Kweli Max Ndiye Yeye: Kwanini Sina Hofu

Kweli Max Ndiye Yeye: Kwanini Sina Hofu

Kwa tunapoelekea sasa naona litokee la kutokea tu ili iwe itakavyokua maana tunaanza kuichezea wenyewe na ikitoweka ni ngumu kuirudisha.

Tupo tayari kwa...
tunaanza kuichezea nini?
amani au?
bora litokee la kutokea, ni lipi hilo?
vita au?


vyovyote iwavyo nakuunga mkono
 
Wewe unafikiri CCM ni dubwasha flani ndio maana tunaingia chaka sana. Hivi JK angegombea uraisi kupitia chadema ungemrudisha madarakani kwavile kapitia chadema? Tuna safari ndefu mno kujielewa!
Tatizo tunalokabiliwa nalo sasa ni mfumo.
Yaani nchi yetu inaendeshwa kwa mfumo wa chama kimoja wakati tupo kwenye mfumo wa vyama vingi. Na huo mfumo ndo siraha ya ccm. Hawataki kuubadili maana wanajua itakula kwao.
Hebu jiulize, rais ndo anateua tume ya uchaguzi
Rais ndo anateua watendaji mbali mbali wa serikali
Rais ndo anateua jaji mkuu
Kwa mfumo wa vyama vingi unadhani atateua watu ambao wapo kinyume na sera za chama chake hata kama hao watu wanausimamia ukweli?
Jibu ni hapana. Lazima ateue makada wa chama chake ili wakilinde chama.
Ili kuing'oa mizizi hiyo ambao sasa imeshakua mikubwa kiasi kwamba inaogopesha, ni lazima wananchi wakikatae hicho chama kwa nguvu zote. Na ili kukikataa kwa amani, ni lazima waangushwe kwenye uchaguzi haijalishi anawekwa nani. Ila kwa nguvu ambazo umma inazo, ukiamua kwa pamoja, hakika lazima wataachia ngazi.
Hiyo itakua ni hatua moja tumeipiga tayar.

Naomba nimalizie kwa kusema, kama kweli lowassa alikua mchafu na wewe hukupenda agombee urais, basi ungefamya kampen hata kwa mh rungwe. Mbona wengine tulimchagua mama wa act na leo hatujutii kupoteza kura zetu maana haya yanayotokea tulishajua yatatokea
 
Hahahaha wewe ni moja wao wavuta bange make ktk post wala comment yangu hakuna Tusi lkn Wewe umejaza matusi kibao kwenye comment yako.
Unaona sasa yaleyale neno "mjinga" limekuwa tusi hebu kafungue kamusi ya kiswahili ukipata tafsiri yake rudi tuongee. Ina maana Baba wa Taifa alivyokuwa akitaja neno "ujinga" ni moja ya maadui wa maendeleo ya Taifa hili alikuwa akitukana?
 
Watu wenye mawazo mbadala wawe kutoka chama tawala au upande wa pili wanapokosoa serikali ni vema wakaonekana kama chachu badala ya kuchukuliwa kama waasi. Rais ajue siyo omniscience(kujua kila kitu) na kwamba kilichomfanya atuongoze ni Mungu alimpa fursa ili awe mbele sisi tuwe nyuma yake. Hata mfalme Sulemani pamoja na kuwa na hekima na busara nyingi bado alipata ushauri wa kuongoza kutoka makundi mbalimbali na hiyo ilimfanikisha.

Mfalme Daudi katika Biblia alipozini na mke wa Uria (2 Samweli 12) na kumpeleka mumewe vitani akauwawa alijiwa na Nabii Nathan na huyu nabii alimweleza ukweli live na adhabu Mungu atakayompa(soma zaidi utaelewa). Huyu mfalme hakusema akamatwe auwawe bali alitoa jibu moja tu "NIMEMFANYIA BWANA DHAMBI".

Nathan baada ya ujumbe huu aliondoka kwenda nyumbani kwake na hakutafutwa wala kuuuawa. Baadaye mtoto aliyezaa na mke wa Uria akaugua hadi kufa.
Ingekuwa Nabii Nathan yuko Tanzania leo akamwambia rais hivyo angekamatwa kwa kutoa maneno ya uchochezi nk.

Tunamwomba rais ajue critics pia wanamsaidia kuwa focused. watu wakuogopa ni rebels wanaotumia silaha kuuawa watu lakini kama watu wakikukosoa ukachukulia positive yale mazuri ukchukua na mabaya ukayaacha basi unaonekana uko gentleman kama JK.

Kinyume na hivyo utaonekana tu mtu mwenye INFERIORITY COMPLEX.
Rais alitakiwa awatumie akina Max kama jicho la tatu badala ya kuwaona wahalifu
 
""WAPI TUTAESEMEA MADUKU-DUKU YETU?,UKIRIPOTI DIRECTLY UOVU,UNATAJWA KWA MHALIFU..
•BASI PELEKENI NCHI MPENDAVYO NYIE NA SI TUTAKAVYO SIE..""
 
Nguvu inayotumika kwenye mambo ya 'hovyo hovyo' na yasiyokuwa ya msingi ingetumika kwa maendeleo ya watu ingeacha legacy kubwa kuliko nguvu inayotumika kukusanya kimabavu makusanyo kiduchu kwa maendeleo ya vitu! Hapa ndipo napoiliona anguko kuu la utawala unaoonesha dalili za kushindwa katika hatua za mwanzo kabisa za utawala! Shame!
 
Watu wenye mawazo mbadala wawe kutoka chama tawala au upande wa pili wanapokosoa serikali ni vema wakaonekana kama chachu badala ya kuchukuliwa kama waasi. Rais ajue siyo omniscience(kujua kila kitu) na kwamba kilichomfanya atuongoze ni Mungu alimpa fursa ili awe mbele sisi tuwe nyuma yake. Hata mfalme Sulemani pamoja na kuwa na hekima na busara nyingi bado alipata ushauri wa kuongoza kutoka makundi mbalimbali na hiyo ilimfanikisha.
Mfalme Daudi katika Biblia alipozini na mke wa Uria (2 Samweli 12) na kumpeleka mumewe vitani akauwawa alijiwa na Nabii Nathan na huyu nabii alimweleza ukweli live na adhabu Mungu atakayompa(soma zaidi utaelewa). Huyu mfalme hakusema akamatwe auwawe bali alitoa jibu moja tu "NIMEMFANYIA BWANA DHAMBI". Nathan baada ya ujumbe huu aliondoka kwenda nyumbani kwake na hakutafutwa wala kuuuawa. Baadaye mtoto aliyezaa na mke wa Uria akaugua hadi kufa.
Ingekuwa Nabii Nathan yuko Tanzania leo akamwambia rais hivyo angekamatwa kwa kutoa maneno ya uchochezi nk.
Tunamwomba rais ajue critics pia wanamsaidia kuwa focused. watu wakuogopa ni rebels wanaotumia silaha kuuawa watu lakini kama watu wakikukosoa ukachukulia positive yale mazuri ukchukua na mabaya ukayaacha basi unaonekana uko gentleman kama JK. Kinyume na hivyo utaonekana tu mtu mwenye INFERIORITY COMPLEX.
Rais alitakiwa awatumie akina Max kama jicho la tatu badala ya kuwaona wahalifu
Mkuu umenena jambo jema. Napata mashaka na mwenendo wa serikali ya sasa. Wakati mwingine nahisi Lawrence Mafuru ni mtu jasiri alipomkosoa bosi wake hadharani wakati hakuna hata Waziri aliyejaribu kufanya hivyo
 
Mkuu umenena jambo jema. Napata mashaka na mwenendo wa serikali ya sasa. Wakati mwingine nahisi Lawrence Mafuru ni mtu jasiri alipomkosoa bosi wake hadharani wakati hakuna hata Waziri aliyejaribu kufanya hivyo
***
-->>ALIMKOSOA TU, HAPOHAPO IKAJIBU.
•""WISDOM MATTER,WISDOM MATTER,WISDOM MATTER.""
•HOW YOU CAN BE VERY PRRFECT AND 100% CORRECTLY UNDER THE SUN.
 
Najua Shida ni Baadhi ya Majukwaa shida si JF yote! Ndio maana haya yanatokea! Lakini humu kuna wabunge wa Vyama Vyote wachache wanao tumia ID za kweli!

Jambo ambalo JF watakosea ni kukubali kutoa taarifa za watumiaji wake! Ni herii JF ifungwee kwa muda lakini sio kutoa Taarifa....Hataweza Kufunga Social Networks Zote kwa sababu serikali haina Wataalamu hao! Lakini Mimi ninaona As wana JF lazima tufanye kitu cha Ziada! Na ikitokea Kuwa Alie kamatwa Anahitaji Dhamana Basi tufanya mchango wa Wazi kumchangia kiasi Chote cha Fedha kuonesha tunamuhitaji na tunahitaji JF watumiaji 360,000 tukileta Vurugu za Michango wao wataipata picha kwa tunahitaji JF
 
Democracy and freedom of speech is very expensive, if we think we can't afford it let's get prepared to follow Northern Korea's suit. Hakuna njia nyingine.
 
