Kwanini ninagombea Ubunge wa EAC - My Case!

Kwanini ninagombea Ubunge wa EAC - My Case!

Willy,

Mafanikio mema mkuu. Usikatishwe na kelele za haters wa hapa JF.

Muhimu ni conviction yako katika hiyo kazi unayoomba. Ninaamini ukifanikiwa utasaidia kuingiza mtazamo mpya na mawazo mapya huko EA.

Kikubwa tu mkuu ukifanikiwa usituangushe. Watanzania ni mabingwa sana wa maneno lakini vitendo sifuri. Jikite kwenye kutatua matatizo na bahati mbaya kwenye EA yapo mengi sana.

Nimepitia majina ya wagombea na una qualifications zote za kutuwakilisha vizuri kuliko wengi wa hao waliopitishwa maana uzoefu ni mwalimu mzuri kuliko elimu ya madarasa. Inahitaji uwezo kuingia huko kwenye mameli na mpaka ukafika sehemu na kufanya mambo yako bila kubebwa na mtu. Hiyo ndio shule ya maana na ya kweli na sio kuwa na uwezo mkubwa wa kukariri ili kufaulu mitihani.

Wengine tungependa kuona watu wengi ambao wamepikika hapa JF wanachukua nafasi za uongozi kwa faida ya nchi yetu.

Mafanikio mema mkuu,
Mtanzania aka Mwakalinga.

Mtanzania
Kweli sie watz ni ma haters, lakini hii isiwe kigezo cha kutuzuia kuuliza watu maswali magumu na mepesi, nafikiri wewe ni muumini mzuri unayeamini kwamba kila anayetaka uongozi inabidi awe anaulizwa kwanza aliwahi kufanya nini na anategemea kufanya nini, kama hawezi kujibu hayo kunasababu tena nyingine ya kuongoza?

Mfano, anaongelea common visa ati akiongelea local watakuwa na free movement. Hapo sijamwelewa vizuri.
Je leo ukipata VISA ya UK utaenda UJERUMANI jibu ni hapana
Je raia wa UK anaweza kwenda ujurumani jibu ni ndiyo, anaweza fanya biashara huko jibu ni ndiyo. Na je ukipata VISA/working permit ya UJERUMANI unaweza fanya kazi Poland? jibu ni hapana.

Kuna kitu humo ndani amekielezea naomba nikili sijakielewa labda kama ana mda aje atuelezee tena. Yani hiyo common visa inauhusiano gani na local movement? na pia hiyo common visa itasaidia je kukuza uchumi?

Kingine anaongelea kama umeingia EAC basi usiogope usonge mbele, aa wapi bwana lazima uangalie na interest za nchi, mbona DAUDI KAMERUN alikataa ku sign ile sheria ya EU ya akina Sarkosy na Angela?

Unaposaini kitu ama kukikubali lazima uone nchi itanufaika kivipi? mfano hiyo common visa itawanufaisha wakenya tu, kwa sababu wao wana ndege yao na ni cheap kutua nairobi kuliko kutua Dar. Pili Nairobi ni karibu kwenda serengeti/kilimanjaro kuliko kutoka Dar.
Sasa wabunge lazima tuwaulize watalinda vipi masilahi yetu.
 
Nimesoma post nyingi hapa na nilichobaini Willy anakuwa more attacked kwa sababu ya UCCM na wala sio WILLY as Willy. Jamani ebu tuache party affiliations na tujadili issues badala ya mtu. Willy kwangu mimi is a hero kwani kile kitendo cha kuthubutu kutia mguu katika jukwa la siasa (field) sio jambo jepesi. Willy ni mpambanaji pamoja na madhaifu yake ambayo to me ni madogo. Wengi tupo hapa lakini kusogelea jukwaa live ni pamoto, tutambue katika siasa hizi tunazocheza nazo tunapaswa kutambua no body is perfect (no an angel here despite God alitimua baadhi yao kwa mapungufu pia).

