Kwanini Nyerere hakumkubali Lowassa?

Kwanini Nyerere hakumkubali Lowassa?

KUNDI LA LOWASSA KUMNANGA MWALIMU NYERERE KABURINI AMA KWELI NGUVU ZA FEDHA HUTIA WATU UKICHAA HATA KAMA NI ZA K-ISHETANI!!!

Enyi madalali wa Mh Lowassa kwa wapiga kura wa nchi hii,

Chezea vitu vyote Tanzania hii kwa kadri utakavyoona ni vema na inafaa LAKINI unapoligusa jina la Mwalimu Nyerere kwa kujadili mizaha kama hii wenye akili hawatolumbana nawe ila walalahoi wengi wa nchi hii hujui tu ni kwa kiasi gani utakua umewatonesha moyoni mbele ya dhuluma za VITENDO VYA KIKATILI VYA MAFISADI vilivyofanya maisha yasiwe maisha tena nchi hii.

Nasema chezeeni Richmond, Dowans, endeleeni kwani mnasita kitu gani hapo; kachezeeni pia Symbioni, TANESCO, chezeeni CCM huko hata jina la Rais Kikwetekaichezeeni huko ILA wa kumnanga Mwalimu Nyerere kwa mambo ya kihayawani humu na kote kwingineko ... be warned, hilo si jina la kuuzia dagaa masokoni. Wana-Lowassa katucheeni zaidi na zaidi kifisadi WaTanzania tulio hai maana pindi utakaporusha tu ka-shilingi kwenye sakafu la kanisa au msikiti tayari WaTanzania tutakua tushasahau yote na kukimbilia haraka haraka kumfungulia mfalme Edward lango la Ikulu Magogoni akatawale!!!!!

Ni nani atakayeweza kukuzuia kitu nchi hii; endelea mkuu kachezee kila kitu, cheza, cheza tu. Hata haya matatizo lukuki ya taifa kulala gizani kila uchao sababu ya makovu ya Richmond yote ni mapambo tu tena ya kujitakia sisi wenyewe. Yale mamilioni 150,000,000/- uliotulazimisha kwa umasikini wetu kukulipa wewe kila siku iendayo kwa Mungu shauri ya ulaghai kwa TANESCO hivi sasa ndio wakati wa kuzitumia kisawasawa kila kona ya nchi hii mpaka kila mtu atakapogundua kwamba kweli kidume nchi hii Edward Lowassa wa Monduli; nunua kila kitu wala usiache wajumbe wote ndani ya CCM mikoa kwa vipapatio vya kuku na ubwabwa, kanunue na tume ya uchaguzi upya, magazeti yote kwa kazi ya fedha si ndio hizo bana! LAKINI kwa kuchezea jina la Mwalimu Nyerere kupitia kwa walevi hawa mtandaoni mkome kabisa!!!!!!!!

Naam, kwa kundi hili linaloongozwa na nguvu za fedha za ki-mashetani, waache kundi la Lowassa wamnange salama Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, WaTanzania tunasubiri kwa hamu kubwa sana tu
KUJA KUONA MWISHO WAKE hizi lugha chafu kama atapona mtu hapo kisiasa. Jibu ni 2015 hata CCMkirongwe vipi na fedha za MAFISADI.

Haya ndiyo matatizo ya wacheza kolokolo. Wapi hapo Nyerere amesemwa vibaya? Wapi hapo nyere amekashifiwa? Je kusema alikuwa na chuki ni kosa? Kusema alitumia propaganda ni kosa? Naona umepita mithiri ya tractor lenye jembe butu, unafyeka na kuacha magugu nyuma. Tengeneza maelezo yako yakae vyema.
 
kwa nn nyerere amuonee lowassa! Mbona kituko? Lowasa anakoelea ni kubaya, sijui anautaka urais hata kwa gharama gani!
 
Nakupongeza Jumakidogo,kwani yaonesha wazi kabisa wewe ni msemaji mzuri tu.Lakini ulichokiandika kinafaa kutamkwa kuzimu labda hawamfahamu Lowasa.yeye ni mwizi asilia na hakuna njia ya kufanya tabia yake hiyo imtoke hata kama ana nia ya kuacha udokozi.Imeshakuwa kama ngozi sasa na yamfaa akubali kurudi nyumbani aachane na siasa.Na kinachomfanya ang'ang'ane huko bungeni ni kuwa,anatafuta njia ya kujilinda zaidi adui zake wasipate mwanya wa kuhoji chanzo cha mali zake.Ajue kuwa hakuna mmbongo anayempenda na hakuna sababu ya yeye kuchafua magazeti.Yeye asubiri tu aachie ubunge uone wahuni watakavozikomba mali zake.

