JembeNaNyundo
JF-Expert Member
- Dec 9, 2016
- 533
- 652
Jembe Na Nyundo
That's what I'm talking about! Kuna washauri wanamuingiza shimoni Rais wetu ....
Na. M. M. Mwanakijiji
- Mimi ni Miongoni mwa Waasisi wa JF
- Uhuru wa Maoni na Kujieleza Usitishiwe
- Max Mello Aachiliwe Ndani ya Masaa 24
- Kuungwa Mkono Haina Maana Kukubaliwa Lolote
Kwanza kabisa niseme kuwa mimi ni mmoja wa waanzilishi wa mtandao huu. Siyo tu miongoni mwa wanachama wa mwanzo lakini pia miongoni mwa watu waliokaa na kufanya majadiliano ya kuihamisha jukwaa la mijadala tangu ikiwa bcstimes na baadaye Jambo Forums na hatimaye Jamiiforums.
Tulihamisha kutoka bcstimes kwa sababu haikuwa na facilities na uwezo tunaoutaka kuweka kuisimamia. Tulihama kutoka Jambo Forums hadi JamiiForums kufuatia kukamatwa kwa Max na Mike mwezi Februari 2008 na mtu mmoja (alikuwa kada wa chama fulani) kuchukua jina la Jambo Forums na kugoma kuturudishia! Ili tusipotee sana tukaamua kuiita JamiiForums (ili kubakia na initial zile zile za JF - ikiwa ni sababu mojawapo).
Mimi ndiye mbunifu wa msemo wa "where we dare (to) talk openly".
Walipokamatwa kina Max nilienda hadi BBC na kujenga hoja ya kuwa uhuru wa maoni haulindi maoni mazuri tu nayale tunayoyapenda, bali unalinda hasa maoni mabovu, tusiyoyapenda na nikasema kuwa "unalinda hata maoni ya kijinga"! Ukweli huu wa miaka nane nyuma naamini bado ni ukweli uliopo sasa.
Max na wenzetu waliopo nyumbani walichukua jukumu la kujaribu kurasimisha mtandao huu kuwa kampuni ili sehemu yake moja isiwe inafanywa gizani na kuweka taratibu mbalimbali za kuhakikisha uhuru wa maoni unakuwepo na watu wanaotaka kutumia majina halisi wanafanya hivyo -wakati ule karibu wote tulikuwa tunatumia majina ya kiuandishi (pen names). Lakini pia hatukutaka kuzuia watu wengine kuendelea kuandika under pseudonyms. Sababu yake ni kuwa ili kuweza kupata habari, kuchochea mijadala na kuwapatia Watanzania habari kwa undani na maoni bila kuogopa adhabu basi tuliacha iwe hivyo.
Hili lilisaidia mtandao huu kufichua baadhi ya kashfa nyingi na mbalimbali bila ya watu kuhofia kujulikana kwani hadi hivi sasa Tanzania haina Sheria ya kumlinda mfichua uovu! (whistle blower protection act). Hivyo, ni kwa kutumia mitandao hii na namna ya usiri ndio maana hili la kuwa na pen names limeendelea na ninaamini litaendelea kwa muda mrefu ujao.
Ni kwa sababu hiyo kwanza sijashtushwa na kukamatwa kwa Max wala kushtushwa na ujio wa sheria ya Cybercrime. Vyote hivi ni vitu ambavyo nilivitarajia bila kujali nani angekuwa mshindi mwaka jana. Vitu hivyo vingekuwa tofauti tu kama upinzani wa kweli ungeshinda mwaka jana. Hilo pembeni.
Kumkamata Max na kujaribu kumlazimisha au kuilazimisha JamiiForums kutoa majina ya watu ili kufanya kazi ya serikali iwe rahisi au kuwafanyia serikali kazi ambayo wao wanapaswa kuifanya ni dalili ya uzembe uliopitiliza. Hili nililsema mwaka 2008 na nalirudia tu tena. Serikali ina jukumu la kufanya kazi yake lakini ni lazima ijaribu kufanya kazi yake kwa weledi wake wote.
Serikali ina uwezo (wa kifedha na kiutaalam) wa kufuatilia mawasiliano ya watu kwa mujibu wa sheria. Haiwezekani mtu aamue tu kutaka jina la fulani kwenye mtandao kwa sababu tu huyo fulani kaandika habari au kitu ambacho labda serikali inaamini wananchi hawakupaswa kukijua (kiwe cha kweli au la).
Lakini kubwa ni kuwa JF ina wanachama 360,000 hivi, sidhani kuna mtu yeyote anaamini Max anaweza kujua majina yote ya kweli au ya kiuandishi ya wanachama wote. Hata mtu akitumia jina la John Marko, ni vigumu kujua kama kweli ni jina lake kulinganisha na mtu anayejiita "Kifuu cha Nazi". Inawezekana anayeitwa Kifuu cha Nazi ndilo jina lake kweli na yule anayejiita John Marko ndiye anatumia jina la kiuandishi!
Kubwa zaidi hata hivyo ni kuwa badala ya kuhangaika na "nani kasema nini" ni vizuri serikali ihangaike na "Nani kafanya nini"! Lakini kama tunataka kufuatilia "nani kasema nini" ni vizuri zaidi kujali "nini kimesemwa na nani" na hivyo kuangalia na kutoa majibu muafaka na yenye kuridhisha. Tatizo la maswali ni kuwa hata ukamate wote wanaoyauliza kwa kadiri kwamba huyajibu maswali ya, maswali yataendelea kuulizwa tu hata na wale wasiyoyauliza hadharani!.
Hivyo basi, ni maoni yangu na naweza kusema ni wito wangu kuwa vitisho kwa vyombo vya habari, mitandao ya kijamii au watu wanaoikosoa havina sababu ya msingi na Max Mello aachiliwe bila masharti yeyote na kuwa serikali imwombe radhi kwa usumbufu na kutambua mchango mkubwa JamiiForums imeutoa kwa Tanzania na kwa tasnia ya habari kuanzia 2006.
Niseme tu kuwa Max aachiliwe bila masharti y0yote ndani ya masaa 24 yajayo, kinyume cha hivyo mtatulazimisha waanzilishi hasa wa mtandao huu kufunga JamiiForums Tanzania na ofisi zake na kuurudisha gizani na hivyo siyo tu kuwakosesha hata nafasi ya kuwafikia wananchi wengi ambao wanatumia mtandao huu kupata habari kwa usahihi ndani na nje ya nchi lakini pia kutoa nafasi kwa watoa maoni wa ndani ya serikali kuwafikia wapiga kura na wananchi.
Haki ya Watanzania kupata habari, kujieleza kwa uhuru na kutoa maoni ni kubwa zaidi kuliko hata misimamo yetu baadhi yetu ya kuunga mkono mabadiliko ambayo tumeyaona. Kama nilivyowahi kusema kuna gharama ambayo watu wanaweza kukubali kuilipa kwa ajili ya mabadiliko wanayoyataka, lakini kuna gharama nyingine hailipiki.
MMM
Kuna vitu huwezi kuvielewa kama umejaa ushabiki. Chadema messed up na hili limeunguza vingi sana. Tuache lawama tusimame na utaifa wetu ili tujenge Taifa bora kwa vizazi vinavyokuja.Tuendelee kuisifu tu serikali hii ya awamu ya tano. Si ndio huyu Mwanakijiji aliyeona ni bora ccm ishinde? Sasa tusilalamike. Hiyo lugha ya "upinzani wa kweli" haina tija kwa taifa letu, la msingi lilikuwa ccm itoke. Tuache tu tupate matokeo ya kuunga mkono ccm. Bado kwa staili hii kila mtu atafikiwa, ni zamu mpaka tuisome namba.
Labda swali dogo tu kwako,
Tukiacha ya kua wewe ni mmojawapo ya Waanzilishi, je wewe nawe sasa ni Mmojawapo ya wamiliki au wanahisa wa huu mtandao??
Tulisema mapema sana kuwa huyu mtu hafai kuwa juu ya watu bali chini ya mtu, tukapuuzwa, haya sasa kila mtu anafumbwa mdomo.teh! teh!,
kwa leo sisemi kitu kwa kuwa sasa nchi imeingia gizani,imetumbukia shimoni.
ila sisi tulianza kusema mapema,karibuni nanyi mjiunge,sasa tumekuwa wengi
Na. M. M. Mwanakijiji
- Mimi ni Miongoni mwa Waasisi wa JF
- Uhuru wa Maoni na Kujieleza Usitishiwe
- Max Mello Aachiliwe Ndani ya Masaa 24
- Kuungwa Mkono Haina Maana Kukubaliwa Lolote
Kwanza kabisa niseme kuwa mimi ni mmoja wa waanzilishi wa mtandao huu. Siyo tu miongoni mwa wanachama wa mwanzo lakini pia miongoni mwa watu waliokaa na kufanya majadiliano ya kuihamisha jukwaa la mijadala tangu ikiwa bcstimes na baadaye Jambo Forums na hatimaye Jamiiforums.
Tulihamisha kutoka bcstimes kwa sababu haikuwa na facilities na uwezo tunaoutaka kuweka kuisimamia. Tulihama kutoka Jambo Forums hadi JamiiForums kufuatia kukamatwa kwa Max na Mike mwezi Februari 2008 na mtu mmoja (alikuwa kada wa chama fulani) kuchukua jina la Jambo Forums na kugoma kuturudishia! Ili tusipotee sana tukaamua kuiita JamiiForums (ili kubakia na initial zile zile za JF - ikiwa ni sababu mojawapo).
Mimi ndiye mbunifu wa msemo wa "where we dare (to) talk openly".
Walipokamatwa kina Max nilienda hadi BBC na kujenga hoja ya kuwa uhuru wa maoni haulindi maoni mazuri tu nayale tunayoyapenda, bali unalinda hasa maoni mabovu, tusiyoyapenda na nikasema kuwa "unalinda hata maoni ya kijinga"! Ukweli huu wa miaka nane nyuma naamini bado ni ukweli uliopo sasa.
Max na wenzetu waliopo nyumbani walichukua jukumu la kujaribu kurasimisha mtandao huu kuwa kampuni ili sehemu yake moja isiwe inafanywa gizani na kuweka taratibu mbalimbali za kuhakikisha uhuru wa maoni unakuwepo na watu wanaotaka kutumia majina halisi wanafanya hivyo -wakati ule karibu wote tulikuwa tunatumia majina ya kiuandishi (pen names). Lakini pia hatukutaka kuzuia watu wengine kuendelea kuandika under pseudonyms. Sababu yake ni kuwa ili kuweza kupata habari, kuchochea mijadala na kuwapatia Watanzania habari kwa undani na maoni bila kuogopa adhabu basi tuliacha iwe hivyo.
Hili lilisaidia mtandao huu kufichua baadhi ya kashfa nyingi na mbalimbali bila ya watu kuhofia kujulikana kwani hadi hivi sasa Tanzania haina Sheria ya kumlinda mfichua uovu! (whistle blower protection act). Hivyo, ni kwa kutumia mitandao hii na namna ya usiri ndio maana hili la kuwa na pen names limeendelea na ninaamini litaendelea kwa muda mrefu ujao.
Ni kwa sababu hiyo kwanza sijashtushwa na kukamatwa kwa Max wala kushtushwa na ujio wa sheria ya Cybercrime. Vyote hivi ni vitu ambavyo nilivitarajia bila kujali nani angekuwa mshindi mwaka jana. Vitu hivyo vingekuwa tofauti tu kama upinzani wa kweli ungeshinda mwaka jana. Hilo pembeni.
Kumkamata Max na kujaribu kumlazimisha au kuilazimisha JamiiForums kutoa majina ya watu ili kufanya kazi ya serikali iwe rahisi au kuwafanyia serikali kazi ambayo wao wanapaswa kuifanya ni dalili ya uzembe uliopitiliza. Hili nililsema mwaka 2008 na nalirudia tu tena. Serikali ina jukumu la kufanya kazi yake lakini ni lazima ijaribu kufanya kazi yake kwa weledi wake wote.
Serikali ina uwezo (wa kifedha na kiutaalam) wa kufuatilia mawasiliano ya watu kwa mujibu wa sheria. Haiwezekani mtu aamue tu kutaka jina la fulani kwenye mtandao kwa sababu tu huyo fulani kaandika habari au kitu ambacho labda serikali inaamini wananchi hawakupaswa kukijua (kiwe cha kweli au la).
Lakini kubwa ni kuwa JF ina wanachama 360,000 hivi, sidhani kuna mtu yeyote anaamini Max anaweza kujua majina yote ya kweli au ya kiuandishi ya wanachama wote. Hata mtu akitumia jina la John Marko, ni vigumu kujua kama kweli ni jina lake kulinganisha na mtu anayejiita "Kifuu cha Nazi". Inawezekana anayeitwa Kifuu cha Nazi ndilo jina lake kweli na yule anayejiita John Marko ndiye anatumia jina la kiuandishi!
Kubwa zaidi hata hivyo ni kuwa badala ya kuhangaika na "nani kasema nini" ni vizuri serikali ihangaike na "Nani kafanya nini"! Lakini kama tunataka kufuatilia "nani kasema nini" ni vizuri zaidi kujali "nini kimesemwa na nani" na hivyo kuangalia na kutoa majibu muafaka na yenye kuridhisha. Tatizo la maswali ni kuwa hata ukamate wote wanaoyauliza kwa kadiri kwamba huyajibu maswali ya, maswali yataendelea kuulizwa tu hata na wale wasiyoyauliza hadharani!.
Hivyo basi, ni maoni yangu na naweza kusema ni wito wangu kuwa vitisho kwa vyombo vya habari, mitandao ya kijamii au watu wanaoikosoa havina sababu ya msingi na Max Mello aachiliwe bila masharti yeyote na kuwa serikali imwombe radhi kwa usumbufu na kutambua mchango mkubwa JamiiForums imeutoa kwa Tanzania na kwa tasnia ya habari kuanzia 2006.
Niseme tu kuwa Max aachiliwe bila masharti y0yote ndani ya masaa 24 yajayo, kinyume cha hivyo mtatulazimisha waanzilishi hasa wa mtandao huu kufunga JamiiForums Tanzania na ofisi zake na kuurudisha gizani na hivyo siyo tu kuwakosesha hata nafasi ya kuwafikia wananchi wengi ambao wanatumia mtandao huu kupata habari kwa usahihi ndani na nje ya nchi lakini pia kutoa nafasi kwa watoa maoni wa ndani ya serikali kuwafikia wapiga kura na wananchi.
Haki ya Watanzania kupata habari, kujieleza kwa uhuru na kutoa maoni ni kubwa zaidi kuliko hata misimamo yetu baadhi yetu ya kuunga mkono mabadiliko ambayo tumeyaona. Kama nilivyowahi kusema kuna gharama ambayo watu wanaweza kukubali kuilipa kwa ajili ya mabadiliko wanayoyataka, lakini kuna gharama nyingine hailipiki.
MMM
Tuendelee kuisifu tu serikali hii ya awamu ya tano. Si ndio huyu Mwanakijiji aliyeona ni bora ccm ishinde? Sasa tusilalamike. Hiyo lugha ya "upinzani wa kweli" haina tija kwa taifa letu, la msingi lilikuwa ccm itoke. Tuache tu tupate matokeo ya kuunga mkono ccm. Bado kwa staili hii kila mtu atafikiwa, ni zamu mpaka tuisome namba.
Hiyo domain ya Jamboforums huyo mwanasiasa aliwarudishia? Maana inaonesha registrant ni Maxence Melo!!!
Baada ya JF kupata cyber attack mwaka jana nilianza kuhisi JF sio salama tena,Max Namuomba MUNGU akulinde kwenye hiki kipindi kigumu
Wewe ni mnafiki tu mng'ata na kupuliza.Nina donge kifuani hadi kuchangia nashindwa, naomba Mungu anipe wepesi juu ya serikali hii.!
Mkuu, tuliona hali hiyo lakini nafikiri limejikita zaidi kwenye mgawanyo wa majukumu kati ya Mike na Max.
Bado najiuliza walikosea wapi kwenye ile "cyber attack", labda mkuu Mwanakijiji atakuwa na "head up" kadhaa.
kwenye page ya hapo juu umewapinga wale ambao page ya pili umekiri "kuunga mabadiliko unayayoona" (naomba ufafanuzi).Pia page ya juu umehukumu hata wale ambao hawajawahi kushika dola kwamba ukitabiri kwamba hata kama nao wengeshinda wangekuja na sheria hii labda ingekuwa "upinzani wa kweli ungeshinda"(kwa mujibu wako) .Yafaa kuandika bila propaganda(kung'ata na kupuliza)Ni kwa sababu hiyo kwanza sijashtushwa na kukamatwa kwa Max wala kushtushwa na ujio wa sheria ya Cybercrime. Vyote hivi ni vitu ambavyo nilivitarajia bila kujali nani angekuwa mshindi mwaka jana. Vitu hivyo vingekuwa tofauti tu kama upinzani wa kweli ungeshinda mwaka jana. Hilo pembeni.
Haki ya Watanzania kupata habari, kujieleza kwa uhuru na kutoa maoni ni kubwa zaidi kuliko hata misimamo yetu baadhi yetu ya kuunga mkono mabadiliko ambayo tumeyaona. Kama nilivyowahi kusema kuna gharama ambayo watu wanaweza kukubali kuilipa kwa ajili ya mabadiliko wanayoyataka, lakini kuna gharama nyingine hailipiki.
MMM
Kuna vitu huwezi kuvielewa kama umejaa ushabiki. Chadema messed up na hili limeunguza vingi sana. Tuache lawama tusimame na utaifa wetu ili tujenge Taifa bora kwa vizazi vinavyokuja.