Tukiendelea kuhusudisha vyama hapa na kutumia kigezo cha kumkatisha tamaa mtu kwa sababu ni Magamba haya mambo yatatugharimu in future. Huyu ni Kijana mwenzetu na kiukweli ana moyo wa kupambana japo mwanzoni nilidhani anatania. Tumuunge mkono na kama ana madhaifu yake much better kumuelimisha na sio kumu-insult yeye na hasa familia yake.

Wengi wetu tumetangaza hapa kuwania baadhi ya majimbo kibao, tambueni huko si kwepesi hivyo kwani dhambi hizi tunazoziasisi hapa ndizo tutakazo kutana nazo jukwaani kisiasa. Hakuna atakaye kosa shutuma,skendo ama tusi jukwaani. Narudia tena ni vizuri hapa tujadili issues (ideas) na wala sio mtu (people) ama matukio (events).
Unafiki wa namna hii ndo umefanya hii nchi kubaki maskini. Kumsema mtu kuwa alifeli form four kuna uhusiano gani na chama. Kumuuliza kuhusu free movement of labor kuna vyama hapo? Yeye kaja hapa kujipima muache akabiliane na changamoto kamwe hatutambembeleza hapa kama unavyotushawishi.
 
My profile:
1. Born in Tukuyu.
2. Jamhuri Primary School, Mnazi Mmoja; DSM.
3. Kwiro Secondary School, Mahenge; Morogoro.
4. Kidatu Sugar Instituon, Kilombero; Morogoro.
5. DSM Marine Engineering School (DMTU), DSM.
6. Field Kagera Sugar Factory, Kyaka; Bukoba.
7. Field Mv. Bukoba, Mwanza; Mv. Mwongozo & Liemba; Kigoma.
8. JKT Oljoro/Makuyuni, Camps; Arusha.
9. CMB Marine Engineering Insistute; Antwerpen, Belgium.
10. Field CMB-Belgian Shipping Line ( as Assistant Engineer)
11. Worked Tanzania/Chinese Shipping Company; DSM/Hongkong.
12. Associate Degree in Criminology & Police Science; Westchester College in New York, USA.
13. BA in Political science, Lehman University at New York City, USA.
14. One year Internship at Dominican Republic Permanent Representative to the UN, General Assembly; New York; USA.
15. Worked at Sterycircle Inc, as Class A Haz Mat & Poison at Disposal Facilities. Dealing with (Transportation + Financial Covering the Incinerator)
16. Started CCM branch in New York City, USA.

- Now aspiring to represent our Nation, to the EAC Assembly.

William.

CV inatisha .
Nakutakia mafanikio mema
 
Mimi mpaka nipate majibu yangu ndio naondoka ama sivyo nitaendelea unless Jestina afanye naye interview ya pili ili aweke wazi hii misimamo yake

Kimya chako William kinanifanya nijiulize

wewe ukipata kweli tutakupata kwenye simu yako kweli?

Tunajua kama Dr Shayo ni Dr Feki sasa naomba sana uwe Kamanda wa ukweli njoo uweke wazi mambo au kubali yaishe ili tufunike kombe mwana haram apite

....................................................................................................................

Nimesikiliza interview yake aliyoifanya ambayo imepostiwa michuzi blog. Inaonekana huyu yuko out of touch na maendeleo ya dunia

Hoja zake kubwa ni hizi:

1. Anasema hakuna haraka ya kujiunga na Federation kwa sababu wananchi hawajaelemishwa...ni kweli kabisa lakini amesahau kuwa hili suala halikuanza kuangalia leo wala jana na si kazi ya nchi zingine kuwapa wa Tanzania elimy juu ya hii federation.

2. Amesema kuwa Tanzania itapata matatizo ya uchumi kama Greece ambayo imepata matatizo ya uchumi kwa sababu imeingia kwenye Euro. Lakini ukweli ni kuwa si kweli matatizo ya Greece ya uchumi ya Greece hayakutokana na kujiunga na Euro bali matatizo ya Greece yametokana na Greece (serikali) kutokuwa makini kwenye spending yao,cheap lending and failure to implement financial reforms ambayo essentially iliacha Greece kuwa badly exposed wakati global economic downturn ilipostruck. Hii haiuhusiani na Greece kujiunga na EU .

3. Amesema kuwa watanzania wengi walipo nje (diaspora) ni wepesi kukosoa serikali na utawala nyumbani kwa sababu ni CHADEMA...sijui kazitoa wapi hizi data lakini naaamini kuwa William amekuwa too simplistic na accusations zake. In short anataka kuwafanya waTanzania wajinga kiasi cha kuwa no one can think critically and independently na hatuna option zaidi ya CHADEMA.

4. William anasema kuwa angefurahi sana kama National Service ikarudishwa ili kurejesha uzaelndo kwa vijana lakini ukweli kasahau:

a) Kwa nini iliondolewa in the first place

b) Uzalendo hauwezi kupatikana kwa kulazimishana

c) Atapata wapi budget ya kuirudisha hiyo National service

d) Uzalendo haupatikani kama serikali haitazami wananchi wake

5. William amesema kuwa anaunga mkono kila kitu ambacho serikali ya sasa inakifanya. Hii inatisha sana kwa mwana JF na mtu aliyesoma na kuishi nje ya nchi. Inamaana William ana unga mkono mpaka mabaya ambayo serikali imeyafanya. This is dangerous thinking, hata huyo Nyerere hakuunga mkono kila kitu ambacho serikali ilikuwa inafanya iweje huyu amekuja na kutoa endorsement ya 100% bila ya kuwa critical kwenye mabaya, akiingia inamaana William atakuwa na rubbestamp kila kitu huko serikalini? Is this the hope we can believe in? kweli?

6. Amesema kuwa Tanzania middle class wamekuwa wengi....well ukweli ni kuwa tanzania ina population ya almost 44 million na the so called middle class ni less than 8% sasa na ni wale wale ambao ni watoto wa kishua na extension zao. Namshauri williama atoke aende rufiji, Mkuranga Kisarawe na tendahimba kama atakuta middle class hata mmoja.

7. Anasema kuwa watu walipo nje wasikae nje na kulalamika. ukweli ni kuwa the entire system imekamwata na wale wale. Na nathubutu kumwambia atuletee list ya wana diaspora waliorudi na wakapewa nafasi ya kufanya mabadiliko kama alivyofanya kagame wa Rwanda's government ambaye serikali yake ilikuwa aggresive kwenye ku recruit highly educated members of the Diaspora....na waliporudi wakapewa nafasi ya kufanya mabadiliko na yanaoneka. Sasa william nitajie idara hata moja iliyopewa watu waliokuwa Diaspora na ambayo imepewa nafasi ya kufanya mabadiliko?

Je william anajua:

a) It takes 4months to register a business in Tanzania na it costs about 800 usd? wakati Rwanda it only takes 15 minutes and costs nothing!

b) Je anajua kuwa 70% ya Watanzania ni under 30 ambao wako detached na political elites ambao wako out of touch na maendeleo

c) Je William anajua kuwa hao vijana ambao wamezaliwa early 1990's ambao amewapatronise kwenye interview ndio hao hao leo wanapiga kura?

d) Je william anajua kuwa BRELA walinunua software ya bilioni 2 ambaoilitakiwa ifanye kufanya biashara Tanzania iwe ni rahisi lakini mpaka leo ile kitu imefeli, pesa zimetumika na so far imefanyiwa sabotage ili watu waendelea kula rushwa pale BRELA...cha ajabu waziri Nyalandu analijua hili, Waziri Mary Nagu analijua hili and no one cares.

8. William anasema kuwa viongozi wafungue FACEBOOK pages lakini haoni kama hiyo ni ndoto ya alinacha kwani commander in chief ofisi yake (Ikulu) haina website sasa why should someone like Mary Nagu au Nchimbi have a facebook page?

9. William anasema kuwa achievements zake kubwa ilikuwa ni kuandaa sherehe ya kumpokea Asha Migiro alipoteuliwa kuwa Dpeuty SG wa Ban Ki Moon, mimi binafsi sioni kama hiyo ni issue na sioni kama ni achievement ya maana.

10 Anasema kuwa alikuwa instrumental kuanzisha jumuiya ya Watanzania New York na kwa hili nampa pongezi.

In short sijapenda generalisations zake na kwa inter interview ya 1 hour nilitegemea kupata mawazo yaliyobobea na mapya toka kwa mwana JF na mwana diaspora ambaye anaenda kutuwasilisha.

