Kwanini watu wa hali ya chini wanamchukia sana Rais Samia?!

Kwanini watu wa hali ya chini wanamchukia sana Rais Samia?!

Tofauti yetu na nchi nyingine ni kwamba sisi Rais anahamasisha bei kupanda ilhali marais wengine wanapambana kutafuta ahueni ya wananchi wao.
Kwamba serikali ya Tanzania haichukui hatua yoyote kudhibiti ongezeko la bei ya bidhaa sokoni ndiyo unachomaanisha? Hebu tuweni wakweli jamani
 
Hali ya maisha ni ngumu duniani kote.
Ni mtanzania asiye na akili tu ndiye atampigia kura huyu bibi, hali ya maisha imekuwa ngumu sana na victims ni hao hao wananchi wenye maisha magumu.

Sasa ikitokea wakamruhusu kukalia hicho kiti kwa mara nyingine basi nitaamini Tanzania ina raia wa ajabu kuwahi tokea tangu dunia kuumbwa.
 
Wiki jana nikiwa safarini kuelekea magharibi mwa Tanzania nilijipa kazi ya kutafiti uungwaji mkono wa Rais Samia kwa wananchi anaowaongoza.

Asilimia 90 ya watu wa hali ya chini hawamkubali Samia! Na ndani ya hizo 90% 50 yao hawataki kabisa hata kulisikia jina lake.Iliniogopesha!

Hali hiyo ilikuwa tofauti kwa wafanyabiashara.Wengi wao wanadai hawasumbuliwi hasa na mambo ya risti za EFD na kwalo wanadai wanapiga pesa kwa lugha ya mtaani.

Kazi iendelee.
Majibu haya hapa, mtangulizi wake alitatua kero hapohapo yeye atakuja mwezi wa saba
 

Attachments

  • VID-20220413-WA0012.mp4
    7.4 MB
Nchi hii imerudi kwa Watu wanaostahili;sasa ni ya Wasomi, Wanasiasa na Wafanyabiashara!

Kama haupo kwenye hayo Makundi utasaga meno—-

Magufuri alidhulumu sana haki za hayo makundi na masikini walifurahia Alipopora democracy, Alipokataa Serikali kutafutia ajira Watu wake na alipowanyanganya Wafanyabiashara mali zao kwa nguvu!
 
JPM alihakikisha watu wa hali ya chini wanapata nafuu na siku zote aliwapigania sana watu wa hali ya chini lakini huyu hana muda na watu hawa wa hali ya chini.
Yeye yupo zaidi na watu walioshiba, na ambao miaka yote walikuwa kwenye mfumo wa serikali au chama, kwa hiyo hawana shida kiuchumi hata kidogo.
Bei za vitu zikishapanda, mwathirika mkuu na anayebeba tozo zote za bidhaa hiyo ni mlaji wa mwisho kabisa, yaani wale Babu, Bibi, Mama, Baba zetu na watu wengine kule vijijini kwetu.
 
Harafu MSI generalise Sana ,watu wengi wa mjini ndio unaweza sema hawamkubali lakini maeneo ya Vijijini kwenye miradi ya Afya,maji, barabara na shule huko ni wafuasi wa ccm dam dam..

Kumbuka ndio wengi na ndio wanaofeel Hali halisi,,watu wa mjini huwa hawaoni impacts ya miradi ya serikali Kwa sababu wao Wana options nyingi.
 
Wiki jana nikiwa safarini kuelekea magharibi mwa Tanzania nilijipa kazi ya kutafiti uungwaji mkono wa Rais Samia kwa wananchi anaowaongoza.

Asilimia 90 ya watu wa hali ya chini hawamkubali Samia! Na ndani ya hizo 90% 50 yao hawataki kabisa hata kulisikia jina lake.Iliniogopesha!

Hali hiyo ilikuwa tofauti kwa wafanyabiashara.Wengi wao wanadai hawasumbuliwi hasa na mambo ya risti za EFD na kwalo wanadai wanapiga pesa kwa lugha ya mtaani.

Kazi iendelee.
Mfumuko wa bei

Kutokuwatumbua watumishi wa mbele ya tv

Hayo ni baadhi

Wanyonge hawapendi kumuona mwenye nacho akifanikiwa
 
Nani keshawahi ona ripot za CAG zimewahi fanyiwa Kazi
 
Kwani kipindi gani watu wa hali ya chini walimkubali rais aliyepo madarakani?.kwani msemo wa hali mbaya na vyuma kukaza ulikuja kipindi gani?
 
Sijui ni kura ngapi zitamtoa Rais Samia madarakani 2025, torati iliandikwa
 
Nilikumkuta mwanakijiji mmoja anasikitika, eti siku hizi hakuna Rea tena 27,000, kuna Samira 300,000
Kwani kijijini umeme mpaka leo ni shilingi ngapi? Acheni lawama sizizo za msingi umeme bei kijijini haujabadilika ni ile ile 27000.labda huyo mzee anaishi mjini
 
Back
Top Bottom