Kwanini hivi jamani...

Kwanini hivi jamani...

Mhh kwani kutongozwa dhambi?? Hapo ni ww kukataa au kukubali sasa ukikubali huko pm mkishindwana kuja kusema huku yanatuhusu nini?? Kweli binadamu mnapenda kujaribu yani unatongoza mtu usiemjua ukikuta ni dada ako je?? Ok mm naona kwanza kujianika umetongozwa ni ushamba uliopitiliza ndo kwamba tujue unatongozwa sana au?? Be mature guys. Na nyie wanaume mtu akikukatalia isiwe ndo chanzo cha bifu mbaki marafiki tuu na uheshimu privacy yake.
Mpendwa
 
Maisha yanaenda kasi sana...hv ni kweli wadada wamekuwa desperate kimapenzi kiasi hiki?mpaka kufikia hatua ya kuchukuliana na wengine walifikia hatua ya kutoleana siri zote za PM zao hapa sebuleni,Mtoto wa kike kweli kabisa unajua fulani na fulani wana mahusiano na wewe unaenda mbali zaidi kujiingiza humohumo kwa kidume huyohuyo...hv huwa mnatafakari kabla?Na wewe mwanaume mwenzangu hivi hujiulizi huyu binti kama anajua fika kwamba una mahusiano na flani halafu still anajileta kwako hv unapata tafsiri gani juu ya huyo binti????
Mkuu mbuzi kufia kwa muuza supu sio kosa...
 
Ni kutokukua kiakili....

Ni kuwa hawajakomaa......

Nanhapo ndio umuhimu.wa kuwa na mipaka unapokuja...

(Ila binadamu tuna guts...unamtongoza mtu kwa kuwa tu uneona avatar ...)
Salaam jf members

Hivi inakuaje watu wazima wenye familia zao,wanakua wanashindwa kua na busara,hekima na uvumilivu?

Hivi jf hapa ni kama nyumbani kwetu sisi ni wanafamilia moja au majirani tunaoishi pamoja kama ndugu.

Sasa nashangaaa na kupatwa na bumbuazi haswaa nikiona wanajamii moja tunashindwa kustiriana kama ndugu au marafiki wa dhati kwa kweli inaumiza sana na kustaajabisha.

Yaani humu sisi sote ni watu wazima,wasomi na wasio wasomi,lakini leo hii watu wa humu wengine tuna mambo ya ajabu ajabu mpaka yanatia aibu

Kutongozana ni jambo la kawaida sana katika jamii kama hii,lakini sasa humu mwingine akimla 'nyama'msichana basi ndo anajutaa atamtangaza mpaka ajutee..unabaki kua topic tena miaka mia
Mdada nae akitongozwa basi anakuja kumlipua mwanaume wa watu loohh...!!!
Wengine mnawateta watu PM siku mkilipuana mnaumbuana yoootee..

Wengine mnakutana PM,mnapena contacts mnakutana hukoo baadae mnaanza kuwacompare na kuwacontrast kama bidhaa vile

Na wengine msiojijua na kujielewa sasa yaani nyie ndo shida tupu!!ninyi ndo vichaa nashindwa hata kuwaweka kundi lipi...
Unapewa picha ya mtu 'either PM or whasaap'then unaexpose kwa wengine wasiomjua yule mtu..na kuwaambia yule ni nani...!!


Wengine tena wakiwa na mahaba tunajua jf nziima siku wakiachana wanatoleana ya moyoniii yooote looo ...

Kuna wengine ni waongo balaaa yaani kusambaza umbea tu usiomhusu na unaomuhusu...

Jamani tuweni na hekima na busara binadamu ni kiumbe mwenye mapungufu lakini sasa yakizidi ni shidaa...

Tuheshimiane sana tukilana,kukimbiana gesti,kukopana tuuchune tu jamani kibingwa kwani shilingi ngapi...hata tukikataliwa pia tujifunze kupiga kimyaa tu...!!

Hata kama ninyi ni wapenzi msijipambanue saana vile maana dah!mkiachana mwingine akapata"goma"lingine humu mnatupa shida sana kunnua bando la kusoma umbea .

Ni hayo tu kwa leo!!!Mengine mtaongezea


sent from motorola bapa and nokia jeneza
 
Ni kweli, you need 3D eye to ascertain spoilers.

Yaani kweli Khantwe umeshindwa kunijua jukwaani basi tumehamia Pm more than two weeks or on month unashindwa kunijua mimi ni mtu wa namna gani japo 40%... au nikishakuja pm tu fasta umenipa namba, umenipa location.... hahaha aigoo
Fursa hizi....
 
Kwanza mvujisha taarifa na mvujishwaaji wa hizo taarifa wanatakiwa wajitathimini wote. Wengi wao huwa ni matahira wote.

Ni kweli mtu akikufuata pm amekuamini. Hivyo na wewe mfuatwa unapaswa utunze siri.
But ile siku wewe ulivujisha pm yangu.
Nashukuru Mungu kwamba sikuandika cha kutisha wala sikumsema mtu sijui ningeficha wapi sura yangu.
Hivi unakumbuka pia kuna vitu uliongea na wewe? Haukuviandika mbona.?
Hata hivyo nimeshindwa kujizuia kukuuliza hili.
sumbai unisamehe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi naona kikubwa ni kuheshimiana.
Sidhani kama mtu unaweza ukaonana nae mkawa na mahusiano mkaheshimiana halafu baadae mje mtangazane.
Tatizo lazima mmoja aanze kumchokoza mwenzake... Na kumwonyeshea dharau za wazi..
Sasa geniveros unadhani mtu atamalizaje hasira yake bila kuandika madhaifu yako na wewe?
Mimi Mtu nikishakuwa na mawasiliano naye hata nikikuta anatukanwa mahali napita kama sioni.
Kwa sababu nikichangia lazima atachukia na akichukia kama ana udhaifu wangu atauleta tuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzi mzuri sana huu. Yaani mimi mwenyewe naogopa kweli kuomba vitu PM.
 
Back
Top Bottom