Kwanini stand ya Mnazi Mmoja haina sehemu ya abiria kupumzika wakisubiria usafiri?

The Burning Spear

JF-Expert Member
Dec 23, 2011
3,444
8,297
Naziuliza mamlaka za jiji la Dar es Salaam.

Inakuwaje pale stand ya Mnazi Mmoja hapajajengwa vibanda kwa ajili ya kujikinga na mvua au jua.

Naongelea hasa huku kwenye daladala za Kinyerezi, Segerea. Mburahati na vibajaji vinavyo enda city centre.

Vibanda hivi Husaidia pia mtu kupumzila pale anaposubiri usafiri pengine ni mgonjwa au mzee, Nikiangalia vituo vingi vya daladala vina maeneo ya abiria kupumzika.

Kwanini Mnazi Mmoja hamna?
 
Back
Top Bottom