bless on
JF-Expert Member
- May 22, 2026
- 743
- 1,733
Unajua kwamba watu waliodharauliwa sana katika nyakati fulani za maisha, hubaki na kumbukumbu inayowafanya watafute heshima na kuthaminika kwa namna yoyote. Hujawahi kuona watu waliozaliwa kwenye familia zenye nguvu ya pesa, ni watulivu sana, hawajioneshi na siyo rahisi kujua kama ni watoto wa kishua. Lakini kuna wale ikitokea baba kapata unafuu kidogo, ni lazima dunia nzima ijue. Hii ni kawaida kwa watu waliotamani heshima kwa muda mrefu.
Waliozaliwa na kukulia kwenye 'mkate na cheese' hawajawahi kukosa heshima, kwa hiyo hawahangaiki kuitafuta wala kujipa uthibitisho sababu wanajua wao wenyewe ndiyo heshima wala hawahitaji kukuonesha chochote ili uwaheshimu. Wale rachirachi mara nyingi hawana uhakika kama wanaheshimiwa, wana tatizo la inferiority complex, ni lazima watafute uthibitisho wa heshima na kukubalika.
Utajuaje kama una hilo tatizo, ukiona unapokuwa na hali nzuri kidogo, hutulii mpaka watu wajue, basi tambua wewe ni mhanga. Wengine akishapokea kimshahara ni lazima aanzie bar na kuzungusha raundi kwa walevi kadhaa. Hii yote ni sababu ndani yake anahisi anahitaji uthibitisho wa heshima au thamani ambayo anadhani hakuwahi kuwa nayo.
Kuna wengine hubeba mabegi ili kwenda kupiga picha viwanja vya ndege na kupost mitandaoni. Ukweli ni kwamba, waliozoea kupanda ndege tangu utotoni huwa hawahangaiki na shughuli hizo. Kuna watu humu mitandaoni wanasafiri kila siku na wanakula maisha kisawasawa lakini hawakumbuki kabisa ku post. Ni kwa sababu hayo ni maisha yao, hawaoni ajabu kwa lolote na wanadhani watu wote wanaishi hivyo.
Mtoto aliyezaliwa na kukulia kwenye familia ya viongozi, huwa anaenda ikulu kucheza na anamuona rais au waziri mkuu kama mjomba au ndugu, hawezi kuhangaika kuuonesha ulimwengu kuwa anajuana nao. Lakini kina ngwapangu wakipiga picha na mkuu wa wilaya ni lazima apost mitandao yote na maneno "God did"🤣🤣
Anyway sina lengo la kukandia mtu ila najaribu kukuonesha jinsi ambavyo akili zetu haziwezi kuficha upungufu fulani tulionao.