Kwanini Nyerere hakumkubali Lowassa?

Kwanini Nyerere hakumkubali Lowassa?

Nyerere alimkataa lowassa kwa vile yeye na baba yake waliuza kijiji kizima na watu ndani huko umachame na baadaye kukimbilia ummasaini ambako walipata hifadhi na kulelewa na familia ya marehemu moringe sokoine. Jeje wajua lowassa ni mchagga wa machame? Jiulize ni kipi kilimfanya abadilishe kabila na kujiita mmasai?

Wamasai hawana tabia za ajabu zikiwemo uroho wa madaraka na wizi wa mali za umma.

Ni mmeru sio mchaga wala mmasai!
 
Kwa sifa ulizompa mwalimu hapo juu. Watanzania wengi watakuwa wanafiki. Kwa nini leo hamyaenzi mambo yaliyoasisiwa na gwiji leo mnataka kuyabomoa. Azimio la Arusha si limevunjwa mbele yake. Kazi ya watu kutembea kwa miguu kutoka Mbambabay mpaka Butiama ikawa haina thamani tena. Mndai serikali ya Tanganyika leo, je huo si unafiki na dharau kwa mwalimu? Mnahoji faida za muungano leo, huo siyo unafiki?
hata msemeje tumeziba maskio,lowasa ni fisadi na kamwe hawezi kuwa rais wa nchi hii na kwa taarifa yako tumeshajua nguvu zake zinakotoka zaidi licha ya marekani pia tumegundua ni agent na tumeanza vita vya kiroho mpaka kieleweke! si unajua vita vyetu si juu ya damu na nyama bali juu ya..................... na.................................
 
Mtolewa bana!, Nguvu zake zinatoka wapi vile?
 
Acheni NYERERE aitwe NYERERE!!! Hakun kiongoz yyt anaeweza kucmama nae hapa Tz, alikuw anashika jembe analima, na bado hakuna asset yyt unaeza mnyooshea kidole kuw ni mali yake na amekuw magogoni 25 yrs, leo EL uwaziri mkuu tu hata 5yrs haijfika bt mali zake chungu nzima, NYERERE alikuw mzalendo wa ukweli na mwenye kuona mbali, aliyoyapinga yote cc 2kajiona wajanja leo yanatutokea puani, nasikia mpk KIA EL ataka kununua, kisa inasemekana KIA yote pale ni Tanzanite full, wana lowasa kwa hili la Nyerere mmegonga mwamba kajpangeni upya!!!!!!!!!!!!!!
 
Nilimpenda sana Lowassa ila kwa Kumchjafua Nyerere naona Bora nimpende Mtikila
Imani na itikadi kali juu ya siasa ya ujamaa na kujitegemea ni kirusi kilichokuwa kimeathiri kwa kiasi kikubwa mfumo wa ufahamu wa baba wa Taifa mwalimu Nyerere na, kuamini kuwa hakuna kitakachofanya nchi isonge mbele zaidi ya siasa ya ujamaa na kujitegemea. Msimamo uliosababisha chuki kwa wajasiriamali wengi waliojitolea nguvu zao halali kuongeza vipato, mmojawapo akiwa Lowassa.

Chuki ambayo iliibuka wazi wakati wa kinyang'anyiro cha kuwania urais mwaka 1995. Kwa kuwa Nyerere tayari alikuwa ameshajichagulia mtu wa kumrithisha kiti kilichokuwa kinaachwa na mzee wa ruksa. Wengine waliokuwa na nia ya kuwania kiti hicho akawaundia zengwe la kuwaangusha.

Mmoja wa wanasiasa walioathirika na propaganda hizo ni mheshimiwa LOWASSA ambaye hivi sasa mamilioni ya watanzania wanategemea ukombozi wa kweli kutoka kwake. Mwingine aliyeathiriwa na zengwe la NYERERE ni rais wa sasa Mh JM KIKWETE.

Hakuna siri kuwa MKAPA ndiye aliyekuwa chaguo la wazi la mwalimu kiasi cha kutumia kila aina ya ushawishi wake kuhakikisha kuwa LOWASSA na KIKWETE wanaanguka. Kinachosikitisha, zaidi ya miaka 15 imepita sasa bado kuna Watanzania ambao wanaamini kile kilichosemwa na NYERERE dhidi ya LOWASSA.

Propaganda ni kitu kibaya sana, mtu anaweza kuujengea hoja uongo na kuwa ukweli na, watu wakashikilia misimamo wakitetea uongo uliogeuzwa na mwana propaganda kuwa ukweli.

NYERERE alimkataa LOWASSA kwa kisingizio cha kivuli cha ubepari, kwa bahati mbaya wakati huo hakukuwa na mtu wa kumuuliza NYERERE kwa nini hakupambana na ubepari wa LOWASSA wakati wa utawala wake badala yake iwe wakati wa uchaguzi ambao unafanyika mbali na awamu yake ya uongozi? Hapa mtu makini ataamini kuwa propaganda hizo zilikuwa zinaongozwa na chuki binafsi na wala sio uzalendo.

