Wosia mzito wa William Malecela (Le Mutuz) kwa CCM, Wapinzani, Serikali na kwa JamiiForums uzingatiwe na kutekelezwa ili tuendelee kumuishi

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,567
Wanabodi,
Hii ni makala yangu kwenye Nipashe ya leo.
Screen Shot 2023-05-21 at 12.41.02 AM.png
Screen Shot 2023-05-21 at 12.41.28 AM.png

Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa, ambazo huwa na swali, likifuatiwa na hoja, kisha jibu utalitoa wewe mwenyewe.

Swali la mada hii ni Je

Wosia mzito wa William Malecela (Le Mutuz) kwa CCM, Wapinzani, Serikali na kwa JamiiForums uzingatiwe na kutekelezwa ili tuendelee kumuishi, au baada ya kufa,anakuwa ndio mwisho wake na kila kitu chake?.​

Wiki iliyopita kwenye safu hii niliandika Buriani ya Benard Membe, na Wiki hii ni Buriani nyingine, hii ni buriani ya mtu wa kawaida tuu ambaye sio kiongozi wa CCM, wala sio kiongozi wa serikali, ni mtu tuu wa kawaida aliyefahamika na wengi, hivyo maneno ya mtu wa wengi ni maneno ya wengi na sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, hii ni makala ya kuitaka CCM, serikali, wapinzani kuzingatia sana wosia wa mtu huyu!.

Huyu ni William Malecela, ambaye anajulikana sana kwa jina maarufu la Le Mutuz, kutokana na kuendesha ukurasa wake wa Le Mutuz Super Brand kwenye mitandao ya kijamii, hivyo kuna wengi wanaomfahamu zaidi William kutokana na umaarufu wake wa kwenye mitandao ya kijamii kama Le Mutuz, hivyo sifa zake kama William Malecela, kujikuta zimeishia Jamiiforums pekee. William Malecela alifariki ghafla wiki iyopita na kuzikwa kijijini kwao Mvumi Dodoma siku ya Jumatano iliyopita.

Wosia.
Wosia ni maneno ya mwisho ya marehemu anayoyaacha kuzungumzia jambo fulani, wosia huo unaweza kuwa wa maneno ya kuambiwa au kuandikwa. Wosia huu wa William Malecela kwa CCM serikali, ni wosia wa maneno ya kuzungumza, ambapo aliyasema bila kupanga, ni tulikutana tuu viwanja vya Saba Saba, nikamfanyia mahojiano impromptu, na kwavile sasa tuko kwenye dunia ya kimtandao, wosia huu nimeurekodi kwenye video na kuutupia kwenye mtandao wa YouTube, baada ya kupokea taarifa ya kifo chake, nilipoyasikiliza tena "Mahojioano William Malecela na Pasco Mayalla" ndio sasa nimegundua kumbe huu ni wosia anaihusia serikali, CCM, na wapinzani.

Poleni Sana Wafiwa Wakiongozwa na The Malecelas.
Kunapotokea msiba wowote, wafiwa wakuu wa kwanza ni familia yake, hivyo kwanza nitoe pole zangu kwa familia yake, mkewe na watoto wake, pole kwa familia ya Mzee John Samwel Malecela, pole kwa familia yake ya JF, pole kwa wanamitandao kumpoteza mwanamtandao mwenzao, pole kwa CCM kumpoteza mwanachama wake ambaye ni mmoja wa wana CCM Wazalendo na wakweli kabisa toka ndani ya nafsi zao, na pole kwa Watanzania wote kumpoteza Mtanzania mwenzetu, haijalishi alikuwa nani, thamani ya mtu ni utu, hivyo binadamu yoyote akitangulia pole ni stahiki.

Mimi ni mtu wa mastori mastori, hivyo sasa nakuja kwenye mastori story ya Pasco, kama wewe sio mtu wa mastori story, jump to conclusions.

Mastori ya Pasco, Mimi na Malecelas
Japo mimi ni Msukuma, ila nimezaliwa mjini. Wazazi wangu walikuwa waserekali hivyo siku zote tinaishi kwa kuhamia hama.
Mwaka 1976 tukiwa jijini Mwanza, nikisoma shule ya Nyakahoja, Baba Mzee Mayalla alipata matatizo ya kazini, tukalazimika kurushwa kijijini!. Mwaka uliofuata, Mzee alifuatwa kijijini na "wazee wa kazi", kilichofuata naomba nikiruke, ila mimi na dada yangu mkubwa Maria, tulifuatwa kijijini kwa kukosolewa na Baba yangu mdogo, Mzee Mathew Kasanga, tukaja kuishi nyumbani kwake, eneo la Drive In Flats. Hivyo mimi nimeingia jijini Dar es Salaam kwa kuja kwa ndege, hivyo mwenzenu mambo ya kukwaa pipa, tulianza zamani. Hapa jijini nimejiunga na Shule ya Msingi ya Oyster Bay darasa la 4. Hapo shuleni tumesoma watoto wa wakubwa wote wa enzi za Nyerere, kuanzia watoto waliokuwa waliishi Msasani kwa Nyerere, watoto wa Kawawa , Watoto wa Mzee Malecela na watoto wa mawaziri wote akiwemo mtoto wa Ali Hassan Mwinyi aitwae Husein. Mimi nilikuwa darasa moja na Mwendwa Malecela, dasanini tulikuwa na watoto wengine 8 wa mawaziri., huku ndugu yake Mwendwa aitwae Catherine (RIP) (nilimpenda) alikuwa darasa moja nyuma yetu, darasa la 3, Mdogo wake Mkwawi Ippy Malecela (RIP) akiwa madarasa mawili nyuma yetu darasa la 2 na dada mtu, Dr. Seche Malecela, alitutangulia madarasa mawili mbele alikuwa darasa la 6. Enzi za Nyerere, Malecela akiwa Waziri Mkuu na Makamo wa kwanza wa rais, tulikuwa tunakwenda kucheza kwao, walikuwa na mbuzi wengi. Enzi hizo watoto wa Malecela walikuwa wanakuja shule kwa kutembea kwa miguu!.

Nikiwa sekondari ya Tambaza, mtoto mkubwa wa Malecela, Senyagwa (RIP), alikuwa A level PCM, na nikiwa kidato cha tatu, Dr. Seche Malecela alikuja Tambaza kusoma PCB.

Mwendwa tukaja kukutana naye tena kwenye fani ya sheria, maana mimi japo ni mwandishi wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea, pia ni mhitimu wa shahada ya sheria toka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, UDSM na wakili wa kujitegemea.

Mmoja ya rafiki zangu akawa ana date na binti mwingine wa familia hii Dr. Irene, (RIP). Nikaja kuwa MC wa harusi ya binti wa Malecela, na kote huko sikuwahi kufahamiana na William.

Ni mpaka nilipokwenda jijini New York, nchini Marekani kwenye Ubalozi wetu UN pale New York, ndipo nikatambulishwa kwa shemeji yetu Mke wa Le Mutuz, ndipo nikamfahamu William. Tukaanza kukutana kutana zile pati za Watanzania, mimi pia na wife wangu tuliishi US. Kuna safari moja nilikuwa narejea Tanzania, tukasafiri ndege moja na wife wa Le Mutuz na wale watoto wake wawili.
Tukaja kukutana tena na William kwenye Mtandao maarufu kabisa wa kijamii nchini Tanzania, kuliko mitandao yote, mtandao wa Jamiiforums au kwa kifupi, JF.

William Malecela alipokuja kugombea ubunge wa Bunge la Africa Mashariki, EALA, akanitafuta, nikampa support. Kuna wakati nikiwa Dodoma akanikaribisha nyumbani kwa Mzee Malecela kisha tuka drive all the way from Dom to Dar ndipo nikamjua William kwa karibu zaidi na kwa ukweli zaidi.

Kukutana Kujuaana na Kuwa Marafiki na William Malecela Le Mutuz
Mimi na William tukawa marafiki, tukikutana viwanja tofauti tofauti vya burudani, na kama vilivyo vikombe kabatini kuna wakati tukapishana kauli, alikuwa ni mwepesi kukasirika, mtu mkweli akikasirika, hachelewi kukiwasha ila pia mwepesi kusamehe!. Kumbe William sio mlevi, hanywi pombe, wala havuti sigara, hili tunafanana, maana hata mimi sinywi pombe, wala sivuti sigara, ila kama William, tunapenda starehe na burudani hizi na zile!, tunaishi sasa kwa kuponda raha kwa starehe za kula, kunywa as if tutaishi milele, huku kila siku ukiufurahisha moyo wako as if utakufa kesho, hivyo kula raha leo, kula vizuri, lala pazuri, pata raha leo, kesho itajijua yenyewe!. Naomba kukiri wazi life style ya Le Mutuz, ndio was my life style, kula bata sana, kujirsha sana, kuendekeza starehe sana, na yale mambo yetu yale ndio usiseme!. Tunaamini Mungu alimuumba binadamu ili upate raha, kula vizuri, Vaa vizuri, ishi mahali pazuri, endesha gari zuri, oa mke mzuri, au date wa babes wazuri. Ishi kwa raha leo as if utakufa kesho, na wakati huo huo ukijipanga as if utaishi milele.
William Malecela, A Man With A Heart of Gold
Kuna watu wengi ni watu wenye roho mbaya, akiona kuna mchongo fulani, hakupi connection, William alikuwa ni mtu mwenye roho nzuri. Ni William Malecela, Le Mutuz ndie aliyenitambulisha mimi kwenye mtandao wa YouTube channel, na video yangu ya kwanza kwenye YouTube ni video ya mahojioano na William Malecela ambayo video hii ndio usia ambao William Malecela ametuachia milele, nataka wana CCM wote haswa viongozi, watu wa serikali na sisi wana jf, tusikilize kwa makini wosia huu na ikiwezeka tuuishi.

William Malecela Kada Mtiifu na Mkweli Daima wa CCM, at Heat!, He Was Born and Breed CCM!, Amekufa CCM!
Chama cha Mapinduzi CCM, kina taratibu zake za ukosoaji kufanywa na wanachama wake, kinataka ukosoaji wowote wa CCM, ukifanywa na mwana CCM, ukosoaji huo ufanyike kwenye vikao vya ndani. William alikuwa hakopeshi!.

William Malecela Aliipenda CCM na Kuitetea CCM, Lakini Hakuwa Chawa!
Siku hizi kupitia mitandao ya kijamii, kumeibuka vikundi vya kusifia wakiijiita machawa. William Malecela ni mwana CCM, aliyeipenda CCM kwa dhati ya moyo wake na kiitetea CCM kwa nguvu zake zote ila hakuwa chawa kwasababu pia aliikosoa CCM, wazi wazi na sio kupitia vikao vya ndani.

Ni katika mahojiano haya William Malecela alitoa usia mzito kwa Chama chake CCM, na serikali yake, kwa wapinzani na kwa wana JF. Je William Malecela alitoa wosia gani kwa serikali, CCM, wapinzani na kwa Jf?.

Kwa wenye uwezo to listen in between the words, karibu hapa

Kwa wasio na uwezo to read in between the lines and to listen in between the words, juma lijalo nitawamegea wosia huu tits and bits nitawatafunia, nyie kazi yenu itabakia ni kumeza tuu!.

Wasalaam
Paskali
 
Le Mutuz.. Le Mobimba... Le Akili Kubwaz... Boma Yee... Boma Liwanza.. Mwili Nyumba, Shati unafunika Vitz... U know?

Ila Mkuu Mayalla tukitoa ushabiki wako kwa Magufuli, maandiko mengine yote hua unayatendea haki sana.
Shida yako wewe mgibeoni,ni chuki kwa jpm,labda kwa sababu una ka asili ka wiziwzi na kutokuwa msafi!?,huwa sioni ni kwa nini unamchukia jpm,na pasco hawez kuandika ili kukufurahisha wewe,anatakiwa auandike ukweli kama ulivyo.sasa watu wapuuzi kama wewe unapomtaka pastor eti aache ushabiki kwa jpm!, unaonyesha wazi wewe hujui lolote kuhusu pasco,pastor hajawahi kuwa mshabiki wa magufuli hata siku moja.
 
Watu wengi wamemjua William Malecela baada ya mitandao kupata umaarufu ila wanaomjua kabla ya mitandao wanaweza kumwelezea vizuri.
Kawaida rais akienda nje ya nchi huwa anazungumza na watanzania walioko huko na pia watanzania walioko huko wanapata nafasi ya kumwuliza maswali. William Malecela alikuwa anapenda kuuliza maswali magumu kama vile baba yake hakuwa kiongozi. Moja ya maswali yanayokumbukwa no lile alilomuuliza rais wa awamu ya tatu kwanini viongozi wanaochaguliwa ni walewale maana Toka azaliwe amekuwa akisikoa majina ya viongozi yaleyale.
Mungu amlaze mahali pema peponi
 
Kweli..
 
Wanabodi,
Hii ni makala yangu kwenye Nipashe ya leo.
View attachment 2629490View attachment 2629492
Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa, ambazo huwa na swali, likifuatiwa na hoja, kisha jibu utalitoa wewe mwenyewe.

Swali la mada hii ni Je

Wosia mzito wa William Malecela (Le Mutuz) kwa CCM, Wapinzani, Serikali na kwa JamiiForums uzingatiwe na kutekelezwa ili tuendelee kumuishi, au baada ya kufa,anakuwa ndio mwisho wake na kila kitu chake?.​

Wiki iliyopita kwenye safu hii niliandika Buriani ya Benard Membe, na Wiki hii ni Buriani nyingine, hii ni buriani ya mtu wa kawaida tuu ambaye sio kiongozi wa CCM, wala sio kiongozi wa serikali, ni mtu tuu wa kawaida aliyefahamika na wengi, hivyo maneno ya mtu wa wengi ni maneno ya wengi na sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, hii ni makala ya kuitaka CCM, serikali, wapinzani kuzingatia sana wosia wa mtu huyu!.

Huyu ni William Malecela, ambaye anajulikana sana kwa jina maarufu la Le Mutuz, kutokana na kuendesha ukurasa wake wa Le Mutuz Super Brand kwenye mitandao ya kijamii, hivyo kuna wengi wanaomfahamu zaidi William kutokana na umaarufu wake wa kwenye mitandao ya kijamii kama Le Mutuz, hivyo sifa zake kama William Malecela, kujikuta zimeishia Jamiiforums pekee. William Malecela alifariki ghafla wiki iyopita na kuzikwa kijijini kwao Mvumi Dodoma siku ya Jumatano iliyopita.

Wosia.
Wosia ni maneno ya mwisho ya marehemu anayoyaacha kuzungumzia jambo fulani, wosia huo unaweza kuwa wa maneno ya kuambiwa au kuandikwa. Wosia huu wa William Malecela kwa CCM serikali, ni wosia wa maneno ya kuzungumza, ambapo aliyasema bila kupanga, ni tulikutana tuu viwanja vya Saba Saba, nikamfanyia mahojiano impromptu, na kwavile sasa tuko kwenye dunia ya kimtandao, wosia huu nimeurekodi kwenye video na kuutupia kwenye mtandao wa YouTube, baada ya kupokea taarifa ya kifo chake, nilipoyasikiliza tena "Mahojioano William Malecela na Pasco Mayalla" ndio sasa nimegundua kumbe huu ni wosia anaihusia serikali, CCM, na wapinzani.

Poleni Sana Wafiwa Wakiongozwa na The Malecelas.
Kunapotokea msiba wowote, wafiwa wakuu wa kwanza ni familia yake, hivyo kwanza nitoe pole zangu kwa familia yake, mkewe na watoto wake, pole kwa familia ya Mzee John Samwel Malecela, pole kwa familia yake ya JF, pole kwa wanamitandao kumpoteza mwanamtandao mwenzao, pole kwa CCM kumpoteza mwanachama wake ambaye ni mmoja wa wana CCM Wazalendo na wakweli kabisa toka ndani ya nafsi zao, na pole kwa Watanzania wote kumpoteza Mtanzania mwenzetu, haijalishi alikuwa nani, thamani ya mtu ni utu, hivyo binadamu yoyote akitangulia pole ni stahiki.

Mimi ni mtu wa mastori mastori, hivyo sasa nakuja kwenye mastori story ya Pasco, kama wewe sio mtu wa mastori story, jump to conclusions.

Mastori ya Pasco, Mimi na Malecelas

William Malecela, A Man With A Heart of Gold

Kuna watu wengi ni watu wenye roho mbaya, akiona kuna mchongo fulani, hakupi connection, William alikuwa ni mtu mwenye roho nzuri. Ni William Malecela, Le Mutuz ndie aliyenitambulisha mimi kwenye mtandao wa YouTube channel, na video yangu ya kwanza kwenye YouTube ni video ya mahojioano na William Malecela ambayo video hii ndio usia ambao William Malecela ametuachia milele, nataka wana CCM wote haswa viongozi, watu wa serikali na sisi wana jf, tusikilize kwa makini wosia huu na ikiwezeka tuuishi.

William Malecela Kada Mtiifu na Mkweli Daima wa CCM, at Heat!, He Was Born and Breed CCM!, Amekufa CCM!
Chama cha Mapinduzi CCM, kina taratibu zake za ukosoaji kufanywa na wanachama wake, kinataka ukosoaji wowote wa CCM, ukifanywa na mwana CCM, ukosoaji huo ufanyike kwenye vikao vya ndani. William alikuwa hakopeshi!.

William Malecela Aliipenda CCM na Kuitetea CCM, Lakini Hakuwa Chawa!
Siku hizi kupitia mitandao ya kijamii, kumeibuka vikundi vya kusifia wakiijiita machawa. William Malecela ni mwana CCM, aliyeipenda CCM kwa dhati ya moyo wake na kiitetea CCM kwa nguvu zake zote ila hakuwa chawa kwasababu pia aliikosoa CCM, wazi wazi na sio kupitia vikao vya ndani.

Ni katika mahojiano haya William Malecela alitoa usia mzito kwa Chama chake CCM, na serikali yake, kwa wapinzani na kwa wana JF. Je William Malecela alitoa wosia gani kwa serikali, CCM, wapinzani na kwa Jf?.

Kwa wenye uwezo to listen in between the words, karibu hapa

Kwa wasio na uwezo to read in between the lines and to listen in between the words, juma lijalo nitawamegea wosia huu tits and bits nitawatafunia, nyie kazi yenu itabakia ni kumeza tuu!.

Wasalaam
Paskali

Nimesikiliza between word to word ameongea kitu kinachoishi na Kwa mtazamo wangu CCM hawa wapendi watu wenye mtazamo huu huonekana kama waasi........

Kaka paschal kipindi Cha the late JPM watu waligeuka kua vikundi vya kusifu na kuabudu ukikosoa unaonekana muhaini ( praise power wa Lumumba)

Ukichagua upinzani siwaletei maji..mara siwaletei maendeleo 😊 huko ni kuendeshwa kijima....

Pia hata kauli za mama anaupiga mwingi mara sijui chawa wa mama nazo still ni maigizo ya wachumia tumbo.....

Ukiwa mkweli kama the late JPM Kwa hii CCM hautoboi round unaenda Kule ambapo watu wakienda hawarudi......
 
Wanabodi,
Hii ni makala yangu kwenye Nipashe ya leo.
View attachment 2629490View attachment 2629492
Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa, ambazo huwa na swali, likifuatiwa na hoja, kisha jibu utalitoa wewe mwenyewe.

Swali la mada hii ni Je

Wosia mzito wa William Malecela (Le Mutuz) kwa CCM, Wapinzani, Serikali na kwa JamiiForums uzingatiwe na kutekelezwa ili tuendelee kumuishi, au baada ya kufa,anakuwa ndio mwisho wake na kila kitu chake?.​

Wiki iliyopita kwenye safu hii niliandika Buriani ya Benard Membe, na Wiki hii ni Buriani nyingine, hii ni buriani ya mtu wa kawaida tuu ambaye sio kiongozi wa CCM, wala sio kiongozi wa serikali, ni mtu tuu wa kawaida aliyefahamika na wengi, hivyo maneno ya mtu wa wengi ni maneno ya wengi na sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, hii ni makala ya kuitaka CCM, serikali, wapinzani kuzingatia sana wosia wa mtu huyu!.

Huyu ni William Malecela, ambaye anajulikana sana kwa jina maarufu la Le Mutuz, kutokana na kuendesha ukurasa wake wa Le Mutuz Super Brand kwenye mitandao ya kijamii, hivyo kuna wengi wanaomfahamu zaidi William kutokana na umaarufu wake wa kwenye mitandao ya kijamii kama Le Mutuz, hivyo sifa zake kama William Malecela, kujikuta zimeishia Jamiiforums pekee. William Malecela alifariki ghafla wiki iyopita na kuzikwa kijijini kwao Mvumi Dodoma siku ya Jumatano iliyopita.

Wosia.
Wosia ni maneno ya mwisho ya marehemu anayoyaacha kuzungumzia jambo fulani, wosia huo unaweza kuwa wa maneno ya kuambiwa au kuandikwa. Wosia huu wa William Malecela kwa CCM serikali, ni wosia wa maneno ya kuzungumza, ambapo aliyasema bila kupanga, ni tulikutana tuu viwanja vya Saba Saba, nikamfanyia mahojiano impromptu, na kwavile sasa tuko kwenye dunia ya kimtandao, wosia huu nimeurekodi kwenye video na kuutupia kwenye mtandao wa YouTube, baada ya kupokea taarifa ya kifo chake, nilipoyasikiliza tena "Mahojioano William Malecela na Pasco Mayalla" ndio sasa nimegundua kumbe huu ni wosia anaihusia serikali, CCM, na wapinzani.

Poleni Sana Wafiwa Wakiongozwa na The Malecelas.
Kunapotokea msiba wowote, wafiwa wakuu wa kwanza ni familia yake, hivyo kwanza nitoe pole zangu kwa familia yake, mkewe na watoto wake, pole kwa familia ya Mzee John Samwel Malecela, pole kwa familia yake ya JF, pole kwa wanamitandao kumpoteza mwanamtandao mwenzao, pole kwa CCM kumpoteza mwanachama wake ambaye ni mmoja wa wana CCM Wazalendo na wakweli kabisa toka ndani ya nafsi zao, na pole kwa Watanzania wote kumpoteza Mtanzania mwenzetu, haijalishi alikuwa nani, thamani ya mtu ni utu, hivyo binadamu yoyote akitangulia pole ni stahiki.

Mimi ni mtu wa mastori mastori, hivyo sasa nakuja kwenye mastori story ya Pasco, kama wewe sio mtu wa mastori story, jump to conclusions.

Mastori ya Pasco, Mimi na Malecelas

William Malecela, A Man With A Heart of Gold

Kuna watu wengi ni watu wenye roho mbaya, akiona kuna mchongo fulani, hakupi connection, William alikuwa ni mtu mwenye roho nzuri. Ni William Malecela, Le Mutuz ndie aliyenitambulisha mimi kwenye mtandao wa YouTube channel, na video yangu ya kwanza kwenye YouTube ni video ya mahojioano na William Malecela ambayo video hii ndio usia ambao William Malecela ametuachia milele, nataka wana CCM wote haswa viongozi, watu wa serikali na sisi wana jf, tusikilize kwa makini wosia huu na ikiwezeka tuuishi.

William Malecela Kada Mtiifu na Mkweli Daima wa CCM, at Heat!, He Was Born and Breed CCM!, Amekufa CCM!
Chama cha Mapinduzi CCM, kina taratibu zake za ukosoaji kufanywa na wanachama wake, kinataka ukosoaji wowote wa CCM, ukifanywa na mwana CCM, ukosoaji huo ufanyike kwenye vikao vya ndani. William alikuwa hakopeshi!.

William Malecela Aliipenda CCM na Kuitetea CCM, Lakini Hakuwa Chawa!
Siku hizi kupitia mitandao ya kijamii, kumeibuka vikundi vya kusifia wakiijiita machawa. William Malecela ni mwana CCM, aliyeipenda CCM kwa dhati ya moyo wake na kiitetea CCM kwa nguvu zake zote ila hakuwa chawa kwasababu pia aliikosoa CCM, wazi wazi na sio kupitia vikao vya ndani.

Ni katika mahojiano haya William Malecela alitoa usia mzito kwa Chama chake CCM, na serikali yake, kwa wapinzani na kwa wana JF. Je William Malecela alitoa wosia gani kwa serikali, CCM, wapinzani na kwa Jf?.

Kwa wenye uwezo to listen in between the words, karibu hapa

Kwa wasio na uwezo to read in between the lines and to listen in between the words, juma lijalo nitawamegea wosia huu tits and bits nitawatafunia, nyie kazi yenu itabakia ni kumeza tuu!.

Wasalaam
Paskali

For a long time, I have heard this name of Lemutuz, but I knew it was just another scumbag in town with money. It was only until he died the other day that I found out that he was Malecela's first child.

I have thoroughly read your article, but I am just sad for many basic reasons.
 
Back
Top Bottom