Kwanini Nyerere hakumkubali Lowassa?

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Mwaka 1995, Lowassa na JK walikodi pamoja ndege ndogo binafsi kutoka Dar hadi Dodoma kwa madhumuni ya kurudisha fomu za kugombea Uraisi kupitia tiketi ya CCM............................................

Walipokuwa wakihojiwa na vyombo vya habari wote kwa pamoja walijivunia ujana wao na uzoefu walioupata serikalini kama ndivyo vigezo vya kufikiriwa kupandishwa cheo......................................

Nyerere alijikongoja kutoka Butiama hadi Chamwino (Ikulu ndogo ya Dodoma).........................na kwenye vikao vya kuchuja majina ya wagombea Uraisi tiketi ya CCM....................................Nyerere aliweka bayana ya kuwa kijana Lowassa alikuwa hafai nafasi hiyo ya Uraisi kwa sababu zifuatazo:-

a) Kwa nyadhifa chache tu alizopewa serikalini na ndani ya chama na kwa muda mfupi sana Lowassa alizitumia nafasi hizo kujilimbikizia mali.....................nafasi tajwa ni pamoja na Ubunge wa Taifa, ujumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa nafasi ambazo ni za kubebwa kwenye mbeleko za kiuteuzi tu na vigezo vya teuzi tajwa ni lelemama tupu...................................................

b) Akiwa waziri aliendelea kujilimbikizia mali na kuonyesha udhaifu mkubwa kiuongozi kwenye nchi hii inayofuata misingi ya kikatiba ya ujamaa na kujitegemea....................................................

c) Alinunua vyombo vya habari na kuvitumia kikamilifu katika kuwaghilibu watanzania ya kuwa yeye yu bora kiuongozi kuliko wengineo wote jambo ambalo si la kweli hata chembe......................................

d) Mbali ya ubinafsi uliokithiri tajwa, Lowassa alikuwa na mikwaruzo na wale wasiomkubali na huku akijenga kambi yake ndani ya ccm na hivyo kuleta migawanyiko ya kikabila na kipato na kuwa tishio la usalama wa utaifa............


kamati kuu iliafiki pendekezo la Nyerere na jina la Lowassa likatupwa kapuni......................

lowassa hakukata tamaa hata baada ya mjasiria mali Mkapa kutomteua kwenye baraza la mawaziri kutokana na kashfa za ufisadi lakini alikuwa rafiki yake Abdulrhaman Kinana aliyempigia debe hadi akarudishwa kwenye safu ya walaji...................................

Ikumbukwe mwaka 1995 Kinana ndiye aliyekuwa meneja wa kampuni za Mkapa ..................kwa hiyo kazi ni kulipana fadhila tu............

Baada ya mjasiria mali Mkapa kuachia ngazi, Waziri Mkuu wa wakati huo Bw. Tluway Sumaye ndiye aliyeonekana ni tishio haswa............................na mkakati ukaundwa wa kumthibiti ambao kwa kiasi kikubwa ulihitaji Lowassa amwachie JK kwa makubaliano ya Jk kumteua kuwa PM............................that is where Lowassa kissed off his burning dream of being our next president...........................hakuna PM aliyewahi kuvunja huo mwiko except Nyerere...................................

Kutokana na demokrasia ya kujuana ndani ya vikao vya CCM Jk akawa mgombea Uraisi wa CCM na the rest is history..................

sasa Lowassa matarajio yake kuukwaa Uraisi yameota mbawa baada ya wenzie ndani ya ccm kudai wamejivua gamba.........................lakini lengo ni kuhakikisha ya kuwa katika succession politics of 2015...........................CCM will not be distracted by offical graft allegations now well epitomized by Lowassa....................................kwa hiyo panga pangua........................CCM itaonekana kwa wapigakura haswa wa vijijini kuwa imejisafisha kama Lowassa atajivua gamba....................and time is running out on him after his closest ally.....................Rostam Aziz amebwaga manyanga.........................................................if Lowassa will overcome the pressure and stay put CCM may as well hand power to Chadema today.................................and forget the presidency in 2015.......................................the choices are as stark as that..................................

Angelic Nyerere must be laughing at the wickdeness in Lowassa by now.............................that his words continue to haunt lowassa's political career like a colossus...............................
May Nyerere's soul continue to rest in peace....................
 
CCM WOTE SI WAADILIFU NA SI WATENDAJI

LOWASA SI MUADILIFU ILA NI MTENDAJI

HAWANA UJANJA 2015 MGOMBEA WA CCM NI LOWASA

NA HAPO NDIPO CHADEMA TUNAICHUKUA NJI HII KIULAINI

kama kumsukuma mlevi dampo
 
CCM WOTE SI WAADILIFU NA SI WATENDAJI

LOWASA SI MUADILIFU ILA NI MTENDAJI
HAWANA UJANJA 2015 MGOMBEA WA CCM NI LOWASA

NA HAPO NDIPO CHADEMA TUNAICHUKUA NJI HII KIULAINI


kama kumsukuma mlevi dampo


hizi njozi haziwezi kutokea.......................ccm are not that stupid and chadema ought to brace for a tougher fight for power at the helm
 
Mwalimu Nyerere apumzike kwa amani....alifanya kazi kubwa sana na moja ya kazi kubwa sana ni kuona mbali ndo maana hata huyu ki..meo asingepata kama Mwalimu angekuwepo

true..........................................despite being hurtful to many of JK and Lowassa adulators....................
 
