Majibu ya utafiti wako ni sahihi. Mimi pia niliwahi kuufanya utafiti kama wako na nikapata majibu kama yako.
Nilichokibaini ni hiki:-
-Watu wengi Wa chini uelewa wao upo chini sana. Hawamkubali Rais Samia kwa kuwa anaonekana ni mtu anayefuata taratibu tulizojiwekea kama Taifa. Na nyingi ya taratibu hizo ni kama vile haziwa-favour. Wanaona bora Rais aliyepita ambaye alikuwa anaamua kwa hisia tu. Yeye ndiye alikuwa sheria, Sera na mwongozo.
Watu wengi Wa chini (wenye uelewa ulio chini) hupenda matokeo ya papo kwa papo. Akikamatwa mwizi basi hapo hapo hukumu ipite. Lakini useme mwizi afikishwe kituo cha Polisi, Polisi wakiona anafaa kupewa dhamana..wampe dhamana na wakimfikisha mahakamani na labda mahakama imwachie huru kwa kuwa ushahidi haukutosha, basi wananchi hawataelewa.
Lakini pia, Wananchi wengi Wa chini wameumizwa na usafishaji Wa miji. Walizoea Rais "Wa wanyonge" ambaye aliruhusu Biashara holela popote pale. Sasa huyu Wa sasa anataka kila kitu kifanywe kama kinavyoelekezwa.
Sababu ya 3, watu wengi wa chini hawaamini kwamba jinsia KE haiwezi kuongoza. Na wengine hawamkubali kutokana na mahali alipotoka pamoja na dini yake.
Watu Wa chini pia wana kawaida ya kuamini uzushi. Huwa hawajishughulishi katika kutafuta ukweli. Na katika hili, wanaamini uzushi Wote wa watu kama akina Veronica France.
Mwisho ni hulka za masikini na za kimasikini kuamini kuwa matajiri wamepata utajiri wao kwa kuwanyonya masikini. Sasa wanapoona serikali inawatambua na inawa-treat matajiri fairly basi wanapata hisia kuwa matajiri wameishika serikali na serikali haipo upande wao.
Na mwisho kabisaaa..ni uongo Wa awamu iliyopita kuwa inatekeleza miradi yote kwa pesa za ndani. Watu waliaminishwa na waliamini. Wenye akili hawakuamini. Sasa wanaposikia awamu ya sasa inakopa na inaweka wazi kuwa inakopa, basi watu Wa chini wanapata la kusema.
Nawasilisha