Kweli Max Ndiye Yeye: Kwanini Sina Hofu

Kweli Max Ndiye Yeye: Kwanini Sina Hofu

Ninachokiona hapa ni sawa na timu za mpira baada ya dakika ya 90 huongezewa dakika kidogo kufidia muda uliopotezwa uwanjani kwa sababu mbalimbali, lakini hutokea timu moja kulalamika mpinzani wake anapendelewa kwani nini ziongezwe dakika 6?? Anatafutiwa goli hili hali dakika ni za woote kila timu ina uwezo wa kufunga goli, kwani nini serekali ya ccm ione JF inawanufaisha zaidi UPINZANI??
 
Kwa tunapoelekea sasa naona litokee la kutokea tu ili iwe itakavyokua maana tunaanza kuichezea wenyewe na ikitoweka ni ngumu kuirudisha.

Tupo tayari kwa...
 
Kwanza najiuliza huyu amekuwa mfalme?kwamba atatawala milele?miaka 5 ni sekund xhache ndio maana shetan hutia kiburi watawala ili wajione kwamba kwao hakuna umauti!maandiko yanasema hakuna baraka yeyote katika uhalifu !hata akina Herode na kaisaria wamebakia kama onyo Na fundisho kwa watawala dharimu ;!nivizur kuheshim watu Na kuwapa stahiki zao ili jina lako liandikwe ktk kitabu cha uzima!wakowap akiba IDD AMIN DADA .SAMUEL DORE , SADAM HUSSEIN?ADOLF HITLER!?Na wengine wengi! Jibu nchi hii niyetu sote tumeiridhi toka kwa mababu zetu nasiio Mali ya Ccm!
 
Na. M. M. Mwanakijiji

  • Mimi ni Miongoni mwa Waasisi wa JF
  • Uhuru wa Maoni na Kujieleza Usitishiwe
  • Max Mello Aachiliwe Ndani ya Masaa 24
  • Kuungwa Mkono Haina Maana Kukubaliwa Lolote

Kwanza kabisa niseme kuwa mimi ni mmoja wa waanzilishi wa mtandao huu. Siyo tu miongoni mwa wanachama wa mwanzo lakini pia miongoni mwa watu waliokaa na kufanya majadiliano ya kuihamisha jukwaa la mijadala tangu ikiwa bcstimes na baadaye Jambo Forums na hatimaye Jamiiforums.

Tulihamisha kutoka bcstimes kwa sababu haikuwa na facilities na uwezo tunaoutaka kuweka kuisimamia. Tulihama kutoka Jambo Forums hadi JamiiForums kufuatia kukamatwa kwa Max na Mike mwezi Februari 2008 na mtu mmoja (alikuwa kada wa chama fulani) kuchukua jina la Jambo Forums na kugoma kuturudishia! Ili tusipotee sana tukaamua kuiita JamiiForums (ili kubakia na initial zile zile za JF - ikiwa ni sababu mojawapo).

Mimi ndiye mbunifu wa msemo wa "where we dare (to) talk openly".

Walipokamatwa kina Max nilienda hadi BBC na kujenga hoja ya kuwa uhuru wa maoni haulindi maoni mazuri tu nayale tunayoyapenda, bali unalinda hasa maoni mabovu, tusiyoyapenda na nikasema kuwa "unalinda hata maoni ya kijinga"! Ukweli huu wa miaka nane nyuma naamini bado ni ukweli uliopo sasa.

Max na wenzetu waliopo nyumbani walichukua jukumu la kujaribu kurasimisha mtandao huu kuwa kampuni ili sehemu yake moja isiwe inafanywa gizani na kuweka taratibu mbalimbali za kuhakikisha uhuru wa maoni unakuwepo na watu wanaotaka kutumia majina halisi wanafanya hivyo -wakati ule karibu wote tulikuwa tunatumia majina ya kiuandishi (pen names). Lakini pia hatukutaka kuzuia watu wengine kuendelea kuandika under pseudonyms. Sababu yake ni kuwa ili kuweza kupata habari, kuchochea mijadala na kuwapatia Watanzania habari kwa undani na maoni bila kuogopa adhabu basi tuliacha iwe hivyo.

Hili lilisaidia mtandao huu kufichua baadhi ya kashfa nyingi na mbalimbali bila ya watu kuhofia kujulikana kwani hadi hivi sasa Tanzania haina Sheria ya kumlinda mfichua uovu! (whistle blower protection act). Hivyo, ni kwa kutumia mitandao hii na namna ya usiri ndio maana hili la kuwa na pen names limeendelea na ninaamini litaendelea kwa muda mrefu ujao.

