Kwanini Levina Mukasa alijiua UDSM?

Kwanini Levina Mukasa alijiua UDSM?

Mhh...Hii habari imenisikitisha sana. Hivyo naomba uongozi wa UDSM pamoja na ule wa DARUSO mjiuzulu ili kulinda heshima yenu kama wanataaluma mbele ya jamii. Hii ni kutokana na kushindwa kudhibiti kundi haramu la PUNCH ndani ya hiyo taasisi kubwa ya elimu nchini .
mkuu umekupuka
 
Nilisoma O level Tambaza na A level Ilboru, Tambaza bang ilivutwa wazi wazi summit, ila wengi wa wavuta bangi wa Tambaza, walitoka na DIV 1 kali!, kuna akina sisi tulitamani nasi DIV 1, hivyo nilipoenda Ilboru, in seach of DIV one, nikajaribu!, very unfortunately, mimi ilinituma vibaya!, badala ya ku concentrate, ilinituma mambo mengine!, na shule yetu ilikuwa boys only!. Ilibidi kuingia mtaani kutafuta na nikikosa nilitembea hadi Mianzini kwenda "kununua!". Just imagine pori lile la Ilboru, umbali ule mpaka town, usiku wa manene, mwanafunzi ana cross boda peke yake!.

Wenzangu wakanieleza bangi inakutuma kile unachofikiria, nikajaribu tena na tena kujifikirisha masomo, ile kupiga tuu puff ya kwanza, mawazo yale yale mabaya yalinijia hivyo nikaacha!. Ilifikia kiwango cha hata nikiisikia tuu harufu mwingine anavuta, mwili unasisimka kuhitaji "mambo yetu yalee!" hivyo nikaacha kabisa, unless once in a while for pleasure purpose only!.

Ila hao hao waliokuwa wavuta bangi wa enzi hizo, sasa hivi wengi wako very successful men!.

Wanafunzi wanaosoma boys only, wanakabiliwa na tatizo la kisaikolojia liitwalo "male chauvinism", wanapontaka msichana, hujiona its their right kumpata, na akikataa pia its right kumbaka!, na wengi hubakwa hawasemi, hawalalamiki na baadhi ya mahusiano huanza kwa kumbaka ndipo kisha hupenda!.

Pia kuna type ya wanawake wananatatizo liitwalo "masochisim" hivyo huitwa macho women, hawa huderive sexual satisfaction kwa kufanyiwa violance kama kubwakwa!, hivyo hata untake vipi, hakubali, ila anajilengesha ili utumie force, ikiwemo kumvutia chumbani kwako, kumvua nguo kwa nguvu, akiona zinataka kuchanika, anaachia zitoke, then anaishikilia pichu sometimes unaichana!, akilala kitandani, anafunga miguu ufanye kazi kuifungua!, ukifanikiwa, utamnote she enjoys very much!, tena anajiachia haswa!. Wanawake hawa wanataka kuwa "concqured", ili wamkubalie mtu, lazima awe "the conqueror", hawa "male chauvinism", wakikutana na "macho women" wana blend.

Kuna type ya wanawake wanainatwa "feminine" hawa hata mfuate vipi, uonyeshe unampenda vipi, hawakubali ng'o mpaka akupende yeye!. Hawa thamani yao ni "uanamke wao!", ukimfuata fuata huku hakupendi, anakuona kero, una ghasi!. Mwanamke wa type hii, akikutana na hawa "male chauvinism", its trouble!. Marehemu Levina was this type, a "feminist!". Alipokerwa, alichukua hatuo zote za kuripoti, bila kupata msaada wowote!, take it from me, hiyo siku alipofight, "alibakwa!" hakusema kuepuka aibu, ikaishia kusemwa kuwa she was only harrased not abused!. Kwa vile kitu cha thamani kubwa kuliko kitu kingine chochote kwake was her "feminity" na kuna mtu kaja kujichukulia kwa nguvu as if ni yake!, then akajisikia she was degraded to the botom line, hivyo life kwake haina thamani tena!, kuliko kuishi na machungu, bora ajiue!.

NB. Watu wote wanao commit suicide, hutanguliwa na msongo wa mawazo, by the time anauchukua uamuzi wa kujitoa roho, anakuwa under "insanity!". Ila pia wanaowasababishia haya nao huwa hawabaki salama!, usually "karma" takes care of them.

Ila pia pale UDSM, watu wa Engineering ndio siku zote hujiona vidume!, mimi nimeingia chuo enzi za Prof. Luhanga, by that time, wale top management watano wa juu, 4 kati yao ndio walikuwa ma engineer, mmoja tuu ndio alikuwa fani nyingine!, sikujihusisha kabisa na siasa za Daruso, ila engineering ndio walikuwa na upper hand!. Nakumbuka kuna wakati nilimpigia kampeni dada mmoja wa Law ili awe VC, we spent much, lakini alishindwa na mtu wa engineering!.

Rip Levina Mukassa, shujaa mdogo mwanamke!.

Pasco.
i love it!
 
Hawa Punch hawakuwa na adabu kabisa. Nakumbuka waliwahi kumpanchi hata mkuu wa nchi mwaka wa 1995. "It was so embarrassing!" :embarassed2:
Sidhani kama ilikuwa huo Mwaka....!ni nyuma zaidi mwishoni au mwanzoni mwa miaka ya 90
hahaha Huyo aliyemchora Mwinyi akinanihii na Waziri wake yule mama Mkomoro aliyetokea Zanzibar Mke wa Megji ni lisikia alikuja julikana ni Mbatia....huyu aliyepewa Ubunge wa Dezo.... alifukuzwa Chuo na sijui kama alimalizia pale UDSM Nakumbuka hiyo Picha ilivuma sana na ilikaa sana pale Notice Board habari ikavuma tulivutiwa kwenda kuitizama hatukuikuta... Nilisikitika sana tuliambiwa kuna jamaa anachora michoro hakosei kumbe alikuwa ni Mbatia lol hili sakata akilisoma litamuuma sana Member wa PUNCH... Kuna kipindi cha uchaguzi kisa cha Mbatia na Mwinyi kiliibuliwa then kikafunikwa sijui ni kwa ajili ya Aibu ya Mzee Mwinyi!

Hawa jamaa wanatakiwa watafutwe kama lile kundi la NAZI Germany wapewe hii kesi ya kale... Mbatia apigwe Ban ya Siasa pia... Kuhusu kifo cha Levina kinasikitisha Sana...

Tambaza Boys kulikuwa na Mtu anaitwa PUZO nae alinyanyasa sana wanafunzi wenzake na makonda na washabiki wa timu zilizokuwa zinacheza na Tambaza...
 
hii habari ya kitambo sana ila imenisikisha sana. Alale pema Levina
 
huyu Levina Mukasa... ni dada yake na mtunzi mahiri wa nyimbo za kikatoliki bwana... BERNARD MUKASA

Na Yule binti wa DUCE Aliyechomwa kisu mwaka 2008 pale Mabibo Hosteli (jina limenitoka) ni Mtoto wa Nguli mwingine wa Nyimbo za Kikatoliki PF MWARABU (KOCHA)
What a Coincidence??
 
Asante kwa kutukumbusha hiki kisa, kisa ambacho kilimsikitisha yoyote mpenda haki. Lakini tukio hili, ulikuwa ndio mwisho wa Mzee Punch. Nilikuwa namjua Levina kwa karibu sana. Mimi mwenyewe wakati huo nilikuwa hapo chuoni na nilikuwa naishi Hall moja na Levina. Yote yaliyomtokea kabla ya kuamua kujiua nilipata nafasi ya kuyafahamu na kwa namna moja au nyingine nilijitahidi kuweka mambo sawa ili hali aliyokuwa nayo Levina isije ikaleta madhara, bahati mbaya mhusika akunielewa lakini baada ya Levina kuwa amekunywa sumu, huyu mtu alinifuata na kujuta ni kwa nini hakufuata ushauri wangu, mtu huyu ndiye pekee aliyekuwa na uwezo wa kuepusha alichoamua kukifanya Levina.

Wakati ule, kaka yake Levina ambaye wanashare Baba na Mama Mr. Deo Mukasa alikuwa mwaka 3, Bcom. Na yeye hakuweza kuyaokoa maisha ya mdogo wake, kwani hakujua kama mdogo wake angeamua kufanya alichokifanya.

Ukware wa kijana wa kikurya Saloti kwa mgongo wa Mzee Punch ulimtoa roho binti wa watu. Watu tulikasirika na ilibidi Ma-engineer wazikimbie meza walizokuwa wanadai ni wao tu wanaopashwa kukaa.

RIP Levina.

Tiba

Pole sana Tiba ntungaya kwa kujitahidi kuokoa Maisha ya Levina ila ndio hivyo Shetani alimzidi akatumia mwanya huo huo mtoto wa watu majonzi yote akaamua kujimaliza.... nimekumbuka Gazeti la Kasheshe ukilikosa Jimalize....

Yaelekea ulimfahamu haswa Marehemu.... ila kwa kosa lake la kujiua nakosa hali ya kusikitika.... kwani amejihukumu... nadhani huyo kijana wa kikurya kama bado yu hai hali yake ina majonzi yasiyosahaulika... kama vipi atafutwe watu wamufahamu vizuri....
 