William kama mawazo yako ni hayo then I give up!
 
Nimechelewa kidogo kuiona thread hii na huenda nikasema mambo ambayo yameshasemwa na wengi kwani nimeshindwa kufuatilia makurasa yote yaliyotangulia, nimekwenda kama 1 hadi 5 tu.

Mimi si mshabiki sana wa maelimu ya degree "although I have one" na huwa sipendi sana hii "trend" ya kuulizia uhalisia wa "degree" za mtu kabla ya kumfanyia tathmini. Napenda zaidi kuangalia ulichowahi ku-deliver kuliko wingi wa vyeti ulivyopata na mtiririko wake.

Wasi wasi wangu mkubwa kwa EAC ni kuwa inaonekana tunaenda kinyume na matukio halisi. Hali halisi ni kuwa kwa Africa "Mega countries are all failures". Yaani ni kuwa ukweli wa mambo unaonesha kuwa Africa Manchi makubwa kwa maeneo na uwingi wa watu ni Manchi yaliyoshindwa! Huo ndo uzoefu katika Afrika; Congo ilivyo ni karibu sawa na Somalia, Sudan Imegawanyika juzi juzi tu, Ethiopia iligawanyika miaka kadhaa iliyopita, Nigeria ni Matatizo Makubwa ya rushwa na leo Boko Haram, Algeria na mambo ya FIS: angalau siku hizi Algeria iko Kimya kidogo, Misri tunaona wote yanayoendelea kule (Twaweza sema ni democratic revolution) lakini Misri haijawai kuwa mfano wa kuigwa. Sasa tunapotaka kuungana katika EAC, kwa kisingizio kuwa ukubwa utatuongezea nguvu za kiuchumi kwa kufanya "collective bargaining"; hivi hapa Africa tunafuata mfano gani??

Ni kitu gani kinadhihirisha kuwa ukubwa wa nchi utatupa faida kiuchumi? Hivi mambo ya kijamii yanayoisumbua sana Afrika; Ukabila, Ukoo, Udini; tumeyaangalia kweli?

Ndugu yangu William naomba utusaidie kujibu baadhi ya maswali hayo. Elimu yako ya kiutendaji zaidi kuliko ki "bookish" zaidi naamini itakufanya uwe halisia zaidi na kuangalia mambo katika sura ya "ki-pragmatic" zaidi kuliko kishule shule!!
 
sasa mbona sioni kilichokusukuma kugombea??....

Ni kweli atueleze ataifanyia nini EAC akichaguliwa kuwa mbunge? Hatujaona any oustanding legacy aliyofanya nchini.
Mimi namshauri akagombee jimbo lililokuwa la Baba yake he can do something kuliko Lusinde asiyekuwa na hekima.
 
Mtanzania
Kweli sie watz ni ma haters, lakini hii isiwe kigezo cha kutuzuia kuuliza watu maswali magumu na mepesi, nafikiri wewe ni muumini mzuri unayeamini kwamba kila anayetaka uongozi inabidi awe anaulizwa kwanza aliwahi kufanya nini na anategemea kufanya nini, kama hawezi kujibu hayo kunasababu tena nyingine ya kuongoza?

Mfano, anaongelea common visa ati akiongelea local watakuwa na free movement. Hapo sijamwelewa vizuri.
Je leo ukipata VISA ya UK utaenda UJERUMANI jibu ni hapana
Je raia wa UK anaweza kwenda ujurumani jibu ni ndiyo, anaweza fanya biashara huko jibu ni ndiyo. Na je ukipata VISA/working permit ya UJERUMANI unaweza fanya kazi Poland? jibu ni hapana.

Kuna kitu humo ndani amekielezea naomba nikili sijakielewa labda kama ana mda aje atuelezee tena. Yani hiyo common visa inauhusiano gani na local movement? na pia hiyo common visa itasaidia je kukuza uchumi?

