Kweli Max Ndiye Yeye: Kwanini Sina Hofu

Kweli Max Ndiye Yeye: Kwanini Sina Hofu

Kuna watu humu ndani hamjajua nchi hii hasa ccm.watawala wa ccm kila wanapokaa iwe lumumba au ikulu uwa wanajiuliza nn sababu ya kura zao kushuka na idadi kubwa ya watu kuichukia ccm.Moja ya sababu kubwa ni mitandao ya kijamii,magazeti na ndio maana sheria zinakuwa kali sana kila kukicha.wao kwa imani yao na tafiti zao za wataalamu wa rumumba wamezunguka nchi nzima wanajua kuwa ili waendelee kutawala vema ni kufungia vyombo vyote vya habari na kuweka sheria kali.na ndio maana mkuu wa nchi aliwai tamka kuwa anatamani kuzima mitandao ya kijamii ili siku anafungua watu waone nn kinafanyika utadhani mitandao ndonitaonyesha sisi tumelala

Huwa naona kama Rais anaogopa media mithili ya mtoto mdogo anayeogopa picha ya kutisha ambayo haina madhara yeyote kiuhalisia. Na hapo huwa napata mashaka sana na uwezo wake wa kung'amua mambo muhimu kwa mustakabali wa hili taifa. Najiuliza watu kufanya mikutano ya hadhara au kutoa maoni yao kwa uhuru kunamuathiri vipi yeye Rais kufanya kazi yake kama siyo woga uliopitiliza!
 
Then anaiga mbinu za watu walioingia madarakani kutokea msituni!!
Aachie ngazi then aende msituni ndio aje afanye tabia za msituni!!
Kwa sasa anachojitafutia laana tu toka kwa Mungu kwa damu za watu wasio na hatia!
 
Na bado huu ni mwanzo tu, lazima wote tutanyooka. Mlidhania Hapa Kazi tu ni kupiga pushup.
Baada ya kuifufua ATCL, kinachofuata ni kuifufua TBC, Daily news. Tutasikiliza habari kupitia vyombo vya taifa tu, na vyombo vingine vitajiunga.
 
Mwanakijiji huu sio muda wa kulaumu au kutisha ... Hatutishiki na usitujaribu maana hatujaribiwi.
Muda bado kaka mabadiliko yanakosti zake kama unataka kuzima ile rangi ulioitetea haidhuriki na kuzima kwako wewe zima tuu.
 
Mwanakijiji au we ndie maraika alienenwa kuja kuzima mitandao ya jamii.
 
Tuliposema kuhusu udikteta si baadhi mlituita wapiga dili au nyumbu?
Haya sasa,hiyo ndiyo style
 
Ngoja nianze kutafuta mitandao ya Kenya nitakuwa nashiriki mijadara huko
Nakuunga mkono. Kama JF ilivyo na "Kenyan News", basi tutafute "Tanzanian Jukwaa" kwenye mitandao ya Kenya; tutafungukia hata huko.
 
  • Thanks
Reactions: Izc
Nimefikiria sana lakini nimekosa kitu cha kusema katika hili.. Nawasihi wote mkasome Mithali 12:1 Mkapate kupona!
 
mleta mada ni kati ya vinyonga hatari sana hapa JF.

hii mada angeandika mtu mwingine,ningeipa kipaombele,lakini kwa kuwa aliyeandika ni mnafiki toka kundi lile lile ,naipuuza.
Hapo ndipo utaamini Watanzania tu watu wanafki kuliko wote ulimwenguni..

Kwakuwa maslahi yake (mwanahisa) yanaanza kuguswa anateremsha povu la maana
 
Mm sio mtaalamu sana wa uandishi wa makala,ila hoja yangu itaeleweka kiasi.Haya yanayoendelea kuhusu,kuwasumbua waandishi,wamiliki wa vyombo vya habari,kuweka kwa sheria kali,Ni matokeo ya tafiti ambazo zilifanyika kutoka kwa wale wataalamu wa chama ccm,katika kuona
Huwa naona kama Rais anaogopa media mithili ya mtoto mdogo anayeogopa picha ya kutisha ambayo haina madhara yeyote kiuhalisia. Na hapo huwa napata mashaka sana na uwezo wake wa kung'amua mambo muhimu kwa mustakabali wa hili taifa. Najiuliza watu kufanya mikutano ya hadhara au kutoa maoni yao kwa uhuru kunamuathiri vipi yeye Rais kufanya kazi yake kama siyo woga uliopitiliza!
 
Huwa naona kama Rais anaogopa media mithili ya mtoto mdogo anayeogopa picha ya kutisha ambayo haina madhara yeyote kiuhalisia. Na hapo huwa napata mashaka sana na uwezo wake wa kung'amua mambo muhimu kwa mustakabali wa hili taifa. Najiuliza watu kufanya mikutano ya hadhara au kutoa maoni yao kwa uhuru kunamuathiri vipi yeye Rais kufanya kazi yake kama siyo woga uliopitiliza!
Ishu sio rais pekee ishu ni ccm ndo imeamua haya yote,ukiona nape,mwakyembe na masaju wanajua dhumuni la haya yote
 
Na. M. M. Mwanakijiji

  • Mimi ni Miongoni mwa Waasisi wa JF
  • Uhuru wa Maoni na Kujieleza Usitishiwe
  • Max Mello Aachiliwe Ndani ya Masaa 24
  • Kuungwa Mkono Haina Maana Kukubaliwa Lolote

Kwanza kabisa niseme kuwa mimi ni mmoja wa waanzilishi wa mtandao huu. Siyo tu miongoni mwa wanachama wa mwanzo lakini pia miongoni mwa watu waliokaa na kufanya majadiliano ya kuihamisha jukwaa la mijadala tangu ikiwa bcstimes na baadaye Jambo Forums na hatimaye Jamiiforums.

Tulihamisha kutoka bcstimes kwa sababu haikuwa na facilities na uwezo tunaoutaka kuweka kuisimamia. Tulihama kutoka Jambo Forums hadi JamiiForums kufuatia kukamatwa kwa Max na Mike mwezi Februari 2008 na mtu mmoja (alikuwa kada wa chama fulani) kuchukua jina la Jambo Forums na kugoma kuturudishia! Ili tusipotee sana tukaamua kuiita JamiiForums (ili kubakia na initial zile zile za JF - ikiwa ni sababu mojawapo).

Mimi ndiye mbunifu wa msemo wa "where we dare (to) talk openly".

Walipokamatwa kina Max nilienda hadi BBC na kujenga hoja ya kuwa uhuru wa maoni haulindi maoni mazuri tu nayale tunayoyapenda, bali unalinda hasa maoni mabovu, tusiyoyapenda na nikasema kuwa "unalinda hata maoni ya kijinga"! Ukweli huu wa miaka nane nyuma naamini bado ni ukweli uliopo sasa.

Max na wenzetu waliopo nyumbani walichukua jukumu la kujaribu kurasimisha mtandao huu kuwa kampuni ili sehemu yake moja isiwe inafanywa gizani na kuweka taratibu mbalimbali za kuhakikisha uhuru wa maoni unakuwepo na watu wanaotaka kutumia majina halisi wanafanya hivyo -wakati ule karibu wote tulikuwa tunatumia majina ya kiuandishi (pen names). Lakini pia hatukutaka kuzuia watu wengine kuendelea kuandika under pseudonyms. Sababu yake ni kuwa ili kuweza kupata habari, kuchochea mijadala na kuwapatia Watanzania habari kwa undani na maoni bila kuogopa adhabu basi tuliacha iwe hivyo.

Hili lilisaidia mtandao huu kufichua baadhi ya kashfa nyingi na mbalimbali bila ya watu kuhofia kujulikana kwani hadi hivi sasa Tanzania haina Sheria ya kumlinda mfichua uovu! (whistle blower protection act). Hivyo, ni kwa kutumia mitandao hii na namna ya usiri ndio maana hili la kuwa na pen names limeendelea na ninaamini litaendelea kwa muda mrefu ujao.