Mtu makini ataamini kuwa NYERERE alikuwa anajua kuwa, ujasiriamali wa LOWASSA haukuwa haramu ndiyo maana hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi yake.

Ni wakati sasa kwa wale waliorithi habari za mapokeo dhidi ya LOWASSA na kujiaminisha kuwa ni mtu asiyefaa. Wafikirishe akili zao kwa makini na sote kwa pamoja tumuunge mkono mtu huyu iwapo atasimama kwa ajili ya kuomba nafasi ya kuliongoza Taifa hili.
 
Kwa hiyo ulitaka waziri mkuu atembelee baiskeli na sungusungu ndiyo wawe walinzi wake?

Kwani sasa EL anatembelea nini na kilichomfanya aende na msafara ule ni nini? Angemtembelea marehemu ng'ombe wake aliyekufa kama anavyotembelea ng'ombe zake leo bila msafara ingekuwa na ubaya gani?
Hata hivyo hukuielewa mantiki yangu. Nilitaka kuonyesha ubinafsi alionao kiasi cha kuona mali za umma si kitu muhimu kama ng'ombe wake mmoja.
 
Maneno yako ni mazuri pia, lakini yafaa utamke na uweke wazi. Ameiba nini na nini? Ameiba ibaje? Alivyoviiba viko wapi ili wananchi wajue, mwizi hukamatwa na kushitakiwa. Amekamatwa na nani na kithibiti kiko wapi. Njoo na vielelezo vyenye ushahidi hapa wala si maneno ya kufikirika.

Hebu wacha kututania yakheeeeeeee!
 
Imani na itikadi kali juu ya siasa ya ujamaa na kujitegemea ni kirusi kilichokuwa kimeathiri kwa kiasi kikubwa mfumo wa ufahamu wa baba wa Taifa mwalimu Nyerere na, kuamini kuwa hakuna kitakachofanya nchi isonge mbele zaidi ya siasa ya ujamaa na kujitegemea. Msimamo uliosababisha chuki kwa wajasiriamali wengi waliojitolea nguvu zao halali kuongeza vipato, mmojawapo akiwa Lowassa.

Chuki ambayo iliibuka wazi wakati wa kinyang'anyiro cha kuwania urais mwaka 1995. Kwa kuwa Nyerere tayari alikuwa ameshajichagulia mtu wa kumrithisha kiti kilichokuwa kinaachwa na mzee wa ruksa. Wengine waliokuwa na nia ya kuwania kiti hicho akawaundia zengwe la kuwaangusha.

Mmoja wa wanasiasa walioathirika na propaganda hizo ni mheshimiwa LOWASSA ambaye hivi sasa mamilioni ya watanzania wanategemea ukombozi wa kweli kutoka kwake. Mwingine aliyeathiriwa na zengwe la NYERERE ni rais wa sasa Mh JM KIKWETE.

Hakuna siri kuwa MKAPA ndiye aliyekuwa chaguo la wazi la mwalimu kiasi cha kutumia kila aina ya ushawishi wake kuhakikisha kuwa LOWASSA na KIKWETE wanaanguka. Kinachosikitisha, zaidi ya miaka 15 imepita sasa bado kuna Watanzania ambao wanaamini kile kilichosemwa na NYERERE dhidi ya LOWASSA.

Propaganda ni kitu kibaya sana, mtu anaweza kuujengea hoja uongo na kuwa ukweli na, watu wakashikilia misimamo wakitetea uongo uliogeuzwa na mwana propaganda kuwa ukweli.

NYERERE alimkataa LOWASSA kwa kisingizio cha kivuli cha ubepari, kwa bahati mbaya wakati huo hakukuwa na mtu wa kumuuliza NYERERE kwa nini hakupambana na ubepari wa LOWASSA wakati wa utawala wake badala yake iwe wakati wa uchaguzi ambao unafanyika mbali na awamu yake ya uongozi? Hapa mtu makini ataamini kuwa propaganda hizo zilikuwa zinaongozwa na chuki binafsi na wala sio uzalendo.

Mtu makini ataamini kuwa NYERERE alikuwa anajua kuwa, ujasiriamali wa LOWASSA haukuwa haramu ndiyo maana hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi yake.

Ni wakati sasa kwa wale waliorithi habari za mapokeo dhidi ya LOWASSA na kujiaminisha kuwa ni mtu asiyefaa. Wafikirishe akili zao kwa makini na sote kwa pamoja tumuunge mkono mtu huyu iwapo atasimama kwa ajili ya kuomba nafasi ya kuliongoza Taifa hili.

