Aliyekuwa Mbunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Fred Lowassa, amesema kazi kubwa iliyo mbele kwa sasa ni kuhakikisha chama hicho kinapata kura za kutosha katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Lowassa ametoa kauli hiyo leo, Ijumaa Septemba 12, 2025, wakati akishiriki kampeni za CCM, akiahidi kuendelea kushirikiana na wanachama wengine kuwahamasisha wananchi kukipa kura chama hicho.
“Juzi nilikuwa nafuatilia ziara za Mama Samia, nikamsikia Dk Bashiru Ally akielezea hali ambayo Rais aliikuta nchini. Akiwa Katibu Mkuu Kiongozi serikalini na Katibu Mkuu wa CCM, alishuhudia changamoto zilizokuwepo wakati wa Covid-19, Mama Samia alipoingia madarakani, alibeba miradi yote iliyoanzishwa na hayati John Magufuli na akaikamilisha. Tunampongeza sana,” amesema Lowassa.
Ameongeza kuwa baada ya kumaliza miradi ya Magufuli, Rais Samia amefanikisha upatikanaji wa huduma muhimu nchini zikiwemo maji, umeme na miradi ya maendeleo katika wilaya mbalimbali