Ilikuwaje siku uliyofumania/ uliyofumaniwa?

Ilikuwaje siku uliyofumania/ uliyofumaniwa?

Jobless_Billionaire

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2022
Posts
5,456
Reaction score
13,831
Habari zenu wakuu.. Poleni na majukumu na harakati za hapa na pale, gharama za maisha zinapanda ila tunapanda nazo hakuna kukata tamaa.

Kuna visa kama viwili viliwahi kunitokea back in the days vya kufumaniwa ambavyo sikuwahi kumueleza yeyote.

Cha kwanza kilikuwa hivi.

Kuna mwaka nilipata kazi mkoa fulani kwenye shirika moja lisilo la kiserikali. Ilikuwa ni nje ya mkoa niliokuwa nikiishi awali. Sasa kwenye mtaa niliokuwa nimepanga, kulikuwa na mwanamke mmoja ni kama alitokea kunizimia sana. Hatukuwahi kuwa na mazoea sababu alikuwa ni mke wa mtu, ila ishara za uzinzi zilinijulisha hivyo.

Kuna siku ikatokea pale mtaani kuna sherehe nyumba moja ya mshua fulani, na ndio mwenyekiti wa mtaa huo na ananikubali sana yule mzee, alizoea kuniita mwanaye, nilikuwa sehemu ya wahudhuriaji, yule bidada vilevile. Kutokana na huo mchanganyiko ndio ikawa mwanzo wa kuanzisha mazoea nae na mawasiliano tukabadilishana rasmi.

TUlikuwa tunapigiana simu mara mojamoja ndani ya ile wiki ya kwanza tena majira ya mchana na ilikuwa ni salamu tu na si love affairs ingawa kulikuwa kuna kujikanyaga kimaongezi ambapo haikuhitaji C tatu kujua kunapo jambo hapo.

Siku moja alinipigia simu usiku, nikashtuka kwanza sababu najua kaolewa inakuwaje anipigie muda ambao kwa namna yoyote mumewe anaweza kuwa nyumbani? Nikapokea, tukasalimiana ikabidi nimuulize kwanini apige muda huo akasema mumewe kasafiri. Basi tukaongea sana usiku ule hadi kuhitimisha kuwa tuwe wapenzi ila kwa siri sana. Roho za tamaa na uzuri wa bidada wala sikujali kama jamaa yake anaweza kunifanyia vibaya kama tupo Sodoma siku akija kugundua.

Usiku huohuo bidada akaanza kulazimisha aje kwangu alale, nikamzuia. Akaomba tutoke ikiwezekana ila nikakataa pia sababu ni mwanzo tu isije kuwa anataka kuniharibia tu. Basi tukawa wa kuwasiliana tu, siku kama ya tatu ikawa ndio siku ya kuonana nae rasmi, kwakuwa walikuwa hawajazaa haikuwa shida. Tulionana na niliichakaza vibaya mno. Bibie ana kimwili ka wastani tu, ni slim halafu mimi nimeenda hewani kumzidi kwa hiyo nilikuwa nafanya nnavotaka, iwe nimembebelea au nimembananisha bado iliwezekana, maamuzi yalikuwa kama ya Lowassa tu kuhama chama. Na yeye alidai anapenda kudeka kwenye mwili ulioenda air (hewani) kama wangu.

Basi bwana kadri muda ulivyozidi kusogea nikanogewa, akanogewa pia. Ikawa ndio mchezo wetu kukutana na kumwaga moto. Siku moja yule mzee mwenyekiti aliniita akaniuliza kuhusu mie na yule bidada mke wa mtu, nikashtuka sana kwa sababu sikutegemea kama anaweza kuwa anafahamu, na kajuaje ilhali mimi naamini najua kutunza siri? Mzee alinionya akaniambia acha kabisa mara moja. Nikaitikia kwa kichwa huku nikiwa na hofu pia sababu mambo yashakuwa exposed.

Nikataka kukata mazoea na bidada ila ilikuwa ngumu sababu alichokionja alidai hakuwahi kukipata. Basi nikapumbazwa na maneno ya kudeka nikaona potelea pote, nikaendelea kuburuza, kumbuka muda huo bado mumewe hajaja.

