Kwanini Watanzania tuko hivi? Ni laana gani?

Kwanini Watanzania tuko hivi? Ni laana gani?

KanyeWest_Tz

Senior Member
Joined
Jul 18, 2026
Posts
162
Reaction score
321
Ila aisee kwanini sisi watanzania tuko hivi?
Ni laana gani tuliyo nayo sisi?

Katika pita pita mitandaoni nimejikuta nashangaa why! Watu wana make fun of juma jux. Ndo hao hao walomcheka akiwa haijawa na ndoa, ila leo kaingia kwenye ndo kawa kituko tena?

Hii ndo sababu watu hawakai kwenye ndoa maana nje kuna wachawi wengi wameachika, wana stress, hawana maisha so wanatumia kila wawezalo kuweka mtu chini.

Na kuna mtu akaja na uzi ambao uko titled. "Jux kayakanyaga huko"
Thread 'Jux kayakanyaga huko! Waja wanauliza kwanini kakonda sana?' https://www.jamiiforums.com/threads...-waja-wanauliza-kwanini-kakonda-sana.2461981/

Sasa unajiuliza Kwahiyo kumbe ulikua unasubiri ayakanyage?

Mbona kipindi anasajiliwa Warner music stori zake hazikuvuma? Kwanini hakupata support kutoka huku kwa watu wake ila wanaijeria?
images-2.jpeg

Lakini pia haitoshi... Humu Jukwaani japo mimi sio mchangiaji sana huwa naona jinsi watu wanavurugwa wakiona mtu kawazidi kila kitu kwenye hoja.

Kuna member anaitwa Elevenn au de Gunner ambae binafsi huwa napendezwa na uandishi wake ila watu wanamcrash kisa anapenda kujiona.

Kujiona kwake kuna uhusiano gani na wewe? Je kwanini usistick kwenye mada na sio mtu? Watu humu ni kama wale wale tu wa mitaani.. Ni wana nongwa na chuki binafsi. Haya sasa mtu akipigwa ban wewe unapata faida gani?

Sasa hivi kuna movement za kumchokoza mtu makusudi alafu wanakusema kwa mods umewatukana. Si ni utoto na ujinga kabisa huo?

Yaani kuna muda nasema hili li nchi limelaanika kabisa.

Ukija kwenye siasa nako. Watanzania wa abaki kuongelea vichochoroni, hawana guts za kupigania haki zao, wanasiasa wanalambana miguu tu, yaani imekuwa bora ya wakoloni. Hii nchi kuishi inabidi ujifanye zombie tu kwa kweli.

Ni kheri hata wakoloni kuliko mtanzania aliyeshika nyadhfa. Huwa wanakua kama mbogo.

Hivi watanzania ni nani aliye waroga nyie? Jamani hivi na nyie mnaona kawaida tu?

Kwakweli mimi naona bora mjerumani arudi tu, awanyooshe watanzania. Hakuna watu humu, kuna nyumbu tu wanaotembea.

Nawasilisha
 
Usiwaze sana , welcome to the reality of our society.
Kwa nini nisiwaze mkuu? Yaani nisiwaze existence ya vitu vya hovyo namna hii kweli?

Au labda nafsi zenu zilisha kufa kabisa? Maana hii nayo sio kawaida. Mtoto hazaliwi akiwa na hate ila mazingira humshape. Na kizazi kinazidi kuharibika siku baada ya siku
 
Baada ya kukwambia usiwaze, umesoma hapo mbele nimekwambia nini?

Au haujui kusoma vizuri?
 
Hakuna muujiza utakaotokea. Solution ni moja tu, mind your own business. Kila mtu apambane na hali yake, tafuta hela yako ili uishi maisha unayotaka.

Ukitegemea mindset za wabongo zibadilike utazeeka kwa stress bure. Focus on your own circle, mengine tuwaachie wenyewe.
Sawa mkuu
Ila japo kuna ukweli ndani yake. Hiyo ni self centered solution.. Hauwezi kuona mtoto wa jirani kaharibika then ukafumba macho. Unakuwa ni kama vile hauna soul. Inakuwa ni kama jamii inayo kuzunguka haimatter kabisa
 
Mkuu nadhani utakuwa haufahamu uhalisia wa jamii yenyewe kwa sasa, siku hizi ukijifanya unamsaidia mtoto wa jirani asiharibike, jirani huyo huyo atakugeuka na kukuita mchawi au mbea!

Jamii yetu imeshaharibika kuanzia kwenye ngazi ya familia, the social fabric is torn apart, Ili kuisaidia hii jamii, hauhitaji huruma ya mtu mmoja mmoja, tunahitaji institutional overhaul kila mtu awajibike kwenye nafasi yake.
 
Sasa hapo tutarekebisha kweli?
 
Kwa sababu asilimia kubwa sisi ni wa vipato vidogo (masikini)

Tunaofurahishwa wote ni wale hohe hahe 😂
Tajiri muda wake mwingi anautumia kwenye miradi yake hawezi ku focus na maisha binafsi ya mtu kiasi hicho

By the way comment za waja zinanichekesha
Watu wapo serious free jukusi 🤣🤣
 
Back
Top Bottom