Salum Fumo

New Member
Jan 3, 2018
4
1
HEBU TUZUNGUMZE HILI, ILE BUSTANI YA MNAZI MMOJA (Kwenye Mnara wa Uhuru)

Pale Dar es salaam hususan City Centre i.e Kariakoo, Mnazi Moja. Kwa haraka haraka hakuna sehemu mfano wa Garden ya watu walau kuweza kupumzika from mihangaiko na mizunguko ya mjini. Hakuna pia open space ambayo mtu unaweza ukakaa ukatulia na kaPC kako ukapiga ishu zako, labda ukae kwenye kituo cha magari, uingie msikitini ama kwenye mgahawa. Hali ni tofauti na pale Zanzibar. Nisiseme mengi.

Hii garden ya Uhuru kwanini isienziwa kwa kugeuzwa kuwa public space. Ndani yake kukawa na services kama public working place, mini library, stationery, Restaurant, Ice cream shop; pamoja na sehemu za kupumzika zenye Vimbweta, nyasi nzuri ama just baraza tuu. Yaani uwekezaji mdogo tuu unafanyika. Ndani kuna vijiwe nongwa kama vile vya kahawa na drafti. Yaani kitu kama hiko.

Sijuzi professionally niseme vipi but siishi kupawaza pale. Nadhani pangeweza hata kuweka hadhi mpya ya ule mnara wa mwenge wa uhuru.

Na kama itakuwa na tija katika uendeshaji wa Bustani na kuchangia pato la wilaya tunaweza sema kuingia mule ndani labda tunatozwa Buku unalipia kwa njia tofautitofauti ikiwezekana kunakuwa na entrace ID kwa wateja wa mara kwa mara kwamba mtu unalipia zako kwa mwezi ama mwaka unapewa card unaingia zako ila service kule ndani unalipia, yaani isiwe bure kabisa ili kuepusha unnecessary msongamano pale ndani.

Hili litakuwa msaada mkubwa sana kwa watu wengi wenye uhitaji wa maeneo kama haya ya kupumzika. Public space moja ambayo ipo walau kwa urahisi kuipata na kupumzika ni ile ya mbele ya benki ya NBC posta pale na kuna moja ipo station japa ambayo technically sio bustani ila ipo na sakafu fresh na kivuli cha kutosha kiasi imekuwa ni sehemu nzuri ya watu kupumzika.

Hili wazo naona lina tija kuliko kulihudumia eneo kama lile la ukumbusho ilhali tunaweza kulienzi kwa kutufaidisha wananchi wenyewe.

Mnazi Mmoja.jpg

Nimewasilisha.
 
Ni central park gani hapa duniani inalipiwa?
Sina ufahamu mpana kiasi hiko kwa nchi za nje but kwa hapa kwetu mfano mzuri pale zanzibar, hawalipii. Ila nadhani hata ikiwa ni free entrance itakuwa poa pia just management iwe nzuri.
 
Back
Top Bottom