Siku hazikuganda, mumewe akarejea. Tulijitahidi sana kujizuia lakini tabia ikishajijenga ni ngumu sana kuishape... Ikawa ni ngumu hata kukutana tena. Nakumbuka tangu mumewe arudi nilikutana na bibie mara moja nikafanikiwa japo alikuwa rahisi sababu ya ugumu wa kupata nafasi. Ile mara ya pili ndio balaa lilipokujia.

Siku hiyo Bidada alitoka jioni kama saa 11 kwake anaenda nyumbani kwao mara moja. Sasa wakati anarudi ilikuwa mida kama saa tatu kasoro usiku akaomba anione angalau kwa dakika 10 tu sababu ya ufinyu wa nafasi sababu ya uwepo wa mumewe. Nikakubali, tukakutana kachochoro kamoja mbali kidogo na mtaani, huwa hakana jam sana kwa usiku kama ule. Nafsi ni kama ilikuwa inakataa ila kibri cha ubinadamu kiliniongoza. Kumbe ni kama kuna watu walikuwa wanaspy, sijajua waliorganize vipi hadi kujua tutakuwa eneo hilo, na walijuaje na nani aliorganize, I don't know.

Tulipokutana haikuishia story tu, ikabidi kapigwe kamechi ka kuibaiba. Baada ya kumaliza nikaona tochi zimewashwa toka pande moja ya chochoro kutuelekea, watu kama wanne halafu zikasikika sauti za kugadhabika zikisema tulieni hapohapo.. yule bidada nikasikia anasema Mungu wangu, mme wangu huku anajiliza kipumbavu.. aisee nguvu zikaisha nikawaza hata nikikimbia hawa ntawaacha wote kweli? Na hata nikithubutu, wakiniitia mwizi maana yake maisha yanatamatikia hapo. Akili ikawaza haraka sana kwamba leo, ndio ile siku naenda kutatuliwa kama pazia la hekalu.. nikaona noo, ikabidi nichanganye miguu kujinusuru, liwalo na liwe. Bora kufa umepambana kuliko kufa kizembe

Sasa kutokana na uhafifu wa mwanga nikakimbia bila hata kujua naelekea wapi wala ninapokanyaga, kama kona tatu naona njemba zinakuja tu, bahati baya nikaenda kukanyaga shimo la maji taka ya bafu nikateleza na kuanguka mguu ukawa kama umeshtuka.. aisee, nilijaza mtaa. Nilipigwa makofi na zile njemba utadhani zenyewe ndio zenye mke, ila mhusika akawa analia tu kwanini unatembea na mke wangu.. nilibebwa juu juu hadi kwa mwenyekiti. Wahuni hawakujali nimeenda hewani wala nini. Ndio nikaamini kumbe ukifumaniwa hakunaga cha mbavu nene, lazima unywee hata ukiwa kijeba kama Undertaker

Ilikuwa aibu siwafichi.. Kule kwa mwenyekiti baada ya muda tukabaki kama watu nane nahojiwa hapo.. Suala ikawa waende polisi ila mwenyekiti akawa kama ananikingia kifua kwa namna fulani akidai tuyamalize hukuhuku.

Acheni tu aisee.. nililala palepale sababu niliogopa nikienda kulala home naweza kuchomewa ndani au waniijie wanipelekee moto. Asubuhi walikuja wakuu wa pale kazini, ikawa ni vikao tu. Muda huo mguu ulioshtuka umevimba vibaya mno hata kutembea siwezi.. Ilinitoka Milioni 2 na laki tatu jamaa ndio akawa mpole aisee. Akiba karibu yote ikaenda kwenye msala. Na hapo nikawa naona kama bado jamaa ataniendea kwa Sangoma, sababu ni cama alikuwa calm kiaina flani, wasiwasi ukabaki kwangu. Kazini hawakunifukuza, wakanihamishia tu mkoa mwingine.

Baada ya kupata unafuu wa mguu nikamtafuta jamaa nikiwa siamini kama yameisha upande wake, nikamuachia na vitu vyote vya ndani nikaondoka na huo mkoa aisee. Sijajua walimalizaje na mkewe , ila ulipita muda sana nikiwa mkoa mwingine huo bidada akanicheki tena.. nikavunja kabisa ile line ya simu. Tunaonana kwenye social networks tu..

Kwakuwa tumeumbiwa kusahau, nikajichanganya tena kwenye mkasa wa pili..

******

MKASA 02

Baada ya fumanizi lile nilijiapiza kutojihusisha na wake za watu. Ikapita kama mwaka mmoja na miezi saba, nikaja kuingia kwenye mahusiano na bidada mmoja alikuwa mmiliki wa salon moja ya kike kali sana pale mjini. Kwa bahati mbaya hakunieleza kama alikuwa kaolewa, alichoniambia yupo single. Ni pisi moja ya viwango vya kimataifa, first class kabisa.

Huyu tulienjoy sana wasaa nae, sikuwahi kuzingatia tena kuuliza habari za kuwa kaolewa ila niliridhika na jibu lake la awali. Nilikaa na huyu mwanamke kwa muda mrefu hadi kipindi ambacho alikata ghafla mawasiliano na kuniambia mume wake karejea, alikuwa kaolewa ila hakuniambia. Roho iliniuma sana sababu nilikuwa nampenda kupindukia.

Sikuridhika, siku moja nikaenda pale ofisini kwake kwa hasira sana nikitaka akanieleze kwanini alinidanganya. Kufika pale nikawaka vibaya, maneno makali mixer kibesi utadhani nilimfungulia hiyo ofisi. Nikaondoka kurudi home.

Siku iliyofuata demu aliomba tuonane sehemu, nje kabisa ya mji. Tukaongea akaomba radhi kunidanganya kuwa hajaolewa, akaniahidi tutafanya kwa siri na mimi nijitahidi kiwa msiri ili anipoze roho yangu. Tukaendelea kuponda raha kwa kujificha ficha.

Siku moja usiku nimekaa bar, wakaja wanaume wawili wasukuma, mmoja akaanza kuniuliza dogo kwa nini unatembea na mke wangu? Unajua nimemtoa wapi huyo mwanamke na nimemgharamia kiasi gani hadi hapo alipo? Hata hiyo ofisi aliyonayo huwezi kuwa na hela hiyo ya kumfungulia (kwa sauti za kulewa). Mie nasikiliza tu huku mwili ushaingia ubaridi, sijui nini kinafuata.. Alichoniambia huyo jamaa ni kuwa kuanzia siku hiyo niachane kabisa na mke wake vinginevyo nitaishia pabaya.

Nilitoka hapo muda huohuo baada ya wale jamaa kuondoka. Nikawa nawaza nani kanichoma? Nikaja kumuuliza bidada ila nae akadai hafahamu na wala hajaambiwa au kuulizwa kitu. Nikamwambia demu afanye kama hatufahamiani. Nilifuatilia kujua yule jamaa ana michongo gani nikaambiwa huwa anafanya biashara ya mang'ombe na ana pesa chafu vibaya mno kwahiyo huwa anasafirisha kupeleka mjini daslamu. Kama mwezi mmoja ukakata, demu akaanza kunitafuta tena muda huo nishamove on. Nikarubunika tukaendelea na mambo yetu.

Muda ukaenda, Siku moja nikiwa natembea pembeni ya barabara majira kama saa tisa mchana nilikoswa kugongwa na gari iliyokuwa speed kali sana, bahati nzuri nilirukia miferejini, tofauti na hapo biashara ilikuwa inaisha. Sikujali sana wala sikuhusianisha kivyovyote ila nilichukulia ni ulevi au ni siku mbaya tu

NIlikuja kuugua homa moja kali sana, nikawa mtu wa ndani tu kwa muda kidogo, yule bidada ilibidi mchana moja aje kuniona na kunihudumia walau msosi wa mchana tu. Wala hata sikuichapa. Kipindi hicho mume wake yupo ukumbike. Sasa aliporudi nyumbani, mume wake akaanza kumuwashia moto, ulikuwa wapi? Alijaribu kudanganya ila alipigika vibaya mno. Ni kama jamaa alikuwa ana details zote za mienendo ya mke wake, hadi ninapoishi sasa, ukumbuke jamaa lina hela na machawa kibao na ndio waliofanya upelelezi.

Bibie alipigika hadi akanyoosha maelezo aisee, ikawa jamaa aletwe nilipo. Wakaja, na wale machawa wote wakapigiwa simu wakaja wamebeba mafimbo yao ya kisukuma, wengine sime na mashuka yao. Muda huo sielewi nimejivalia mabukta tu ndani halafu kifua wazi, nimejiacha sielewi kama nakuja kuwashiwa tanuri. Kama saa kumi mlango wa ghetto ukagongwa, sauti ya kike nikasikia. Nikaenda kufungua nikakuta watu kama 12 nje pamoja na yule jamaa mwenye mke aliyenipa onyo siku ile kule baa.

Nikataka kurudi ndani ili nivae walau shati ila majamaa makali kishenzi yakaniambia toka nje bwana mdogo leo tunakuua, yakapiga na maneno ya mkwara ya kisukuma. Nikatoka nje mzee, nikawekwa mtu kati, nikapigwa mtama na kofi zito la usoni nikajikuta chini huku damu zinatoka puani na mdomoni.

Maswali sasa, dogo nilikuambia nini kuhusu huyu mwanamke? Haukusikia, sasa ulitaka tufikie huku.. jamaa lilikuwa limevaa yale ma-sandals ya ngozi og likanikanyaga teke la kichwani, yale mapambe ni kunichapa tu. Hapo watu wamejaa mno, ukizingatia ni mapema. Nilipigika sana. Jamaa akawa anasema siku ananionya alimsikia mke wake anataja jina langu akiwa anaota mara kadhaa, aliamua kuniulizia kimyakimya hadi kunipata..

Jamaa akanikumbusha hadi siku niliyokoswa gari, alikuwa ni yeye anataka kunimaliza baada ya kugundua bado natembea na mkewe.. Jamaa aliongea kwa uchungu hadi akaanza kulia, alilalamika kuhusu uwekezaji kwa bidada halafu anakuja kugongewa na mtu sina mbele wala nyuma. Nilipigika mbaya aisee. Hapo wazazi wamepigiwa simu wakaja chap wanalialia eti msituulie mwanetu. Jamaa likauliza, umeshamt....mba mara ngapi mke wangu? Na wazazi wapo aisee.. nikadanganya mara mbili, nikakanyagwa teke la kichwani ili niseme ukweli. Ikabidi niseme tu. Nikaulizwa tema ilikuwa na condom au hivyohivyo? Huku jamaa analia. Nikajibu vyote, nilichezea stiki balaa, hata nguvu za kukinga na mikono sina sababu imeshavimba, haiwezi kugadi tena zaidi ya kutoneshwa. Kwahiyo nilikula za mbavu, mgongo, tumbo na kila sehemu..

Mwenyekiti na mabalozi walikuja ikawa ponapona yangu aisee.. watu wakasambaa ikawa mambo ya pande ya jamaa, mimi, wazazi wangu na serikali za mtaa. Haikuwa rahisi. Wazazi walinipambania sana hapa. Jamaa ilifikia time akaelewa kidogo , alikataa hata fidia sababu ya ukwasi alio nao. Alisema tu tutaonana hata kwingineko. Ikaisha hivyo. Sikuweza kutembea kwa wiki karibu mbili, mwili umevimba, nikawa wa kukandwa maji huku bi mkubwa ananibembeleza nisife😂😂. Nilipopata ahueni nikaondoka mkoani ili jamaa asije kuniua kabisa.

Siku narudi home baada ya muda kupita, nilimuona yule bidada kajipaukia. Tukasalimiana akaniambia walishaachana na jamaa kitambo tu sababu ya uchenjeu wake.. akataka kuniletea habari za mahaba nikamwambia we GUMA nini (mama Amina voice).