CCM WOTE SI WAADILIFU NA SI WATENDAJI LOWASA SI MUADILIFU ILA NI MTENDAJI hizi njozi haziwezi kutokea.......................ccm are not that stupid and chadema ought to brace for a tougher fight for power at the helm
CCM wamekuwa wajinga muda mrefu na inavyoonekana wataendelea kuwa wajinga! Mtu akionekana kutetea maslahi ya umma km Tirdo Muhando, Magufuli, nk kwao ni adui mkubwa na wanafanya kila njia kumnyamazisha! As long as CCM wataendelea kuwa genge la ulaji, pamoja na hila zao za kuvua magamba feki na kuiacha sumu iwe pale pale, they are going down to history!
 
CCM WOTE SI WAADILIFU NA SI WATENDAJI

LOWASA SI MUADILIFU ILA NI MTENDAJI



hizi njozi haziwezi kutokea.......................ccm are not that stupid and chadema ought to brace for a tougher fight for power at the helm

2015 UTAKUWA RUTASHUBAMBELE,SUBIRI UONE NCHI INAVYOENDA MIKONONI MWA MAGWANDA.LOWASA NDIE MGOMBEA PEKEE WA URAISI WA CCM amini usiamini
 
RUTASHUBANYUMA ....unatetea ufisadiiiiii! Inaonekana wewe unamuunga mkono LOWASA....kweli WATZ tumeishiwa ndio Maana WAKENYA hutucheka.....Yaani tunaona kama hakuna kiongozi Mwingine zaidi ya Fisadi LOASA?!!!!!!
 
Tunamngoja Zitto agombee 2015 tumchague bila kujali kama anatokea chama cha magwanda. Mwengine yoyote kutoka magwanda, hatumpi urais.
 
RUTASHUBANYUMA ....unatetea ufisadiiiiii! Inaonekana wewe unamuunga mkono LOWASA....kweli WATZ tumeishiwa ndio Maana WAKENYA hutucheka.....Yaani tunaona kama hakuna kiongozi Mwingine zaidi ya Fisadi LOASA?!!!!!!

sidhani kama hata umenielewa....................ninamtetea vipi wakati nasema hatufai.................................lol
 
Natamani sana NIMBEBE MAGUFULI NIMUAPISHE AWE JUU YA RAIS.ILA SIJUI CHEO NIIITEJE.NAONA URAIS HAUTOSHI

huyu waziri wa bomoabomoa asije hata kukubomolea pango lako............................be careful watu ambao jk na mkapa kwa upamoja wao wamewakumbatia..............
 
[h=2][/h]
Tunamngoja Zitto agombee 2015 tumchague bila kujali kama anatokea chama cha magwanda. Mwengine yoyote kutoka magwanda, hatumpi urais.

Tumwombee afya kwanza kwa sababu anaelekea ukingoni ..........................
 
2015 UTAKUWA RUTASHUBAMBELE,SUBIRI UONE NCHI INAVYOENDA MIKONONI MWA MAGWANDA.LOWASA NDIE MGOMBEA PEKEE WA URAISI WA CCM amini usiamini

time is the best teacher.................................
 
Wana Jamvi,

Nimesoma thread hii nikakumbuka mamabo ya nyerere na Lowasa.

Sitaki kutia chumvi, endeleeni wenyewe! tafadhali someni
Link: http://www.jambofor ums.com/showthre ad.php?t= 11092


SALAAM KWA MH. EDWARD LOWASA NA WENZAKE KUHUSU KUSEMA UKWELI (TRUTH) NA SUALA ZIMA LA UADILIFU NA UWAJIBIKAJI WA VIONGOZI TANZANIA

Nimemsoma Askofu Mokiwa kuhusu uadilifu na uwajibikaji wa viongozi wa serikali. Nianze kwa nukuu ya Sir Francis Bacon; samahani kwa kuileta kwenu kwa kiingereza, One of the schools of the Grecians, examines the matter of Truth and is at a stand to think what should be in it, that men should love lies, where neither they make for pleasure, as with poets, nor for advantage, as with the merchants but it is for the lies sake.

TRUTH is a naked and open daylight that does not show the masks, and mummeries and triumphs, of the world half so stately and daintily as could lights. Truth may perhaps come to the price of a pearl, that shows best by day but it will not rise to the price of a diamond or carbuncle, that shows best in varied lights. A mixture of a lie does ever add pleasure…Truth is the sovereign good of human nature.

The first creature of God, in the works of the days was the light of the sense; the last was the light of reason and his Sabbath work ever since is the illumination of his Spirit. First he breathed light upon the fore of the matter or chaos, then he breathed light into the fore of man and still he breathes and inspires light into the face of his chosen.

