Kwanini watu wa hali ya chini wanamchukia sana Rais Samia?!

Kwanini watu wa hali ya chini wanamchukia sana Rais Samia?!

Nchi hii imerudi kwa Watu wanaostahili;sasa ni ya Wasomi, Wanasiasa na Wafanyabiashara!

Kama haupo kwenye hayo Makundi utasaga meno—-

Magufuri alidhulumu sana haki za hayo makundi na masikini walifurahia Alipopora democracy, Alipokataa Serikali kutafutia ajira Watu wake na alipowanyanganya Wafanyabiashara mali zao kwa nguvu!
 
Wiki jana nikiwa safarini kuelekea magharibi mwa Tanzania nilijipa kazi ya kutafiti uungwaji mkono wa Rais Samia kwa wananchi anaowaongoza.

Asilimia 90 ya watu wa hali ya chini hawamkubali Samia! Na ndani ya hizo 90% 50 yao hawataki kabisa hata kulisikia jina lake.Iliniogopesha!

Hali hiyo ilikuwa tofauti kwa wafanyabiashara.Wengi wao wanadai hawasumbuliwi hasa na mambo ya risti za EFD na kwalo wanadai wanapiga pesa kwa lugha ya mtaani.

Kazi iendelee.
Watu wajinga marekani hawachagui Raisi
Tuwe na katiba ambayo watu wenye akili ndo watuchagulie raisi
 
Pamoja na kwamba maisha ni kama msumari na nyundo lkn mi namkubali sana maza mjengo! Ana uvumilivu wa hoja pinzan lkn pia ni muwazi tofauti na ngosha! Huu ugumu mbona ni muendelezo tu! Tofaut kwamba tulikuwa hatuna pa kuongelea kwan ilikuwa ukipanua tu domo sandarusi au kupotezwa kuna kuhusu!
 
Majibu ya utafiti wako ni sahihi. Mimi pia niliwahi kuufanya utafiti kama wako na nikapata majibu kama yako.

Nilichokibaini ni hiki:-
-Watu wengi Wa chini uelewa wao upo chini sana. Hawamkubali Rais Samia kwa kuwa anaonekana ni mtu anayefuata taratibu tulizojiwekea kama Taifa. Na nyingi ya taratibu hizo ni kama vile haziwa-favour. Wanaona bora Rais aliyepita ambaye alikuwa anaamua kwa hisia tu. Yeye ndiye alikuwa sheria, Sera na mwongozo.

Watu wengi Wa chini (wenye uelewa ulio chini) hupenda matokeo ya papo kwa papo. Akikamatwa mwizi basi hapo hapo hukumu ipite. Lakini useme mwizi afikishwe kituo cha Polisi, Polisi wakiona anafaa kupewa dhamana..wampe dhamana na wakimfikisha mahakamani na labda mahakama imwachie huru kwa kuwa ushahidi haukutosha, basi wananchi hawataelewa.

Lakini pia, Wananchi wengi Wa chini wameumizwa na usafishaji Wa miji. Walizoea Rais "Wa wanyonge" ambaye aliruhusu Biashara holela popote pale. Sasa huyu Wa sasa anataka kila kitu kifanywe kama kinavyoelekezwa.

Sababu ya 3, watu wengi wa chini hawaamini kwamba jinsia KE haiwezi kuongoza. Na wengine hawamkubali kutokana na mahali alipotoka pamoja na dini yake.

Watu Wa chini pia wana kawaida ya kuamini uzushi. Huwa hawajishughulishi katika kutafuta ukweli. Na katika hili, wanaamini uzushi Wote wa watu kama akina Veronica France.

Mwisho ni hulka za masikini na za kimasikini kuamini kuwa matajiri wamepata utajiri wao kwa kuwanyonya masikini. Sasa wanapoona serikali inawatambua na inawa-treat matajiri fairly basi wanapata hisia kuwa matajiri wameishika serikali na serikali haipo upande wao.

Na mwisho kabisaaa..ni uongo Wa awamu iliyopita kuwa inatekeleza miradi yote kwa pesa za ndani. Watu waliaminishwa na waliamini. Wenye akili hawakuamini. Sasa wanaposikia awamu ya sasa inakopa na inaweka wazi kuwa inakopa, basi watu Wa chini wanapata la kusema.

Nawasilisha
Nafikiri "research proposal" ulioandika na hatimaye kufanya utafiti ilikuwa kurasa zaidi ya 100. Ripoti ya utafiti wako itafikia labda kurasa 200. Nasema hivi maana ukiangalia kwa haraka hypotheses zisizoshahibiana/ zisizofanana zilikuwa zaidi 20. Na hii inatokana na results summary. What a research and what a document. Ila nikilanganisha majibu na maoini yako kwenye nyuzi mbalimbali ambazo huwa unachangia yaliyoandikwa yaliandikwa kama mawazo, ni lini yaligeuka kuwa utafiti. Is it a coincidence that your views changed to be research results or for that matter research based facts!
 
Moja huwezi kupendwa na kila mtu...

Pili kuna wale bendera fuata upepo hawajui hata wanamchukia kwa lipi...

Tatu kuna wale wa team fulani... mmoja akisema hili basi team nzima wanaimba nyimbo hiyo hiyo...

Nne kuna wale wadandia treni kwa mbele...
 
Ni mtanzania asiye na akili tu ndiye atampigia kura huyu bibi, hali ya maisha imekuwa ngumu sana na victims ni hao hao wananchi wenye maisha magumu.

Sasa ikitokea wakamruhusu kukalia hicho kiti kwa mara nyingine basi nitaamini Tanzania ina raia wa ajabu kuwahi tokea tangu dunia kuumbwa.
Huyu Bibi hafai kuwa kiongozi. Kipofu hawezi ongoza njia.
 
Huyu Bibi hafai kuwa kiongozi. Kipofu hawezi ongoza njia.
Si mara ya kwanza kwake kutoa kauli zenye utata na kupitia kauli hizo ndio maana RAIS wa Marekani Mh. Biden anamkwepa mara zote pindi anapozuru nchi hiyo, hii ni mara ya pili kwenda Marekani ila anaishiwa kukabidhiwa wasaidizi tu..
 
Fanya utafiti, maeneo yenye masikini wengi, ukiishi hapo hutoboi, full uchawi, majini nakadhalika, masikini huwa hawapendani na hawapendi matajiri.

Nenda kigoma ujiji, ukijenga nyumba mpya kesho unaamka umekufa, hawataki maendeleo, mtoto akiwa na akili anarogwa akili, anakuwa zezeta, Kuna mikoa ambayo ukienda kwenu, siku ya kuondoka huagi.

Hawa magufuli aliwaaminisha kwamba kuwa masikini ni fahari, kuwa mnyonge ni fahari, hawakubali kumuona mtu yeyote anafanya juhudi walau ajenge nyumba ya bati, watamsema mji mzima, wengi huamua kujenga mbali na makwao.

Samia anahubiri utajiri, anahubiri mafanikio, hawa wanataka mtu awahubirie umasikini na unyonge, fitina na majungu.
We umeshawai kufika kwao Mama Samia uone kulivyo duni alafu unasema ana ubili utajir watu ambao hawapendi utajiri ni watu kutoka Zanzibar wao Wana ridhika na umasikin
 
Ni mtanzania asiye na akili tu ndiye atampigia kura huyu bibi, hali ya maisha imekuwa ngumu sana na victims ni hao hao wananchi wenye maisha magumu.

Sasa ikitokea wakamruhusu kukalia hicho kiti kwa mara nyingine basi nitaamini Tanzania ina raia wa ajabu kuwahi tokea tangu dunia kuumbwa.
Rais wa JMT hachaguliwi kwa box la kura bwashee. Tafakari na chukua hatua kudai katiba mpya.
 
Badala kuuliza swali, tueleze serkali imechukuwa imechukuwa hatua gani kuzuia mfumuko wa bei. Raisi mwenyewe kwa maneno yake amesema bei zitaendelea kupanda. Ni tegemeo letu wananchi, kuwa, raisi angetueleza hatua inazochukuwa serkali kuzuia mfumuko wa bei. Hiyo thamani ya shillingi baada ya mikopo ya kuijenga Zanzibar, sasa hivi im,eshuka kweli. Tusipoangalia kufika mwisho wa mwaka itafikia shillingi elfu tatu kwa $. Serkali yetu imekaa tu inalalama. Hivi karibuni mtasikia Magufuli akisingiziwa kwa mfumuko wa beii, maana kila baya la Magufuli na zuri ni la majizi awamu ya 4 na serkali ya SSH
Kwamba ile press ya Mwigulu na Ashantu Kijaji hukuisikiliza? Mbona waliongea kabisa mikakati wanayokuja nayo kupunguza machungu ya ongezeko la bei za bidhaa nchini? cheki hapa

Kuhusu kushuka thamani kwa fedha yetu sina uhakika una-refer vyanzo gani? Kwasasa naona 1$ = 2322 Tsh ambapo sioni ongezeko kubwa lolote nikilinganisha na ilivyokuwa kabla ya mama kuingia mdarakani.
 
Wiki jana nikiwa safarini kuelekea magharibi mwa Tanzania nilijipa kazi ya kutafiti uungwaji mkono wa Rais Samia kwa wananchi anaowaongoza.

Asilimia 90 ya watu wa hali ya chini hawamkubali Samia! Na ndani ya hizo 90% 50 yao hawataki kabisa hata kulisikia jina lake.Iliniogopesha!

Hali hiyo ilikuwa tofauti kwa wafanyabiashara.Wengi wao wanadai hawasumbuliwi hasa na mambo ya risti za EFD na kwalo wanadai wanapiga pesa kwa lugha ya mtaani.

Kazi iendelee.
Power of being BRAIN WASHED by the decomposed man
 
Wiki jana nikiwa safarini kuelekea magharibi mwa Tanzania nilijipa kazi ya kutafiti uungwaji mkono wa Rais Samia kwa wananchi anaowaongoza.

Asilimia 90 ya watu wa hali ya chini hawamkubali Samia! Na ndani ya hizo 90% 50 yao hawataki kabisa hata kulisikia jina lake.Iliniogopesha!

Hali hiyo ilikuwa tofauti kwa wafanyabiashara.Wengi wao wanadai hawasumbuliwi hasa na mambo ya risti za EFD na kwalo wanadai wanapiga pesa kwa lugha ya mtaani.

Kazi iendelee.
Wewe Suzy Elias ndiye humkubali Rais Samia na umekuja na ID hii immediately baada ya reshufffle ya November 2021 kuja kuandika threads za kumponda Januari Makamba na Samia.

Huo utafiti wako wa 90% umeutumia tu kuhalalisha unachofikiri.

Anyway approval ni kitu kingine na kupiga kura ni kitu kingine. Ila Samia ndiye best president kwa Tanzania tunapotoka kipindi cha DIKTETA aliyekandamiza demokrasia na uhuru wa maoni na kuvuruga uchumi wetu
 
Kwa sababu hawataki kulipa Kodi,wamezoea vya bure na kulishwa neno la wanyonge huku wakiliwa na Wazalendo wa Chato kama hivi 👇

View attachment 2189699

View attachment 2189700

View attachment 2189701

View attachment 2189702

View attachment 2189703
Vyote hivyo kwa watu wa hali ya chini hawana habari navyo kabisa ! Wao kinachowasumbua ni mfumuko wa bei tu !! Ukiweza kudhibiti utakuwa nao ! Ukishindwa ujue unalo ! Hawatakuelewa ukiwaambia Ukraine wala Urusi !!
 
Ila we dada unachuki na madam Rais sijui kwann sijui.
Kwa nini hatuwezi kuwa wakweli. Kama tunampenda Mama tumuambie ukweli.
Kundi namba moja nibkina mama. Yaani wamekata tamaa na wanamchukia sana. Hawa ndio wanaoonja ugumu wa maisha ndio wajasiria mali wadogo ndio wanaoenda sokoni ndio wanaosumbuka na familia.
Ni kweli chuki kwa mama ni kubwa sana.
Kwa kuwa bado miaka 3 mbele arekebishe mambo vinginevo kweli CCM atalazimika kuiba kura kama inataka kubaki madarakani
 
Wanaomdanganya hawampendi !! Walisha shauriwa humu jf kwamba kama hawaamini waende kwa GROUND wakajionee !!
 
Fanya utafiti, maeneo yenye masikini wengi, ukiishi hapo hutoboi, full uchawi, majini nakadhalika, masikini huwa hawapendani na hawapendi matajiri.

Nenda kigoma ujiji, ukijenga nyumba mpya kesho unaamka umekufa, hawataki maendeleo, mtoto akiwa na akili anarogwa akili, anakuwa zezeta, Kuna mikoa ambayo ukienda kwenu, siku ya kuondoka huagi.

Hawa magufuli aliwaaminisha kwamba kuwa masikini ni fahari, kuwa mnyonge ni fahari, hawakubali kumuona mtu yeyote anafanya juhudi walau ajenge nyumba ya bati, watamsema mji mzima, wengi huamua kujenga mbali na makwao.

Samia anahubiri utajiri, anahubiri mafanikio, hawa wanataka mtu awahubirie umasikini na unyonge, fitina na majungu.
Heri maskini wa mali kuliko akili. Wewe ni maskini wa akili. Unaamini kwenye kulogwa mpaka karne hii!
 
Kwa nini hatuwezi kuwa wakweli. Kama tunampenda Mama tumuambie ukweli.
Kundi namba moja nibkina mama. Yaani wamekata tamaa na wanamchukia sana. Hawa ndio wanaoonja ugumu wa maisha ndio wajasiria mali wadogo ndio wanaoenda sokoni ndio wanaosumbuka na familia.
Ni kweli chuki kwa mama ni kubwa sana.
Kwa kuwa bado miaka 3 mbele arekebishe mambo vinginevo kweli CCM atalazimika kuiba kura kama inataka kubaki madarakani
Wiki mbili zilizopita nilikuwa kijijini. Kuna kina mama kadhaa ambao walikuwa walikuwa ni CCM miaka yote na ni wale watu wasio na elimu, watu wa vijijini. Nilishangaa sana kukuta wanalalamika na kusema ''huyu mama hawezi uongozi''. Mawazo yangu ni haya: Rais Samia analaumiwa bure. Tatizo ni kuwa CCM imeshafika kikomo cha maarifa na sasa hivi ipo madarakani tu kwa sababu ya vyombo vya dola. Wanachotakiwa kufanya ni kubadilisha mfumo mzima wa uongozi, waruhusu ushindani halali ili kupata viongozi bora wenye upeo wa kuongoza. Haya mambo ya kupeleka wabunge wa hovyo hovyo kama kina babu Tale bungeni kwa kutumia nguvu yanazidi kuididimiza. Haya ukienda huko kwa wakuu wa wilaya na mikoa na viongozi wote wa kuteuliwa utakuta wamejaa wapigaji wasiyo na vision yoyote ya uongozi kwa sababu hakuna ushindani kwenye kuwapata.
 
Back
Top Bottom