iko wapi Lybia ambayo wananchi wake walifaidi kila kitu kutoka kwa utawala lakini wakanyimwa kuongea, wakaamua kuingiza taifa kwenye shida kubwa! Acheni watu waongee na fanyieni kazi yale mnayoona ni kweli na ya uongo yaacheni.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

  • Mimi ni Miongoni mwa Waasisi wa JF
  • Uhuru wa Maoni na Kujieleza Usitishiwe
  • Max Mello Aachiliwe Ndani ya Masaa 24
  • Kuungwa Mkono Haina Maana Kukubaliwa Lolote

Kwanza kabisa niseme kuwa mimi ni mmoja wa waanzilishi wa mtandao huu. Siyo tu miongoni mwa wanachama wa mwanzo lakini pia miongoni mwa watu waliokaa na kufanya majadiliano ya kuihamisha jukwaa la mijadala tangu ikiwa bcstimes na baadaye Jambo Forums na hatimaye Jamiiforums.

Tulihamisha kutoka bcstimes kwa sababu haikuwa na facilities na uwezo tunaoutaka kuweka kuisimamia. Tulihama kutoka Jambo Forums hadi JamiiForums kufuatia kukamatwa kwa Max na Mike mwezi Februari 2008 na mtu mmoja (alikuwa kada wa chama fulani) kuchukua jina la Jambo Forums na kugoma kuturudishia! Ili tusipotee sana tukaamua kuiita JamiiForums (ili kubakia na initial zile zile za JF - ikiwa ni sababu mojawapo).

Mimi ndiye mbunifu wa msemo wa "where we dare (to) talk openly".

Walipokamatwa kina Max nilienda hadi BBC na kujenga hoja ya kuwa uhuru wa maoni haulindi maoni mazuri tu nayale tunayoyapenda, bali unalinda hasa maoni mabovu, tusiyoyapenda na nikasema kuwa "unalinda hata maoni ya kijinga"! Ukweli huu wa miaka nane nyuma naamini bado ni ukweli uliopo sasa.

Max na wenzetu waliopo nyumbani walichukua jukumu la kujaribu kurasimisha mtandao huu kuwa kampuni ili sehemu yake moja isiwe inafanywa gizani na kuweka taratibu mbalimbali za kuhakikisha uhuru wa maoni unakuwepo na watu wanaotaka kutumia majina halisi wanafanya hivyo -wakati ule karibu wote tulikuwa tunatumia majina ya kiuandishi (pen names). Lakini pia hatukutaka kuzuia watu wengine kuendelea kuandika under pseudonyms. Sababu yake ni kuwa ili kuweza kupata habari, kuchochea mijadala na kuwapatia Watanzania habari kwa undani na maoni bila kuogopa adhabu basi tuliacha iwe hivyo.

Hili lilisaidia mtandao huu kufichua baadhi ya kashfa nyingi na mbalimbali bila ya watu kuhofia kujulikana kwani hadi hivi sasa Tanzania haina Sheria ya kumlinda mfichua uovu! (whistle blower protection act). Hivyo, ni kwa kutumia mitandao hii na namna ya usiri ndio maana hili la kuwa na pen names limeendelea na ninaamini litaendelea kwa muda mrefu ujao.

Ni kwa sababu hiyo kwanza sijashtushwa na kukamatwa kwa Max wala kushtushwa na ujio wa sheria ya Cybercrime. Vyote hivi ni vitu ambavyo nilivitarajia bila kujali nani angekuwa mshindi mwaka jana. Vitu hivyo vingekuwa tofauti tu kama upinzani wa kweli ungeshinda mwaka jana. Hilo pembeni.

Kumkamata Max na kujaribu kumlazimisha au kuilazimisha JamiiForums kutoa majina ya watu ili kufanya kazi ya serikali iwe rahisi au kuwafanyia serikali kazi ambayo wao wanapaswa kuifanya ni dalili ya uzembe uliopitiliza. Hili nililsema mwaka 2008 na nalirudia tu tena. Serikali ina jukumu la kufanya kazi yake lakini ni lazima ijaribu kufanya kazi yake kwa weledi wake wote.

