Imani na itikadi kali juu ya siasa ya ujamaa na kujitegemea ni kirusi kilichokuwa kimeathiri kwa kiasi kikubwa mfumo wa ufahamu wa baba wa Taifa mwalimu Nyerere na, kuamini kuwa hakuna kitakachofanya nchi isonge mbele zaidi ya siasa ya ujamaa na kujitegemea. Msimamo uliosababisha chuki kwa wajasiriamali wengi waliojitolea nguvu zao halali kuongeza vipato, mmojawapo akiwa Lowassa. Chuki ambayo iliibuka wazi wakati wa kinyang'anyiro cha kuwania urais mwaka 1995. Kwa kuwa Nyerere tayari alikuwa ameshajichagulia mtu wa kumrithisha kiti kilichokuwa kinaachwa na mzee wa ruksa. Wengine waliokuwa na nia ya kuwania kiti hicho akawaundia zengwe la kuwaangusha. Mmoja wa wanasiasa walioathirika na propaganda hizo ni mheshimiwa LOWASSA ambaye hivi sasa mamilioni ya watanzania wanategemea ukombozi wa kweli kutoka kwake. Mwingine aliyeathiriwa na zengwe la NYERERE ni rais wa sasa Mh JM KIKWETE. Hakuna siri kuwa MKAPA ndiye aliyekuwa chaguo la wazi la mwalimu kiasi cha kutumia kila aina ya ushawishi wake kuhakikisha kuwa LOWASSA na KIKWETE wanaanguka. Kinachosikitisha, zaidi ya miaka 15 imepita sasa bado kuna Watanzania ambao wanaamini kile kilichosemwa na NYERERE dhidi ya LOWASSA. Propaganda ni kitu kibaya sana, mtu anaweza kuujengea hoja uongo na kuwa ukweli na, watu wakashikilia misimamo wakitetea uongo uliogeuzwa na mwana propaganda kuwa ukweli. NYERERE alimkataa LOWASSA kwa kisingizio cha kivuli cha ubepari, kwa bahati mbaya wakati huo hakukuwa na mtu wa kumuuliza NYERERE kwa nini hakupambana na ubepari wa LOWASSA wakati wa utawala wake badala yake iwe wakati wa uchaguzi ambao unafanyika mbali na awamu yake ya uongozi? Hapa mtu makini ataamini kuwa propaganda hizo zilikuwa zinaongozwa na chuki binafsi na wala sio uzalendo. Mtu makini ataamini kuwa NYERERE alikuwa anajua kuwa, ujasiriamali wa LOWASSA haukuwa haramu ndiyo maana hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi yake. Ni wakati sasa kwa wale waliorithi habari za mapokeo dhidi ya LOWASSA na kujiaminisha kuwa ni mtu asiyefaa. Wafikirishe akili zao kwa makini na sote kwa pamoja tumuunge mkono mtu huyu iwapo atasimama kwa ajili ya kuomba nafasi ya kuliongoza Taifa hili.