so ndo ilikuwa KKK ya mlimani wakati huo na ilikuwa nadhumuni lipi na kinanani walikuwa ma founder wa hii?...kati ya maswali ya kujiuliza huenda hata wakina Ulimboka na wote waliopata mateso ya kinyama pale mabwepande ni source kama sio product ya PUNCH
Binafsi nilivyoiona PUNCH hakikuwa chombo cha wanafunzi peke yao. Kama nilivyosema awali, kwanza lugha iliyotumika katika makala zake ilionekana kusheheni ujuzi wa fani mbalimbali (madaktari, wahandisi, waandishi wa habari, wachumi, polisi, usalama wa taifa, n.k). Kuna matoleo mengine yalikuwa ni ya uchunguzi wa kina wa jambo (investigative), kiasi kwamba mwanafunzi wa kawaida asingekuwa na uwezo wa kifedha kukamilisha uchunguzi huo. Makala nyingine ziliianika serikali au taasisi zake, jambo ambalo lilikuwa gumu kuwezekana pasipo mkono wa nje ya Mlimani.
Lingine linaloonesha kuwa PUNCH hawakuwa wanafunzi peke yao, ni ule uwezo wa kutundika makala hizo sehemu nyeti, kama jengo la utawala pasipokushikwa wahusika.
PUNCH vile vile ilikuwa ni vent ya kuikosoa serikali katika mazingira ya chama kimoja na uchache wa vyombo vya habari. Enzi hizo watu, wakiwemo watawala, walipanda magari kuja Mlimani kusoma matoleo ya PUNCH.
Nakiri kabisa kuwa PUNCH ilikuwa na madhara ya kibaguzi (hasa kwa wasichana-waliokuwa wachache vilevile), lakini kuna na mambo mazuri (postive) ambayo PUNCH imechangia katika ustawi wa Taifa hili.
Nguvu ya PUNCH nilivyoiona, lazima ilikuwa na patrons wenye nguvu, nje na ndani ya Chuo, ingawa sisemi Shivji alikuwa mmoja wao.