WW Mzee Mwanakijiji ndo chimbuko la yote haya... endeleza maslahi ya kigango usituyeyushe hapa ...
Na. M. M. Mwanakijiji

  • Mimi ni Miongoni mwa Waasisi wa JF
  • Uhuru wa Maoni na Kujieleza Usitishiwe
  • Max Mello Aachiliwe Ndani ya Masaa 24
  • Kuungwa Mkono Haina Maana Kukubaliwa Lolote

Kwanza kabisa niseme kuwa mimi ni mmoja wa waanzilishi wa mtandao huu. Siyo tu miongoni mwa wanachama wa mwanzo lakini pia miongoni mwa watu waliokaa na kufanya majadiliano ya kuihamisha jukwaa la mijadala tangu ikiwa bcstimes na baadaye Jambo Forums na hatimaye Jamiiforums.

Tulihamisha kutoka bcstimes kwa sababu haikuwa na facilities na uwezo tunaoutaka kuweka kuisimamia. Tulihama kutoka Jambo Forums hadi JamiiForums kufuatia kukamatwa kwa Max na Mike mwezi Februari 2008 na mtu mmoja (alikuwa kada wa chama fulani) kuchukua jina la Jambo Forums na kugoma kuturudishia! Ili tusipotee sana tukaamua kuiita JamiiForums (ili kubakia na initial zile zile za JF - ikiwa ni sababu mojawapo).

Mimi ndiye mbunifu wa msemo wa "where we dare (to) talk openly".

Walipokamatwa kina Max nilienda hadi BBC na kujenga hoja ya kuwa uhuru wa maoni haulindi maoni mazuri tu nayale tunayoyapenda, bali unalinda hasa maoni mabovu, tusiyoyapenda na nikasema kuwa "unalinda hata maoni ya kijinga"! Ukweli huu wa miaka nane nyuma naamini bado ni ukweli uliopo sasa.

Max na wenzetu waliopo nyumbani walichukua jukumu la kujaribu kurasimisha mtandao huu kuwa kampuni ili sehemu yake moja isiwe inafanywa gizani na kuweka taratibu mbalimbali za kuhakikisha uhuru wa maoni unakuwepo na watu wanaotaka kutumia majina halisi wanafanya hivyo -wakati ule karibu wote tulikuwa tunatumia majina ya kiuandishi (pen names). Lakini pia hatukutaka kuzuia watu wengine kuendelea kuandika under pseudonyms. Sababu yake ni kuwa ili kuweza kupata habari, kuchochea mijadala na kuwapatia Watanzania habari kwa undani na maoni bila kuogopa adhabu basi tuliacha iwe hivyo.

Hili lilisaidia mtandao huu kufichua baadhi ya kashfa nyingi na mbalimbali bila ya watu kuhofia kujulikana kwani hadi hivi sasa Tanzania haina Sheria ya kumlinda mfichua uovu! (whistle blower protection act). Hivyo, ni kwa kutumia mitandao hii na namna ya usiri ndio maana hili la kuwa na pen names limeendelea na ninaamini litaendelea kwa muda mrefu ujao.

Ni kwa sababu hiyo kwanza sijashtushwa na kukamatwa kwa Max wala kushtushwa na ujio wa sheria ya Cybercrime. Vyote hivi ni vitu ambavyo nilivitarajia bila kujali nani angekuwa mshindi mwaka jana. Vitu hivyo vingekuwa tofauti tu kama upinzani wa kweli ungeshinda mwaka jana. Hilo pembeni.

Kumkamata Max na kujaribu kumlazimisha au kuilazimisha JamiiForums kutoa majina ya watu ili kufanya kazi ya serikali iwe rahisi au kuwafanyia serikali kazi ambayo wao wanapaswa kuifanya ni dalili ya uzembe uliopitiliza. Hili nililsema mwaka 2008 na nalirudia tu tena. Serikali ina jukumu la kufanya kazi yake lakini ni lazima ijaribu kufanya kazi yake kwa weledi wake wote.

Serikali ina uwezo (wa kifedha na kiutaalam) wa kufuatilia mawasiliano ya watu kwa mujibu wa sheria. Haiwezekani mtu aamue tu kutaka jina la fulani kwenye mtandao kwa sababu tu huyo fulani kaandika habari au kitu ambacho labda serikali inaamini wananchi hawakupaswa kukijua (kiwe cha kweli au la).