It is a pleasure , to stand upon the shore and to see ships tossed upon the sea, a pleasure to stand in the window of castle and to see a battle, and the adventures thereof below. "But no pleasure is comparable to standing upon the Vantage ground of TRUTH (a hill not to be commanded and where the air is always clear and serene) and to see the ERRORS, wanderings, and mists, and tempests in the valley below, so always that this prospect be with pity and not with swelling or pride. Certainly, it is heaven upon earth, to have a man's mind more in charity, rest in providence and turn upon the POLES OF TRUTH."

To pass from theological and philosophical truth, to the truth of civil business, it will be acknowledged, even by those who do not practice it, that clear and sound dealing, is the honor of man's nature; and that mixture of falsehoods, is like a alloy in coin of gold and silver, which may make the metal work the better but it embaseth it. For those winding and crooked courses, are the goings of the serpent, which goes barely upon the belly and not upon the feet. There is no vile , that does so cover a man with SHAME as to be found FALSE and PERTIFIDIOUS" . Mwisho wa kunukuu.

Naam, tazama ahadi ya 8 ya mwanachama wa CCM, inasema, " NITASEMA KWELI DAIMA, FITINA KWANGU MWIKO" mwisho wa kunukuu.
Ndugu zangu waheshimiwa wote waliotajwa katika sakata la Richmond napenda wasome kwa kurudia mara kadhaa nukuu hiyo niliyoanza nayo hapo juu katika mstakabali mzima wa kutukuza kwa unyenyekevu kitu kinaitwa kusema UKWELI (TRUTH). Wahenga walisema UKWELI UNAUMA. Ni vizuri tu wote tukakubaliana hivyo. Huo ndio ustaarabu.

Ndio utu kusema ukweli. Tuhuma hizo nzito zinazowakabili wakizijibu pasipo kukiri kitu kinaitwa UKWELI na badala yake wakaendekeza majigambo , uwongo na tukafanya hivyo mahali pasipo husika hawalitakii Taifa letu la Tanzania mema. Katika hili hawatakiwi kutumia jaziba au hasira. Tena wakumbuke kuwa Mh. Edward Lowasa, na Karamagi na Msabaha walipewa nafasi halali Bungeni. Pale walichokifanya kwa bahati mbaya walitawaliwa na jazba na hasira " ANGER ".

Ndugu zangu, kuhusu hasira naomba niwaase kama mtaalam mmoja kwa jina SENECA alivyosema kuwa ukikumbwa na hasira (samahani kwa kunukuu kwa kiingereza)"there is no other way but to meditate and ruminate well upon the effects of anger, how it troubles man's life. The best time to do this is to look back upon anger when the fit is thoroughly over. Anger is like ruin, which breaks itself upon that, it falls. The scripture teaches us to possess our souls in patience. Whosoever is out of patience is out of possession of his soul. Men must not turn bees" Mwisho wa kunukuu.

Katika makala yangu iliyopita Salaam kwa Mawaziri wa Mhe. J.Kikwete kuhusu uadilifu na uwajibikaji kwa sehemu kubwa nilizungumzia juu ya mawaziri bila kumtaja Mheshimiwa Edward Lowasa. Mb wa Monduli. Kwa haya aliyoyafanya baada ya kuomba kwa Spika Bungeni na kupewa nafasi ya kwanza ajieleze kuhusu ufisadi wa Richmond, namtafadhalisha asome na kurudia mara kadhaa nukuu niliyoanza nayo hapo juu sambamba na hiyo ya mtaalamu SENECA. Napenda niseme kuwa kwa yale aliyosema Bungeni na Monduli na katika mahijioano ya TVT, bwana Lowasa nasema "si mkweli hata chembe moja".

Waandishi wa habari wengu tu wamekwisha mchambua kwa usahihi jinsi asivyokuwa mkweli, asivyo muadilifu anavyopenda kusifiwa kwa gharama yoyotena asivyolitakia mema Taifa letu. Narudia, asome kwa utulivu nukuu zote mbili nilizoanza nazo hapo juu. Kama Mwanasheria Mkuu, Mwanyika na wenzake Lowassa hakuridhika na ushauri wao juu ya Richmond na kuona kuwa ulikuwa na madhara kitaifa, kwanini hakutafuta ushauri wa ziada? Je? Hizo ndizo rasilimali watu pekee nchini katika ushauri wa kiserikali? Je, Vyuo Vikuu na Mahakama Kuu hakuna wataalam wa kisheria wa kuisaidia serikali? Did he leave any stone un-turned?

Kwa mapenzi mema na nchi yetu na mwana (CCM) napenda niwape mfano hai wa Bwana Lowasa asivyo muadilifu na asivyopenda kuwajibika kichama CCM na kiserikali. Tanzania nzima mtakumbuka kuwa huyu mheshimiwa Edward Lowasa alikuwa ni mmoja wa wagombea wa nafasi ya Urais mwaka 1995 na akaenguliwa kwa hoja nzito ya kutokuwa muadilifu na marehemu Baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere, kwa ukweli (wala sio tuhuma) kuwa alikuwa amejilimbikizia mali nyingi kwa kipindi kifupi ndani ya CCM na Serikali.Muda mfupi alikuwa ni mtumishi wa CCM, muda mfupi kama Mkurugenzi wa kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha.

Mfano hai wenyewe uko hivi; tufuatane kwa kuusoma tafadhali:-

Mara baada ya kurudi Butiama, 1995, baada ya kuenguliwa kugombea nafasi ya urais, siku moja mapema asubuhi Bwana Lowasa alonipigia simu na kusema yafuatayo: "Bwana Kasori, naomba uende kumwambia Baba wa taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere, aende Monduli kusaidia kusafisha jina langu ili nisikose ubunge kutokana na yale aliyonisema Dodoma".

Nilishikilia mkono wa simu (TTCL) kwa zaidi ya nusu saa tukiwa tunazungumza na hatimaye mimi nilipata ujasiri wa kumwambia Bwana Lowasa kuwa siwezi kwenda kusema maneno hayo kwa Baba wa taifa na kwamba akitaka aje Butiama na nitamruhusu waongee ana kwa ana. Nikanyamaza na hatimaye yeye akawa wa kwanza kukata simu. Hiyo ikawa itifaki njema kwangu!

Kesho yake tena asubuhi nilipokea simu, safari hii akawa ni mheshimiwa Mzee Rashidi Mfaume Kawawa. Kwa maneno yake alisema "Bwana Kasori,jana ulizungumza na Edward Lowasa; naomba ufikishe ombi lake kwa Baba wa taifa tafadhali". Kutokana na heshima ya Mheshimiwa Mzee Kawawa, nilikubali na nikaenda na kabla ya hapo nilimuomba Mzee Kawawa akae karibu na simu ili nimpe jibu muda si mrefu.

Nilimueleza Baba wa Taifa kuwa "Mheshimiwa Edward Lowasa kupitia kwa Mhe. Mzee Rashidi Mfaume Kawawa anaomba usaidie kusafisha jina lake kule jimboni kwake Monduli ili asikose ubunge kutokana na yale uliyomsema katika Kamati Kuu ya CCM Dodoma". Jibu la Baba wa Taifa alilonipa ni kuwa "Nenda umwambie Mzee Rashidi Mfaume Kawawa asiwe mjinga kama Lowasa"!

Watanzania wote, leo March19, 2008, nawaomba radhi kuwa jibu hilo kwa uzito wa maneno hayo kuwa "Kawawa asiwe mjinga kama Lowasa" kweli kwa kuzingatia heshima kati ya wazee hao wawili; "Kawawa sikumwambia hivyo"! Badala yake nilimdanganya (nawaomba radhi tena watanzania) jibu nililompa Mzee Kawawa ni kuwa juma lililokuwa linafuata tungekuwa Dar es Salaam na kwamba aje Msasani aongee na Baba wa Taifa. Mhe. Kawawa alikubali. Nikarudi kwa Baba wa taifa kusema uongo (naomba radhi tena) kuwa "Mzee Kawawa ameomba mzungumze tatizo la Lowasa tutakapofika Dar es Salaam". Baba wa taifa alikubali na akaagiza nimuombe Mhe. mzee Kawawa kuwa Lowasa na Guninita na wapambe wengine wa Lowasa wote wafike Msasani.

Siku ya siku ikafika. Tukawepo Msasani na Mhe.mzee Kawawa akaja. Lowasa hakuwepo! Sababu anazijua mwenyewe.(muulizeni maana nasema ukweli). Mkutano ulipoanza mzungumzaji wa kwanza nikawa mimi, kueleza lengo la mkutano. Mzungumzaji wa pili alikuwa Baba wa Taifa na swali la kwanza ni kuuliza Lowasa yuko wapi?

Bila kupoteza wakati Mwalimu alisema "Rashidi , huyu Kasori ananiambai eti niende Monduli nikasafishe jina la Mhe. Lowasa eti asikose ubunge kwamba nilimchafulia Dodoma katika Kikao cha Kamati Kuu ya CCM. Kutokana na ombi lako nilimtuma akuambie usiwe mjinga kama Lowasa. Kasori alikuambia eh?

"Oneni , huko nyuma tayari nilishasema uongo kwa kutosema maneno hayo kwa Mhe. mzee Kawawa. Kweli hilo kurudiwa na Baba wa Taifa kwa Mzee Kawawa mbele yangu lilisababisha kalamu yangu kuanguka, nikatetemeka na nikatokwa na jasho jingi mbele ya hao wazee!!! Bila kutegemea na kwa mshangao mkubwa Mhe. mzee Kawawa alikubali kwa kuitikia "NDIO ALINIAMBIA". Mwalimu akacheka sana!!!! Sababu sijui hadi leo kwa nini alicheka sana.

Kwa kuendelea, Mwalimu alimwambia Mzee Kawawa kuwa "Kasori ana umri mkubwa kuliko Lowasa. Kasori alipata taabu sana kufikisha kwangu ombi la Lowasa na aliniambia kuwa jana yake alikuwa amekataa ombi la Lowasa. Sasa nasema kuwa kwa umri wangu mimi mzee, Lowasa ni mtoto wangu tena mdogo sana.

Kwa heshima mliyonayo kwangu na kwa chama cha Mapinduzi mtanishangaa sana mkisikia niko Monduli eti nipo kwenye majukwaa nasafisha jina Bwana Lowasa asikose ubunge. Kweli Lowasa ni jasiri sana kusema maneno hayo. Hayo ningeambiwa na Kasori tu ningesita kumuamini. Lakini kwamba hata wewe Rashidi ulitumiwa kusema maneno hayo! Huyu Lowasa ni jasiri sana!!. Lakini kwa nini hajatuambia ukweli kuhusu mali hizo ambazo ni nyingi kuliko mimi ambaye nimekuwa Rais wenu kwa kipindi kirefu? Sasa Bwana Rashidi, nakuomba hivi, kamwambie mwenyekiti wa CCM Mhe.

Mwinyi aitishe wajumbe wote wa Kamati Kuu, chagueni tarehe na mahali popote Tanzania, mimi nitakuja kumsafisha Bwana Lowasa na nitagharamia mkutano huo kwa hela zangu. Kamwe msitumie hela za chama wala serikali. Monduli sitokwenda,umesikia eh?". Mkutano ukaisha hapo Msasani. Hadi uchaguzi 1995, unafanyika na kumalizika Baba wa Taifa hakwenda Monduli. Alichukia sana tabia za Lowasa na alimfahamu kama mtu muongo na mwenye kiburi.

Hadi Baba wa Taifa anafariki, sikuwahi na hata niandikapo makala hii sija sikia wala kusoma popote ambapo Lowasa anakanusha alivyolimbikiza mali akiwa mtumishi wa CCM na serikali kwa muda mfupi kiasi cha kumzidi Rais wa Kwanza !!!

Sasa anatuhumiwa na vyombo vya habari kununua sehemu ya Ranchi za Taifa kwa kuandika majina ya wanafamilia! Kama hilo nalo ni kweli, ningekuwa mimi nisingeota tena kugombea URAIS n.k Tanzania. Bora kuendelea na biashara kwa uwazi kuliko kupitia mgongo au wa serikali au wa chama ( CCM). Huo ndio ushauri wangu kama mwana CCM kwa Lowassa.

Angalia tunavyofanya "total transgression of CCM regulations and ethics." Kamati kuu 1995 ilimwona Mhe. Lowassa hana uadilifu. Mhe. Mkapa baada ya kuingia madarakani baada ya muda si mrefu sijui ni kwa kikao gain cha CCM na taasisi ipi ya serikali akamwona Lowassa ni safi na akamweka katika safu yake ya baraza la mawaziri.

Huyu bwana akaendelea na huo usafi hadi akaukwaa uwaziri mkuu 2005. Yote haya yanatia shaka kama kweli ndani ya CCM na Serikali tuna benki sahihi za takwimu za mienendo kitabia ya wanachama na watumishi wetu kama si kubebana kwa majina tu! Nilinunua gazeti la mzalendo nikampa Baba wa Taifa na aliposoma kuwa Lowassa ni Waziri alimaka AHH!! Katika hili nabaki nimeduwaa hasa tunapopeana madaraka makubwa ya kuendesha nchi kimzaha tu.

Tukumbuke kuwa kwa kila kitu na kwa dini yoyote Mungu huweka wazi mambo mahali na kwa muda atakao yeye.( Time and space) ya Mwalimu J.K Nyerere juu ya Lowassa tuliyapuuza. Sasa Mungu kayaanika! Basi tuone hizi tuhuma za RICHMOND n.k, Mikataba ya Madini, EPA zitakavyoshughuliki wa.

Ni huyu Lowasa leo anasema kanyimwa "Natural Justice" hakuulizwa na kamati , kaonewa, kamati ya Mwakyembe inauonea wivu uwaziri mkuu wake na ni mahiri wa kuchukizwa mikataba mibovu na kudhalilika! Oh kweli? Hivi Lowassa amewahi kusoma wasifu wa kila mmoja wa hao? Bila kupima uzito, busara na hekima ya maneno yake anasema ameachia ngazi kama alivyofanya Mhe.Alli Hassan Mwinyi, Peter Kisumo, Peter Siyovelwa n.k. Hivi CCM yetu hawa ndiyo viongozi tulio nao ngazi za juu? Wasio sema ukweli? Tukumbuke na kukiri kwa dhati wajibu wa wanachama wa CCM , katika katiba (ccm) inasema 15 (7) " kuwa tayari kujikosoa na kukosolewa…

Watanzania wenzangu haya anayosema Lowasa yanafanana na nukuu niliyoanza nayo? Fikiria nairudia tena "For those winding and crooked courses, are the goings of the serpent, which goes basely upon the belly and not upon the feet! There is no vile that does cover a man with shame as to be found false and pertifidious" Niharakishe kusema hapa kuwa viumbe vyote ambavyo havikupenda kusema ukweli Mungu aliviadhibu kwa kuvifanya vitembelee matumbo yao milele nyoka wakiwemo! Lowasa, Mwanyika, Hosea na wenzake naomba kama nilivyoanza, tafadhali wasome hiyo nukuu mara kadhaa na waielewe na kuizingatia.

Watanzania wanawashangaa, wanadharau na kuchukizwa na viongozi wasiopenda kusema ukweli kwa maisha magumu waliyo nayo ambayo wao wanawazomea kwa dharau kuwa ni wavivu na wachovu wa kufikiri. Wanasahau kuwa hawa watu wa kawaida ndio wanaozalisha kile kinacholipa mishahara na marupurupu yao. Kama viongozi wakuu wa CCM, katika hili daima kumbukeni wajibu wenu kwa mujibu wa katiba ya CCM, ibara ya 15 (4) kuwa wakati wote mkweli, mwaminifu na raia mwema wa Tanzania. Onekaneni hivyo kwa vitendo tafadhali. Utaratibu huu wa kusema uongo unadhoofisha amani na utulivu Tanzania.

Hayo niliyasema niko tayari kuyasema bungeni akiwepo Lowasa ikibidi. Hatuwezi kukubali nchi hii kuendelea kuwa na viongozi wa aina hii. WAWE WAKWELI, WASEME UKWELI TU. WANAPOKOSEA HARAKA NA KWA UKWELI NA UNYENYEKEVU WAOMBE RADHI KWENYE VYAMA VYAO, SERIKALINI NA KWA WANANCHI. NI UPUUZI WA HALI YA JUU KUJITETEA OVYO NA KUINGIZA UKABILA ( LOWASSA NA OLE NAIKO) HATA KWA MAKOSA YALIYO DHAHIRI.

Katika mahojiano na TVT Lowassa alikiri kuwa alishindwa kuvunja mkataba wa RICHMOND. Sababu alizitaja. Sawa. Waziri mkuu kama mtendaji mkuu wa Serikali, kwa mujibu wa kanuni za kudumu za utumishi wa umma ( Toleo 1994), kifungu F33, makosa yake kiserikali ni haya yafuatayo; 33( xi) omission which is against public interest. 33(xiii) negligence occasioning loss to the employer ( yaani serikali na taifa kwa ujumla). 33( xiv) gross negligence in the performance of duty. Kama mtendaji mkuu wa shughuli zote nzito za serikali bwana Lowassa hana namna ya kujitetea kwa makosa hayo yaliyodhahiri ambayo TANESCO imeendelea kudhoofishwa na RICHMOND kwa yeye kuogopa kutumia utaalam nje ya wale aliowaamini.

Mbona tuna vyuo vikuu, je, aalivitumia kikamilifu? Mbona kwa maswala yasiyo na maslahi ya maana tumezoea sasa kukodi wataalam wa nje? Kwanini hakujiridhisha katika maeneo yote hayo? Tatizo hili ni kubwa sana maana watanzania sasa wanatozwa viwango vikubwa sana kulipia umeme ikiwa ni pamoja na sehemu za uzalishaji zenye kutumia umeme achilia mbali malipo ya capacity charges? Nani anabisha kuwa kwa huu mkataba wa RICHMOND n.k Bwana Lowassa na Wenzake waliweka sahihi za kifo siyo kwa TANESCO tu bali pia cha kuvuruga maendeleo ya nchi yetu na kuendeleza umasikini?

Katika yote haya ambayo yamesemwa, Bwana Lowassa na wenzake wajue kuwa kama watanzania, we have a compelling moral case for complaining against him. There is also a compelling case that is in Tanzania's self interest. Recently many trade agreements already have made the poorest countries worse off. Such agreement already have condemned to death thousands of our people . Corporations of whatever name do strip Tanzania of its natural resources leaving behind a trail of environmental devastation etc.

This is done through very poor legal frameworks. Nimuhimu tukawa na viongozi waaminifu, waadilifu na wasema ukweli. Kwa haya yanayotendeka, something is fundamentally wrong with our government. Kwa kila maamuzi tunayoyafanya mara zote tuzingatie ni kwa maslahi ya nani; yale ya Taifa ni kipaumbele cha kwanza. Tuzingatie matumizi mazuri ya rasilimali zetu daima. Duniani ziko serikali nyingi tu ambazo zimevunja mikataba mibovu.

Kwa ziara nyingi ambazo viongozi wetu wanafanya na baada ya wanahabari kupigia kelele RICHMOND, kwanini Lowassa huko nje hakutaka kujifunza namna ya kuvunja mikataba mibovu? Yaani umahiri wake uliishia mkataba wa maji Dar es salaam na kiwanja cha Mnazi Mmoja? Mikakati yetu ya maendeleo imekuwa haileti tija iliyokusudiwa moja ya sababu ikiwa a flawed vision of development. Successful countries have a broader vision of what development entails and a more comprehensive strategy for bringing it about.

It is very unfortunate that in the majority of developing countries Tanzania included the nation – state has been weakened thoroughly! Haya maamuzi yanayofanywa na viongozi kama Lowassa ndiyo matokeo ya kutojua namna ya kuthibiti na kutumia kwa uangalifu fursa za kitu kinaitwa UTANDAWAZI.

Government that attempt to control capital flows find themselves unable to do so, as individuals find ways of circumventing the regulations. A county may want to raise the minimum wage, but discovers it can't, because foreign companies operating there will decide to move to a county with lower wages. Situmeona jinsi waziri Chiligati ( waziri wa kazi wa wakati huo) alivyohenyeshwa na wakubwa – wawekezaji kukataa kulipa kima cha chini hapa Tanzania? Wengine wamepunguza kazi ndugu zetu na sasa ni katika kundi la Machinga.

Waziri mkuu wa wakati huo Lowassa alisaidiaje? KIMYA! Dhahiri kinachoonekana hapo ni sense of powerlessness. Kwa kukumbatia matajiri na wakubwa wa nje, kupitia utanzawazi, baadhi ya viongozi wetu kama inavyojidhihirisha kupitia RICHMOND n.k. find their ability to act eroded. These days it is the order of the day for the electorate to see its government bending before foreigners wenye (mitaji). Day in day out democracy is being systematically undermined.

When the electorate shouts through the media etc, no body listens! Wanataka sifa tu. The electorate feels being thoroughly betrayed. Whether we like it or not, it is perceived, quite rightly, I think the way globalization is currently managed is not consistent with democratic principles. Little weight is given to the concerns and voices of ordinary people and the poor! Kwa kiburi cha wakubwa kutosikia, kutopenda kukosolewa Tanzania inaendelea kubaki masikini. Lowassa na wenzake wangekuwa makini na mahiri katika kusikiliza waandishi wa habari mapema RICHMOND n.k isingetufikisha tulipo sasa ambapo kila siku tunapoteza fedha nyingi. Tusingekuwa na tume juu ya tume ambazo baadhi tunazibeza kwa kejeli hata kwa kutumia chama (CCM).

CCM kweli tunasoma na kuzingatia kwa vitendo wajibu wa mwanachama wa CCM kifungu 15(3) na 15 (4) na 15(7) pamoja na ahadi za mwanachama wa CCM (3) na (4), na (8). Hivi CCM sasa ni mali na jina la mtu; kwamba hivyo mtu akikosolewa hamtaki kuona kakosa na mko tayari chama kife kwa ajili ya mtu mmoja au kundi dogo tu la watu? Nendeni Butiama mtupe majibu tafadhali. Uwezo, busara na nia vyote mnavyo. Ningekuwa Lowassa Butiama nisingeenda. Yeye kwenda huko ni kejeli kwa Baba wa Taifa.

BADO TUTAENDELEA KUWASEMA WENZAO KUHUSU MIKATABA YA HOVYO NA UKWAPUAJI WA RASILIMALI ZA NCHI HII. HOJA YA MWANASHERIA MKUU WA ZANZIBAR BWANA IDD PANDU HASSAN- " Lowasa kutostahili kuitwa Waziri mkuu Mstaafu" ni muhimu ikazingatiwa sambamba na utata wa stahili za mafao. Haitoshi kuimba utawala wa sheria na kumbe inapofika kwa wakubwa tunakunja na kunyonga sheria zetu. Sheria ni Msumeno. Someni Pensions Ordinance cap 371 sambamba na kanuni za kudumu za utumishi wa umma toleo la (1994) kifungu F53 (d) na (e). Tusiwe na kigugumizi katika hili.Tujifunze yaliyojiri hapo jirani Kenya hivi majuzi.

Namalizia kwa kusema "Tuheshimu na kudumisha kitu UKWELI". Kwa viongozi, zingatieni na kwa unyenyekevu heshimuni viapo vyenumnapokabidhiwa madaraka. Baba wa Taifa daima katika mkoba wake alibeba Bibilia na Azimio La Arusha. Nyinyi kwa kipindi hiki kigumu cha ufisadi na kukithiri kwa rushwa na mikataba mibovu; bebeni daima photo-copy za viapo vyenu pamoja na Bibilia au Koran pamoja na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mnazo dini zenu. Sikusikia yeyote akiapa kwa dini za asili kwa Rais au kwa Spika wa Bunge.

Nawashukuru watanzania, Mhe. Spika na Waandishi wa habari ambao wamekemea maneno ya Lowasa na wenzake baada ya kikao cha Bunge.

Namshukuru sana Mhe. William H. Shelukindo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji na Biashara kwa kuwasilisha hoja ya kuundwa kwa kamati ya kuchunguza Richmond na shukran maalum nazitoa kwa Dr. Mwakyembe na wajumbe wote walioshughulikia suala la Richmond na kuwasilisha taarifa Bungeni kwa uadilifu mkubwa sana.

Mwisho nawashukuru Watanzania wote na nchi za nje walionipongeza na kunipa moyo kuhusu makala zangu za kukemea ukwepuaji rasilimali za nchi BoT. yenye kichwa cha habari "Salaam kwa Mawaziri" Namshukuru Rais Kikwete. Namshukuru pia Mhariri gazeti la Rai namba 748 na 749.

Halmashauri kuu ya CCM inayokutana Butiama naitakia mafanikio makubwa katika maazimio watakayofikia . baada ya hapo muonekane mmedhamiria kutenda kwa kuleta maendeleo yenye kuzingatia uadilifu na uwajibikaji . viongozi wabovu wawajibishwe tu. Watanzania wengi leo bado wanamlilia Mwalimu J.K. Nyerere hasa kwa matatizo kama haya ya mikataba mibovu ya Madini, RICHMOND n.k. Wanasema sorry Mwalimu lived ahead of his time. Alituangazia kwa mengi, hakuna wa kutu tetea leo kwa matatizo yote haya.

