Kwanini wanaume JF wepesi sana kutuma hela?

Kwanini wanaume JF wepesi sana kutuma hela?

Maisha bwana! Wakati mimi nikiwa seriously kuomba msaada wa hata buku kisa me dume bc wananiona fala tu, but kuna mwingine anawatest tu wamtumie hela but n KE basi wamejitoa kweli kweli.
So sad, mwanaume kusaidia mwanaume mwenzake ni kazi but kusaidia mwanamke ni mwepesi sana. Right now mwanaume ukiwa na shida mtumie mwanamke kuexpress shida yako as if ni yake, trust me atasaidiwa sana but like ungetumia identity yako mwanaume.

But utofauti, ni mwanamke kumsaidia mwanamke mwenzake yupo easy sana, huwa hawajari kama wanao uwezo wa kusaidia, na siyo mwanamke mwenzake tu but hata kwa wanaume huwa wanasaidia wakiguswa na shida iliyoelezewa.
But niseme tu, kumsaidia mtu si cases ili mradi umeguswa, kwa maana huwezi kujua nani atakaye kusaidia kesho. Huwezi jua kabisa, narudia huwezi kujua kabisaaa.
My respect kwa sam2000 popote ilipo. Bro I respect you forever.
Saidia, saidia jamaa saidia.
Watoto yatima saidia,
Chokola saidia,
Wasio jiweza saidia
Siyo kisa pisikali tu ndo usaidie.
😪😪😪
 
Wewe hao umewatoa chimbo gani, kwenye jukwaa la siasa, utani, chitchat, au mmu
Mji mzito huu.
Chit chat kule wamejaa watoto watoto tuuu hata hela hawana 😂😂😂
 
Una ujasiri umeweza kutoa no? Aisee hakuna kitu naogopa kama kumpa no yangu mtu wa mitandaon hasa jf wasiojulikana
 
Ni kwasababu tunaguswa sana na matatizo ya mwombaji
Na tuna moyo wa kusaidia inahitajika mwanaume siyo kiumbe dhaifu mungu amemjalia utashi sana
 
Kambi ya mtu mmoja haitaprove nadhari ya mleta mada kwamba wanaume wa jf ni warahisi kutoa pesa
Nataka sample size iwe kubwa kubwa
Tuna modify tu theory ya mleta mada....na sample zinakua adjusted accordingly..ondoa shaka
 
Naona umekuja kutuonyesha ujinga wako humu...

Unaomba omba hela hovyo

Hlf watu unaowaomba sababu ni wastaarabu wame assume una shida kweli wakakusaidia umeamua kuwalipa kwa kuwafungulia uzi wa kuwadhalilisha hili wajione wajinga kwa kukusaidia wewe omba omba.

Acha utoto.
 
Hii imenifikirisha sana!

Kwa kawaida mimi huwa si mtu wa kupiga mizinga, kwasababu nina kipato cha kujitosheleza na kubaki akiba kubwa tu.

But last week nikaona nijaribu kuomba watu kadhaa hela kama kuwajaribu tu. Huwezi kuamini, yaani bila hata wao kuwaza mara mbili mbili, wale watu wote 5 walituma hela kwenye simu yangu. Na kilikuwa ni kiasi kikubwa tu cha pesa kwa usawa huu wa Magu.

Swali ninalojiuliza: Inakuwaje katika nyakati hizi za ulimwengu wa mitandao ya kijamii, mtu anakuamini kirahisi rahisi tu na kukutumia pesa zaidi ya laki 1 bila hata ya kuwa anakufahamu? Je JF tuna ukarimu mkubwa kiasi hicho compared to other platforms?
Kwahiyo nilikosea kukupa msaada?
 
Back
Top Bottom