Kwanini funguo za gari zipo mkononi muda wote?

Kwanini funguo za gari zipo mkononi muda wote?

View attachment 81594

Wengi siku hizi wana tabia ya kutembea huku wameshika funguo za gari, wengine huwa wanazizungurusha kidoleni, wengine wanaziweka juu ya meza(rest, etc)
Hivi huu ni mtego?? Style? Kujisikia?? Au....
Funguo za kufuli(VIRO) za mlangoni kwangu huwaga nazitoa na kuzishika mkononi mara nyingi na kuzirudisha mfukoni kuhakikisha kuwa ninazo, sababu zikipotea kuvunja VIRO sio kazi ndogo.
 
Kwani gari bado ni asset ya kujidai nayo?
 
Gari kitu gani jamani mpaka ubebaji wa funguo iwe issue? wacha mtu abebe ananyojisikia ni la kwake ati.
 
View attachment 81594

Wengi siku hizi wana tabia ya kutembea huku wameshika funguo za gari, wengine huwa wanazizungurusha kidoleni, wengine wanaziweka juu ya meza(rest, etc)
Hivi huu ni mtego?? Style? Kujisikia?? Au....
Nabeba za mlango wa nyumba, tena ya kupanga, nikinunua gari ntaongeza tu.
 
Ninachozungumzia mimini tabia ya mtu kujionyesha kuwa ana gari kwa kushika funguo na mara kwa kuzionyesha. Hata mimi huwa nazishika mkononi maana zinakuwa salama zaidi kuliko kuweka mfukoni ikiwa sina key holder. nafikiri umenielewa Tiba
 
Gari sio deal tena na wala sio sifa
Maana gari sio asset ni liability.

Hata zamani wakati simu zinakuja lilikuwa ni jambo, achia mbali TV na kuvaa viatu

Ukikwazika kwa mtu kuweka funguo kidoleni au mezani jua bado unaishi 'Ngw'ashibhuga'

Mepapendaje hapooooo penye red!!!!!
 
huu ni wivu wa kijinga,je wanaoshika funguo za nyumba je,acheni wivu na funguo za gari zao
 
Ni attitude tu ya watu aisee. Recently niliamua kuweka flash stick kwenye kitambulisho cha kuvaa shingoni manake nikihama nayo naisahau kila mara. Mtu akaniambia namkumbusha zamani ati watu walivaa flash stick shingoni kudolishia! Nikamshangaa tu manake.sijawahi ona mtu amevaa flash nikawaza anaringishia, hata kipindi sijawahi kumiliki!
Kwani gari bado ni asset ya kujidai nayo?
 
Na kwa nini ubebelee mafunguo yote hayo! Sasa hapo una kagari kamoja, ukiwa na magari matatu ya kutembelea na malori mawili ya biashara. Si utahitaji rambo, lol!
Tuliwahi kujadili hili humu ndani...! Kwa uchache tu...funguo wa chumbani, wa mlango wa nje na grill, wa geti, wa gari, wa lock ya gear (kwa baadhi ya magari ya "manual"), za lock ya spare tyre, za mlango wa ofisini, za grill na milango ya ka "frame" kangu....plus key holder! Unaweza kuongezea nyingine hapo!. Sasa hizo zote, hata kama nimevaa jeans kwa kweli inaniwia vigumu kuweka mfukoni. "Mnaokereka" kwa kweli mtusamehe tu! Hapo bado hujaweka na simu (galaxy s3, bb etc)....hiyo suruali lazima itavuka tu!

Inategemea pia na sehemu ulipo...kuna ofisi au maeneo mengine unakuta zaidi ya 70% wana magari...sasa hata kuweka funguo mezani au kushika mkoni pengine sio shida sana
 
na akimiliki kitu kampuni ya kukodisha magari kama X car?

Si atakodi gari la kubebea funguo?

Na kwa nini ubebelee mafunguo yote hayo! Sasa hapo una kagari kamoja, ukiwa na magari matatu ya kutembelea na malori mawili ya biashara. Si utahitaji rambo, lol!
 
Na kwa nini ubebelee mafunguo yote hayo! Sasa hapo una kagari kamoja, ukiwa na magari matatu ya kutembelea na malori mawili ya biashara. Si utahitaji rambo, lol!

hahahahaha!!!! muache mwenzio. labda mwepesi sana anajiongezea kilo dizaini. town upepo mkali atiii
 
Hivi mtu akiwa na gari funguo hazikai mfukoni ni lazima ashike mkononi atembee nazo au ni ushamba tu.:shut-mouth::shut-mouth:
 
Nadhani kwa wengi unakuta sehemu rahis (reflex action) ni kuushika mkononi ukizangatia key holders za magari ya wengi ni kubwa so it is the quickest place esp ukiwa unaenda nearby, na wengi ni mazoea
 
Kwa wanaume kwa sababu hawana bochi naona ni bora kushika mkononi hizo funguo kwani zikiwekwa mifuko yao ya suruali na shati hazikai vizuri mifuko inatuna wanakuwa kama wachuuzi wa Kariakoo
 
ushamba tu.mbona uzi kama huu ulisha pita hapa last year.mm huwa nauweka mfukoni ukimbelea nchi za magharibi utaona walivyo zoea
 
Mazoea tu mbona wadada wanaweka kwenye pochi funguo zao? Wanaume wengi ni mazoea mwingine hata simu ni shida kuweka mfukoni hata kama ni ya tochi, utamshow nani kila mtu ana gari sku hizi!!! na wewe umeonaje kuwa kashika funguo....? au huwa unatafuta funguo za gari?!!!
 
Back
Top Bottom