Last edited by a moderator:
huyu jamaa mwandishi kakosea jina tu, alikua anaitwa Omary Sarota ni mwenyeji wa Mara, kwao ni Musoma mjini sehemu inaitwa Kamunyonge ..
Anatakiwa afunguliwe mashtaka. Damu ya mtu haipotei hivihivi. Mungu ni mwenye kutenda haki siku zote na nina imani ataitendea haki familia ya huyu marehemu dada wa watu
Na wewe binadamu unaeitwa Sarota, Mungu atakuhukumu papa hapa duniani. Damu ya Levina iwe juu yako daima
 
Hao wahusika wote walistahili kuuawa pia, kuanzia na huyo Omari Saloti. Angekuwa ni dada yangu au mtoto wangu ningewasaka na kuwashikisha adabu wote kimya kimya.
 
Hao wahusika wote walistahili kuuawa pia, kuanzia na huyo Omari Saloti. Angekuwa ni dada yangu au mtoto wangu ningewasaka na kuwashikisha adabu wote kimya kimya.
Mkuu nakuunga mkono. Anatakiwa awindwe huyu Sarota na apelekwe kwenye vyombo vya sheria.
Damu ya huyu dada wa watu iko mikononi mwake
 
Dah. .asante EMT. .RIP Levina.


Unyanyasaji wa kijinsia na kisaikolojia ni hatari sana. Sikonge sio kila mtu ni jasiri au sijui niseme jeuri kiasi cha kuweza kupambana na hayo mambo mpaka mwisho bila kutetereka. Kuna watu ambao wakishaumizwa kihisia wanapoteza kabisa "self worthy". Kitendo cha Levina kubakwa (kama ambavyo wengi wamesuggest ilitokea ila hakutaka kusema) kilimfanya ajione hana thamani tena. Matusi, kuchorwa na fujo alijitahidi kupambana navyo kwa kutafuta msaada hapa na pale. Ila kitendo cha kubakwa ndio kilikuwa 'breaking point' kwake. Hakuona afanye nini tena ama apiganie nini maana mwanzo alikuwa analinda uanamke wake na sasa hanao tena so she gave up.

Hata angeenda JKT pengine isingesaidia maana kuke hawamfundishi mwanamke namna ya kujithaminisha, wanafundisha ujasiri.

Hii story inasikitisha sana ila inasisimua kwa namna ya kutamanisha kujua zaidi. Kashaijabutege , Pasco , watu8 , EMT, TIMING na wengine mnaojua zaidi kuhusiana na hilo kundi la PUNCH embu tuelezeni zaidi. Hao jamaa walikuwa wanapata wapi ujasiri wa kufanya mambo waliyofanya mpaka wanaogopwa na uongozi wa chuo? Members walikuwa wanaingia vipi?
Tena miaka ile kiasi flani wadada walikua wanajitunza sana sasa tukio hilo kwake lilikua kubwa sana hebu jiulize unauweka wapi uso wako baada ya kufanyiwa yote hayo. Tena jamii inakutenga na kukuona mkosefu mno.
 
Mbona mimi nakumbuka kama huyu alijirusha ghorofani?

Kuna wawili. Kuna mmoja alijirusha toka ghorofani kama unavyokumbuka halafu kuna huyu aliyejiovadozi.

Ngoja nikipata muda nitazimwaga data za huyo mwingine.
 
Heeee haya yalitokea hapahapa tanzania mkuu?

Dizaini zamani wanafunzi wa kiume walikua wanaume hasa sio vishalobalo vya siku hizi hata ngumi havijui kuikunja
Tena enzi hizo nauli ya daladala kwa mwanafunzi ilikua shilingi moja basi makonda walitunyanyasaje wanafunzi, lkn wanafunzi wa tambaza walikua wanawapa kichapo makonda acha tu. kuna jina lilikua linavuma kama nakumbuka ni PUZA or something like that huyo alikua tishio.
 
Kuzuiwa kwa siasa za kipinzani (nchi nzima wala sio ndani ya vyuo vikuu pekee) ilifanya watu waanzishe vikundi vya siri.

Naamini punch ilikua sio kikundi cha wanafunzi pekee, kwa vyovyote ilikua ni zaidi ya uanafunzi. Vitendo vyao vilionyesha kuwa ni watu waliokua na nyenzo nyingi na walikua wana nidhamu ya hali ya juu. Walikua na uwezo wa kuchunguza mambo hata ya nje ya chuo....haya mambo yalihitaji rasilimali nyingi, ikwemo fedha, sidhani kama wanafunzi walikua na uwezo huu. Kulikua na aina ya mwendelezo wa uwepo wa punch ambao haukuwa wa kiunafunzi.

Bado naiona punch kama sauti ya upinzani uliokatazwa hapa nchini......japo wanafunzi walitumia vibaya nguvu za punch!

Hilo la kudhalilisha ndiyo lilikuwa lengo la msingi kwani wakati wa Nyerere mazungumzo ya siasa vyuo vikuu yalikuwa limited.
 
Back
Top Bottom