Kwanini Levina Mukasa alijiua UDSM?

Kwanini Levina Mukasa alijiua UDSM?

Kama kitu kinaweza sababisha kifo, hakina faida tena hata kama msaada wake ni mkubwa kivipi.

Tukubali tu kuwa watu tunatofautiana sana. Hayo mapenzi ya hadharani, yanaweza kuonekana hadharani kwa kundi fulani lakini si kwa watu wote. Na mara nyingi tabia lazima zitofautiane kwenye jamii.

Mara nyingi katika jamii za kiafrika, makundi ya kurekebisha tabia huwa yanakuwa so harsh kwa wanawake na wanamme wanapewa unafuu.

Anyway, historia iliandikwa na leo tunajifunza, japo ilipoteza maisha ya innocent and naive soul, na familia ilipoteza mtoto, dada, binamu, shangazi n.k.

Ila hiki kisa kilitakiwa kiwe documented vizuri kwa ajili ya jamii angalau tulikotoka, tulipofika na tunakotaka kwenda kwenye suala zima la unyanyasaji wa kijinsia. Sijui TNGP, TAMWA wala TAWLA kama wanakijua hiki.
Dr Diana wa TNGP alikuwa mwaka wa kwanza, hivyo anafahamu kisa hiki vizuri.
 
Nakumbuka alikuwa wenyeji wa Biharamuro Kagera
. Sio ajabu akawa ndugu na aliyekuwa Mgombea ubunge kupitia CCM katika jimbo hilo.
Mkuu ni kweli akina Mukasa ni wenyeji wa Biharamulo, na Mh. Dr. Oscar Mukasa alikuwa mbunge kati ya 2009-2010 kabla ya kuangushwa na Dr. Mbassa.
 
Inasikitisha sana ukatili wa kijinsia wanaume tukisema utokomezwe utatokomezwa tu

Waliwa-Punch viongozi wengi sana wakati ule. Viongozi wa juu jabisa kutukanwa walikuwa ni Marehemu Balozi/Waziri Hassan Diria (Mzee wa Muche au Mustachi) ambaye walimchora kama Mwanamke na wakaandika HASSA SINDIRIA na akiwa kapiga nzinga wa Sindiria.

Rais Ali Hassab Mwinyi yeye walimchora na kumtukana matusi mazito kabisa ya nguoni na hadi mwenyewe kama Binadamu, alilalamika sana kwa kitendo hicho.

Pichani, Mar. Hassan Diria akiwa Waziri wa mambo ya nje akiwa na Marehemu MJ, uwanja wa ndege Dar es salaam.

michael+jackson+diria.jpg

Hii picha imenikumbusha marehemu MJ alipokuja Dar. Nafikiri ni miaka ya mwanzoni ya tisini. Marehemu Diria alikuwa waziri wa mambo ya nje. Katika mapokezi hiyo inasemekana Diria aliwapanga wanae wampatie maua MJ akushuka kwenye ndege ili na wapate chance ya kumuona MJ kwa karibu.
 
Gender based violance bado sana ki bongo hata ukiangalia hao kina munkya wamepewa ubunge kwa kuvua nguo zao na wengine wengi lol
 
Nimekosa sababu ya ku LIKE hii mada

Nimejiuliza tu kuwa hivi niki LIKE ndo nitakuwa nimependa aliyofanyiwa huyo dada au nitakuwa nime LIKE kitu gani hasa?

Mambo haya yalikuwepo sana nyakati hizo

Siku hizi naona kama yamefifia sana!
1907486_3929808261418_1238797964_n.jpg
 
Lizzy, naona unechapia maneno yako mwenyewe sasa. Ni kweli kuwa huyu dada alinyanyaswa sana ki-hisia na hata kupigwa kama ilivyoandikwa ila kusema ALIBAKWA, hilo si kweli.

Hii sababu kuwa hakuenda JKT nayo ilichangia, hiyo si muhimu sana ila wengi wanasema kama angelikwenda JKT, basi hata angelifahamu jinsi ya kujilinda au kujihami na unyanyasaji huo. Sijui kama ulipita JKT za miaka hiyo ya zamani kwani huko nako Wasichana walinyanyaswa sana ila wengine bado wakikuwa ng'ang'ari.

Uzuri wa JKT ni kuwa mnaingia wote na kuanza kunyung'unywa wote. Kwamba kuna Mdada atateswa zaidi, hiyo inatokea na pia kuna wanawake vichaa vilevile. Nilishaona Koplo akimwambia dada mmoja "Wee Dominika, una nguvu sana...." yule Mdada akamjibu "Afande,jaribu bahati yako uone kazi...." Watu walivunjika mbavu si kawaida.

Uhusiano wa Wasichana na Wavulana wakiwa JKT huwa unakuwa Mkubwa sana na kila msichana anaanza kuwachukulia Wanaume kama wenzake tu. Anaweza hata kuoga pamoja nao. Na kweli kabisa JKT tulikuwa tunaoga kwenye distance fupi sana yaani kama mita 10 hivi tofauti. Huwezi kuanza kutafuta kichaka au bafu kwa sababu muda huo hautoshi. Pia unakuwa umechoka hata tamaa huna.

Hizi habari nilizisikia kutoka kwa ndugu yake Marehemu ambaye ndiye aliniambia kwa undani zaidi kuhusu kifo chake kwani mie sikukifahamu kwa ukaribu zaidi. Na hii sababu ni yeye aliniambia na ukiiangalia kwa asilimia fulani ina ukweli ndani yake. Wasichana waliopitia JKT, huwezi kumnyanyasa kirahisi. Pia ukiwa JKT, huko unajenga urafiki na makundi tofauti sana ambayo huwa hayajali Kabila, uwezo wa fedha, shule uliyosoma, jinsia nk. Na hao hao watu, ukishafika UDSM miaka hiyo au Chuo kikubwa chochote, basi wanasimama imara kukutetea.

Pia napingana na Dada Chemi kwa kusema kuwa Mzee Punch alishambulia Wanawake pekee au alikuwa kwa ajili ya Wanawake. Walishashambuliwa watu wa akila aina. Walishambuliwa Waalimu, Mawaziri (Hassan Diria) na hadi Rais Ali Hassan Mwinyi.

Malengo ya Punch zamani yalikuwa ni kuirekebisha jamii na kushambulia unyanyasaji. Ila kama ilivyo vitu vilivyofanywa na binadamu, Punch ilianza kuacha njia yake na kuanza kwenda PERSONAL. Ilianza kutumika kama kifaa cha kulazimisha mapenzi, kunyanyasa watu, kulipa kisasi, kulazimisha mambo, mbali kabisa na malengo yake ya mwanzo. Hii ikawa ndiyo msumali wa mwisho kwenye kaburi la Mzee punch. Pia kuanguka kwa Ukoministi na nchi kufunguka zaidi kwa watu kuangalia wenzetu wanaishi vipi, ilianza kupelekea Vijana/Wanachuo kuanza kubadilika.

Nasikia kuna dada alikuwa anaitwa Asha na alipokuja Jesse Jackson (USA) basi akaomba apigwe naye busu. Kesho yake wakamtoa ukutani. Ila kwa mtu au Mdada wa namna hiyo, tayari inakuwa mnahangaika tu kwani kashafyatuka tayari. Walijitahidi hadi kuanza kuita Scale au Unit ya Nyege ni ASHA.

Mwingine nasikia alikuwa akigawa uroda kwa mwalimu na hawapi wenzake, basi wakamchora pia anagawa uroda mezani na mto wake ni Simu ya mezani. Ila hapa walichorwa wote, Mwalimu na Mwanafunzi. Kuna mama nasikia alikuwa Mwalimu wa Netball au sijui mchezo gani sijui. Basi akafanya upendeo kwenye kuchagua wachezaji na wakaenda huko wakafungwa. Basi wakamtoa kuwa yale magoli ndiyo yamesababisha akawa Mjamzito (ni kweli alikuwa na Mimba).

Hivyo, unaweza kuona kabisa ni kweli Wanawake walishambuliwa zaidi ila Wanaume pia wanalishambulia. Na mara baada ya kuanza vita na Serikali, nafikiri wanawake walisahaulika kabisa na ikaanza vita kati ya Wanasiasa (wengi wanaume) na wao Punch.

Wakati walimtundika Rais Mwinyi, si kuwa walimtundika mara moja hapana. Ilikuwa ni kila siku. Mwisho ikaamulika kuwa Cafeteria wawekwe Walinzi usiku mzima. Basi hadi imefika saa 11 alfajiri, nasikia Punch akawa amekwama kuweka Punch lake. Jamaa wakaenda kuwasha mto Bweni moja wapo. Wale Polisi kuona moto, wakakimbia kwenda kuzima, na walipokuja kurudi, wakakuta wanafunzi wanaingia kupata Chai ya asubuhi na Ukutani juu kabisa, Mwinyi amening'inizwa. Ilibidi uongozi na serikali wawaombe wasifanye hivyo na wakawaondoa Walinzi wote . Kesho yake hakukuwa na PUNCH.

Dah. .asante EMT. .RIP Levina.


Unyanyasaji wa kijinsia na kisaikolojia ni hatari sana. Sikonge sio kila mtu ni jasiri au sijui niseme jeuri kiasi cha kuweza kupambana na hayo mambo mpaka mwisho bila kutetereka. Kuna watu ambao wakishaumizwa kihisia wanapoteza kabisa "self worthy". Kitendo cha Levina kubakwa (kama ambavyo wengi wamesuggest ilitokea ila hakutaka kusema) kilimfanya ajione hana thamani tena. Matusi, kuchorwa na fujo alijitahidi kupambana navyo kwa kutafuta msaada hapa na pale. Ila kitendo cha kubakwa ndio kilikuwa 'breaking point' kwake. Hakuona afanye nini tena ama apiganie nini maana mwanzo alikuwa analinda uanamke wake na sasa hanao tena so she gave up.

Hata angeenda JKT pengine isingesaidia maana kuke hawamfundishi mwanamke namna ya kujithaminisha, wanafundisha ujasiri.

Hii story inasikitisha sana ila inasisimua kwa namna ya kutamanisha kujua zaidi. Kashaijabutege , Pasco , watu8 , EMT, TIMING na wengine mnaojua zaidi kuhusiana na hilo kundi la PUNCH embu tuelezeni zaidi. Hao jamaa walikuwa wanapata wapi ujasiri wa kufanya mambo waliyofanya mpaka wanaogopwa na uongozi wa chuo? Members walikuwa wanaingia vipi?
 
Wanaweza, tatizo ni ushahidi,beyond reasonable doubt!

Kweli mkuu, inawezekana kabisa hakuna hata mafaili Police....... Kwa hapo criminal case itakuwa ngumu!! Lakini la madai nafikiri linawezekana kabisa ............ na chuo au Wizara husika ikalipishwa fidia!! Kama issue ilifikia mpaka kwenye ngazi za utawala wa chuo basi kuna uzembe mkubwa sana ulifanyika. Hata hao akina Victor na Omari wanaweza kupelekwa kama mashahidi kwenye kesi hiyo ya madai.
 
Serikali nayo ilikua lege lege hadi anaacha wahuni wanatamba. Sahvi Mkandala hacheki na watu wa vurugu kama hao waulize walipoishia wanaharakati.Sasa hivi hata Revo Square kwishney.
 
Kesi ya madai standard of proof ni beyond reasonable doubt au preponderance of the evidence?

Si alijinyonga, ulisababisha ajinyonge, manslaughter- Unaweza fungua kesi zote mbili, madai -standard of proof- balance of probability , na manslaughter -beyond reasonable doubt (not beyond doubt)
 
Si alijinyonga, ulisababisha ajinyonge, manslaughter- Unaweza fungua kesi zote mbili, madai -standard of proof- balance of probability , na manslaughter -beyond reasonable doubt (not beyond doubt)

Based on the preponderance of the evidence, nafasi ya kushinda kesi ya madai ni kubwa zaidi kuliko ya jinai.

Kwenye jinai hapo itakuwa rahisi sana kutilia shaka usababishi wa moja kwa moja wa watuhumiwa.
 
Back
Top Bottom