Serikali ina uwezo (wa kifedha na kiutaalam) wa kufuatilia mawasiliano ya watu kwa mujibu wa sheria. Haiwezekani mtu aamue tu kutaka jina la fulani kwenye mtandao kwa sababu tu huyo fulani kaandika habari au kitu ambacho labda serikali inaamini wananchi hawakupaswa kukijua (kiwe cha kweli au la).

Lakini kubwa ni kuwa JF ina wanachama 360,000 hivi, sidhani kuna mtu yeyote anaamini Max anaweza kujua majina yote ya kweli au ya kiuandishi ya wanachama wote. Hata mtu akitumia jina la John Marko, ni vigumu kujua kama kweli ni jina lake kulinganisha na mtu anayejiita "Kifuu cha Nazi". Inawezekana anayeitwa Kifuu cha Nazi ndilo jina lake kweli na yule anayejiita John Marko ndiye anatumia jina la kiuandishi!

Kubwa zaidi hata hivyo ni kuwa badala ya kuhangaika na "nani kasema nini" ni vizuri serikali ihangaike na "Nani kafanya nini"! Lakini kama tunataka kufuatilia "nani kasema nini" ni vizuri zaidi kujali "nini kimesemwa na nani" na hivyo kuangalia na kutoa majibu muafaka na yenye kuridhisha. Tatizo la maswali ni kuwa hata ukamate wote wanaoyauliza kwa kadiri kwamba huyajibu maswali ya, maswali yataendelea kuulizwa tu hata na wale wasiyoyauliza hadharani!.

Hivyo basi, ni maoni yangu na naweza kusema ni wito wangu kuwa vitisho kwa vyombo vya habari, mitandao ya kijamii au watu wanaoikosoa havina sababu ya msingi na Max Mello aachiliwe bila masharti yeyote na kuwa serikali imwombe radhi kwa usumbufu na kutambua mchango mkubwa JamiiForums imeutoa kwa Tanzania na kwa tasnia ya habari kuanzia 2006.

Niseme tu kuwa Max aachiliwe bila masharti y0yote ndani ya masaa 24 yajayo, kinyume cha hivyo mtatulazimisha waanzilishi hasa wa mtandao huu kufunga JamiiForums Tanzania na ofisi zake na kuurudisha gizani na hivyo siyo tu kuwakosesha hata nafasi ya kuwafikia wananchi wengi ambao wanatumia mtandao huu kupata habari kwa usahihi ndani na nje ya nchi lakini pia kutoa nafasi kwa watoa maoni wa ndani ya serikali kuwafikia wapiga kura na wananchi.

Haki ya Watanzania kupata habari, kujieleza kwa uhuru na kutoa maoni ni kubwa zaidi kuliko hata misimamo yetu baadhi yetu ya kuunga mkono mabadiliko ambayo tumeyaona. Kama nilivyowahi kusema kuna gharama ambayo watu wanaweza kukubali kuilipa kwa ajili ya mabadiliko wanayoyataka, lakini kuna gharama nyingine hailipiki.

MMM
Katika watu wa hovyo kabisa ni wewe.Huwa unacheza siasa za kirungu yeye hapa sana.Sasa uliowatetea huwezi wadhibiti hata wewe mwenyewe?Ndio shida ya ukarunguyeye km wa Pasco. Unaomba nini hapa wakati waliomshikilia ndio huwa kipindi cha uchaguzi unaandika thread ndeefu na amkala kila mahali kutetea roho zao.Ipo siku utabaki wewe na wao.
 
Huwezi kuhalalisha ubaya kwa ubaya, wewe. Halafu huwezi kufananisha haki ya kutokupata record ya threads ulizoanzisha hapa JF na mtu kuwekwa rumande na kunyimwa dhamana bila sababu za msingi. Wewe umeshawahi kuwasiliana na uongozi wa JF kuwasilisha hayo malalamiko yako? Uongozi wa JF wameenda mpaka mahakamani kudai haki kwa amani. Sasa unawezaji kufananisha frustrations zako na tukio wanalopitia uongozi wa JF.
Hatujajua particulars of the case. Lests not speculate.

Inawezekana issue ikawa entirely different from JF
 
sielewi unapotishia kufunga mtandao wakat unajua fika ndicho wanachokitamani miaka yote.
 
Naamini umemaanisha kufuta.
Kuna mdau kaonesha wewe ni mpya hivyo huu muziki bado hujazijua steps.

Nimependa unavyojiuliza kua kwanini members hatuwezi kufuta threads? Ila umeshindwa kwenda mbele na kutambua kua;
Ulichoanzisha kikiwa ni mwiba kwa mtu husika huku kina faida kwa majority, huyo mtu akakutaka uufute uzi na ukaufuta maana yake majority watakua wamenyimwa haki yao kubwa tu, kuzuia hilo ufunguo wa kufuta uzi upo kwa wasimamizi.

Ingia fanya utafiti wa kusearch net uwajue wamiliki, kuhusu hisa obviously hata mimi nigekua Melo nisingeruhusu kuuza hisa vipi kama mwanahisa mpya ni kirusi? (Ingawa sijui kama hisa hua hazitangazwi).
Mengine piga simu ofisini kwao naamini. utaelekezwa.

Pia uache kufananisha JF na nchi.
Xenforo inaruhusu mwanzisha mada kuifuta/ku edit kichwa cha mada/kuweka member kwenye ignore list etc

Hivyo siri ya kutowapa members hizo options humu JF anazo Mike na Max lakini hawana justification whats so ever

Kuhusu leadership na ownership hii nayo kwa nini inakuwa siri? Why the secrecy? Maana kila mmoja sasa anasema ni owner mara Mbarak mara Max mara Mike mara William mara pascal sasa who is who? Leo mwenzako kakamatwa mbona wao mpaka sasa wako kimya?

Nijuavyo JF is no longer just an underground site. It's a media company hivyo ni muhim wakawa transparent not only kwenye vision lakini pia objectives,strategic na business continuity plan etc

Max Mike na team yenu it's about time mkataba run this entity as a business na sio pressure group tuu inayotegemea kudra na mchango kama kanisa.

Ikiwezekana go off air even for 3 months ili mkirudi mnarudi upya Ikiwezekana na plan B kama.vile ownership na hosting ya forum ikawa nje nyinyi mnaweza kurun just the small portion..jamiiTV

Lakini mkiweka egos mbele mtakwama kwenye hizi zama za Magufuli
 
Mimi Kama wanataka Jina Langu waniulize hapa Live Nitawapa hapa hapa, Hawana haja ya Kumtesa Kijana wa Watu, The Lord is my Shield who shall I fear? Makonda au Magufuli? Hao ni watu au Miungu? Msidanganyike hawa Watawala waheshimuni wakistahili heshima lakini Ukweli ni Kuwa they are Nothing but mortals!
Yes we are mortal beings ......
Wako wapi Mobutu Sesedeko?
 
Kuna haja ya kuelimisha watumiaji wa JF namna ya matumizi sahihi ya mitandao. Uhuru wa kuhabarishana haubarikiwi kwa kuvunja sheria nyingine! Tujifunze kufanya mambo kwa kiasi na kwa utaratibu!

Hata huko kwa walioianzisha hii mitandao, bado kuna sehemu serikali inaingia pale panapotokea uvunjifu wa sheria!

If you tweet jokes about killing Trump, the Secret Service will find you.

Kejeli, uzushi, matusi sidhani kama lilikua lengo la awali forum ilipoanzishwa. Siku za karibuni kumetokea mabadiliko makubwa yanayopelekea umuhimu wa kuwepo kwa regulations Kali! Moderators wajitahidi kudeal na members wanaopelekea mambo kama haya kutokea!
Ni lazima kuipenda serikali?
 
Lakini mkuu MMM mimi kuna siku nilikuambia humu humu, Haya mnayoyashangilia kwa sasa na kuyabariki hata pale mtu anaposigina katiba kuna siku yataangamiza hii nchi.. Well, nilionekana mimi CHADEMA, Kila anayeongea yeye ni CHADEMA! Well tutulie tubatizwe maana Yohana mbatizaji yuko Mtu Yordan akiwabatiza kwa maji!
 
Back
Top Bottom