Tangu hapo sitaki hata kusikia wake za watu
 
Habari zenu wakuu.. Poleni na majukumu na harakati za hapa na pale, gharama za maisha zinapanda ila tunapanda nazo hakuna kukata tamaa.

Kuna visa kama viwili viliwahi kunitokea back in the days vya kufumaniwa ambavyo sikuwahi kumueleza yeyote.

Cha kwanza kilikuwa hivi.

Kuna mwaka nilipata kazi mkoa fulani kwenye shirika moja lisilo la kiserikali. Ilikuwa ni nje ya mkoa niliokuwa nikiishi awali. Sasa kwenye mtaa niliokuwa nimepanga, kulikuwa na mwanamke mmoja ni kama alitokea kunizimia sana. Hatukuwahi kuwa na mazoea sababu alikuwa ni mke wa mtu, ila ishara za uzinzi zilinijulisha hivyo.

Kuna siku ikatokea pale mtaani kuna sherehe nyumba moja ya mshua fulani, na ndio mwenyekiti wa mtaa huo na ananikubali sana yule mzee, alizoea kuniita mwanaye, nilikuwa sehemu ya wahudhuriaji, yule bidada vilevile. Kutokana na huo mchanganyiko ndio ikawa mwanzo wa kuanzisha mazoea nae na mawasiliano tukabadilishana rasmi.

TUlikuwa tunapigiana simu mara mojamoja ndani ya ile wiki ya kwanza tena majira ya mchana na ilikuwa ni salamu tu na si love affairs ingawa kulikuwa kuna kujikanyaga kimaongezi ambapo haikuhitaji C tatu kujua kunapo jambo hapo.

Siku moja alinipigia simu usiku, nikashtuka kwanza sababu najua kaolewa inakuwaje anipigie muda ambao kwa namna yoyote mumewe anaweza kuwa nyumbani? Nikapokea, tukasalimiana ikabidi nimuulize kwanini apige muda huo akasema mumewe kasafiri. Basi tukaongea sana usiku ule hadi kuhitimisha kuwa tuwe wapenzi ila kwa siri sana. Roho za tamaa na uzuri wa bidada wala sikujali kama jamaa yake anaweza kunifanyia vibaya kama tupo Sodoma siku akija kugundua.

Usiku huohuo bidada akaanza kulazimisha aje kwangu alale, nikamzuia. Akaomba tutoke ikiwezekana ila nikakataa pia sababu ni mwanzo tu isije kuwa anataka kuniharibia tu. Basi tukawa wa kuwasiliana tu, siku kama ya tatu ikawa ndio siku ya kuonana nae rasmi, kwakuwa walikuwa hawajazaa haikuwa shida. Tulionana na niliichakaza vibaya mno. Bibie ana kimwili ka wastani tu, ni slim halafu mimi nimeenda hewani kumzidi kwa hiyo nilikuwa nafanya nnavotaka, iwe nimembebelea au nimembananisha bado iliwezekana, maamuzi yalikuwa kama ya Lowassa tu kuhama chama. Na yeye alidai anapenda kudeka kwenye mwili ulioenda air (hewani) kama wangu.

Basi bwana kadri muda ulivyozidi kusogea nikanogewa, akanogewa pia. Ikawa ndio mchezo wetu kukutana na kumwaga moto. Siku moja yule mzee mwenyekiti aliniita akaniuliza kuhusu mie na yule bidada mke wa mtu, nikashtuka sana kwa sababu sikutegemea kama anaweza kuwa anafahamu, na kajuaje ilhali mimi naamini najua kutunza siri? Mzee alinionya akaniambia acha kabisa mara moja. Nikaitikia kwa kichwa huku nikiwa na hofu pia sababu mambo yashakuwa exposed.

Nikataka kukata mazoea na bidada ila ilikuwa ngumu sababu alichokionja alidai hakuwahi kukipata. Basi nikapumbazwa na maneno ya kudeka nikaona potelea pote, nikaendelea kuburuza, kumbuka muda huo bado mumewe hajaja.

Siku hazikuganda, mumewe akarejea. Tulijitahidi sana kujizuia lakini tabia ikishajijenga ni ngumu sana kuishape... Ikawa ni ngumu hata kukutana tena. Nakumbuka tangu mumewe arudi nilikutana na bibie mara moja nikafanikiwa japo alikuwa rahisi sababu ya ugumu wa kupata nafasi. Ile mara ya pili ndio balaa lilipokujia.

Siku hiyo Bidada alitoka jioni kama saa 11 kwake anaenda nyumbani kwao mara moja. Sasa wakati anarudi ilikuwa mida kama saa tatu kasoro usiku akaomba anione angalau kwa dakika 10 tu sababu ya ufinyu wa nafasi sababu ya uwepo wa mumewe. Nikakubali, tukakutana kachochoro kamoja mbali kidogo na mtaani, huwa hakana jam sana kwa usiku kama ule. Nafsi ni kama ilikuwa inakataa ila kibri cha ubinadamu kiliniongoza. Kumbe ni kama kuna watu walikuwa wanaspy, sijajua waliorganize vipi hadi kujua tutakuwa eneo hilo, na walijuaje na nani aliorganize, I don't know.

Tulipokutana haikuishia story tu, ikabidi kapigwe kamechi ka kuibaiba. Baada ya kumaliza nikaona tochi zimewashwa toka pande moja ya chochoro kutuelekea, watu kama wanne halafu zikasikika sauti za kugadhabika zikisema tulieni hapohapo.. yule bidada nikasikia anasema Mungu wangu, mme wangu huku anajiliza kipumbavu.. aisee nguvu zikaisha nikawaza hata nikikimbia hawa ntawaacha wote kweli? Na hata nikithubutu, wakiniitia mwizi maana yake maisha yanatamatikia hapo. Akili ikawaza haraka sana kwamba leo, ndio ile siku naenda kutatuliwa kama pazia la hekalu.. nikaona noo, ikabidi nichanganye miguu kujinusuru, liwalo na liwe. Bora kufa umepambana kuliko kufa kizembe

Sasa kutokana na uhafifu wa mwanga nikakimbia bila hata kujua naelekea wapi wala ninapokanyaga, kama kona tatu naona njemba zinakuja tu, bahati baya nikaenda kukanyaga shimo la maji taka ya bafu nikateleza na kuanguka mguu ukawa kama umeshtuka.. aisee, nilijaza mtaa. Nilipigwa makofi na zile njemba utadhani zenyewe ndio zenye mke, ila mhusika akawa analia tu kwanini unatembea na mke wangu.. nilibebwa juu juu hadi kwa mwenyekiti.

Ilikuwa aibu siwafichi.. Kule kwa mwenyekiti baada ya muda tukabaki kama watu nane nahojiwa hapo.. Suala ikawa waende polisi ila mwenyekiti akawa kama ananikingia kifua kwa namna fulani akidai tuyamalize hukuhuku. Acheni tu aisee.. nililala palepale sababu niliogopa nikienda kulala home naweza kuchomewa ndani au waniijie wanipelekee moto. Asubuhi walikuja wakuu wa pale kazini, ikawa ni vikao tu. Muda huo mguu ulioshtuka umevimba vibaya mno hata kutembea siwezi.. Ilinitoka Milioni 2 na laki tatu jamaa ndio akawa mpole aisee. Akiba karibu yote ikaenda kwenye msala. Na hapo nikawa naona kama bado jamaa ataniendea kwa Sangoma, sababu ni cama alikuwa calm kiaina flani, wasiwasi ukabaki kwangu. Kazini hawakunifukuza, wakanihamishia tu mkoa mwingine.

Baada ya kupata unafuu wa mguu nikamtafuta jamaa nikiwa siamini kama yameisha upande wake, nikamuachia na vitu vyote vya ndani nikaondoka na huo mkoa aisee. Sijajua walimalizaje na mkewe , ila ulipita muda sana nikiwa mkoa mwingine huo bidada akanicheki tena.. nikavunja kabisa ile line ya simu. Tunaonana kwenye social networks tu..

Kwakuwa tumeumbiwa kusahau, nikajichanganya tena kwenye mkasa wa pili..
mshangazi ulining'ata ukaniachia makovu
 
Back
Top Bottom