Mungu Ibariki Tanzania. Mungu Ibariki Africa.

Samwel. H. Kasori
Katibu mstaafu wa
J.K.Nyerere
0754 372141
 
CCM wamekuwa wajinga muda mrefu na inavyoonekana wataendelea kuwa wajinga! Mtu akionekana kutetea maslahi ya umma km Tirdo Muhando, Magufuli, nk kwao ni adui mkubwa na wanafanya kila njia kumnyamazisha! As long as CCM wataendelea kuwa genge la ulaji, pamoja na hila zao za kuvua magamba feki na kuiacha sumu iwe pale pale, they are going down to history!

let work on this excellent dream and ensure it matures into fruition................
 
Is it fair to say Mwalimu was right about Lowassa being power hungry and corrupt?
Yericko Nyerere: Kwa nini Nyerere ali-veto kumkataa Lowasa?

Kwa nini Hayati Baba wa Taifa alitumia kura yake ya veto kumkataa Lowasa kwa sababu iliyoitwa na inayoaminika mpaka sasa kuwa "Lowassa ana utajiri mkubwa usio na ufafanuzi alioupata kwa mda mfupi tu akiwa mkurugenzi wa AICC?"

Ikumbukwe ni kuwa hoja hiyo ya Mwalimu Nyerere ilikuja baada ya Lowassa na wapambe wake kukodi ndege binafsi kutoka Arusha kwenda Dodoma kuhudhuria vikao vya uteuzi wa urais mwaka 1995, kitendo
hiki kilimfedhehesha sana Mwalimu na wazalendo wengine na hata kufikia kuliondoa jina la fisadi huyu nguli wa Tanzania,

Je leo utajiri wa Lowassa umekuwa halali?

Mamlaka ya mapato Tanzania inaweza kututhibitishia uhalali wa kodi alipayo mtu huyu?

Tangu afukuzwe uwaziri mkuu mwaka 2007 taarifa za kuaminika kutoka vyanzo muhimu nikuwa Lowassa alitenga Tsh12 bilioni kwa ajili ya kujitakasa, ambapo mpaka leo hii ameshatumia Tsh8 bilioni, je pesa hii ameipata wapi? Imelipiwa kodi kiasi gani? Atairudishaje akiwa rais?

Ili kuhuisha mjadala huu hebu niwaeleze jambo muhimu dhidi ya mtu huyu aitwae Edward Ngoyai Lowasa,

Labda niwaelekeze watafiti watafute faili la EL la enzi za TANU pale Lumumba. Mzee Paul Sozigwa suala hili analifahamu fika.

Ndiyo, Mwl. Nyerere alichukizwa na tabia ya Lowasa ya kujitajirisha kwa kuiba mali ya umma. Lowasa, licha ya tuhuma za wizi enzi akiwa AICC, kujimilikiaha majumba ya Masajili wa Majumba wakati akiwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mijini, Mwl. Nyerere alikuwa akifahamu wizi wa Lowasa tangu enzi za TANU. Kati ya mwaka 1974 na 1977 Lowasa aliiba pesa za TANU alizopewa kusamia ujenzi wa ofisi ya TANU Arusha.

Badala ya kujenga ofisi ya TANU Lowasa alinunua kiwanja na kujenga nyumba yake binafsi. Jambo hilo lilipogundulika mwaka 1982, lilimkasirisha sana Mwl hivyo kuamuru afukuzwe kwenye chama. Ni marehemu Edward Moringe Sokoine ndiye alimwombea msamaha kwa Mwl. Nyerere abadilishiwe adhabu.

Edward Lowasa alipewa adhabu mbadala; kuhudhuria kazini Ofisi Ndogo ya Chama Mtaa wa Lumumba kila siku bila kukosa, kuwa kazini masaa 8 bila kutoka lakini bila kupangiwa kazi yoyote hadi Chama kingeona ametubu na hatimaye apangiwe kazi nuingine. Lowasa alitumikia adhabu yake hadi Sokoine alipofariki.

Hiyo ndio sababu kuu ya Mwl. Nyerere kumkatalia Lowasa kugombea urais.

Kikwete, Mkuchika, Twaha Khalifan, Kinana, Bagenda na Msekwa wanajua ukweli wote kuhusiana na jambo hili. Ila maadamu kwa sasa hakuna tena maadili ya uongozi wa kisiasa nchini Tanzania, Lowassa anaweza kuachiwa awatawale wezi, wala rushwa na mediocre wa nchi hii.

"Kuna watu wasipokuelewa maneno na matendo yako, mshukuru Jah, wewe bado unafikra chanya, wakianza kukuelewa jichunguze ni wapi umeanguka maana umeanza kuwaza kama wao."

Published on2/07/2014 02:55:00 AM
 
Lowassa ni mwizi, mbadhirifu, fisadi, mchafu na sasa amekuwa muuaji. Anaua maadui zake kisiasa kwa kuwalisha sumu, sijui hizi mbinu za kigaidi kajifunzia Nigeria ama Israel alikoenda kuhiji?
 
Back
Top Bottom