Kingine anaongelea kama umeingia EAC basi usiogope usonge mbele, aa wapi bwana lazima uangalie na interest za nchi, mbona DAUDI KAMERUN alikataa ku sign ile sheria ya EU ya akina Sarkosy na Angela?

Unaposaini kitu ama kukikubali lazima uone nchi itanufaika kivipi? mfano hiyo common visa itawanufaisha wakenya tu, kwa sababu wao wana ndege yao na ni cheap kutua nairobi kuliko kutua Dar. Pili Nairobi ni karibu kwenda serengeti/kilimanjaro kuliko kutoka Dar.
Sasa wabunge lazima tuwaulize watalinda vipi masilahi yetu.
Mkuu Mkama,
Mimi sina matatizo na mnaomwuliza William maswali, nina tatizo na hao wanaomtukana.

Pia tukumbuke William ni mmoja wapo tu. kama yeye atashinda hapa kujibu maswali wakati wenzake hawapo au hawaulizwi hitasaidia sana maana tutakuwa tunamkaanga William kwasababu tu tunamfahamu.

Kwa muda wote William amekuwa muwazi hapa na wengi tunajua msimamo wake miaka na miaka. Tumsaidie kwa maswali ya kumjenga na sio kumtegea au kumbomoa.
 
Heri yako kura nyingi mjengoni ni ya magamba na magamba mengi yamepitia mikononi mwa babako angekuwa mtoto wa mlalahoi asingefika hatua uliofikia kwenye mchujo wa magamba, pamoja na ubaharia wako.umetumia kodi ya wtz sasa unatafuta mahali pa kustaafia.
 
- My Bro we chose to join the EAC so now we need to work towards eliminating Fears, we need to work hard and find a way to balance our economic stand with other EAC members using the best asset in our disposal, I mean our land!

- How do you join the EAC and later claim that you want nothing to do with the EAC Viza, I am reading you right? I mean we need one Viza for EAC in order to Micro-economy, our people must free to move around so that with open policies on trade they can sell and buy products from point one to point B without interruptions, understand that sometimes the markets requires guarantee of movement of the people and security for their products and their lives.

- I do not believe in fear minded policies which you seem to preach and believe in!

William.

William,

..mimi sikubaliani na suala la kuruhusu watu waingie Tanzania bila passport.

..nasema hivyo kwasababu bado Tanzania haina national IDs wala ssn system.

..pia utalinda vipi ARDHI katika mazingira kama hayo ya kuruhusu Wanyarwanda,Wakenya,Waganda,na Warundi waingie Tanzania?

..pia tutalinda vipi soko letu la AJIRA ambapo unemployment ni kubwa mno?

..zaidi, with one visa to east africa kuna formula gani ya kugawana mapato.

..check this: Kenya has 9% of lake victoria, Uganda has 42%, and Tanzania has 49%. naomba unieleweshe faida tutakazozipata ktk matumizi ya rasilimali za lake victoria ikiwa tutafungua mipaka yake.

..pia Kenyatta Airport inapokea ndege nyingi kuliko KIA na Dar. Kenya imekuwa ikilaghai watalii kwamba vivutio vya Tanzania viko Kenya. Katika mazingira hayo kuna faida gani kuruhusu watalii toka Kenya waingie Tanzania bila malipo yoyote? Pia Tanzania sera yake ni kuwa na watalii wachache wakubwa, wakati Kenya ni mass tourism. Katika mazingira hayo how do we deal with Kenya wanapotu-pressure tufungue mpaka wa Golongoja[mbugani serengeti]??

..unadhani Tanzania itajikwamua namna gani toka kuwa wazalishaji wa malighafi ktk east africa, kwenda kuwa wazalishaji wakubwa wa bidhaa za viwandani?

NB:

..nakushauri uje kwenye International Forum ya JF huko ndiko mijadala ya East African Community imepamba moto.
 
Mkuu Mkama,
Mimi sina matatizo na mnaomwuliza William maswali, nina tatizo na hao wanaomtukana.

Pia tukumbuke William ni mmoja wapo tu. kama yeye atashinda hapa kujibu maswali wakati wenzake hawapo au hawaulizwi hitasaidia sana maana tutakuwa tunamkaanga William kwasababu tu tunamfahamu.

Kwa muda wote William amekuwa muwazi hapa na wengi tunajua msimamo wake miaka na miaka. Tumsaidie kwa maswali ya kumjenga na sio kumtegea au kumbomoa.

Mtanzania
Ni kweli unachokiongea, binafsi hatumtegei maana tunauliza kutokana na maelezo yake mwenyewe, hiyo ya kusema wanzake hawapo sioni kama ni kigezo zaidi maana ni yeye mwenyewe ndo ameianzisha. Angeaizisha mwingine kwa kumsema William wala ni singe mhoji na wala sitomhoji kitu ambacho hajakiongelea mwenyewe.

Siku hizi ktk usaili (interview) wa kazi hasa ma engineer huwa wanauliza uliyoandika kwenye cv yako na waliyoolozesha kwenye Job Description (JD) yao. Ukiona wamekuuliza nje ya JD na CV yako basi jua hapo jamaa anakutegeshea, unless labda ktk kujieleza ulienda huko.

Mie sitaki kumtegea wala kumubomoa na uliza tu, ni jinsi gani ama kuna uhusiano gani kati ya common visa na local movements ktk nchi hizi. Na hiyo common visa inauhusiano upi ktk uchumi wa nchi hasa Tanzania.

Na je haoni common viza ni mtego wa wakenya kuchukuwa watalii wote? Si kwa sababu kenya wana utalii mzuri hapana ni kwa sababu kenya wana KENYA AIWAYS, ni ndege nzuri kiungo kikubwa na inamilikiwa na wakenya yeye haoni kuna potentials za kuuwa utalii na si utalii tu hata airport zetu zote.

Kivipi uwanja wa jommo kinyata ni wao na ndege ni yao kwahiyo watacheza na bei ya ticket tu, basi kwisha kazi airport za bongo na utalii kwisha.
Sasa hivi nafikiri wanashindwa kufanya hivyo kwa sababu ya visa, maana tunaweza ku-compasate kwa kufanya viza juu na viongilio ktk sehemu za utalii juu, sasa mtalii anaona bora atue bongo. Vinginevyo wakiruhusu tu hiyo mie naona ndo bongo kwisha ktk utalii na hata airports.
 
William,

..mimi sikubaliani na suala la kuruhusu watu waingie Tanzania bila passport.

..nasema hivyo kwasababu bado Tanzania haina national IDs wala ssn system.

..pia utalinda vipi ARDHI katika mazingira kama hayo ya kuruhusu Wanyarwanda,Wakenya,Waganda,na Warundi waingie Tanzania?

..pia tutalinda vipi soko letu la AJIRA ambapo unemployment ni kubwa mno?

..zaidi, with one visa to east africa kuna formula gani ya kugawana mapato.

..check this: Kenya has 9% of lake victoria, Uganda has 42%, and Tanzania has 49%. naomba unieleweshe faida tutakazozipata ktk matumizi ya rasilimali za lake victoria ikiwa tutafungua mipaka yake.

..pia Kenyatta Airport inapokea ndege nyingi kuliko KIA na Dar. Kenya imekuwa ikilaghai watalii kwamba vivutio vya Tanzania viko Kenya. Katika mazingira hayo kuna faida gani kuruhusu watalii toka Kenya waingie Tanzania bila malipo yoyote? Pia Tanzania sera yake ni kuwa na watalii wachache wakubwa, wakati Kenya ni mass tourism. Katika mazingira hayo how do we deal with Kenya wanapotu-pressure tufungue mpaka wa Golongoja[mbugani serengeti]??

..unadhani Tanzania itajikwamua namna gani toka kuwa wazalishaji wa malighafi ktk east africa, kwenda kuwa wazalishaji wakubwa wa bidhaa za viwandani?

NB:

..nakushauri uje kwenye International Forum ya JF huko ndiko mijadala ya East African Community imepamba moto.

Yani viza itolewe kenya harafu mgawane mapato, mhh. Mtai juaje viza ngapi zimetolewa labda nielimishe hapo?
Wakenya wanapenda kucheza sana na saikoloji mie siamini sana hata news yao ya ku strike oil turkana, ni saikoloji game ili tuingie kingi.
 
Lugha gongana hapa.

Wewe Nyani Ngabu, hiyo lugha iko sawa, usije ukadhani ni kiingereza, hiyo ni lugha aliyokuwa anaongea Idi Amin, si kiingereza ila ina maneno mengi ya kiingereza.

I do support Mr Malecela's aspirations, but i will not be tricked into believing that he is going to do anything significant if he is elected. It has been a while since EALA came into being, so far it has been a money wasting organ. Very symbolic, toothless and is behaving like a lapdog.

Kama Bw Malecela una la kutaka kutusaidia watanzania, ungejaribu kugombea Mtera halafu uingie mjengoni. Kule ndio kuna kazi ya kuweza kutusaidia watanzania wenzako. EALA ni pesa tu na jina,wanayofanya yote ni yale yaliyoamuliwa na sekretariati na yaliyoamuliwa na mabaraza ya mawaziri ya nchi mbalimbali. Kwa hiyo hakuna utrakachotoa kichwani mwako na kusikilizwa. Lakini nakuunga mkono, na ukipata ubunge kule naomba ukusanye nguvu ya kuingia Dodoma katika siku zijazo, huko ndio kuna kazi.
 
Kunta Kinte wacha hizo! Kiingereza sio lugha yetu acha ulimbukeni na ushamba. Alichoandika kinaeleweka kabisa. Unajua nini ma-niga wa kuchovya huwa mnafikiri lugha ni elimu. Mbona wazungu wanapokosesea Kiswahili husemi lugha gongana, Wewe ni mtumwa wa hali ya chini sana unayejifanya umegeuka m-amerika mweusi Koma kabisa na elimu yako feki ya kwenye makaratasi.

Duh! Haya bana...mimi ni mtumwa wa hali ya chini ninayejifanya "m-amerika mweusi".
 
Mkuu Malecela, na wazalendo wengine. Tunatakiwa kuwa more realistic tunapozungumzia EAC. Ukiangalia kwa sasa unaona wazi kabisa kuwa Tanzania iko weak kwa Kenya, possibly weak kwa Rwanda. Kenya inajua wazi inataka nini katika EAC (specifically kutoka kwa Tanzania), lakini mpaka sasa Tanzania hatujaweza ku-think kama nchi na kujua tunataka nini kutoka kwa jumuiya ya Afrika Mashariki.

Malecela wewe unaishi NEw York. Tunaoishi hapa Tanzania tunajua ninin kinaendelea, jaribu kutemnbelea duka lolote mtera angalia bidhaa utaona asilimia 90 made in Kenya, vuka kenya angalia bidhaa madukani hakuna hata moja toka TZ, wajinga wengine wanajisifia kuwa tumeuza mahindi na raw materials nyingine na kuwa na favourable balance of trade against Kenya, bila kujua wakenya wanaprocess na kuja kutuuzia tena sisi wenyewe.
Angalia soko la ajira, angalia sasa wanavyotokwa mate na ardhi kule Arusha, angalia wanavyotumia mbuga zetu za utalii, wanaalika watalii kwao wanawakamua halafu watalii wanakuja Tanzania weupe.

Kenya itaka iwe centre ya EAC na TZ iwe periphery, kitu hiki kinaonekana wazi na wakenya wanajua kabisa kuwa lengo ni hilo na mwelekeo ndio huo. Ukiangalia unaona wazi kabisa kuwa Kenya ndio investor mkubwa kwa Tanzania, uliza Tanzania ime-invest nini Kenya, hakuna. Serikali yetu bado imelala, haijui inataka nini kwenye EAC,hata wabunge ndio basi.

Kama hujui kitu ni bora usijiingize kwenye kitu hicho, unakuwa safe kuliko unapojiingiza. The fear we have has grounds, the threat of EAC to the well being of Tanzania is real, sio hofu hewa. Sababu ya kuifanya EAC ya kwanza ivunjike bado ipo haijawa addressed, Tanzania bado imelala.

Tukiuliza ni nini tumefanya cha kiujiandaa kuwa equal partner na Kenya kwenye EAC tangu jumuiya irudishwe tena, jibu tutakalopata utasikia tumeandika karatasi hii, tumesema hili na line, lakini hakuna something tangible to show.
 
William J. Malecela,

  • I wish you had kept quiet, most of us might have given you some slack, the benefit of doubt.
  • It isn't what you know that gets you into trouble, it's what you know for sure that just ain't so.
  • As time goes by you are bound to be disappointed by the things you didn't do than by the ones you did.
  • It is always better to get your facts right first and then distort them as much as you please.
  • Lies travel real fast and will always come first in a race against truth and that is the naked truth!
  • I wish you had stuck to Kiswahili, the ridiculousness of My Case might not have shown so glaringly.
Kwa nini nagombea Ubunge wa EAC - My Case! Yes, your case indeed! Thank God...As Mark Twain would put it, "The trouble ain't that there is too many fools, but the lightning ain't distributed right!
 
Mtanzania
Ni kweli unachokiongea, binafsi hatumtegei maana tunauliza kutokana na maelezo yake mwenyewe, hiyo ya kusema wanzake hawapo sioni kama ni kigezo zaidi maana ni yeye mwenyewe ndo ameianzisha. Angeaizisha mwingine kwa kumsema William wala ni singe mhoji na wala sitomhoji kitu ambacho hajakiongelea mwenyewe.

Siku hizi ktk usaili (interview) wa kazi hasa ma engineer huwa wanauliza uliyoandika kwenye cv yako na waliyoolozesha kwenye Job Description (JD) yao. Ukiona wamekuuliza nje ya JD na CV yako basi jua hapo jamaa anakutegeshea, unless labda ktk kujieleza ulienda huko.

Mie sitaki kumtegea wala kumubomoa na uliza tu, ni jinsi gani ama kuna uhusiano gani kati ya common visa na local movements ktk nchi hizi. Na hiyo common visa inauhusiano upi ktk uchumi wa nchi hasa Tanzania.

Na je haoni common viza ni mtego wa wakenya kuchukuwa watalii wote? Si kwa sababu kenya wana utalii mzuri hapana ni kwa sababu kenya wana KENYA AIWAYS, ni ndege nzuri kiungo kikubwa na inamilikiwa na wakenya yeye haoni kuna potentials za kuuwa utalii na si utalii tu hata airport zetu zote.

Kivipi uwanja wa jommo kinyata ni wao na ndege ni yao kwahiyo watacheza na bei ya ticket tu, basi kwisha kazi airport za bongo na utalii kwisha.
Sasa hivi nafikiri wanashindwa kufanya hivyo kwa sababu ya visa, maana tunaweza ku-compasate kwa kufanya viza juu na viongilio ktk sehemu za utalii juu, sasa mtalii anaona bora atue bongo. Vinginevyo wakiruhusu tu hiyo mie naona ndo bongo kwisha ktk utalii na hata airports
.

Mkuu at least wewe unasema wazi kuwa unaifikiria Tanzania na maslahi yake. Tatizo ni kuwa watu wanasoma theories kwenye vitabu, lakini hawaangalii facts na realities on the ground. Umetoa mfano mzuri sana wa airpot. Tanzania tunayo moja tu, ndege hatuna (do not tell me boeing ya mwaka 1950 inaweza ku-compete ya ndege mpya za kenya)

Angalia wabunge wa Tanzania walioiwakilisha Tanzania. Kina Nangale, Sepetu, Marando, Kinana etc, then kina Kaborou na wengine, sijasikia hata mmoja akiongelea real issues, wanaongea ma-theories yaliyoandikwa vitabuni, lakini what is on the ground can not be seen. Kenya inafanya kazi kuua utalii Tanzania, kuua viwanda Tanzania, kuua employement opportunities za watanzania kwa kivuli cha EAC, hakuna anayestuka. Angalia idadi ya wakenya wanaofanya kazi Tanzania, nenda Kenya uangalie kuna watz wangapi. Lazima tujiandae kuwa equal partners na Kenya kwanza, tukifikia kuwa equal partners tunaweza kufikiri kuondoa visa.
 
Back
Top Bottom