Hotuba ya Rais Samia yawabubujisha machozi Watanzania utafikiri wamefungiwa kwenye chumba chenye moshi wa kuni mbichi

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,301
9,727
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa hakika Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania Mh Mama Samia Suluhu Hasssan mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge ameteka hisia za watanzania na kuwabubujisha machozi utafikiri watu ambao wamefungiwa kwenye chumba chenye moshi mkali wa kuni mbichi. Ameongea na kutoa hotuba nzito na yenye hisia kali sana kwa Taifa letu.

Kwa uchungu mkubwa na hisia kali sana na upendo mkubwa sana kwa watanzania amewaasa na kuwataka viongozi wote hasa wakuu wa mikoa kwenda kwa wananchi kuwasikiliza kero zao na kuzipatia majibu.amewataka wafanye kazi kwa kujituma na bidii ya hali ya juu pamoja na kuwatendea watu haki. ameendelea kuzungumza kwa uchungu na hisia kali sana kama mama mlezi wa Taifa kuwataka viongozi na wote kuachana na masuala ya makundi katika kuwaongoza watu.

Akaendelea kuzungumza na kueleza kinaga ubaga na kwa ujasiri wa hali ya juu mithili ya wanajeshi wanaorudi kutoka vitani na ushindi mkononi wa kukomboa ardhi ya Taifa lao, kuwa yeye ni Rais wa wote na ndio maana amekuwa akiteua watu wote bila ubaguzi wa aina yoyote ile kwa misingi ya aina yoyote ile.na kusema kuwa yeye anachoangalia ni kazi na uchapa kazi wa mtu na siyo kingine.

Kwa hakika Mungu yupo ndani ya moyo wa Rais Samia na Anaendelea kufanya kazi katika Taifa letu kupitia Rais Samia. Ni nadra sana kupata kiongozi aina ya Rais samia.ni mama mkweli sana,ni mama mwenye upendo na uzalendo wa dhati kwa Taifa letu,ni mama mwenye uchungu na watanzania na maisha yao,ni mama anayetamani na kutaka kuona kila mtanzania anajisikia fahari kuzaliwa Tanzania,ni mama anayetaka kuona keki ya Taifa inafika katika meza ya kila mtanzania,ni mama mwenye hamu ya kutaka kuona watanzania wanatendewa haki pasipo kuonewa wala kunyonywa wala kudhulumiwa haki zao.

Ni mama anayetamani kuona mkono wake unamfikia kila mtu na kumpa msaada kila mwenye kuhitaji msaada,ni mama na mlezi mwenye kiu na hamu ya kutaka kuona wananchi wanaishi kwa furaha ,amani na upendo pasipo chuki wala kinyongo wala visasi katika mioyo yao. Rais samia ni mama mnyenyekevu na mwenye hofu ya Mungu.ni mama ambaye jina lake linaendelea kuchorwa na kurembwa kwa wino wa dhahabu kila uchwao katika mioyo ya watanzania,kutokana na kuweka alama na kugusa maisha ya kila mtanzania.

Ndio maana leo ukienda kwa watumishi wa umma au wakulima au vijana au wafanyabiashara au wajasiriamali au wakina mama n.k.wana mengi sana ambayo wanaendelea kumshukuru Rais Samia kwa kuwatendea mengi mema na mazuri sana ,mfano vijana wanaendelea kumkumbuka kwa kuwapa maelfu ya ajira,wengine wanamkumbuka na kufurahia namna walivyo pandishwa madaraja mserereko na kulipwa stahiki zao ,wengine kupewa mbolea za Ruzuku,wengine kufurahishwa na mazingira mazuri ya biashara na namna hali ilivyo nzuri ya kimahusiano baina ya wafanyabishara na TRA.

Hakuna mahali unapoweza ukaenda usikute alama na mikono ya mama yetu mpendwa Mama Samia.ni mpango wa Mungu Mwenyewe kumuinua mama huyu mkarimu na mwenye hofu ya mungu.ndio maana leo tunamuona akihubiri habari za haki, upendo,kupinga ubaguzi wa aina yoyote ile pamoja na kuhimiza umoja , mshikamano na upendo miongoni mwetu Watanzania.ndio maana tunamuona akisema kuwa yeye ni mama wa wote na mlezi wa Taifa letu. Mungu atupe nini tena Watanzania? Katupatia mfariji wa Taifa tunataka nini tena?

Tukilia anatufuta machozi na kutubembeleza wanae mpaka tunyamaze ,tukionewa anamkamata aliyetuonea na kumpa onyo kali,tukiwa kwenye shida anatupa faraja na matumaini na kutusaidia,tukiwa na mizigo anatutua na kubeba mwenyewe.tunalelewa vizuri mpaka watoto wa majirani wanatamani wangezaliwa kwenye nyumba yetu na familia yetu ya Tanzania.chakula tunapewa ,maji tunapewa na mavazi tunapewa na kianzio cha maisha nacho tunapewa kwa anayetaka kwenda kujitegemea .tunataka nini kwa mama yetu jamani? Embu tumuache mama yetu aendelee kufanya kazi bila kumbugudhi hovyo hovyo.

Tusikubali mtu yeyote atutukanie mama yetu huyu mpendwa.mtu akimtukana mama yetu tuone kuwa tumetukanwa wote na sote tunyanyuke kumkemea huyo mtu mpaka ajuwe namna tulivyo na upendo mkubwa kwa mama yetu huyu mzazi na mlezi wa Taifa letu.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
IMG-20240313-WA0002.jpg
 
Kwa hizi bange unazoandika hapa za 'kububujikwa' machozi sahau kuhusu teuzi, utaishia kama Suphian Juma kualikwa kwenye vikao vya umoja wa akina mama wa CCM 🤣

Alafu leo hii amewakana, hawatambui nyie chawa!
Kwani Lini nimewahi kusema mimi ni chawa.mimi kazi yangu ni kuzungumza ukweli tu
 
Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.View attachment 2933726
Hana makundi!🤣
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom