Kwanini watu wa hali ya chini wanamchukia sana Rais Samia?!

Kwanini watu wa hali ya chini wanamchukia sana Rais Samia?!

Ni vile wananunua mafuta ya kupikia shilingi elfu tisa kwa lita moja.

Ni vile kipande cha sabuni ya jamaa wananunua kwa mia saba.

Ngano kilo elfu mbili

Ngoja wengine waongezee
 
Sababu nyingine watu hawapendi watu wapate maendeleo.Hayati aliwaaminisha watu kwamba mtu ukiendelea kidogo tu ni mwizi.
Mpaka ikapelekea mtu anatumbuliwa hadharani na watu wanashangilia.
 
Magu alikuwa na mapungufu yake but wanainchi walikuwa wanaona kuwa anabana matumizi,

Tunajua Safari za rais zinakata pesa Sana na magu hakusafiri Kwa muda wote

So hata kama alikuwa mwizi Sisi ambao tunaibiwa tulimwamini

Now Bilion 7 Kwa ajili ya documentary, Safari za nje ni kila siku
Huko kubana matumizi hayo matumizi tuliyo yabana tumetumia kwenye nini?
 
Huko kubana matumizi hayo matumizi tuliyo yabana tumetumia kwenye nini?

Kwenye mambo mengi Tu, hata barabara ya moroco mwenge ni faida ya kubana matumizi Leo tunapita kwenye njia 4
 
Ni mtanzania asiye na akili tu ndiye atampigia kura huyu bibi, hali ya maisha imekuwa ngumu sana na victims ni hao hao wananchi wenye maisha magumu.

Sasa ikitokea wakamruhusu kukalia hicho kiti kwa mara nyingine basi nitaamini Tanzania ina raia wa ajabu kuwahi tokea tangu dunia kuumbwa.
Toka lini Tanzania kura za wananchi zikamweka madarakani Rais??
 
Ni mtanzania asiye na akili tu ndiye atampigia kura huyu bibi, hali ya maisha imekuwa ngumu sana na victims ni hao hao wananchi wenye maisha magumu.

Sasa ikitokea wakamruhusu kukalia hicho kiti kwa mara nyingine basi nitaamini Tanzania ina raia wa ajabu kuwahi tokea tangu dunia kuumbwa.
Tatizo sio kura za wananchi ila ni katiba mbovu na tume ya uchaguzi ya mchongo
 
Ukijinasibuu na falsafa ya ubepari huku unafuata sera ya ujamaa lazima mambo yawe kinyume!
Marekani ni mabepari, ccm wajamaa! Wapinawapi?
 
HAo watu wa hali ya cheni wengi wao ni wajinga wakutupwa.
 
Kwani kijijini umeme mpaka leo ni shilingi ngapi? Acheni lawama sizizo za msingi umeme bei kijijini haujabadilika ni ile ile 27000.labda huyo mzee anaishi mjini
Imebadikika mkuu, wale waliolipia kabla ya 2021 ni 27000, Ila wapya ni miatatu mkuu
 
Hatuzungumzii nchi nyingine ya kwetu kwanza Hali NI ngumu Sana huku vijijini watu mbolea imepanda tunataka kuona Serikali yetu inatusaidiaje katika Hali hii ho wanje na wenyewe wamaserikali zao.Tuone naafuu ya maisha yetu haijalishi wengine
 
Wiki jana nikiwa safarini kuelekea magharibi mwa Tanzania nilijipa kazi ya kutafiti uungwaji mkono wa Rais Samia kwa wananchi anaowaongoza.

Asilimia 90 ya watu wa hali ya chini hawamkubali Samia! Na ndani ya hizo 90% 50 yao hawataki kabisa hata kulisikia jina lake.Iliniogopesha!

Hali hiyo ilikuwa tofauti kwa wafanyabiashara.Wengi wao wanadai hawasumbuliwi hasa na mambo ya risti za EFD na kwalo wanadai wanapiga pesa kwa lugha ya mtaani.

Kazi iendelee.
Acha hizo....
Mawazo yako sio ya Watanzania..
 
Asilimia 20 tu ya wafanya biashara ndiyo wanao mkubali samia tena ni wafanya biashara mafisadi ,asili.ia zaidi ya 95% ya watz hatumkubali hata kidogo
 
Ni mtanzania asiye na akili tu ndiye atampigia kura huyu bibi, hali ya maisha imekuwa ngumu sana na victims ni hao hao wananchi wenye maisha magumu.

Sasa ikitokea wakamruhusu kukalia hicho kiti kwa mara nyingine basi nitaamini Tanzania ina raia wa ajabu kuwahi tokea tangu dunia kuumbwa.
Haijawahi kutokea rais wa Tanzania akafurahiwa hata siku moja. Kulalamika sana ni kielelezo cha umaskini wa kichwani zaidi.
 
Wiki jana nikiwa safarini kuelekea magharibi mwa Tanzania nilijipa kazi ya kutafiti uungwaji mkono wa Rais Samia kwa wananchi anaowaongoza.

Asilimia 90 ya watu wa hali ya chini hawamkubali Samia! Na ndani ya hizo 90% 50 yao hawataki kabisa hata kulisikia jina lake.Iliniogopesha!

Hali hiyo ilikuwa tofauti kwa wafanyabiashara.Wengi wao wanadai hawasumbuliwi hasa na mambo ya risti za EFD na kwalo wanadai wanapiga pesa kwa lugha ya mtaani.

Kazi iendelee.
Tupende tusipende Magufuli alikuwa kipenzi cha watu wa hali ya chini na alisimamia vizuri upigaji. SSH alipokuja alidai kuwa yeye atatekeleza yote ya Magufuli. Baada ya muda mfupi akabadilisha kila kitu. Upigaji umerudi kwa nguvu mpya. Awamu ya nne imerudi madarakani kufundisha upigaji. Alirudisha wale waliyotemwa na Magufuli, hii ilikuwa dalili ya kudharau maamuzi ya Magufuli, hasa pale alipomrudisha Nnape na Makamba ambao walihusika kumtukana raisi. Mtu yeyote mwenye akili ata mkuambia that was a big mistake.
Tatizo lingine kubwa kwa watu wa chini ubambikiwa kodi kubwa kwa jina la TOZO huku kodi za matajiri zinafutwa, zinaondolewa, au zinapunguzwa. Hili taifa linabebwa na watu maskini kwa njia za TOZO mbalimbali. TOZO kubwa kwa zote ni ile ya miamala ya simu. Kwa nini wale wote wanaopokea pesa kupitia benki hawatozwi chochote. Kwa nini leo nikimtumia mtu cheki ya shillingi laki 5, anaiweka benki na inaingizwa kwenye akaunti yake bila makato. Lakini nikipokea kamshara kangu kalikokatwa kodi, nikimtumia kaka yangu kaelfu kumi, basi mimi nailipa serkali na yeye pia anailipa serkali. Hii inawaumiza maskini. Maskini akipeleka kuku wake kwenye mnada anakumbana na TOZO na hana wa kumtetea. YOTE haya, wewe untegemea maskini atampenda SSH. Wewe mwenyewe umesema sasa hivi matajiri wanakenua mpaka pengo la mwisho maana nchi sasa inalika, na italika hasa. Naona tunaelekea pale tulipofikia viongozi kuanza kuzomewa kwenye mikutano. Nati sasa zimeingia kutu na ukijaribu kuzilegeza bolt ztakatika. SSH ameziacha hivohivo maana zikikatika gari litapinduka.
 
Wiki jana nikiwa safarini kuelekea magharibi mwa Tanzania nilijipa kazi ya kutafiti uungwaji mkono wa Rais Samia kwa wananchi anaowaongoza.

Asilimia 90 ya watu wa hali ya chini hawamkubali Samia! Na ndani ya hizo 90% 50 yao hawataki kabisa hata kulisikia jina lake.Iliniogopesha!

Hali hiyo ilikuwa tofauti kwa wafanyabiashara.Wengi wao wanadai hawasumbuliwi hasa na mambo ya risti za EFD na kwalo wanadai wanapiga pesa kwa lugha ya mtaani.

Kazi iendelee.
Majibu ya utafiti wako ni sahihi. Mimi pia niliwahi kuufanya utafiti kama wako na nikapata majibu kama yako.

Nilichokibaini ni hiki:-
-Watu wengi Wa chini uelewa wao upo chini sana. Hawamkubali Rais Samia kwa kuwa anaonekana ni mtu anayefuata taratibu tulizojiwekea kama Taifa. Na nyingi ya taratibu hizo ni kama vile haziwa-favour. Wanaona bora Rais aliyepita ambaye alikuwa anaamua kwa hisia tu. Yeye ndiye alikuwa sheria, Sera na mwongozo.

Watu wengi Wa chini (wenye uelewa ulio chini) hupenda matokeo ya papo kwa papo. Akikamatwa mwizi basi hapo hapo hukumu ipite. Lakini useme mwizi afikishwe kituo cha Polisi, Polisi wakiona anafaa kupewa dhamana..wampe dhamana na wakimfikisha mahakamani na labda mahakama imwachie huru kwa kuwa ushahidi haukutosha, basi wananchi hawataelewa.

Lakini pia, Wananchi wengi Wa chini wameumizwa na usafishaji Wa miji. Walizoea Rais "Wa wanyonge" ambaye aliruhusu Biashara holela popote pale. Sasa huyu Wa sasa anataka kila kitu kifanywe kama kinavyoelekezwa.

Sababu ya 3, watu wengi wa chini hawaamini kwamba jinsia KE haiwezi kuongoza. Na wengine hawamkubali kutokana na mahali alipotoka pamoja na dini yake.

Watu Wa chini pia wana kawaida ya kuamini uzushi. Huwa hawajishughulishi katika kutafuta ukweli. Na katika hili, wanaamini uzushi Wote wa watu kama akina Veronica France.

Mwisho ni hulka za masikini na za kimasikini kuamini kuwa matajiri wamepata utajiri wao kwa kuwanyonya masikini. Sasa wanapoona serikali inawatambua na inawa-treat matajiri fairly basi wanapata hisia kuwa matajiri wameishika serikali na serikali haipo upande wao.

Na mwisho kabisaaa..ni uongo Wa awamu iliyopita kuwa inatekeleza miradi yote kwa pesa za ndani. Watu waliaminishwa na waliamini. Wenye akili hawakuamini. Sasa wanaposikia awamu ya sasa inakopa na inaweka wazi kuwa inakopa, basi watu Wa chini wanapata la kusema.

Nawasilisha
 
Kwamba serikali ya Tanzania haichukui hatua yoyote kudhibiti ongezeko la bei ya bidhaa sokoni ndiyo unachomaanisha? Hebu tuweni wakweli jamani
Badala kuuliza swali, tueleze serkali imechukuwa imechukuwa hatua gani kuzuia mfumuko wa bei. Raisi mwenyewe kwa maneno yake amesema bei zitaendelea kupanda. Ni tegemeo letu wananchi, kuwa, raisi angetueleza hatua inazochukuwa serkali kuzuia mfumuko wa bei. Hiyo thamani ya shillingi baada ya mikopo ya kuijenga Zanzibar, sasa hivi im,eshuka kweli. Tusipoangalia kufika mwisho wa mwaka itafikia shillingi elfu tatu kwa $. Serkali yetu imekaa tu inalalama. Hivi karibuni mtasikia Magufuli akisingiziwa kwa mfumuko wa beii, maana kila baya la Magufuli na zuri ni la majizi awamu ya 4 na serkali ya SSH
 
Back
Top Bottom