Ni kwa sababu hiyo kwanza sijashtushwa na kukamatwa kwa Max wala kushtushwa na ujio wa sheria ya Cybercrime. Vyote hivi ni vitu ambavyo nilivitarajia bila kujali nani angekuwa mshindi mwaka jana. Vitu hivyo vingekuwa tofauti tu kama upinzani wa kweli ungeshinda mwaka jana. Hilo pembeni.

Kumkamata Max na kujaribu kumlazimisha au kuilazimisha JamiiForums kutoa majina ya watu ili kufanya kazi ya serikali iwe rahisi au kuwafanyia serikali kazi ambayo wao wanapaswa kuifanya ni dalili ya uzembe uliopitiliza. Hili nililsema mwaka 2008 na nalirudia tu tena. Serikali ina jukumu la kufanya kazi yake lakini ni lazima ijaribu kufanya kazi yake kwa weledi wake wote.

Serikali ina uwezo (wa kifedha na kiutaalam) wa kufuatilia mawasiliano ya watu kwa mujibu wa sheria. Haiwezekani mtu aamue tu kutaka jina la fulani kwenye mtandao kwa sababu tu huyo fulani kaandika habari au kitu ambacho labda serikali inaamini wananchi hawakupaswa kukijua (kiwe cha kweli au la).

Lakini kubwa ni kuwa JF ina wanachama 360,000 hivi, sidhani kuna mtu yeyote anaamini Max anaweza kujua majina yote ya kweli au ya kiuandishi ya wanachama wote. Hata mtu akitumia jina la John Marko, ni vigumu kujua kama kweli ni jina lake kulinganisha na mtu anayejiita "Kifuu cha Nazi". Inawezekana anayeitwa Kifuu cha Nazi ndilo jina lake kweli na yule anayejiita John Marko ndiye anatumia jina la kiuandishi!

Kubwa zaidi hata hivyo ni kuwa badala ya kuhangaika na "nani kasema nini" ni vizuri serikali ihangaike na "Nani kafanya nini"! Lakini kama tunataka kufuatilia "nani kasema nini" ni vizuri zaidi kujali "nini kimesemwa na nani" na hivyo kuangalia na kutoa majibu muafaka na yenye kuridhisha. Tatizo la maswali ni kuwa hata ukamate wote wanaoyauliza kwa kadiri kwamba huyajibu maswali ya, maswali yataendelea kuulizwa tu hata na wale wasiyoyauliza hadharani!.

Hivyo basi, ni maoni yangu na naweza kusema ni wito wangu kuwa vitisho kwa vyombo vya habari, mitandao ya kijamii au watu wanaoikosoa havina sababu ya msingi na Max Mello aachiliwe bila masharti yeyote na kuwa serikali imwombe radhi kwa usumbufu na kutambua mchango mkubwa JamiiForums imeutoa kwa Tanzania na kwa tasnia ya habari kuanzia 2006.

Niseme tu kuwa Max aachiliwe bila masharti y0yote ndani ya masaa 24 yajayo, kinyume cha hivyo mtatulazimisha waanzilishi hasa wa mtandao huu kufunga JamiiForums Tanzania na ofisi zake na kuurudisha gizani na hivyo siyo tu kuwakosesha hata nafasi ya kuwafikia wananchi wengi ambao wanatumia mtandao huu kupata habari kwa usahihi ndani na nje ya nchi lakini pia kutoa nafasi kwa watoa maoni wa ndani ya serikali kuwafikia wapiga kura na wananchi.

Haki ya Watanzania kupata habari, kujieleza kwa uhuru na kutoa maoni ni kubwa zaidi kuliko hata misimamo yetu baadhi yetu ya kuunga mkono mabadiliko ambayo tumeyaona. Kama nilivyowahi kusema kuna gharama ambayo watu wanaweza kukubali kuilipa kwa ajili ya mabadiliko wanayoyataka, lakini kuna gharama nyingine hailipiki.

MMM
Ni kweli bwana MMM nakumbuka sana andiko zako nyingi ktk gazeti la Mwanahalisi kabla kufungwa kwa mda mrefu na baada kufunguliwa ckukuckia tena,kumbe we Ni miongoni mwa waasisi wa JF.....?Ila kitu kimoja nataka kukushauri usifikirie hata siku moja kufunga hili jukwaa hao wanao weweseka ngoja tuone mwisho wao na wakae wakijua haya yana mwisho.
 
Tatizo JF imeingiliwa na wavuta bange wa KLM na tatizo lingine Max nae alikubali kutumiwa na wanasiasa mpk anakubali kuendesha account ya wanasiasa km wakala wao. Amewai kutuhumiwa kulipwa pesa nyingi na mafisadi lkn hakuna Mahala alikanusha. Mbaya zaidi Kuna baadhi ya wanasiasa ukipost tu zao zinafutwa chap chap lkn Mh Rais anatukanwa mpk Basi. Mwisho nakubaliana na Wewe Max kuachwa huru
Acha ujinga hebu mtaje mmoja wa waliomo humu ambaye ni mvuta bangi, unataka kutuaminisha kuwa ukiwa na mawazo tofauti na uliyonayo wewe imani yako huyo mtu ni mvuta bangi, vilevile acha mawazo mgando mtu mwenye akili timamu akituhumiwa kwa jambo fulani sio lazima kujibu bali ni kulipuuza tu hivyo kukaa kimya ni jibu zuri kwa watoa tuhuma. Wewe unapenda kusikia jibu gani kutoka kwake au unataka aseme kweli alihongwa na kama ndivyo unapata faida gani?
 
Acha ujinga hebu mtaje mmoja wa waliomo humu ambaye ni mvuta bangi, unataka kutuaminisha kuwa ukiwa na mawazo tofauti na uliyonayo wewe imani yako huyo mtu ni mvuta bangi, vilevile acha mawazo mgando mtu mwenye akili timamu akituhumiwa kwa jambo fulani sio lazima kujibu bali ni kulipuuza tu hivyo kukaa kimya ni jibu zuri kwa watoa tuhuma. Wewe unapenda kusikia jibu gani kutoka kwake au unataka aseme kweli alihongwa na kama ndivyo unapata faida gani?
Hahahaha wewe ni moja wao wavuta bange make ktk post wala comment yangu hakuna Tusi lkn Wewe umejaza matusi kibao kwenye comment yako.
 
We usihoji uharali wake kama mhasisi wa jf. Bali tathimini Ujumbe na mambo yanayotokea juu ya uhuru wa vyombo vya habari na asasi za kijamii hususani kupitia mawasiliano ya mitandao.

Taifa letu, mawazo yetu.
 
kwanini msifunge tu office mkaziweke pale new York tuchukue kama youtube au instagram na jina libaki lile lile maana ishakuwa kero
Na wakishapeleka pale hakuna ban tena watu tunajiachia kwa raha zetuu
 
Mwanakijiji, upo sawa.

Hata huko Marekani FBI walishindwa kuwalazimisha Apple kufungua simu ya iPhone ya Syed Farook kupitia mahakamani na mwishowe wakawatumia Cellebrite kufungua simu hiyo.

Pia, yule jamaa wa ZU aliporusha makombora yake kutokea London wakti ule raisi JK aliapa kwamba kama yeye ni raisi wa Tanzania basi yule kijana ni lazima angeletwa JNIA.

Serikali inazo nyenzo, vifaa na taaluma ya kubaini wale wote ambao wanarusha taarifa za uzushi, matusi , kejeli na kashfa kwa wahusika.

Hivyo jeshi la polisi lina wajibu wa kutumia nyezo hizo na taaluma waliyo nayo kuwachungua, kuwabaini na kuwakamata kama walivyofanya kwa jamaa wa ZU

Kuwatisha JF kwa kumkamata Maxence Melo ni kitendo cha uonevu.
Labda wana nyenzo ila wataalam hakuna
 
Sidhani kama kuna kifungu cha sheria kinachomlazimisha mmiliki wa social media kutoa taarifa kwa CCM ili awafunge wahusika virobani na kuwatupia mtoni. Watapambana lakini hawatashinda.
 
Sijawahi kuona serikali ya kizezeta kama hii ya sasa hivi.
 
"TUMEIPENDA WENYEWE , Wacha tuisome nambaa eeh, C.C.M MBELE KWA MBELE, ....C.C.M NI ILE OOH C.C.M NI ILE ILE"
 
1481691050786.png
 
Na bado, Hadi miaka kumi, Mtanyooka tu. Mtake msitake, Kutishia kuufunga mtandao wenu kwa serikali ni kicheko.
 
Kuna vitu huwezi kuvielewa kama umejaa ushabiki. Chadema messed up na hili limeunguza vingi sana. Tuache lawama tusimame na utaifa wetu ili tujenge Taifa bora kwa vizazi vinavyokuja.
issue ni max wa jf, chadema imeingiaje humu, tiririka na kilichosemwa, hukawii kusema ngoyai ndio kahusika, wakati kitu kipo wazi
 
Back
Top Bottom