Kwanini ninagombea Ubunge wa EAC - My Case!

Kwanini ninagombea Ubunge wa EAC - My Case!

Wasalaam Aleykum JF!

- Well, we have been running a brutal campaign aspiring to be elected to the EAC assembly, the highest Legislative body among the five Nation's members that includes Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, and Burundi. I believe the times requires now that I stand up and make my case to you the people of who I am and what are my intentions given the opportunity to represent our Nation, next week in Dodoma!

- I do not intend to fake my way through this, but just want to make my case very clear while representing the real me, William if you know what I mean!, SO HELP ME GOD!

MUNGU AIBARIKI TANZANIA NA AIBARIKIE JF KUMKOMA NYAN!

William.

Am afraid I see nothing related to policy,not even something far related to policy.It is as if you are running simply because it is a plum job,an opportunity to a fatty pay check.
 
Nimesikiliza interview yake aliyoifanya ambayo imepostiwa michuzi blog. Inaonekana huyu yuko out of touch na maendeleo ya dunia...na kinachonitisha zaidi William anaelekea kuwa kwenye kundi moja na yule Dr Feki aka Dr Shayo.

Kwa nini Baharia asijibu haya maswali once and for all ?

mimi nataka nihamie kwa Dr Feki lakini kuna hiki kiporo cha Wills

tafadhali fafanua haya kwa faida ya wote humu
..................................................................................





Hoja zake kubwa ni hizi:


1. Anasema hakuna haraka ya kujiunga na Federation kwa sababu wananchi hawajaelemishwa...ni kweli kabisa lakini amesahau kuwa hili suala halikuanza kuangalia leo wala jana na si kazi ya nchi zingine kuwapa wa Tanzania elimy juu ya hii federation.


2. Amesema kuwa Tanzania itapata matatizo ya uchumi kama Greece ambayo imepata matatizo ya uchumi kwa sababu imeingia kwenye Euro. Lakini ukweli ni kuwa si kweli matatizo ya Greece ya uchumi ya Greece hayakutokana na kujiunga na Euro bali matatizo ya Greece yametokana na Greece (serikali) kutokuwa makini kwenye spending yao,cheap lending and failure to implement financial reforms ambayo essentially iliacha Greece kuwa badly exposed wakati global economic downturn ilipostruck. Hii haiuhusiani na Greece kujiunga na EU .


3. Amesema kuwa watanzania wengi walipo nje (diaspora) ni wepesi kukosoa serikali na utawala nyumbani kwa sababu ni CHADEMA...sijui kazitoa wapi hizi data lakini naaamini kuwa William amekuwa too simplistic na accusations zake. In short anataka kuwafanya waTanzania wajinga kiasi cha kuwa no one can think critically and independently na hatuna option zaidi ya CHADEMA.


4. William anasema kuwa angefurahi sana kama National Service ikarudishwa ili kurejesha uzaelndo kwa vijana lakini ukweli kasahau:


a) Kwa nini iliondolewa in the first place


b) Uzalendo hauwezi kupatikana kwa kulazimishana


c) Atapata wapi budget ya kuirudisha hiyo National service


d) Uzalendo haupatikani kama serikali haitazami wananchi wake


5. William amesema kuwa anaunga mkono kila kitu ambacho serikali ya sasa inakifanya. Hii inatisha sana kwa mwana JF na mtu aliyesoma na kuishi nje ya nchi. Inamaana William ana unga mkono mpaka mabaya ambayo serikali imeyafanya. This is dangerous thinking, hata huyo Nyerere hakuunga mkono kila kitu ambacho serikali ilikuwa inafanya iweje huyu amekuja na kutoa endorsement ya 100% bila ya kuwa critical kwenye mabaya, akiingia inamaana William atakuwa na rubbestamp kila kitu huko serikalini? Is this the hope we can believe in? kweli?


6. Amesema kuwa Tanzania middle class wamekuwa wengi....well ukweli ni kuwa tanzania ina population ya almost 44 million na the so called middle class ni less than 8% sasa na ni wale wale ambao ni watoto wa kishua na extension zao. Namshauri williama atoke aende rufiji, Mkuranga Kisarawe na tendahimba kama atakuta middle class hata mmoja.


7. Anasema kuwa watu walipo nje wasikae nje na kulalamika. ukweli ni kuwa the entire system imekamwata na wale wale. Na nathubutu kumwambia atuletee list ya wana diaspora waliorudi na wakapewa nafasi ya kufanya mabadiliko kama alivyofanya kagame wa Rwanda's government ambaye serikali yake ilikuwa aggresive kwenye ku recruit highly educated members of the Diaspora....na waliporudi wakapewa nafasi ya kufanya mabadiliko na yanaoneka. Sasa william nitajie idara hata moja iliyopewa watu waliokuwa Diaspora na ambayo imepewa nafasi ya kufanya mabadiliko?


Je william anajua:


a) It takes 4months to register a business in Tanzania na it costs about 800 usd? wakati Rwanda it only takes 15 minutes and costs nothing!


b) Je anajua kuwa 70% ya Watanzania ni under 30 ambao wako detached na political elites ambao wako out of touch na maendeleo


c) Je William anajua kuwa hao vijana ambao wamezaliwa early 1990's ambao amewapatronise kwenye interview ndio hao hao leo wanapiga kura?


d) Je william anajua kuwa BRELA walinunua software ya bilioni 2 ambaoilitakiwa ifanye kufanya biashara Tanzania iwe ni rahisi lakini mpaka leo ile kitu imefeli, pesa zimetumika na so far imefanyiwa sabotage ili watu waendelea kula rushwa pale BRELA...cha ajabu waziri Nyalandu analijua hili, Waziri Mary Nagu analijua hili and no one cares.




8. William anasema kuwa viongozi wafungue FACEBOOK pages lakini haoni kama hiyo ni ndoto ya alinacha kwani commander in chief ofisi yake (Ikulu) haina website sasa why should someone like Mary Nagu au Nchimbi have a facebook page?




9. William anasema kuwa achievements zake kubwa ilikuwa ni kuandaa sherehe ya kumpokea Asha Migiro alipoteuliwa kuwa Dpeuty SG wa Ban Ki Moon, mimi binafsi sioni kama hiyo ni issue na sioni kama ni achievement ya maana.




10 Anasema kuwa alikuwa instrumental kuanzisha jumuiya ya Watanzania New York na kwa hili nampa pongezi.




In short sijapenda generalisations zake na kwa inter interview ya 1 hour nilitegemea kupata mawazo yaliyobobea na mapya toka kwa mwana JF na mwana diaspora ambaye anaenda kutuwasilisha.




William kama mawazo yako ni hayo then I give up!
 
Utakuwa unamuonea ukimponda kwa kuwa na kiingereza kibovu,laumu mfumo wetu wa elimu kwani sitashangaa hata wewe ukiandika au kuongea hio broken English,ndio mazao ya mfumo wetu mbovu.Wahadhiri wa mlimani tunawaona wanavyopata vigugumizi kwenye kuongea Kiingereza kwenye kipindi cha This week in Perspective...ni tatizo letu sote tuliopitia kwenye mfumo wa elimu ya Tanzania.

Kingereza cha Willy ni kibovu ukichek na muda alioish uzunguni kwa miaka kumi na zaidi.
 
.
Mkuu, naona wewe hujaelewa!

Hawi attacked kwa sababu ya UCCM wake!... hata kidogo! ... mbona kuna watu ndani ya CCM wanakubalika na Watanzania wengi? .. watu makini wenye uelewa, busara na wanaoweka maslahi ya nchi mbele!.

Sasa, hivi wewe unae-mtetea umesoma vizuri anachoandika, ume-read between lines akili yake?, yaani vitu kama IQ na vingine ... sasa huyu bwana IQ au ufahamu wake ni wa chini mno na hicho ndicho kinacho-watatiza watu wengi hapa na wala si UCCM wake!

Sasa mfano mtu anataka kugombania nafasi fulani alafu hajui anaamini nini juu ya hicho kitu, msimamo wake unayumbayumba, hajui madhara au faida ya msimamo atakao-utetea, Je - hajui watanzania wanataka nini kwenye EAC!, hana maono ya kwamba labda in 30 or 50 years from now anataka EAC iwe vipi!.

Sasa ndugu, mtu kama huyo wa nini? - si atatuletea matatizo tu huko mbele ya safari?! - na hata kama yupo kwenye chama chako au hata kama yupo kwenye chama kingine unamweleza tu kuwa atawazamisha Watanzania.

Mkuu, ingawa watu wengi hawaipendi CCM, lakini katika hili ni bora CCM ikatafuta watu wengine makini kwa ajili ya Taifa letu lakini siyo huyu bwana ambae hata hajitambui!

Huyu bwana bado ana u-toto utoto hivi kwenye kichwa chake na ufahamu wake au tuite IQ yeke bado, na hivi vitu si vya darasani, unaweza ukapata hata PhD lakini hivi vitu havijatoka kichwani - sasa huo ni UCCM?

Anaongelea mustakabali wa Tanzania yetu kwenye EAC kama yupo jukwaa la JF-CHIT-CHAT

Sasa ndugu yangu mtu wa dizaini hii .. wa nini?


.

Nilipo bold "ni mapema mno ku generalize kuwa watu wengi hawaipendi CCM huku unatambua ndio hao hao waliopeleka wawakilishi (wabunge) kupitia CCM kwa zaidi ya asilimia 80%" labda uje na agenda hii 2015 kwa sasa no justification.

Whether or not IQ tests are an accurate measure of the intelligence is open to debate. It is difficult to define exactly what constitutes intelligence, it may be the case that IQ scores represent a very specific type of intelligence.

Kwa ujumla IQ ya mtu haipimwi tu kwa elimu ya darasani ila ujengwa na vitu vingi ikiwemo uzoefu kwa kiasi kikubwa.Mtu anaweza kuwa na IQ ndogo katika jambo fulani lakini through experience ama practice akakuza kipaji chake to a certain level of IQ katika suala fulani ambalo mwazoni hakuwa competent sana.

Iwapo mtu huyu ameweza kujisimamia katika kazi zake za Ubaharia na akaperform for almost 20 years sio wa kupuuza hata kidogo. Wenye mashaka naye ingekuwa ni busara kujaribu kudodosa kule alipokuwa anafanyia kazi. Toka mwanzo no body aliyekuja na utetezi humu kuonyesha uwezo wa Willy ni mdogo huko alipokuwa akifanya kazi zaidi ya mwenyewe kuelezea ni jinsi gani aliweza kuisimamia kampuni yake na ika perform well (If we want more, here is the exactly point to start with).

Kuna watu wana IQ kubwa katika "ku analyze mambo" lakini unapokuja kwenye job performance ni balaa. Narudia kuwa huyu ni kijana mwenzetu,MwanaJF maadam ametuonyesha nia hapa tofauti na wenzake ambao sio Member hapa tuna wajibu wa kumjenga,kumuelimisha lakini si kumtukana. Na imani anaweza kuwa Mwanafunzi bora wa kupigiwa mfano hasa atakapoanza kuizoea kazi yake. Pengine ningekubaliana na wewe for the case of his EQ ambayo kimsingi pia ni rahisi kujengwa katika siasa.
 
Naungana na Kiranga 100% this dude ni zigo balaa;

a. Masifa kwa jambo haliwezi (e.g. English); siyo lazima kihivyo lakini anapoombwa aandike kwa kiswahili anaendelea kutoboa kwa english fake hapa

b. Sijaona nini hasa kinamkera kwenye EAC (as it is) au kipi hasa anataka taifa tukifanye kwa faida ya wananchi??

Jamani ccm hii ni hatari kwa Taifa nitaeleza mambo ambayo Taifa litakiwa kuangalia

a. Biashara; taifa hili limekuwa soko la bidhaa kwa mataifa mengine kuna haja ya kuangalia biashara na bidhaa zipi zina affect wananchi na uchumi wtu

b. Ajira na terminal benefits: Tanzania ndio nchi pekee katika jumuia hii yenye sheria nzuri za ajira na mafao kwa wafanyakazi wake; kuna wakenya na warundi wengi wanafanya kazi hapa wanapokea terminal benefit kutoka NSSF na PPF ambazo pia zinachangiwa na mfuko wa hazina..hilo swal ni very complicated hakuna anayeliangalia..

c. Ardhi na Makazi; hilo linajulikana nia za jamaa zetu

d. Fedha na uchumi

List can on, lakini kwa aina hii ya watu; na jinsi yale majadiliano yanavyofanyika ni aibu sana inatakiwa watu wenye kusoma madocuments makubwa kuwa tayari kuwauliza wataalamu etc..

Pia ukiangalia wafanyakazi wengi pale Aursha (technical experts) ni wakenya na ni wazelendo sana kupita wtanzania wachache waliopo; tuna kazi sana wakuu..sijui
 
As far as ubunge kupitia ccm is
concerned hizi kampeni zote ni
kupoteza muda kama hujaandaa
hela za kuhonga wabunge.
Hapo ukweli mtupu chama chenu bro.Willy ni tatizo.
 
Well!better utilizes nation language in order to show what you're going to do for your nation in EAC as MP's if you'll elected
 
- My Bro we chose to join the EAC so now we need to work towards eliminating Fears, we need to work hard and find a way to balance our economic stand with other EAC members using the best asset in our disposal, I mean our land!

- How do you join the EAC and later claim that you want nothing to do with the EAC Viza, I am reading you right? I mean we need one Viza for EAC in order to Micro-economy, our people must free to move around so that with open policies on trade they can sell and buy products from point one to point B without interruptions, understand that sometimes the markets requires guarantee of movement of the people and security for their products and their lives.

- I do not believe in fear minded policies which you seem to preach and believe in!

William.

Is that free movement for local people, has something to do with common visa?
 
Nilipo bold "ni mapema mno ku generalize kuwa watu wengi hawaipendi CCM huku unatambua ndio hao hao waliopeleka wawakilishi (wabunge) kupitia CCM kwa zaidi ya asilimia 80%" labda uje na agenda hii 2015 kwa sasa no justification.

Whether or not IQ tests are an accurate measure of the intelligence is open to debate. It is difficult to define exactly what constitutes intelligence, it may be the case that IQ scores represent a very specific type of intelligence.

Kwa ujumla IQ ya mtu haipimwi tu kwa elimu ya darasani ila ujengwa na vitu vingi ikiwemo uzoefu kwa kiasi kikubwa.Mtu anaweza kuwa na IQ ndogo katika jambo fulani lakini through experience ama practice akakuza kipaji chake to a certain level of IQ katika suala fulani ambalo mwazoni hakuwa competent sana.

Iwapo mtu huyu ameweza kujisimamia katika kazi zake za Ubaharia na akaperform for almost 20 years sio wa kupuuza hata kidogo. Wenye mashaka naye ingekuwa ni busara kujaribu kudodosa kule alipokuwa anafanyia kazi. Toka mwanzo no body aliyekuja na utetezi humu kuonyesha uwezo wa Willy ni mdogo huko alipokuwa akifanya kazi zaidi ya mwenyewe kuelezea ni jinsi gani aliweza kuisimamia kampuni yake na ika perform well (If we want more, here is the exactly point to start with).

Kuna watu wana IQ kubwa katika "ku analyze mambo" lakini unapokuja kwenye job performance ni balaa. Narudia kuwa huyu ni kijana mwenzetu,MwanaJF maadam ametuonyesha nia hapa tofauti na wenzake ambao sio Member hapa tuna wajibu wa kumjenga,kumuelimisha lakini si kumtukana. Na imani anaweza kuwa Mwanafunzi bora wa kupigiwa mfano hasa atakapoanza kuizoea kazi yake. Pengine ningekubaliana na wewe for the case of his EQ ambayo kimsingi pia ni rahisi kujengwa katika siasa.

Siwezi kuongelea hizo asilimia 80% coz wote tumeona na kusikia mengi kuhusiana na namna zinavyopatikana, so zinaweza kuelezea zaidi watu waliopiga kura kuliko waliopigiwa kura!!
Hivi mkuu unaelewa maana ya IQ au unajaribu kuzungusha lugha tu hapo?! Eti IQ inaongezwa na experience!!?
Tuone aibu wakati mwingine jamani!!
 
Mussa Wangota,
Umejitahidi sana kumnadi William Malecela lakini ukweli unabaki pale pale kuwa hachaguliki! Unasema kwako wewe Willy is a hero na kwamba ni mpambanaji mzuri pamoja na madhaifu yake. Kwanza ulipaswa udemonstrate upambanaji wake hapa nchini maana sisi tunajua sehemu kubwa ya maisha yake hasa ya ujana kaishi ughaibuni miaka tele.

Tunachokumbuka ni kuwa baada ya kupata Division IV alikimbia nchi. Swala la kwamba Willy kwako ni hero siyo hoja kwetu maana kuna mtu mwingine anaweza nae akaja hapa akatuambia kwamba Wassira nae ni hero kwake kwa hiyo tumsapoti tumpe Urais. Is that make sense?

Unadai pia wengi wetu tumetangaza hapa kuwania baadhi ya majimbo kibao na kwamba dhambi hizi tunazoziasisi hapa ndizo tutakazokutana nazo kwenye majukwaa ya kisiasa. Na kwamba Hakuna atakaye kosa shutuma, skendo ama tusi jukwaani. Mimi naomba nikuulize hivi Nassari alikuwa na skendo wakati anaomba kura Arumeru? Pia unadai ni vizuri tujadili issues (ideas) na wala sio mtu (people) ama matukio (events) lakini unasahau kwamba hiso issue zinabebwe na ubongo wa mtu ambae nusura afeli Form IV, tutegemee nini katika mang'amuzi ya mambo mazito ndani ya Bunge la EAC?

Mkuu Tumbiri

Kuzungumzia suala la Nassari kama Nassari hapa hasa kwenye personal character nitakuwa namkosea kwani siko deep to that extent perhaps you. Kwa kauli yako inamaana hata wale unaowaamini na kuwashabikia katika siasa (wabunge) hawana maana kwako kwani pia IV walizonazo hazitamaniki kabisa.

Nadhani ni busara kuamini katika ku-deliver (out put to the end of the pipe) badala ya porojo za jukwaani. Binafsi Nassari as a Case Study to you has nothing yet kwani ndio kwanza kapata fursa ya kutuwakilisha so ni mapema mno kuanza kumtathmini (let us give him time). Tumekuwa na tabia ambayo sehemu kubwa ya mijadala yetu ina concentrate kwenye maisha binafsi ya Mtu na sehemu ndogo sana katika issues (ideas). Mfano dhahiri ni katika thread hii ya Willy ambayo personal character imecover sehemu kubwa kuliko agenda yenyewe.

Tumbiri kuna mazingira mengi yanayosababisha mtu kutofanya vizuri katika masomo na pia si wote wenye Division I,II na III ni wazuri kihivyo. Kuna watu leo ni Wasomi wazuri japo wanarecord za IV tena wengine ni Maprofesa. Tazama Division IV ilikuwa ni uwalimu lakini leo walimu wamejiendeleza na kuwa wasomi wakubwa hadi kutoka kufundisha shule za misingi hadi vyuoni na ndio waliotupatia sisi I,II na III tunazolingia leo mitaani.

I hope tumeelewana katika hili Mkuu.
 
William I think u need 2 explain why u want 2 be one of those mps. U haven't said wat u gonna do 4 da benefit of TZ, da EAC in general n da world as a whole. Weka majini Kama ambavyo imeombwa. Otherwise all da best.
 
Siwezi kuongelea hizo asilimia 80% coz wote tumeona na kusikia mengi kuhusiana na namna zinavyopatikana, so zinaweza kuelezea zaidi watu waliopiga kura kuliko waliopigiwa kura!!
Hivi mkuu unaelewa maana ya IQ au unajaribu kuzungusha lugha tu hapo?! Eti IQ inaongezwa na experience!!?
Tuone aibu wakati mwingine jamani!!

Mkuu

Soma vizuri post yangu badala ya kudhani IQ ni ya kuzaliwa tu! (Whether or not IQ tests are an accurate measure of the intelligence is open to debate. It is difficult to define exactly what constitutes intelligence, it may be the case that IQ scores represent a very specific type of intelligence).Tuepuke kumeza kila kitu ila tujaribu kushirikisha vichwa vyetu Mkuu. Kama hujanielewa hapa nitajitahidi kukufafanulia ninacho maanisha.
 
your CV is impressive, however we are more interested to hear what are you going to do for TZ if elected.
 
Mmmm kaka from marine engineering to BA in political science? Na hapo kati nimeona kuna Criminology tena, eh huko kote hukufanikiwa kutoka? What are you going to go during your term?
 
bwana william wewe umeishi marekan 4 twenty years leo unakuja kwa watanzania kuwaambia u want 2 represent them 2 EA assembly utajuaje matatizo ya tz?
 
Back
Top Bottom