Lakini kubwa ni kuwa JF ina wanachama 360,000 hivi, sidhani kuna mtu yeyote anaamini Max anaweza kujua majina yote ya kweli au ya kiuandishi ya wanachama wote. Hata mtu akitumia jina la John Marko, ni vigumu kujua kama kweli ni jina lake kulinganisha na mtu anayejiita "Kifuu cha Nazi". Inawezekana anayeitwa Kifuu cha Nazi ndilo jina lake kweli na yule anayejiita John Marko ndiye anatumia jina la kiuandishi!

Kubwa zaidi hata hivyo ni kuwa badala ya kuhangaika na "nani kasema nini" ni vizuri serikali ihangaike na "Nani kafanya nini"! Lakini kama tunataka kufuatilia "nani kasema nini" ni vizuri zaidi kujali "nini kimesemwa na nani" na hivyo kuangalia na kutoa majibu muafaka na yenye kuridhisha. Tatizo la maswali ni kuwa hata ukamate wote wanaoyauliza kwa kadiri kwamba huyajibu maswali ya, maswali yataendelea kuulizwa tu hata na wale wasiyoyauliza hadharani!.

Hivyo basi, ni maoni yangu na naweza kusema ni wito wangu kuwa vitisho kwa vyombo vya habari, mitandao ya kijamii au watu wanaoikosoa havina sababu ya msingi na Max Mello aachiliwe bila masharti yeyote na kuwa serikali imwombe radhi kwa usumbufu na kutambua mchango mkubwa JamiiForums imeutoa kwa Tanzania na kwa tasnia ya habari kuanzia 2006.

Niseme tu kuwa Max aachiliwe bila masharti y0yote ndani ya masaa 24 yajayo, kinyume cha hivyo mtatulazimisha waanzilishi hasa wa mtandao huu kufunga JamiiForums Tanzania na ofisi zake na kuurudisha gizani na hivyo siyo tu kuwakosesha hata nafasi ya kuwafikia wananchi wengi ambao wanatumia mtandao huu kupata habari kwa usahihi ndani na nje ya nchi lakini pia kutoa nafasi kwa watoa maoni wa ndani ya serikali kuwafikia wapiga kura na wananchi.

Haki ya Watanzania kupata habari, kujieleza kwa uhuru na kutoa maoni ni kubwa zaidi kuliko hata misimamo yetu baadhi yetu ya kuunga mkono mabadiliko ambayo tumeyaona. Kama nilivyowahi kusema kuna gharama ambayo watu wanaweza kukubali kuilipa kwa ajili ya mabadiliko wanayoyataka, lakini kuna gharama nyingine hailipiki.

MMM
 
dah wakifunga jf ntaenda kujamiiana wap mimi tena ooh lord pls avoid this
 
Tuendelee kuisifu tu serikali hii ya awamu ya tano. Si ndio huyu Mwanakijiji aliyeona ni bora ccm ishinde? Sasa tusilalamike. Hiyo lugha ya "upinzani wa kweli" haina tija kwa taifa letu, la msingi lilikuwa ccm itoke. Tuache tu tupate matokeo ya kuunga mkono ccm. Bado kwa staili hii kila mtu atafikiwa, ni zamu mpaka tuisome namba.
Sikutaka kuchangia UZI hu, maandishi yako yamenilazimisha kaka. Na pia sitaki kusema nini kimenilazimisha kuandika, itoshe tu kusema, nime like ulicho kiandika.
 
hiyo ni shida kwa uhuru kwa kutoa maoni ama(free of speech),katiba ya Tanzania 1977 ina ruhusu kujieleza,JamiiForums ni taasisi muhimu kwa watanzania kumkamata Max si haki kwa uhuru wa raia wa Tanzania
 
Nakumbuka wakati wanapitisha hiyo Cybercrime Act nilikuwa ninalalamika sana na watu wengi walikuwa hawaelewi umuhimu wa privacy wengi walisema kwani ninaficha nini mimi sio mhalifu....hizi sheria zao zina maneno ya kijanja janja na mitego ambayo vyombo vya usalama vinaweza kuitumia kukandamiza wananchi.

Bado kuna janga lingine linakuja
20161214_093635.png

Tunakoelekea serikali inaweza kuuza nchi na tusipate uhuru wa kuhoji.

Kwa kuangalia jinsi mambo yanavyoendeshwa na viongozi wetu, hata nguvu ya uzalendo inakwisha kabisa.
 

Attachments

  • 20161214_093635.png
    20161214_093635.png
    40.3 KB · Views: 34
"Natamani malaika washuke wazime mitandao" now I understand
 
Back
Top Bottom