Maneno yako ni mazuri pia, lakini yafaa utamke na uweke wazi. Ameiba nini na nini? Ameiba ibaje? Alivyoviiba viko wapi ili wananchi wajue, mwizi hukamatwa na kushitakiwa. Amekamatwa na nani na kithibiti kiko wapi. Njoo na vielelezo vyenye ushahidi hapa wala si maneno ya kufikirika.
 
KUNDI LA LOWASSA KUMNANGA MWALIMU NYERERE KABURINI AMA KWELI NGUVU ZA FEDHA HUTIA WATU UKICHAA HATA KAMA NI ZA K-ISHETANI!!!

Enyi madalali wa Mh Lowassa kwa wapiga kura wa nchi hii,

Chezea vitu vyote Tanzania hii kwa kadri utakavyoona ni vema na inafaa LAKINI unapoligusa jina la Mwalimu Nyerere kwa kujadili mizaha kama hii wenye akili hawatolumbana nawe ila walalahoi wengi wa nchi hii hujui tu ni kwa kiasi gani utakua umewatonesha moyoni mbele ya dhuluma za VITENDO VYA KIKATILI VYA MAFISADI vilivyofanya maisha yasiwe maisha tena nchi hii.

Nasema chezeeni Richmond, Dowans, endeleeni kwani mnasita kitu gani hapo; kachezeeni pia Symbioni, TANESCO, chezeeni CCM huko hata jina la Rais Kikwetekaichezeeni huko ILA wa kumnanga Mwalimu Nyerere kwa mambo ya kihayawani humu na kote kwingineko ... be warned, hilo si jina la kuuzia dagaa masokoni. Wana-Lowassa katucheeni zaidi na zaidi kifisadi WaTanzania tulio hai maana pindi utakaporusha tu ka-shilingi kwenye sakafu la kanisa au msikiti tayari WaTanzania tutakua tushasahau yote na kukimbilia haraka haraka kumfungulia mfalme Edward lango la Ikulu Magogoni akatawale!!!!!

Ni nani atakayeweza kukuzuia kitu nchi hii; endelea mkuu kachezee kila kitu, cheza, cheza tu. Hata haya matatizo lukuki ya taifa kulala gizani kila uchao sababu ya makovu ya Richmond yote ni mapambo tu tena ya kujitakia sisi wenyewe. Yale mamilioni 150,000,000/- uliotulazimisha kwa umasikini wetu kukulipa wewe kila siku iendayo kwa Mungu shauri ya ulaghai kwa TANESCO hivi sasa ndio wakati wa kuzitumia kisawasawa kila kona ya nchi hii mpaka kila mtu atakapogundua kwamba kweli kidume nchi hii Edward Lowassa wa Monduli; nunua kila kitu wala usiache wajumbe wote ndani ya CCM mikoa kwa vipapatio vya kuku na ubwabwa, kanunue na tume ya uchaguzi upya, magazeti yote kwa kazi ya fedha si ndio hizo bana! LAKINI kwa kuchezea jina la Mwalimu Nyerere kupitia kwa walevi hawa mtandaoni mkome kabisa!!!!!!!!

Naam, kwa kundi hili linaloongozwa na nguvu za fedha za ki-mashetani, waache kundi la Lowassa wamnange salama Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, WaTanzania tunasubiri kwa hamu kubwa sana tu
KUJA KUONA MWISHO WAKE hizi lugha chafu kama atapona mtu hapo kisiasa. Jibu ni 2015 hata CCMkirongwe vipi na fedha za MAFISADI.

Ahsante sana mkuu.
Nyie wana Lowasa tafadhali tafakarini maneno haya kwa busara sana mtayaelewa, lakini mkileta ulevi wenu na kukurupuka mtaishia pabaya. Waulizeni CDM, wanajua technique nzuri za kuwakamata Watanzania na ndo mana kila siku wanazidi kuwapiga bao. Wanaepuka sana kumponda Baba yetu wa Taifa.
Fanyeni mzaha na jina la kilaza wenu toka Msoga lakini siyo jina la Mwalimu Nyerere, MTAPOTEA!.
 
Hivi Nyerere alimsema Lowassa kwa ubepari wake au kwa kujikusanyia mali nyingi kwa kipindi kifupi na bila ya vyanzo vinavyoeleweka?

Mimi siyo shabiki wa sera za Nyerere hata kidogo lakini penye mantiki lazima apewe credit. Hivi mbona yeye mwenyewe ameshindwa kuueleza Umma hivyo vyanzo vyake vya utajiri au anaogopa kurogwa?

Anayetakiwa kuthibitisha vyanzo vyake haramu ni wewe unayemtuhumu. Vinginevyo kama huna ushahidi unakaa kimya tu.
 
Hongera sana mkuu kwa kusema ukweli! Tusubiri wafuasi wa NAPE.

El.na kundi lako muogopeni mungu si siri watanzania ombeni mungu usiku kucha ili hili kundi lisifanikiwe kuingia ikulu
 
Ahsante sana mkuu.
Nyie wana Lowasa tafadhali tafakarini maneno haya kwa busara sana mtayaelewa, lakini mkileta ulevi wenu na kukurupuka mtaishia pabaya. Waulizeni CDM, wanajua technique nzuri za kuwakamata Watanzania na ndo mana kila siku wanazidi kuwapiga bao. Wanaepuka sana kumponda Baba yetu wa Taifa.
Fanyeni mzaha na jina la kilaza wenu toka Msoga lakini siyo jina la Mwalimu Nyerere, MTAPOTEA!.

Akili ni nywele kila mtu ana zake. Soma vizuri maelezo hayo na usitake kukuza mambo. Ni wapi nimemsema vibaya mwalimu hapo?
 
Bora muongelee humuhumu mana mkiongea hadharani,mi ntakuwa wa kwanza kuwapiga mawe,wasemeni wengine lakini siyo Nyerere,huu ni usenge,Nyerere alipigania hii nchi,huwezi kumtukana kwa sababu ya maslahi yako,Lowassa ni mwizi kuliko wezi wote Tz hata yeye mwenyewe analitambua hilo,acha kumtukana Nyerere,unatuudhi sana tena wengine huwa hatuchangii humu kazi yetu ni kusoma tu ila hakika wewe mwehu umenikera hadi nmekuandika,usijaribu tena kumsema Nyerere mana tutakuassassinate wewe na huyo mwizi wetu.
 
Kweli hapa Lowasa unapoteza pesa zako, mtu huyu uliyemtuma anahoja za kutukumbusha maovu yako na pale anaposema mwalimu alikuwa na chuki binafsi na nyie na JK kwa hali hii ya swahiba wako hupati kitu hapa hata utoe chapaa!
 
Akili ni nywele kila mtu ana zake. Soma vizuri maelezo hayo na usitake kukuza mambo. Ni wapi nimemsema vibaya mwalimu hapo?

Tuseme sawa hujamsema vibaya.
Uliposema kwamba mwalimu alikua na chuki binafsi na EL hapo hukumsema vibaya. Hata uliposema alimtengenezea EL zengwe pia hukumsema vibaya na hata uliporopoka kwamba mwalimu alisema uongo napo ulimsema mwalimu vizuri tu.
Tumia akili yako vizuri mkuu siyo useme maneno kama mtu asiyeshirikisha ubongo.
EL nae atakua anapoteza hela zake kama ataajiri kilaza kama wewe usiyeweza kumtetea na kuishia kumkashifu Mwalimu Nyerere.
 
Lowassa asipochaguliwa sasa hivi,haitakuwa kwa ajili ya Nyerere. Na kama ukisema Nyerere,ambaye yuko ndani ya jeneza ndie anayemzuia Lowassa kuwa Rais,I swear this Lowassa fellow will not become Presiident.
 
natumai umekuja kuandika huu upupu baada ya kuhongwa nyamachoma na whisky pale mwika
endelea kujitahidi lakini lowassa kwa urais 2015 ni ndoto za alinacha
 
Tuseme sawa hujamsema vibaya.
Uliposema kwamba mwalimu alikua na chuki binafsi na EL hapo hukumsema vibaya. Hata uliposema alimtengenezea EL zengwe pia hukumsema vibaya na hata uliporopoka kwamba mwalimu alisema uongo napo ulimsema mwalimu vizuri tu.
Tumia akili yako vizuri mkuu siyo useme maneno kama mtu asiyeshirikisha ubongo.
EL nae atakua anapoteza hela zake kama ataajiri kilaza kama wewe usiyeweza kumtetea na kuishia kumkashifu Mwalimu Nyerere.

Mi naona mtoa mada yupo sawa. Kawaida wtz huwa hampendi kuambiwa ukweli. Wote tunakumbuka ilivyokuwa. Ni kweli hayo yalitokea kika mtu anajua. Ingekua sio zengwe iwapo nyerere angekaa kimya na kuacha demokrasia ifanye kazi yake. Ingekuwa fair pia kama asengeweka msimamo juu ya mali za Lowasa. Alikuwa kiongozi mzuri lakinh alikuwa na mapungufu pia. Kwani mtoa mada amemsingizia?
 
Kweli hapa Lowasa unapoteza pesa zako, mtu huyu uliyemtuma anahoja za kutukumbusha maovu yako na pale anaposema mwalimu alikuwa na chuki binafsi na nyie na JK kwa hali hii ya swahiba wako hupati kitu hapa hata utoe chapaa!

Lowasa = Mkaa. I mean yaani hata uuoshe vipi hauwezi kuwa mweupe!!
 
Hongera sana mkuu kwa kusema ukweli! Tusubiri wafuasi wa NAPE.
Majungu matupu na kutumwagia upupu humu barazani. Mbona wakati ule Nyerere alipomsema Lowasa na wapambe wake walikaa kimya?Si Lowasa wala wapambe wake kina Pasco et al waliomtaka Nyerere athibitishe kauli yake dhidi ya Lowasa,miaka 12 baada ya kifo cha Nyerere na kwa kuuchungulia urais,mnakuja na upupu wenu
kumtetea bwana wenu bila haya ya uso!
Mtawadanganya vijana ambao walikuwa watoto wadogo enzi hizo.
 
NA zile ranchi za alizojigawia nao ni uonevu wa Nyerere.

Umenikumbusha mkuu. Kuna siku ng'ombe wa Lowasa alikufa pale ranchi ya Mkata, Lowasa wakati huo akiwa Waziri Mkuu alikwenda na msafara wa Kiserikali na Maaskari wa kumlinda kutoka Dar hadi Mkata! Fikiria thamani ya ng'ombe mmoja wa Lowasa na gharama za Serikali; magari ya Serikali na Walinzi! Matumizi mabaya ya mali za umma, halafu wapambe wanamwaga upupu kuwapotosha watu kwa manufaa ya bwana wao.
 
Imani na itikadi kali juu ya siasa ya ujamaa na kujitegemea ni kirusi kilichokuwa kimeathiri kwa kiasi kikubwa mfumo wa ufahamu wa baba wa Taifa mwalimu Nyerere na, kuamini kuwa hakuna kitakachofanya nchi isonge mbele zaidi ya siasa ya ujamaa na kujitegemea. Msimamo uliosababisha chuki kwa wajasiriamali wengi waliojitolea nguvu zao halali kuongeza vipato, mmojawapo akiwa Lowassa.

Chuki ambayo iliibuka wazi wakati wa kinyang'anyiro cha kuwania urais mwaka 1995. Kwa kuwa Nyerere tayari alikuwa ameshajichagulia mtu wa kumrithisha kiti kilichokuwa kinaachwa na mzee wa ruksa. Wengine waliokuwa na nia ya kuwania kiti hicho akawaundia zengwe la kuwaangusha.

Mmoja wa wanasiasa walioathirika na propaganda hizo ni mheshimiwa LOWASSA ambaye hivi sasa mamilioni ya watanzania wanategemea ukombozi wa kweli kutoka kwake. Mwingine aliyeathiriwa na zengwe la NYERERE ni rais wa sasa Mh JM KIKWETE.

Hakuna siri kuwa MKAPA ndiye aliyekuwa chaguo la wazi la mwalimu kiasi cha kutumia kila aina ya ushawishi wake kuhakikisha kuwa LOWASSA na KIKWETE wanaanguka. Kinachosikitisha, zaidi ya miaka 15 imepita sasa bado kuna Watanzania ambao wanaamini kile kilichosemwa na NYERERE dhidi ya LOWASSA.

Propaganda ni kitu kibaya sana, mtu anaweza kuujengea hoja uongo na kuwa ukweli na, watu wakashikilia misimamo wakitetea uongo uliogeuzwa na mwana propaganda kuwa ukweli.

NYERERE alimkataa LOWASSA kwa kisingizio cha kivuli cha ubepari, kwa bahati mbaya wakati huo hakukuwa na mtu wa kumuuliza NYERERE kwa nini hakupambana na ubepari wa LOWASSA wakati wa utawala wake badala yake iwe wakati wa uchaguzi ambao unafanyika mbali na awamu yake ya uongozi? Hapa mtu makini ataamini kuwa propaganda hizo zilikuwa zinaongozwa na chuki binafsi na wala sio uzalendo.

Mtu makini ataamini kuwa NYERERE alikuwa anajua kuwa, ujasiriamali wa LOWASSA haukuwa haramu ndiyo maana hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi yake.

Ni wakati sasa kwa wale waliorithi habari za mapokeo dhidi ya LOWASSA na kujiaminisha kuwa ni mtu asiyefaa. Wafikirishe akili zao kwa makini na sote kwa pamoja tumuunge mkono mtu huyu iwapo atasimama kwa ajili ya kuomba nafasi ya kuliongoza Taifa hili.
Huyo Ndugu Lowasa anafahamika kwa tabia yake ya ukora! na ni mtu hatari sana hapa Tanzania! usione hivi yeye na kundi lake amesababisha nchi kuwa katika hali ya umaskini.Anajaribu makanisani! hata juzi alikuwa huko mskiltini wakati wa maulid! Jamani tuchunge sana mtu hyu! Akiwa Rais atakuwa kama wale wa Misri wenye kutaka ten percent kwa kila biashara inayofanyika hapa nchini
 
Bora muongelee humuhumu mana mkiongea hadharani,mi ntakuwa wa kwanza kuwapiga mawe,wasemeni wengine lakini siyo Nyerere,huu ni usenge,Nyerere alipigania hii nchi,huwezi kumtukana kwa sababu ya maslahi yako,Lowassa ni mwizi kuliko wezi wote Tz hata yeye mwenyewe analitambua hilo,acha kumtukana Nyerere,unatuudhi sana tena wengine huwa hatuchangii humu kazi yetu ni kusoma tu ila hakika wewe mwehu umenikera hadi nmekuandika,usijaribu tena kumsema Nyerere mana tutakuassassinate wewe na huyo mwizi wetu.

Matusi na vitisho vyako havizuii maoni huru. Ubabe wako katika kuandika sentensi haupindishi ukweli. Hasira zako hadhiathiri chochote katika ninayoamini. Busara zako zilizotuama makalioni ndizo zilizokuelekeza undike matusi badala ya kupinga hoja kwa hoja zenye akili. Hujui, wala sikulazimishi uamini. Mimi ni mtu ninayeyakubali sana mazuri ya mwalimu, yake mengi kuliko mabaya. Lakini ni mtu wa pande mbili. Kama kuna ambacho alikuwa wrong kidogo hatuwezi kukaa kimya.
 
Umenikumbusha mkuu. Kuna siku ng'ombe wa Lowasa alikufa pale ranchi ya Mkata, Lowasa wakati huo akiwa Waziri Mkuu alikwenda na msafara wa Kiserikali na Maaskari wa kumlinda kutoka Dar hadi Mkata! Fikiria thamani ya ng'ombe mmoja wa Lowasa na gharama za Serikali; magari ya Serikali na Walinzi! Matumizi mabaya ya mali za umma, halafu wapambe wanamwaga upupu kuwapotosha watu kwa manufaa ya bwana wao.

Kwa hiyo ulitaka waziri mkuu atembelee baiskeli na sungusungu ndiyo wawe walinzi wake?
 
Strange as it is, when people aspire for the big post, they first have to deal with Nyerere in one way or another. That is what we call a legacy...whether good or bad legacy, is upon the indivual who choose to look at the matter. But for me, Nyerere was the man. He mastered the game and played it very well, not matter how much we try to deny or refuse that fact!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom