Kweli Max Ndiye Yeye: Kwanini Sina Hofu

Kweli Max Ndiye Yeye: Kwanini Sina Hofu

Free Max haraka. Waangalie jinsi ya kutatua matatizo yanayowakumba watanzania sio kudeal na individuals,hapo wanaonyesha wamepotea,Max ni kama tone la maji baharini wasipotatua matatizo yaliyopo itafikia kipindi watakamata nchi nzima na kuiweka ndani ikiwemo na wao wenyewe maana kila mtu atalalamika including themselves.
 
Mwanakijiji, upo sawa.

Hata huko Marekani FBI walishindwa kuwalazimisha Apple kufungua simu ya iPhone ya Syed Farook kupitia mahakamani na mwishowe wakawatumia Cellebrite kufungua simu hiyo.

Pia, yule jamaa wa ZU aliporusha makombora yake kutokea London wakti ule raisi JK aliapa kwamba kama yeye ni raisi wa Tanzania basi yule kijana ni lazima angeletwa JNIA.

Serikali inazo nyenzo, vifaa na taaluma ya kubaini wale wote ambao wanarusha taarifa za uzushi, matusi , kejeli na kashfa kwa wahusika.

Hivyo jeshi la polisi lina wajibu wa kutumia nyezo hizo na taaluma waliyo nayo kuwachungua, kuwabaini na kuwakamata kama walivyofanya kwa jamaa wa ZU

Kuwatisha JF kwa kumkamata Maxence Melo ni kitendo cha uonevu.

Kweli kabisa inawezekaneje umkamate max atoe jina wakat serikal inaweza kwa kila kitu,mnaweza fatilien mmkamate sio max, hana kosa hata kidogo acha wtu waongee watoe sum moyon,kama jambo limegusa lekebisha il wtu wsiseme ndo dawa
Umekunya sehem ukaacha kinyes kukizoa akija mwingne nae atakunya hapohapo hivyo zoa kinyes ili mwngne asifanye hivyo.
 
Mshajiuliza why members hawapewi options za kukuta threads zao walizoanzisha? Kwa nini JF inataka. Kuhodhi kila kitu?

Uongozi haijulikani ni akina nani maana kila mtu anaclaim kuwa yeye ni kiongozi na mwanzilishi na shareholder lakini mbona hakuna shareholders agreements au leadership elections na objectives na strategic plan??

Naamini umemaanisha kufuta.
Kuna mdau kaonesha wewe ni mpya hivyo huu muziki bado hujazijua steps.

Nimependa unavyojiuliza kua kwanini members hatuwezi kufuta threads? Ila umeshindwa kwenda mbele na kutambua kua;
Ulichoanzisha kikiwa ni mwiba kwa mtu husika huku kina faida kwa majority, huyo mtu akakutaka uufute uzi na ukaufuta maana yake majority watakua wamenyimwa haki yao kubwa tu, kuzuia hilo ufunguo wa kufuta uzi upo kwa wasimamizi.

Ingia fanya utafiti wa kusearch net uwajue wamiliki, kuhusu hisa obviously hata mimi nigekua Melo nisingeruhusu kuuza hisa vipi kama mwanahisa mpya ni kirusi? (Ingawa sijui kama hisa hua hazitangazwi).
Mengine piga simu ofisini kwao naamini. utaelekezwa.

Pia uache kufananisha JF na nchi.
 
Tatizo la humu kumejaa uccm na uchadema tu,na ndiyo maana hata hili suala la kukamatwa Max pia linajadiliwa kwa mtindo huo huo wa kivyama vyama.
 
Mwigulu nchemba ni waziri mwenye dhamana hiyo na ni mwanachama wa Jamii Forum verified user...kwa namna moja ama nyingine anaweza kuhusika katika hili...ajitokeze hadharan sasa
 
Yes ...wananchi ndio wenye nchi ..

Ningemshauri JPM kama atasoma uzi huu achukue muda asome kwa makini CONCESSION SPEECH ya RAIS mstaafu wa GHANA MAHAMA, kuna mengi ya kujifunza mle!!!
 
NAUNGANA NA WEWE MZEE MWANAKIJIJI.
MIMI PIA NI MIONGONI MWA WASOMAJI WAKONGWE TANGU JAMBO FORUMS.
NAKIRI KUTOFAUTIANA NA WEWE KATIKA BAADHI YA MADA (POST) LAKINI KWA HILI LA MAX, NIKO PAMOJA NA WEWE KWA ASILIMIA100. HAO WANAOTISHIA JF NA VIONGOZI WAO WAMEKOSA UPEO WA KUJUA MANUFAA KWA UMMA YALIYOKWISHA PATIKANA NA YANAYOENDELEA KUPATIKANA NDANI YA JF. KWA HAKIKA HAKUNA MFANO WAKE NDANI TANZANIA, E A & C AFRICA. JF IKO JUU SANA, KWINGINE SIJUI.
 
Kwa akili za watu kama Mwanakijiji unaweza kuta taarifa zetu zishapelekwa...

Endeleeni kuandika makala za kusifia
 
Unataka kukimbia na hauna break what do you expect?

Nchi inayumba mwanzoni kabisa mwa mteremko mkali sana kilomita kadhaa mbele kuna mto mkubwa sana...je nini kinafuata ?
Rais na wasaidizi wake wameshindwa kuongoza na kushauriana juu ya nini cha kufanya na wapi pa kufanya, nini cha kusema na wapi pa kusema!

Nchi ipo mikononi mwa mtu asiyeweza kuongoza na hakubali kuwa hawezi nchi hii haiitaji mtawala kwa kuwa kuna sheria na katiba ambavyo ni lazima ufuate.
Tunahitaji uhuru wa habari na kujieleza, kupata na kutoa habari kwa muda muafaka. #S T O P C R U E L T Y
US court forces Microsoft to hand over personal data from Irish server

hii ni nchi mwanakijiji amekimbilia kuishi.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

  • Mimi ni Miongoni mwa Waasisi wa JF
  • Uhuru wa Maoni na Kujieleza Usitishiwe
  • Max Mello Aachiliwe Ndani ya Masaa 24
  • Kuungwa Mkono Haina Maana Kukubaliwa Lolote

Kwanza kabisa niseme kuwa mimi ni mmoja wa waanzilishi wa mtandao huu. Siyo tu miongoni mwa wanachama wa mwanzo lakini pia miongoni mwa watu waliokaa na kufanya majadiliano ya kuihamisha jukwaa la mijadala tangu ikiwa bcstimes na baadaye Jambo Forums na hatimaye Jamiiforums.

Tulihamisha kutoka bcstimes kwa sababu haikuwa na facilities na uwezo tunaoutaka kuweka kuisimamia. Tulihama kutoka Jambo Forums hadi JamiiForums kufuatia kukamatwa kwa Max na Mike mwezi Februari 2008 na mtu mmoja (alikuwa kada wa chama fulani) kuchukua jina la Jambo Forums na kugoma kuturudishia! Ili tusipotee sana tukaamua kuiita JamiiForums (ili kubakia na initial zile zile za JF - ikiwa ni sababu mojawapo).

Mimi ndiye mbunifu wa msemo wa "where we dare (to) talk openly".

Walipokamatwa kina Max nilienda hadi BBC na kujenga hoja ya kuwa uhuru wa maoni haulindi maoni mazuri tu nayale tunayoyapenda, bali unalinda hasa maoni mabovu, tusiyoyapenda na nikasema kuwa "unalinda hata maoni ya kijinga"! Ukweli huu wa miaka nane nyuma naamini bado ni ukweli uliopo sasa.

Max na wenzetu waliopo nyumbani walichukua jukumu la kujaribu kurasimisha mtandao huu kuwa kampuni ili sehemu yake moja isiwe inafanywa gizani na kuweka taratibu mbalimbali za kuhakikisha uhuru wa maoni unakuwepo na watu wanaotaka kutumia majina halisi wanafanya hivyo -wakati ule karibu wote tulikuwa tunatumia majina ya kiuandishi (pen names). Lakini pia hatukutaka kuzuia watu wengine kuendelea kuandika under pseudonyms. Sababu yake ni kuwa ili kuweza kupata habari, kuchochea mijadala na kuwapatia Watanzania habari kwa undani na maoni bila kuogopa adhabu basi tuliacha iwe hivyo.

Hili lilisaidia mtandao huu kufichua baadhi ya kashfa nyingi na mbalimbali bila ya watu kuhofia kujulikana kwani hadi hivi sasa Tanzania haina Sheria ya kumlinda mfichua uovu! (whistle blower protection act). Hivyo, ni kwa kutumia mitandao hii na namna ya usiri ndio maana hili la kuwa na pen names limeendelea na ninaamini litaendelea kwa muda mrefu ujao.

Ni kwa sababu hiyo kwanza sijashtushwa na kukamatwa kwa Max wala kushtushwa na ujio wa sheria ya Cybercrime. Vyote hivi ni vitu ambavyo nilivitarajia bila kujali nani angekuwa mshindi mwaka jana. Vitu hivyo vingekuwa tofauti tu kama upinzani wa kweli ungeshinda mwaka jana. Hilo pembeni.

Kumkamata Max na kujaribu kumlazimisha au kuilazimisha JamiiForums kutoa majina ya watu ili kufanya kazi ya serikali iwe rahisi au kuwafanyia serikali kazi ambayo wao wanapaswa kuifanya ni dalili ya uzembe uliopitiliza. Hili nililsema mwaka 2008 na nalirudia tu tena. Serikali ina jukumu la kufanya kazi yake lakini ni lazima ijaribu kufanya kazi yake kwa weledi wake wote.

Serikali ina uwezo (wa kifedha na kiutaalam) wa kufuatilia mawasiliano ya watu kwa mujibu wa sheria. Haiwezekani mtu aamue tu kutaka jina la fulani kwenye mtandao kwa sababu tu huyo fulani kaandika habari au kitu ambacho labda serikali inaamini wananchi hawakupaswa kukijua (kiwe cha kweli au la).

Lakini kubwa ni kuwa JF ina wanachama 360,000 hivi, sidhani kuna mtu yeyote anaamini Max anaweza kujua majina yote ya kweli au ya kiuandishi ya wanachama wote. Hata mtu akitumia jina la John Marko, ni vigumu kujua kama kweli ni jina lake kulinganisha na mtu anayejiita "Kifuu cha Nazi". Inawezekana anayeitwa Kifuu cha Nazi ndilo jina lake kweli na yule anayejiita John Marko ndiye anatumia jina la kiuandishi!

Kubwa zaidi hata hivyo ni kuwa badala ya kuhangaika na "nani kasema nini" ni vizuri serikali ihangaike na "Nani kafanya nini"! Lakini kama tunataka kufuatilia "nani kasema nini" ni vizuri zaidi kujali "nini kimesemwa na nani" na hivyo kuangalia na kutoa majibu muafaka na yenye kuridhisha. Tatizo la maswali ni kuwa hata ukamate wote wanaoyauliza kwa kadiri kwamba huyajibu maswali ya, maswali yataendelea kuulizwa tu hata na wale wasiyoyauliza hadharani!.

Hivyo basi, ni maoni yangu na naweza kusema ni wito wangu kuwa vitisho kwa vyombo vya habari, mitandao ya kijamii au watu wanaoikosoa havina sababu ya msingi na Max Mello aachiliwe bila masharti yeyote na kuwa serikali imwombe radhi kwa usumbufu na kutambua mchango mkubwa JamiiForums imeutoa kwa Tanzania na kwa tasnia ya habari kuanzia 2006.

Niseme tu kuwa Max aachiliwe bila masharti y0yote ndani ya masaa 24 yajayo, kinyume cha hivyo mtatulazimisha waanzilishi hasa wa mtandao huu kufunga JamiiForums Tanzania na ofisi zake na kuurudisha gizani na hivyo siyo tu kuwakosesha hata nafasi ya kuwafikia wananchi wengi ambao wanatumia mtandao huu kupata habari kwa usahihi ndani na nje ya nchi lakini pia kutoa nafasi kwa watoa maoni wa ndani ya serikali kuwafikia wapiga kura na wananchi.

Haki ya Watanzania kupata habari, kujieleza kwa uhuru na kutoa maoni ni kubwa zaidi kuliko hata misimamo yetu baadhi yetu ya kuunga mkono mabadiliko ambayo tumeyaona. Kama nilivyowahi kusema kuna gharama ambayo watu wanaweza kukubali kuilipa kwa ajili ya mabadiliko wanayoyataka, lakini kuna gharama nyingine hailipiki.

MMM

Ulikuwa wapi wewe?. Umetutia moyo sana kwamba kuna watu wenye akili na weredi nyuma ya Jamiiforums. Nikisoma kwa makini uzi huu ninapiga taswila kama ungekuwa mahali fulani hivi.
 
Mkuu MMM usisahau kuwa waliomkamata Max Februari 2008 ni tofauti na waliomkamata sasa, hata kama ni serikali ya chama kile kile! Ni vema kuwa tayari kwa yasiyotarajiwa!
WAnaharakati huwa hawana cha kuogopa. Come what may. Wataendelea kuwepo, na utawaacha utakapo kufa.
 
Tuendelee kuisifu tu serikali hii ya awamu ya tano. Si ndio huyu Mwanakijiji aliyeona ni bora ccm ishinde? Sasa tusilalamike. Hiyo lugha ya "upinzani wa kweli" haina tija kwa taifa letu, la msingi lilikuwa ccm itoke. Tuache tu tupate matokeo ya kuunga mkono ccm. Bado kwa staili hii kila mtu atafikiwa, ni zamu mpaka tuisome namba.
Wote tunataka CCM iondoke tatizo upinzani haukuwa na mgombea mwaka jana.
 
Ngoja kidogo hapo mwisho mbona wao ndio lengo lao?yaani uufunge huu mtandao wewe?hilo si ndio lengo la malaika mkuu wa nchi ile? Hapana bwana pamoja na maelezo yote hitinisho lako sikubaliani nalo
 
Bado miaka mingapi il 2020 tumalize hii shida ? Mamvi hana kampeni ataulizwa tu utagombea hugombei akisema ndio tu ,watu wanarudi nyumbani wanasubiri siku ta kura wafanye yao! Mwe!watu tumechoka asubuhi na mapema! Mtu mbane lakini mwachie domo lake apige mayowe kupunguza maumivu!
 
kikubwa tuache matusi kwani mkuu hakatai kupingwa ila kutukana sio sahihi hata kama una hasira kiasi gani usitukane....
 
Back
Top Bottom