Mwanzisha Mada kaomba Mada yake ifungwe
 
Hakuna ubishi kuwa Tanzania ni ya watanzania wote, kila mtu anayo haki ya kuchaguliwa na kuchagua kiongozi, hii ni pamoja na Mhe. Lowassa anayo haki ya kugombea kuwa Rais ndani ya nchi yake ilimradi ikitimiza matakwa ya kanuni na taratibu za kugombea nafasi hiyo kisha kuweza kuwashawishi wapiga kura wampigie kura. Lakini kama nchi tumekubaliana kuwa Mwl. Nyerere tumpe heshima ya kuwa baba wa taifa letu kutokana na kutuongoza kwa uwadilfu kwa miaka 27 tangu nchi ipate uhuru. Sasa baba wa taifa amekufa bila ya kutengua kauli yake ya kuwakataa Lowassa na John wasigombee nafasi ya urais wa Tanzania kutokana na maono yake.

Je, tukimruhusu Lowassa agombee urais, ipi itakuwa nafasi ya Nyerere kuwa baba wa taifa? Je, bado tutaendelea kuenzi fikra zake? Je, yakitokea yale aliyoyakataa Nyerere kwa Lowassa kuwa rais tutamlaumu nani?

CCM chagueni moja kati ya Lowassa au Nyerere
 
Wewe inaelekea historia ktk akili yako.Nyerere hakumkataza Lowassa asiwe Rais wa TZ.jikumbushe vizuri.alihoji pesa aliokuwa nayo.na kumbuka wagombea walikuwa wengi hivo ilibidi apatikane mmoja na sio lazima Lowassa kipindi kile.mbona hata kikwete aliambiwa asubilie?kwani alitengua kauli yake kabla ya kufa?Lowassa huu ndio muda wake wa kuwa rais wa nchi hii kuanzia 2015.suala la utajiri sio ishu kwa vile hata hao maskini viongozi hawajasaidia lolote zaidi ya kujitajirisha wakiingia madarakani.na pia ufisadi wa lowassa anaotuhumiwa juu ya richmond kumbuka maamuzi hayo asingeweza kuyapitisha peke yake bila boss wake kujua.Ebu mwacheni lowassa awe rais na lazima awe.
 
Lowassa atashinda kugombea urais ndani ya ccm kwa kuwa hakuna wa kumgusa ndani ya chama! Pia kawanunua wajumbe wote wa mikutano halali ya chama hicho!
 
Hakuna ubishi kuwa Tanzania ni ya watanzania wote, kila mtu anayo haki ya kuchaguliwa na kuchagua kiongozi, hii ni pamoja na Mhe. Lowassa anayo haki ya kugombea kuwa Rais ndani ya nchi yake ilimradi ikitimiza matakwa ya kanuni na taratibu za kugombea nafasi hiyo kisha kuweza kuwashawishi wapiga kura wampigie kura. Lakini kama nchi tumekubaliana kuwa Mwl. Nyerere tumpe heshima ya kuwa baba wa taifa letu kutokana na kutuongoza kwa uwadilfu kwa miaka 27 tangu nchi ipate uhuru. Sasa baba wa taifa amekufa bila ya kutengua kauli yake ya kuwakataa Lowassa na John wasigombee nafasi ya urais wa Tanzania kutokana na maono yake.

Je, tukimruhusu Lowassa agombee urais, ipi itakuwa nafasi ya Nyerere kuwa baba wa taifa? Je, bado tutaendelea kuenzi fikra zake? Je, yakitokea yale aliyoyakataa Nyerere kwa Lowassa kuwa rais tutamlaumu nani?

CCM chagueni moja kati ya Lowassa au Nyerere

julius nyerere alikuwa na mtu wake mkapa nisingetarajia amsifie kikwete au yeyote,kama azimio la arusha alikubali litupwe,sembuse kauli zake
 
Wewe inaelekea historia ktk akili yako.Nyerere hakumkataza Lowassa asiwe Rais wa TZ.jikumbushe vizuri.alihoji pesa aliokuwa nayo.na kumbuka wagombea walikuwa wengi hivo ilibidi apatikane mmoja na sio lazima Lowassa kipindi kile.mbona hata kikwete aliambiwa asubilie?kwani alitengua kauli yake kabla ya kufa?Lowassa huu ndio muda wake wa kuwa rais wa nchi hii kuanzia 2015.suala la utajiri sio ishu kwa vile hata hao maskini viongozi hawajasaidia lolote zaidi ya kujitajirisha wakiingia madarakani.na pia ufisadi wa lowassa anaotuhumiwa juu ya richmond kumbuka maamuzi hayo asingeweza kuyapitisha peke yake bila boss wake kujua.Ebu mwacheni lowassa awe rais na lazima awe.

-Kama hawezi kujibu suala la pesa zake alikozipata ataweza nini?

-Kama mkataba mmoja wa RICHMOND ataweza nini?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom