Mlalahoi
JF-Expert Member
- Aug 31, 2006
- 2,182
- 883
Nakubaliana na sifa zote anazomwagiwa Mzee Malecela, ambazo ni haki yake. Amehimili mengi.
Swali langu ni hivi Je Malecela atakumbukwa vipi kwa mwananchi wa kawaida mtaani,mwananchi ambaye hatosumbuka au kujali kama Maalim Seif ndie mrithi wa Makamba (hypothetically), mwananchi ambaye mazao yake yanaoza shambani kwa vile chama cha ushirika/wizara havina msaada kwake, mwananchi ambaye anaji-feel kulia anaposikia "takwimu juu ya takwimu" kuwa uchumi umepanda ilhali maisha yake yanazidi kuwa magumu,mwananchi ambaye anatamani kumtoa mtu meno anaposikia eti "maisha bora hayapatikani kwa kukaa vijiweni" ilhali yeye anadamkia shambani alfajiri na kurejea jioni akiwa hoi huku amepinda mgongo,mwananchi ambae ANAFAHAMU KUWA KUNA WATU WANATAFUNA NCHI YETU LAKINI HANA UWEZO WA KUFANYA CHOCHOTE KWA VILE YEYE SIO KIONGOZI...?(Swali la ziada hapo, je Malecela kama kiongozi anayeheshimika ndani na nje ya CCM alikuwa na mchango gani katika mapambano dhid ya wala rushwa, mafisadi, wabadhirifu, majambazi na wale wote wanaofanya mambo yanayoweza kulipeleka taifa pabaya?)
Swali jingine:
Je, Malecela kwa kutotamka mapema kuwa hana nia ya kuendelea na wadhifa wa makamu wa CCM, haiwezi kujenga picha miongoni mwa wananchi kwamba amebwagwa, and therefore tarnish his image as one of the most influencial leaders CCM has ever had?Nafahamu kuwa ALISHAAMUA KUJIUZULU lakini sikuona mantiki ya kukaa kimya ilopelekea kuwepo speculations za nani atamrithi. Sintiohangaa akijazushiwa kwamba ALILAZIMISHWA KUJIUZULU (which is completely untrue, lakini sometimes uzushi unaweza kuaminika iwapo mazingira yanaupendelea).
Mwisho,nadhani ingekuwa jambo la busara kama Malecela angefanya moja ya haya mawili:
a)Kuandika kitabu cha historia ya maisha yake,na kwa kutumia kitabu hicho pamoja na mambo mengine akafafanua mambo kadhaa ambayo yamekuwa yakisemwa dhidi yake.
b)Kuna hii kauli ya "wananchi can go to hell" ambayo no matter how one might try to downplay it,inaendelea kujichomoza kila wakati unapozungumizwa wasifu wa Malecela. Pengine ingekuwa vema akafafanua alikuwa anamaanisha nini (who knows, pengine alikuwa misquoted au misinterpreted) au kama alisema kwa jazba tu za kisiasa basi itakuwa uungwana kuwaomba radhi hao walioguswa na matamshi hayo.