Kwanini wahandisi hatupewi kipaumbele na wanawake?

Kwanini wahandisi hatupewi kipaumbele na wanawake?

Nimeona mara nyingi wanawake wakiwashobokea Waalimu, Madaktari, Wanasheria na baadhi ya watu wa career fulani fulani cha ajabu nimeona ma Engineer hatupewi priority wala kushobokewa na wanawake sasa swali linakuja hapa; kwanini nyinyi wanawake hamtushobokei sisi ma Engineer au kutupa kipaombele sawa na hao wengine?
Nadhani tatizo ni ma-engineer wa kibongo kukosa ubunifu. Ukiulizwa hata ni nini umekitenda katika engeneering yako huna, unategemea mwanamke akupe priority vipi?
 
Mimi nafikiri tatizo liko kwetu wahandisi, kwa sababu niliwahi kuktana na mama mmoja katika mazungumzo ya hapa na pale akasema kwamba mainjinia wengi wameishia kuoa masekretari!!! Nilivyojiongeza kidogo tu nikakuta kuna kaukweli!!!!
Muda mwingi wanatumia site au kwa ofisi kupiga kazi mkuu, hiyo inaweza kuwa sababu.
 
Sasa kama hata Kiswahili hamjui unashangaa nini. Na wewe ni engineer au wamekuomba uwasemee. Kipaombele ndo nini.
 
Nilidate engineer long time kitambo. Hawajui kuremba wanakwenda straight to the point. "Mimi ninakupenda wewe unasemaje?"
Yaani vile wanavyofanya equations za physics na hesabu ndivyo wanavyotongoza.
Hata ukimzingua engineer anakupa makavu live bila chenga[emoji52]
 
Tatizo engineers mnasubiri sana kusaini certificates za malipo na siku hizi ndio hivyo hadi ulipwe inachukua zaidi ya nusu mwaka. ..!! Wanawake wanapenda papo kwa papo cash sio ooh ...nasubiri malipo bado yapo kwenye process...!
Inamaana siku hizi hawakopeshi?[emoji1] [emoji1]
 
Hamna swaga mna fact hapo ndo mnapowashindwa kila kitu calculation na kukuta umevaa suti na raba ni kawaida
hahahaa kuna Prof mmoja alikuwa anavaa suti na Sandals pale chuo
 
Nilidate engineer long time kitambo. Hawajui kuremba wanakwenda straight to the point. "Mimi ninakupenda wewe unasemaje?"
Yaani vile wanavyofanya equations za physics na hesabu ndivyo wanavyotongoza.
Hahahaa vipi hio hali uliichukuliaje
 
Tatizo engineers mnasubiri sana kusaini certificates za malipo na siku hizi ndio hivyo hadi ulipwe inachukua zaidi ya nusu mwaka. ..!! Wanawake wanapenda papo kwa papo cash sio ooh ...nasubiri malipo bado yapo kwenye process...!
Hahahahaa hatuna helaa sio
 
Kwanza mko serious sana, wakimya mno, halafu mnajisikia kama nini, hakuna kucheka ni amri tu, hivyo hamjui kufuata formula za kutongoza kazi ulevi tu
mkuu asante ila umetutukana sana ahahahaaa
 
MaEngineer tunaleta principles ngumu kwenye mapenzi,wakati mwingine mapenzi ni uongo, sasa engineers kutengeneza uongo ni mgumu sana, tunadeal na facts.
very true kama mimi kwenye uhusiano sijawahi kudanganya
 
Kwa sababu mnajidai hamna time na mamgwine..afu hamna lugha nzuri labda za kutiririka nyie mna lugha zenu za maconcrete basi..ata cl for engineers haijawasaidia kabisa[emoji23][emoji23][emoji23]
CL for engineers ile ya kichoko tu haina msaada ata kidogo
 
Utakuta ni katoto ka mwaka wa kwanza au wa pili hapo UDSM hakana mbele wala nyuma eti kanajiita engineer wakati probably mwisho wa semister to hapo katadisco.....
Hahahaa hio ipo lakini kwanini umwonee wivu lakini??
 
Tena nyie mnajisikia sana;
mlisababisha mwana jf wa mbeya
akajitia kitanzi;
 
Mimi ni bora ningekataliwa kabisa, ila nachapiwa kwa kwenda mbele...!
 
mkuu asante ila umetutukana sana ahahahaaa
Hapana mkuu, yaani wengi niliowaona (japo ni ndugu zangu) ni walevi, halafu wako serious sana, yaani wakimya mno na hawana story
 
Nimeona mara nyingi wanawake wakiwashobokea Waalimu, Madaktari, Wanasheria na baadhi ya watu wa career fulani fulani cha ajabu nimeona ma Engineer hatupewi priority wala kushobokewa na wanawake sasa swali linakuja hapa; kwanini nyinyi wanawake hamtushobokei sisi ma Engineer au kutupa kipaombele sawa na hao wengine?

kwasababu mnavaaga yale mabuti yenu makubwa kama wapanda nguzo za tanesco au wapanda mlima kilimanjaro.
 
Back
Top Bottom