Crystal clear
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 809
- 338
Inasikitisha sana
Hahahaa, Lizzy, huyu Smile ni Mtani wangu. Anataka sana kuolewa SIKONGE na Wanyamwezi wa huku. Ingawa yeye ni Mchaga, ila hata sijui utani na Wanyamwezi kaanza lini, ila basi tu imetokea Mnyamwezi kawa Mpare kwa kuFIKIA. Huu Mwaka hauishi, lazima mtu awe kama SAYARI ya SATURN...... Ili akubali kiharaka haraka, unamnyanyasa kwanza KIJINSIA kama Mzee Punch vile.... Mwisho, kumbuka sisi Wahandisi hata kutongoza hatujui, si umesoma mwenyewe? Hata kama ana miaka 18 na mie nina 58, unamnyanyasa hadi anajiona ni yeye ana 58 na mie nina 18 na kuwa namfanyia MSAADA tu kuwa naye, heheheee 🙂
![]()
![]()
Hii story kwa kweli nimeiandika kwa jinsi nilivyokuwa naikumbuka kwani wakati ikitokea, nilikuwa bado na kamasi puani.
Hahaha!! hayo majina ukiyasikia tu unajua kabisa si salama
Kuna siku mwaka 1993 au 1994 wanafunzi wa WU-TAMBA walitembeza mkong'oto karibia shule zote za msingi na sekondari.
Nakumbuka siku hiyo ilikuwa ni hekaheka mjini hapa, wanafunzi na waalimu walipigwa bila kusahau mali za shule nyingi ziliharibiwa.
aisee mimi sithubutu kurusha mguu wangu kwa mnyamwezi tena! hata uniambie utanipeleka wapi acha niishie kutalii mlima kilimanjaro na misitu yake basi!....khaaa kuna watu wana roho ngumu kama paka bwana
aisee mimi sithubutu kurusha mguu wangu kwa mnyamwezi tena! hata uniambie utanipeleka wapi acha niishie kutalii mlima kilimanjaro na misitu yake basi!....khaaa kuna watu wana roho ngumu kama paka bwana
Omar salot na mark victor wahusika kwenye movie hili wako wapi? Ngoja niende fb naweza yakuta huko
ngoja nikale kuku kwanzaMwanamke mmejaliwa uwezo mkubwa sana kumtawala Mwanaume. Kama hujui wee uliza.
Mwisho kumbuka milele kuwa mie nimekuzwa na Mwanamke, hivyo nawaheshimu sana Wanawake wote duniani.
Sawa Mzee mwenzangu, ngoja nikukimbie na kiburudisho maana Weekend inaanza, ngoja nichukue Bugaluu yangu na Raizon langu nijivike nikaruke mangoma leo jioni. Afro langu linawaka si mchezo sasa hivi.
Mhh...Hii habari imenisikitisha sana. Hivyo naomba uongozi wa UDSM pamoja na ule wa DARUSO mjiuzulu ili kulinda heshima yenu kama wanataaluma mbele ya jamii. Hii ni kutokana na kushindwa kudhibiti kundi haramu la PUNCH ndani ya hiyo taasisi kubwa ya elimu nchini .
Serikali nayo ilikua lege lege hadi anaacha wahuni wanatamba. Sahvi Mkandala hacheki na watu wa vurugu kama hao waulize walipoishia wanaharakati.Sasa hivi hata Revo Square kwishney.
Kwahyo uongozi wa sasa wa UDSM na Daruso wajiuzulu au nimekuelewa vibaya.
so sad, kundi hilo liliendelea hadi miaka ya 2000 japo hali ilibadilika kiasi kwani hadi wanaume walikuwa wakitolewa Punch. Pia kuna wanawake walianzisha kundi lao "MOTHER OF THE LAND" Walikuwa wakiwatoa wanaume sana sana japo haikuwa strong kama PUNCH Original. Wengi sana walifikia uamuzi wa kukatisha maisha yao japo takwimu sahihi zinaweza zisiwepo. Safari ya Usawa wa Kijinsia na kumaliza unyanyasaji wa kijinsia ni ngumu sana kwa kuwa wapo wanaofanya hivyo bila kujua ni unyanyasaji na wapo wanawake wanaofurahia na kuchekelea kwa kuona mwanamke mwenzie ananyanyasika. Mungu azilaze pema roho za marehemu walitutangulia kwa unyanyasi wa kijinsia wa aina yoyote.
Inasikitisha kwa waliokumbwa na dhahama za aina hii....
Punch ilikua nzuri kwenye siasa, nadhani hili la kudhalilisha halikua lengo lao la msingi...nadhani walitumia vibaya nia na uwezo wa punch!!!
bora umeuliza maana shivji nimesoma miaka mitatu pale midahalo mingi aliyowahi kuiendesha ikiwemo kigoda cha mwalimu nyerere hawezi kuonesha kauli ya kidhaifu hivyo haswa katia swala nyeti hvyoProf . shivji huyu huyu ninayemheshimu aliongea kauli dhaifu kama hiyo? Au alikuwa anamaanisha nini kuhusu saga hiyo labda sikuelewa??!!
Asante EMT , watu8 , Kashaijabutege , Kongosho na Pasco kwa kumbu kumbu hii nzuri yenye mafunzo mengi. Mungu amlaze pema peponi shujaa huyu Levina, natamani kusikia picha na historia yake ipo maktaba ya UDSM. Pia itakuwa ni busara kwa waliokuwa member wa hili kundi la PUNCH wakatubu hadharani na jamii itawasamehe, imewezekana SA na Rwanda, waige mfano huo.