Ni kwa sababu hiyo kwanza sijashtushwa na kukamatwa kwa Max wala kushtushwa na ujio wa sheria ya Cybercrime. Vyote hivi ni vitu ambavyo nilivitarajia bila kujali nani angekuwa mshindi mwaka jana. Vitu hivyo vingekuwa tofauti tu kama upinzani wa kweli ungeshinda mwaka jana. Hilo pembeni.

Kumkamata Max na kujaribu kumlazimisha au kuilazimisha JamiiForums kutoa majina ya watu ili kufanya kazi ya serikali iwe rahisi au kuwafanyia serikali kazi ambayo wao wanapaswa kuifanya ni dalili ya uzembe uliopitiliza. Hili nililsema mwaka 2008 na nalirudia tu tena. Serikali ina jukumu la kufanya kazi yake lakini ni lazima ijaribu kufanya kazi yake kwa weledi wake wote.

Serikali ina uwezo (wa kifedha na kiutaalam) wa kufuatilia mawasiliano ya watu kwa mujibu wa sheria. Haiwezekani mtu aamue tu kutaka jina la fulani kwenye mtandao kwa sababu tu huyo fulani kaandika habari au kitu ambacho labda serikali inaamini wananchi hawakupaswa kukijua (kiwe cha kweli au la).

Lakini kubwa ni kuwa JF ina wanachama 360,000 hivi, sidhani kuna mtu yeyote anaamini Max anaweza kujua majina yote ya kweli au ya kiuandishi ya wanachama wote. Hata mtu akitumia jina la John Marko, ni vigumu kujua kama kweli ni jina lake kulinganisha na mtu anayejiita "Kifuu cha Nazi". Inawezekana anayeitwa Kifuu cha Nazi ndilo jina lake kweli na yule anayejiita John Marko ndiye anatumia jina la kiuandishi!

Kubwa zaidi hata hivyo ni kuwa badala ya kuhangaika na "nani kasema nini" ni vizuri serikali ihangaike na "Nani kafanya nini"! Lakini kama tunataka kufuatilia "nani kasema nini" ni vizuri zaidi kujali "nini kimesemwa na nani" na hivyo kuangalia na kutoa majibu muafaka na yenye kuridhisha. Tatizo la maswali ni kuwa hata ukamate wote wanaoyauliza kwa kadiri kwamba huyajibu maswali ya, maswali yataendelea kuulizwa tu hata na wale wasiyoyauliza hadharani!.

Hivyo basi, ni maoni yangu na naweza kusema ni wito wangu kuwa vitisho kwa vyombo vya habari, mitandao ya kijamii au watu wanaoikosoa havina sababu ya msingi na Max Mello aachiliwe bila masharti yeyote na kuwa serikali imwombe radhi kwa usumbufu na kutambua mchango mkubwa JamiiForums imeutoa kwa Tanzania na kwa tasnia ya habari kuanzia 2006.

Niseme tu kuwa Max aachiliwe bila masharti y0yote ndani ya masaa 24 yajayo, kinyume cha hivyo mtatulazimisha waanzilishi hasa wa mtandao huu kufunga JamiiForums Tanzania na ofisi zake na kuurudisha gizani na hivyo siyo tu kuwakosesha hata nafasi ya kuwafikia wananchi wengi ambao wanatumia mtandao huu kupata habari kwa usahihi ndani na nje ya nchi lakini pia kutoa nafasi kwa watoa maoni wa ndani ya serikali kuwafikia wapiga kura na wananchi.

Haki ya Watanzania kupata habari, kujieleza kwa uhuru na kutoa maoni ni kubwa zaidi kuliko hata misimamo yetu baadhi yetu ya kuunga mkono mabadiliko ambayo tumeyaona. Kama nilivyowahi kusema kuna gharama ambayo watu wanaweza kukubali kuilipa kwa ajili ya mabadiliko wanayoyataka, lakini kuna gharama nyingine hailipiki.

MMM

MM hii inauma sana ,mimi nilikuwa mfuatiliaji wa BCS,jambo forum na makala za MM MWANAKIJIJI,..Ambako enzi hizo zilikuwa zile za sauti au maandishi [MM MWANAKIJIJI PODCAST],Kabla sijajiunga rasmi mwaka 2006 kama member JF..ila tuliandika sana hapa juu ya uchaguzi wa 2005 , na kuendelea ...tumeiendesha JF kwa michango ya siri kuanzia hapo hadi pale ilipoweza kusimama yenyewe ...
Mchango wa JF na mkubwa sana ,na waanzilishi wenzake ni kati ya machujaa wa nchi hii.......nadhani tutakubaliana hapa kuwa atakaye kuwa na lengo la kuwaumiza basi hana nia njema na uhuru wetu kama wananchi na hili lisiwe na uchama
 
Nimefikiria sana lakini nimekosa kitu cha kusema katika hili.. Nawasihi wote mkasome Mithali 12:1 Mkapate kupona!
Mkuu anatakiwa ausome huu msitari, especially part ya mwisho ya msitari huu
 
Tuache unafiki

Humu jamiiforums udikteta kwenda mbele watu wanapigwa ban bila kujulishwa ssababu moderators wamekuwa miungu watu wana moderate kutokana na moods zao

Sasa Leo kibao kimegeuka mnalalamika?

Mshajiuliza why members hawapewi options za kukuta threads zao walizoanzisha? Kwa nini JF inataka. Kuhodhi kila kitu?

Au why hakuna namna ya members kujitoa au kujifuta uanachama?

Uongozi haijulikani ni akina nani maana kila mtu anaclaim kuwa yeye ni kiongozi na mwanzilishi na shareholder lakini mbona hakuna shareholders agreements au leadership elections na objectives na strategic plan??



We complain about govt repression huku ndani tunarepress members
 
Tuache unafiki

Humu jamiiforums udikteta kwenda mbele watu wanapigwa ban bila kujulishwa ssababu moderators wamekuwa miungu watu wana moderate kutokana na moods zao

Sasa Leo kibao kimegeuka mnalalamika?

Mshajiuliza why members hawapewi options za kukuta threads zao walizoanzisha? Kwa nini JF inataka. Kuhodhi kila kitu?

Au why hakuna namna ya members kujitoa au kujifuta uanachama?

Uongozi haijulikani ni akina nani maana kila mtu anaclaim kuwa yeye ni kiongozi na mwanzilishi na shareholder lakini mbona hakuna shareholders agreements au leadership elections na objectives na strategic plan??



We complain about govt repression huku ndani tunarepress members

Huwezi kuhalalisha ubaya kwa ubaya, wewe. Halafu huwezi kufananisha haki ya kutokupata record ya threads ulizoanzisha hapa JF na mtu kuwekwa rumande na kunyimwa dhamana bila sababu za msingi. Wewe umeshawahi kuwasiliana na uongozi wa JF kuwasilisha hayo malalamiko yako? Uongozi wa JF wameenda mpaka mahakamani kudai haki kwa amani. Sasa unawezaji kufananisha frustrations zako na tukio wanalopitia uongozi wa JF.
 
Ishu sio rais pekee ishu ni ccm ndo imeamua haya yote,ukiona nape,mwakyembe na masaju wanajua dhumuni la haya yote

Nakupata, Mkuu. Ila kumbuka kwamba JPM siyo tu ni Rais bali ni Mwenyekiti wa chama chake cha CCM. Mwenyekiti wa Chama ndiye "top" kwenye chama na ana uwezo wa kuwaambia hao "washauri" wake: asanteni kwa ushauri ila hili nitafanya na lile sitafanya. He has that power; kama tulivyoshuhudia hivi juzi akienda kinyume na maamuzi ya wasaidizi wake waliokuwa wametoa amri ya kuwaondoa wamachinga huko kanda ya ziwa, lakini yeye akaja na "move" ya tofauti kama kiongozi Mkuu akatengua hayo maamuzi. Kwahiyo mimi bado nipo palepale. Tatizo ni yeye wala siyo wasaidizi wake au chama. After all, yeye ndiye kiongozi mkuu wa chama chake.
 
Back
Top Bottom