Nungunungu
JF-Expert Member
- Feb 13, 2007
- 311
- 13
Ukiacha la kuwadhibiti wapinzani katika chaguzi ndogo za majimbo, sijauona ubaya wa Mzee JM kama kiongozi kwenye chama na serikali.
Masatu pale Gymkhana ilipojengwa Sheraton unaweza kutuambia kiwanja kile kilikuwa cha nani?
Ukiacha la kuwadhibiti wapinzani katika chaguzi ndogo za majimbo, sijauona ubaya wa Mzee JM kama kiongozi kwenye chama na serikali.
Kama kweli huna kashfa nzito ni vyema, lakini nilipouliza nilisema tuwe na kiongozi wa kulinganisha naye, tunaweza kusema mfano waliokuwa mawaziri wakuu waliopita na makamu wa CCM maana ndio alipofika. Tumekuwa na mawaziri wakuu hawa kama sikosei Sokoine (RIP), Kawawa, Msuya, Warioba, Sumaye, Salim A Salim na Kambarage (RIP) sijui pengine nimesahau unaweza kuongeza. Makamu wa vyama naona walio CCM watawafahamu zaidi .............tumlinganishe na hao kwenye kuchapa kazi na tumuhukumu kwa makosa ambayo ni ya kwake.
Kuhusu mchango wake ni mkubwa kwani kuna nchi hapa duniani wanamkumbuka kwa mengi mema aliyofanya, mimi binafsi namkumbuka alipokuwa waziri wa mambo ya nje na mambo yake alivyokuwa anafanya. Vile vile alipokuwa balozi wa Tanzania UK. Katika uongozi wake hajahusishwa na kulihujumu taifa kiuchumi, ufisadi na mambo ya rushwa sijasikia lakini kama kuna member anayo atuwekee hapa.
Ili iweje?
Masatu said:Moja ya kashfa za Malecela ni tuhuma kuhusu kiwanja cha Gymkhana ilipojengwa Sheraton ( Sasa Movenpick ) inasemekana mkuu pale kavuta na ujenzi wa Hotel katika "green" plot ile uligubikwa na mashinikizo yake.
Wataalam wa wizara ya ardhi na wa mazingira na asasi nyingine walipinga sana uvamizi ule
Tunataka kujua ukweli wa maneno yako haya hapa:
...huyu jamaa nilimwona mwendawazimu na nikagundua kwa nini Nyerere alikuwa hampendi ni pale alipo suggest vinchi vidogo dogo kama Rwanda na Burundi ni visumbufu sana why not take them na kuweka serikali ambayo tunaweza kuiweka sawa,huyu jamaa kina Kagame hawataki kumsikia kabisa na angekuwa raisi ungeona uhusiano na hizo nchi ungekuwa kama sumu
This was the best proposal for the Rwanda and Burundi crises. Hao waliogopa kupoteza vi-urais vyao. Waliona na hata leo wanaona vi-urais vyao kuwa ni muhimu zaidi kuliko ustawi wa watu wao.
Soma post yangu ya awali na kisumbue kichwa chako kidogo kusoma kwa makini utakuta jibu la swali lako... acha uvivu
This was the best proposal for the Rwanda and Burundi crises. Hao waliogopa kupoteza vi-urais vyao. Waliona na hata leo wanaona vi-urais vyao kuwa ni muhimu zaidi kuliko ustawi wa watu wao.
Kwa hiyo mkuu tulipovamia Uganda kumtoa Amin, na kuweka serikali yetu tulikuwa wendawazimu, juzi US walipovamia,lakini suggesting kwenda kuvamia hizo nchi na kuweka chini yetu ili kupata serikali makini kwangu huo ni wendawazimu
Tanzania hatuwezi kushindwa kuwapiga hizo nchi kivita, the matter of fact katika dunia tunapewa nafasi ya juu sana kwa uhodari na ukali wa majeshi yetu, hakuna nchi yoyote hapa karibu inayoweza kutuchezea, kwa hiyo Mwalimu angekubali by now kwenye hizo nchi kusingekuwa na matatizo ambayo yanatugharimu hela nyingi sana za walipa kodi katika kugharamia wakimbizi wa kila siku wanaokuja nchini, ambayo ndio hasa ilikuwa argument ya Malecela, against Mwalimu kwamna serikali yetu mpaka leo inapoteza hela nyingi za maendeleo katika kugharamia wakimbizi.na i doubt kama tunaweza kuwapiga hao jamaa kijeshi kirahisi kama inavyoonekana hapa...vita ya kagera tuu mpaka leo effect zake hazijaisha ndio uanze na hao tena ambao hata hawajakuchokoza,Jokakuu historia ya wahutu na watuts ni very complex kwa mimi kuchukua any side ila you sound unajua sana hizo crisis za hii region ingawaje seems uko bias kidogo
Naona huna hoja hapa yalikuwa ni uzushi tu, tuendelee na yaliyo muhimu.
Malecela, alipotaka kupewa kazi ya usuluhishi wa hao watu alikataa kwa kusema wazi kwamba anawaunga mkono Wahutu, kwa hiyo hawezi kutoa haki kwa Watusi
Mkuu Koba,unategemea kagame akae kimya huku watu wakichinjwa kiasi kile na mambo ya congo kule kabila baada ya kusaidiwa kumtoa mobutu na makubaliano yalikuwa lazima azuie interahamwe wasirudie walichofanya maana walipiga camp congo lakini yeye akawageuka na kuwapa silaha interahamwe ...mkuu huoni hapo ni deal chafu