Kwanini Nyerere hakumkubali Lowassa?

Kwanini Nyerere hakumkubali Lowassa?

Lowasa atagombea urais kwa chama kipi, maana mpaka sasa kashavunja miiko na maadili ya chama chake, sasa kama wewe hata chama chako tu hakikutaki, unang'ang'ania nini, hizo fedha anazogawa misikitini na makanisani na kwa vijana wa bodaboda, zitarudi vipi, kama kafikia hatua ya kuchafua nyumba za ibada kwa pesa chafu, itakuwaje akipewa nchi, tutapona kweli, akija kusema hamkunichagua ninyi, zilinichagua fedha tutakataa, na nyinyi mashehe na wachungaji mnaokubali pesa chafu za Lowasa na kuwarubuni waumini wenu wamuone Lowasa ni mzuri, mutawaeleza nini pindi machafuko yatakapoanza, muogopeni Mungu, na kumbukeni yaliyowakuta wenzenu Kenya.
 
Lowasa atagombea urais kwa chama kipi, maana mpaka sasa kashavunja miiko na maadili ya chama chake, sasa kama wewe hata chama chako tu hakikutaki, unang'ang'ania nini, hizo fedha anazogawa misikitini na makanisani na kwa vijana wa bodaboda, zitarudi vipi, kama kafikia hatua ya kuchafua nyumba za ibada kwa pesa chafu, itakuwaje akipewa nchi, tutapona kweli, akija kusema hamkunichagua ninyi, zilinichagua fedha tutakataa, na nyinyi mashehe na wachungaji mnaokubali pesa chafu za Lowasa na kuwarubuni waumini wenu wamuone Lowasa ni mzuri, mutawaeleza nini pindi machafuko yatakapoanza, muogopeni Mungu, na kumbukeni yaliyowakuta wenzenu Kenya.

Ungekuwa ujatumwa tungekuelewa,ila sahauni huyo basha wenu anayelazimisha ndoa za jinsia moja kuingia ikulu
 
Wewe inaelekea historia ktk akili yako.Nyerere hakumkataza Lowassa asiwe Rais wa TZ.jikumbushe vizuri.alihoji pesa aliokuwa nayo.na kumbuka wagombea walikuwa wengi hivo ilibidi apatikane mmoja na sio lazima Lowassa kipindi kile.mbona hata kikwete aliambiwa asubilie?kwani alitengua kauli yake kabla ya kufa?Lowassa huu ndio muda wake wa kuwa rais wa nchi hii kuanzia 2015.suala la utajiri sio ishu kwa vile hata hao maskini viongozi hawajasaidia lolote zaidi ya kujitajirisha wakiingia madarakani.na pia ufisadi wa lowassa anaotuhumiwa juu ya richmond kumbuka maamuzi hayo asingeweza kuyapitisha peke yake bila boss wake kujua.Ebu mwacheni lowassa awe rais na lazima awe.

Labda rais wa Monduli maana sikuhizi hata manzese kuna rais (MADEE)
 
[h=3]Yericko Nyerere: Kwa nini Nyerere ali-veto kumkataa Lowasa?[/h]

Kwa nini Hayati Baba wa Taifa alitumia kura yake ya veto kumkataa Lowasa kwa sababu iliyoitwa na inayoaminika mpaka sasa kuwa “Lowassa ana utajiri mkubwa usio na ufafanuzi alioupata kwa mda mfupi tu akiwa mkurugenzi wa AICC?”

Ikumbukwe ni kuwa hoja hiyo ya Mwalimu Nyerere ilikuja baada ya Lowassa na wapambe wake kukodi ndege binafsi kutoka Arusha kwenda Dodoma kuhudhuria vikao vya uteuzi wa urais mwaka 1995, kitendo
hiki kilimfedhehesha sana Mwalimu na wazalendo wengine na hata kufikia kuliondoa jina la fisadi huyu nguli wa Tanzania,

Je leo utajiri wa Lowassa umekuwa halali?

Mamlaka ya mapato Tanzania inaweza kututhibitishia uhalali wa kodi alipayo mtu huyu?

Tangu afukuzwe uwaziri mkuu mwaka 2007 taarifa za kuaminika kutoka vyanzo muhimu nikuwa Lowassa alitenga Tsh12 bilioni kwa ajili ya kujitakasa, ambapo mpaka leo hii ameshatumia Tsh8 bilioni, je pesa hii ameipata wapi? Imelipiwa kodi kiasi gani? Atairudishaje akiwa rais?

Ili kuhuisha mjadala huu hebu niwaeleze jambo muhimu dhidi ya mtu huyu aitwae Edward Ngoyai Lowasa,

Labda niwaelekeze watafiti watafute faili la EL la enzi za TANU pale Lumumba. Mzee Paul Sozigwa suala hili analifahamu fika.

Ndiyo, Mwl. Nyerere alichukizwa na tabia ya Lowasa ya kujitajirisha kwa kuiba mali ya umma. Lowasa, licha ya tuhuma za wizi enzi akiwa AICC, kujimilikiaha majumba ya Masajili wa Majumba wakati akiwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mijini, Mwl. Nyerere alikuwa akifahamu wizi wa Lowasa tangu enzi za TANU. Kati ya mwaka 1974 na 1977 Lowasa aliiba pesa za TANU alizopewa kusamia ujenzi wa ofisi ya TANU Arusha.

Badala ya kujenga ofisi ya TANU Lowasa alinunua kiwanja na kujenga nyumba yake binafsi. Jambo hilo lilipogundulika mwaka 1982, lilimkasirisha sana Mwl hivyo kuamuru afukuzwe kwenye chama. Ni marehemu Edward Moringe Sokoine ndiye alimwombea msamaha kwa Mwl. Nyerere abadilishiwe adhabu.

Edward Lowasa alipewa adhabu mbadala; kuhudhuria kazini Ofisi Ndogo ya Chama Mtaa wa Lumumba kila siku bila kukosa, kuwa kazini masaa 8 bila kutoka lakini bila kupangiwa kazi yoyote hadi Chama kingeona ametubu na hatimaye apangiwe kazi nuingine. Lowasa alitumikia adhabu yake hadi Sokoine alipofariki.

Hiyo ndio sababu kuu ya Mwl. Nyerere kumkatalia Lowasa kugombea urais.

Kikwete, Mkuchika, Twaha Khalifan, Kinana, Bagenda na Msekwa wanajua ukweli wote kuhusiana na jambo hili. Ila maadamu kwa sasa hakuna tena maadili ya uongozi wa kisiasa nchini Tanzania, Lowassa anaweza kuachiwa awatawale wezi, wala rushwa na mediocre wa nchi hii.

“Kuna watu wasipokuelewa maneno na matendo yako, mshukuru Jah, wewe bado unafikra chanya, wakianza kukuelewa jichunguze ni wapi umeanguka maana umeanza kuwaza kama wao.”

Published on2/07/2014 02:55:00 AM
 
Is it fair to say Mwalimu was right about Lowassa being power hungry and corrupt?

Nauliza hivi ni kiongozi yupi wa mtandao ndani ya CCM ni msafi? hukiacha wakina mwakyeme amboa hawana mtandao ndani ccm? mtaje kwa jina labda hata faa kuwa rais
 
Mkubali ww aanze kwa kuilea familia yako kwanza. Akifanya vizuri utushuhudie ili tumpe nchi yetu aiongoze
 
Lowasa ametumia mali yaan fedha yake nyingi sana kujisaisha ili aonekane mwema. Nawe kwa ujinga wako umemkubali. Kama vipi mchangie ww hela ili aache kutaka kuingia ikulu ku-replace hela yake aliyoitumia.kweli mtu na akili zako timamu unathubutu kumtetea lowassa? Kakupa ngapi na ww kama sio buku saba. Shame on you guys
 
Lowassa ni fisadi tena ni ndumilakuwili kwan anakula na kupuliza. Kwa mung kidogo na kwa shetani kidogo.analaani vitendo vya kikatili huku anavifanya. Huyu ni mtu mbaya sana na hawezi kuongoza dola. Watanzania tusidanganyike kumpa dola huyu atatumaliza
 
kwan nyerere ni nan? Akimkataa m2 inakuwa ndio msimamo wa kumjudge m2. Acheni fikra za kizamani, lowassa ndio anastahili kupewa nchi hii , mpeni mchawi amlee mtoto km ajamkuza,huu msemo tafakari. Acheni upinzani wa kihehere, ccm hakuna anaweza kuwa rais wa ukwel km e l over
si unaona olivyo na upeo mdogo wa kufikiri? Unathubutu kuhoji kuwa nyerere alikuwa nani? Kama hjui uliza wakubwa zako au hata mwanafunzi wa primary atakusaidia ili ujue cha kuchangia. Taizo unadandia gari kwa mbele ndugu utagongwa, ooh
 
Tanzania bila ccm inawezekana jamani. Tubadilike nduguzanguni
 
nyerere ni kiongozi mwenye maono mapana na ndio maana kauli zinajadilika, lowasa hawezi kua rais coz ameonwa mapungufu yake, nyerere alimkataa jakaya mapungufu yakeunayaona, watu walitizama sura na nyerere aliliona akasema kama mzuri pelekeni posa, mbona hamsemi, tungepeleka posa asinge kua rais!
tujifunze kutokana na makosa. Tukumbuke kuwa mwl alimkataa kikwete sisi tukampitisha, leo hii yako wapi. Tusirudie kosa
 
Kile kizazi cha wazalendo wa Africa akina Nyerere kimeshapita. Kizazi kilichopo sasa ni cha wachumia tumbo, tutake tusitake. Sikubaliani na ufisadi unaofanywa na mtu yeyote, lakini wakati mwingine afadhali ya zimwi unalolijua kuliko usilolijua. Kwa kizazi cha sasa sitarajii kupata kiongozi ambaye si fisadi, mwizi, au mnafiki. Jambo la msingi ni kuangalia utendaji wake. Tunaelekea kwenye kutengeneza katiba mpya, nadhani no fursa muhimu kuwa na vipengele vinavyombana rais aliyepo madarakani dhidi ya ufisadi, ugaidi, matumizi mabaya ya madaraka.
Ni mawazo yangu turn wadau.
 
Asiyefunzwa na mamaye----! Mpeni lowasa urais ndo mtanielewa namaanisha nn kwa hii methali ya wahenga
 
kile kizazi cha wazalendo wa africa akina nyerere kimeshapita. Kizazi kilichopo sasa ni cha wachumia tumbo, tutake tusitake. Sikubaliani na ufisadi unaofanywa na mtu yeyote, lakini wakati mwingine afadhali ya zimwi unalolijua kuliko usilolijua. Kwa kizazi cha sasa sitarajii kupata kiongozi ambaye si fisadi, mwizi, au mnafiki. Jambo la msingi ni kuangalia utendaji wake. Tunaelekea kwenye kutengeneza katiba mpya, nadhani no fursa muhimu kuwa na vipengele vinavyombana rais aliyepo madarakani dhidi ya ufisadi, ugaidi, matumizi mabaya ya madaraka.
Ni mawazo yangu turn wadau.
kwahiyo?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom