Kweli Max Ndiye Yeye: Kwanini Sina Hofu

Kweli Max Ndiye Yeye: Kwanini Sina Hofu

Ukiangalia kwa umakini utaona tatizo lililopo limeanzia mbali... vijana wetu wa TISS hawana elimu nzuri, hii ni kutokana na mfumo tunaoutumia kuwasaili na kisha kuwaajili.

Pale JKT ndipo tumewatoa wengi, ikumbukwe mbali na wale wanaopita JKT kwa takwa la wizara ya elimu wapo walioamua kujitolea kwenda baada ya hali ngumu ya maisha, kushindwa kuendelea na masomo , , kuchokwa jamii au wazazi wao na kuona bora waende kusurubiwa huko labda watajifunza... sasa hawa ndio Tunao kwenye secret service watu walio shindwa maisha kisha zali likawaangukia.

TISS si chombo cha ku recruit wajinga wajinga etu anakuwa recruited kisa anauvumilivu wa viboko na adhabu. Mtu wa namna hii hana reasoning skills, anapelekeshwa kwa takwa la boss.

Boss nae ni zao hilo hilo matokeo yake vitu vinavyoamuliwa vinaibua misuguano isiyo ya lazima.

TISS watokane na vijana wetu waliosoma na wenye kitu kichwani. JamiiForums ingeweza kuwa hacked na information zote wangepata bila kumgusa Max.

Max aachiwe ikiwa watawala wanahitaji amani mitandaoni na kwenye nafasi zao zenye dhamana ya wapiga kura.
 
Mwanakijiji, wakati tunaanza awamu ya tano; na mpaka sasa ukiacha thread hii, umekuwa mstari wa mbele kila wananchi walipolalamika dhidi ya matumizi ya mabavu kwa raia wasio na hatia ikiwemo swala la mikutano, kujumuika na mengineyo ambayo ukawa wameyasimamia bila kuchoka wewe uliwapinga kwa kutumia hapa KAZI TU; kunaa maandiko mengi ya aina hiyo ukijua wengine tunaona kama umehusika kumuuza MAX pengine maana ulibadilika kwa kiwango cha aibu na kujishushia heshima adhimu; wenzako waliona mbali mbaya zaidi uliamini kinachofanywa sasa ni sahihi; sijui kwanini hamjuagi viashiria vya matumizi mabaya ya madaraka na kiujumla wewe myumbishaji mkubwa sana wa taifa hili; tulitaka kwenda ktk democrasia wewe unaturudisha nyuma; movement is unstoppable we have to keep on moving na wewe Mwanakijiji uache unafiki
 
Mwigulu nchemba ni waziri mwenye dhamana hiyo na ni mwanachama wa Jamii Forum verified user...kwa namna moja ama nyingine anaweza kuhusika katika hili...ajitokeze hadharan sasa
Hapo sasa ......... Naona Magufuri aanze kwa kuwapiga ban Mawaziri wake wasichangie JF!!

Mwigulu, Kingwangalla. ....!!
 
Serikali inacheza mchezo usioujua lazima wataangukia pua.
 
“Democracy must be something more than two wolves and a sheep voting on what to have for dinner.”
James Bovard.
 
hapa ni uweledi wawahusika katika kwenda na wakati ,katika ulimwengu huu wa digital economy ukifanikiwa kutoa taswira hasi katika jamii umeua morali ya vijana wengi wa IT, Badala ya kuwa wabunifu kama MELO ,kivuli hiki kitawatisha kutoa wazo alilokuwa nalo na akifanikiwa atafanya nje ya nchi sehemu atakayoona mawazo yake ,ubunifu wake unaheshimiwa na kuzingatiwa ,tujali ubunifu ,pia tuungane na ubunifu huo .na tuwafanye vijana wapende kuwa wabunifu ili kuimarisha sekta binafsi katika soko la ajira ,
 
Katika watu wa hovyo kabisa ni wewe.Huwa unacheza siasa za kirungu yeye hapa sana.Sasa uliowatetea huwezi wadhibiti hata wewe mwenyewe?Ndio shida ya ukarunguyeye km wa Pasco. Unaomba nini hapa wakati waliomshikilia ndio huwa kipindi cha uchaguzi unaandika thread ndeefu na amkala kila mahali kutetea roho zao.Ipo siku utabaki wewe na wao.
Kwa ufupi Mwanakijiji ni mnafiki kwenye swala hili.
 
Mkuu anatakiwa ausome huu msitari, especially part ya mwisho ya msitari huu
Mimi nashangaa sana mtu anataka kuongoza taifa gani bila kulaumiwa wala kukosolewa..

Hiki kizazi cha kuhoji mambo..

Mungu mwenyewe analaumiwa kwa kushindwa kumsamehe Adam na kumrudisha Edeni!
 
jamaa ni mnafiki wa kiwango cha juu sana....huyu hana tofauti na wale wasomi wa UDSM idara ya sayansi ya siasa,akina bashiru na bana.
Huyu mwenyewe nimepiga naye kitabu hapo unapo pataja
 
Mwanakijiji, wakati tunaanza awamu ya tano; na mpaka sasa ukiacha thread hii, umekuwa mstari wa mbele kila wananchi walipolalamika dhidi ya matumizi ya mabavu kwa raia wasio na hatia ikiwemo swala la mikutano, kujumuika na mengineyo ambayo ukawa wameyasimamia bila kuchoka wewe uliwapinga kwa kutumia hapa KAZI TU; kunaa maandiko mengi ya aina hiyo ukijua wengine tunaona kama umehusika kumuuza MAX pengine maana ulibadilika kwa kiwango cha aibu na kujishushia heshima adhimu; wenzako waliona mbali mbaya zaidi uliamini kinachofanywa sasa ni sahihi; sijui kwanini hamjuagi viashiria vya matumizi mabaya ya madaraka na kiujumla wewe myumbishaji mkubwa sana wa taifa hili; tulitaka kwenda ktk democrasia wewe unaturudisha nyuma; movement is unstoppable we have to keep on moving na wewe Mwanakijiji uache unafiki
Shushushu huyo mwanakijiji...hana lolote mnafiki tuu aishie marekani. Naingiwa wasiwasi anahusika na hujuma hizi dhidi ya jf na max pia. Born killer always a killah
 
Tulisema mapema sana kuwa huyu mtu hafai kuwa juu ya watu bali chini ya mtu, tukapuuzwa, haya sasa kila mtu anafumbwa mdomo.
Tena tulisema sana kwa maumivu makali. Sasa kila mtu kwa zamu anaisoma namba akiwemo mzee wetu MMM. Anyway, mzee MMM amekuwa objective sana katika maelezo yake. The irony is that hata waliomsapot huyu mkuu sasa wengi wao wanajutia maamuzi yao. Mimi na wewe tuliojua zamani tuko tayari kisaikolojia!
 
Jf ikifungwa waathirika wa mwanzo polisi kitwa wanashinda humu
Bora wamuachie max tu
 
Ukiangalia kwa umakini utaona tatizo lililopo limeanzia mbali... vijana wetu wa TISS hawana elimu nzuri, hii ni kutokana na mfumo tunaoutumia kuwasaili na kisha kuwaajili.

Pale JKT ndipo tumewatoa wengi, ikumbukwe mbali na wale wanaopita JKT kwa takwa la wizara ya elimu wapo walioamua kujitolea kwenda baada ya hali ngumu ya maisha, kushindwa kuendelea na masomo , , kuchokwa jamii au wazazi wao na kuona bora waende kusurubiwa huko labda watajifunza... sasa hawa ndio Tunao kwenye secret service watu walio shindwa maisha kisha zali likawaangukia.

TISS si chombo cha ku recruit wajinga wajinga etu anakuwa recruited kisa anauvumilivu wa viboko na adhabu. Mtu wa namna hii hana reasoning skills, anapelekeshwa kwa takwa la boss.

Boss nae ni zao hilo hilo matokeo yake vitu vinavyoamuliwa vinaibua misuguano isiyo ya lazima.

TISS watokane na vijana wetu waliosoma na wenye kitu kichwani. JamiiForums ingeweza kuwa hacked na information zote wangepata bila kumgusa Max.

Max aachiwe ikiwa watawala wanahitaji amani mitandaoni na kwenye nafasi zao zenye dhamana ya wapiga kura.
Wamejaa humu akina lizaboni,wakudadavua,mwasita etc
 
Back
Top Bottom