Mwanza: Mamlaka zimeshindwa kujenga kibanda cha abiria kusubiria usafiri kwenye kituo cha daladala cha Nata?

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
Mamlaka zitusaidie kuboresha kituo cha daladala cha Nata mazingira ya kituo hicho sio rafiki kwa abiria wengi ambao wanakitegemea kusubiria usafiri wakiwemo wazee na watu wenye ulemavu hasa mvua zikinyesha au wakati wa jua kali.

Kituo hicho ni kati ya vituo vinavyokusanya abiria wengi kwa wakati mmoja lakini cha kushangaza wahusika wameshindwa hata kujenga kibanda cha abiria kusubiria usafiri hali ambayo inatusababishia kadhia kubwa na abiria kusimama eneo lolote bila utaratibu.

Kwenye kituo hicho hakuna eneo rasmi ambalo abiria wanaweza kusubiria usafiri watu wengine wanasimama eneo ambalo ni hatarishi, lakini kuna wakati unakuta eneo hilo likiwa na msongamano zaidi kutokana na machinga kuweka meza zao za biashara sehemu ambazo wamezea kusimama huku mabasi ya baadhi ya kampuni wakati mwingine kupaki eneo hilo kwa muda mrefu jambo ambalo pia linapelekea msongamano wa daladala eneo hilo.

Ni vyema mamlaka kama hawana bajeti kwa sasa wanaweza kuwashawishi wadau wa sekta ya usafiri walioko eneo la Nata linalozunguka eneo hilo ambalo ni kero kwa abiria kujitolea kujenga kibanda kwa ajili ya abiria wengi ambao wengine ufika kwa ajili ya kukata tiketi au kusubiria magari baada ya kushuka, lakini pia wanaweza kushawishi wadau wengine ikiwemo kampuni kujenga kibanda hicho.

Hali ikiendelea kubakia ilivyo ni kuhatarisha usalama wa abiria ambao wanasimama maeneo ambayo sio rafiki lakini pia kwa namna watu wanavyokuwa wamesimama kiholela kwenye maeneo hayo inapelekea mandhari ya pale kuonekana katika taswira hasi.

Licha ya hivyo mamlaka za Jiji la Mwanza ni wakati wa kuwaza nje ya boksi namna ya kujenga vibanda vya abiria kwenye baadhi ya vituo muhimu ambavyo vimezoeleka kuwa na abiria wengi hii itasaidia kuwaondolea kero abiria na itafanya Jiji kuwa katika mandhari nzuri.

IMG_20240108_154418_25.jpg

23370f23-1766-4983-a22d-f6395486f204.jpeg

Duh huo msongamano wawatu ni balaaa!
Bila shaka uongozi utakifanyia kazi ni suala la muda tu

Mitano tena
 
sasa hapo utajenga wapi kibanda ndugu abiria, lakini pia icho sio kituo rasmi.

Hata hivyo mamlaka zimekuskia maoni yako na kwakweli kwa uskivu wa mamlaka zetu, kuna namna ya kufanya angalau kupunguza makali ya jua na mvua zinazowasulubisha vizuri sana kutuoni apo..
Asanti sana na pole sana...
 
Wenye makampuni ya mabusi wanunue maeneo hapo wajenge stendi zao ili kuepusha usumbufu na sio lazima mabusi yote yaishie nata yanaweza kwenda hadi mabatini ili kusudi msongamano upungue
 
huyo aache uhuni sehemu ya kusimama ipo na pametengenezwa vituo kwa magari yanayoingia mjini na yanayotoka labda aseme kivuli ndio hakuna
 
Back
Top Bottom