Kwanini funguo za gari zipo mkononi muda wote?

Chapa Nalo Jr

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2010
Posts
7,520
Reaction score
6,517
Miaka kama kumi iliyopita sio wote walikuwa na simu za mikononi, hivyo wanaume wenye simu walihakikisha simu zao zipo sehemu za wazi( kiunoni au mkononi) kwani ilisemakana(hasa uswahilini) ni rahisi kupata demu ukionekana na simu. Wengine waliazima simu kama anaenda kumwaga sera kwa demu.

Sasa siku hizi mtu akiwa na gari(liwe lake au la) basi atahakikisha ufunguo upo sehemu ya wazi, ataushika kwa mbwembwe uonekane, akifika bar au ofisini atauweka mezeni (funguo zingine kama za milango hufichwa huko mfukoni). Sasa mimi hubaki kujiuliza kuwa ufunguo wa gari hautakiwi kuwekwa mfukoni!? Je au ndio hivyo tena kujionyesha kwamba naye yumo?

Hii tabia ya funguo za gari ni kwa jinsia zote. Je ni mitego kwa mademu na serengeti boys mshoboko? Najiuliza sana!

Mjadala mwingine: Kibongo bongo: How to let ladies know you own a car?
 
Acha wivu wa kike tafuta na wewe ufunguo uwalingishie kama bakora zimekuingia hustle hard,dawa ya bishoo ni kuwa bishoo zaidi yake......
 
Gari ninalo lakini sitembezi ufunguo wa gari yangu kwenye meza za bar.
 
Miaka kama kumi iliyopita sio wote walikuwa na simu za mikononi, hivyo wanaume wenye simu walihakikisha simu zao zipo sehemu za wazi( kiunoni au mkononi) kwani ilisemakana(hasa uswahilini) ni rahisi kupata demu ukionekana na simu. Wengine waliazima simu kama anaenda kumwaga sera kwa demu.

Sasa siku hizi mtu akiwa na gari(liwe lake au la) basi atahakikisha ufunguo upo sehemu ya wazi, ataushika kwa mbwembwe uonekane, akifika bar au ofisini atauweka mezeni (funguo zingine kama za milango hufichwa huko mfukoni). Sasa mimi hubaki kujiuliza kuwa ufunguo wa gari hautakiwi kuwekwa mfukoni!? Je au ndio hivyo tena kujionyesha kwamba naye yumo? Hii tabia ya funguo za gari ni kwa jinsia zote. Je ni mitego kwa mademu na serengeti boys mshoboko? Najiuliza sana!

Dugu yangu, huo ni ulimbukeni kama ulivyokuwa wa simu. Ukishazoeleka pia nao utaisha.

Si unajua tena kwetu huku?Hata kama toleo jipya la ch**p* ndo limeingia utawaona watu uchi uchi......full kutangaza nao wamo!
 
khaa! Hapa umenipata kabisa. Hivi unajua ufunguo wa gari haupenezi kabisa kukaa mfukoni, hasa unapokuwa umekaa sehemu.
 
Miaka kama kumi iliyopita sio wote walikuwa na simu za mikononi, hivyo wanaume wenye simu walihakikisha simu zao zipo sehemu za wazi( kiunoni au mkononi) kwani ilisemakana(hasa uswahilini) ni rahisi kupata demu ukionekana na simu. Wengine waliazima simu kama anaenda kumwaga sera kwa demu.

Sasa siku hizi mtu akiwa na gari(liwe lake au la) basi atahakikisha ufunguo upo sehemu ya wazi, ataushika kwa mbwembwe uonekane, akifika bar au ofisini atauweka mezeni (funguo zingine kama za milango hufichwa huko mfukoni). Sasa mimi hubaki kujiuliza kuwa ufunguo wa gari hautakiwi kuwekwa mfukoni!? Je au ndio hivyo tena kujionyesha kwamba naye yumo? Hii tabia ya funguo za gari ni kwa jinsia zote. Je ni mitego kwa mademu na serengeti boys mshoboko? Najiuliza sana!
Bila kufanya hivyo, utajuaje kama ana gari? Halafu mimi nawapenda wale malimbukeni wanaotembea na ufunguo wa gari mkononi, bega moja juu na jingine chini. Mbona tutakoma, gari yenyewe mtumba.
 
we achana kabisa na uchawi wa kijapan....hiyo kitu haitaisha leo wala kesho ......mambo ya mydia njoo unipick hapa mlimani city unipeleke home mbezi beach na wewe uko mbagala...
 
Bila kufanya hivyo, utajuaje kama ana gari? Halafu mimi nawapenda wale malimbukeni wanaotembea na ufunguo wa gari mkononi, bega moja juu na jingine chini. Mbona tutakoma, gari yenyewe mtumba.

Halafu isije kuta mtu ana ufunguo wa gari kumbe gari hana.
 
Miaka kama kumi iliyopita sio wote walikuwa na simu za mikononi, hivyo wanaume wenye simu walihakikisha simu zao zipo sehemu za wazi( kiunoni au mkononi) kwani ilisemakana(hasa uswahilini) ni rahisi kupata demu ukionekana na simu. Wengine waliazima simu kama anaenda kumwaga sera kwa demu.

Sasa siku hizi mtu akiwa na gari(liwe lake au la) basi atahakikisha ufunguo upo sehemu ya wazi, ataushika kwa mbwembwe uonekane, akifika bar au ofisini atauweka mezeni (funguo zingine kama za milango hufichwa huko mfukoni). Sasa mimi hubaki kujiuliza kuwa ufunguo wa gari hautakiwi kuwekwa mfukoni!? Je au ndio hivyo tena kujionyesha kwamba naye yumo? Hii tabia ya funguo za gari ni kwa jinsia zote. Je ni mitego kwa mademu na serengeti boys mshoboko? Najiuliza sana!

Nilisikia jamaa mmoja akisema kwamba "gari ni uchawi wa kizungu" akimaanisha kwamba hata demu ambae
ana msimamo akikuona na gari zuri basi anageuka kuwa na mkao !!
 
Mhhhhhh! Hayo mambo mbona huku KINO yamepitwa kitambo sanaa! What is FUNGUO!!!!! HUKU WATU WANARINGISHIANA, NDINGA VS USAFIRI!!!!!!!!! "MKO WAPI HAPO CINE CLUB? MI SIWEZI KUWAONA KABISAAA! NJOONI TU MNIFATE HUKU PARKING KWA KWELI!!!" Hapo mnajua keshahongwa NDINGA JIPYA! " Usije! Tusubiri hapo hapo tunakufata" PEOPLE HAVE THE RIGHT KNOW! Mkifika ndo anashuka ili MUMUONE VIZURIIII! Hapo akiona Corrolla zimepaki pembeni "HIVI HIZI NAZO BADO ZINATOKAGA TU, MI NILIDHANI WAMEACHA KUTENGENEZA"(Mswahili akipata ****** hulia Mbwata!) Siku akinyanganywa anakuwa mdogooo kama piriton, Anashuka kwenye BAJAJI kwa machale kama anaingia kwa mganga wa kienyeji. Usipime mtu yupo brajec ya Survey parking zilivo mbali afu anadai afuatwe Parking.!
 
Halafu isije kuta mtu ana ufunguo wa gari kumbe gari hana.

Gari analo ila ANAWEKA MAFUTA YA BUKU 3! AU GARI ZA MWISHO WA MWEZI TAREHE 27-6 Unashangaa Parking ya Ofisi imejaa, baadae mnapishana kwenye dala na vibajaji. MJINI MIPANGO!
 
Yaani mafuta ya buku 3 maana yake taa ya mafuta haijizima kamwe mpaka iungue.
 
Mhhhhhh! Hayo mambo mbona huku KINO yamepitwa kitambo sanaa! What is FUNGUO!!!!! HUKU WATU WANARINGISHIANA, NDINGA VS USAFIRI!!!!!!!!! "MKO WAPI HAPO CINE CLUB? MI SIWEZI KUWAONA KABISAAA! NJOONI TU MNIFATE HUKU PARKING KWA KWELI!!!" Hapo mnajua keshahongwa NDINGA JIPYA! " Usije! Tusubiri hapo hapo tunakufata" PEOPLE HAVE THE RIGHT KNOW! Mkifika ndo anashuka ili MUMUONE VIZURIIII! Hapo akiona Corrolla zimepaki pembeni "HIVI HIZI NAZO BADO ZINATOKAGA TU, MI NILIDHANI WAMEACHA KUTENGENEZA"(Mswahili akipata ****** hulia Mbwata!) Siku akinyanganywa anakuwa mdogooo kama piriton, Anashuka kwenye BAJAJI kwa machale kama anaingia kwa mganga wa kienyeji. Usipime mtu yupo brajec ya Survey parking zilivo mbali afu anadai afuatwe Parking.!

Ha ha ha! We kweli wa Dar!! Unakuta eti mtu unampigia simu "halo, halo ... " anakujibu, "Sorry nadrive X3, nitakupigia baada ya muda".
 
Back
Top Bottom